Bei ya kuzoa taka Mbezi Beach inapangwa kutokana na uhalisia wa mazingira na kipato

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,462
Siku chache baada ya malalamiko kuripotiwa kuhusu gharama za uzoaji taka kwenye makazi ya watu kuwa juu katika baadhi ya mitaa ya Mbezi Beach B, ikidaiwa kuwa kuna kampuni inayotoza Tsh. 15,000 kwa mwezi kwa nyumba badala ya Tsh. 3,000 hadi 5,000 kwa mwezi, ufafanuzi umetolewa.

Malalamiko yako hapa: Kampuni ya kuzoa taka nyumbani Mbezi ya Chini inatuumiza Wananchi, inaongeza bei kutoka Tsh 3,000 hadi 15,000

Mwenyekiti wa Mbezi Beach B, Aisha George akizungumzia malalamiko hayo amesema:

“Viwango vinavyotozwa kwenye utozaji taka ni vya Kisheria na inategemea na eneo, pia ni bei elekezi, tunaamini huwezi kufananisha maeneo yote kuwa sawa.

“Nitolee mfano Mbezi Beach, kuna maeneo ambayo familia kula milo mitatu kwa siku ni shida, lakini yapo maeneo ambayo kuna hoteli kubwa au familia ambazo zina maisha nafuu kuliko maeneo mengine.

“Kingine pia huwa tunaangalia uhalisia, wapo wenye changamoto mbalimbali mfano wajane, wasiokuwa na kazi n.k, tukibaini hilo wanakuja ofisini kwetu tunazungumza nao na wanapewa bei anayoweza kuilipa kulingana na mazingira yake.”

Upande wa Mtendaji Kata ya Kawe, Husna Nondo amesema: “Tuna Sheria ndogo zinazosimamia masuala ya takataka, kwenye Kaya ni wastani wa Tsh. 3,000 hadi 30,000.

“Pamoja na hivyo mwananchi akiwa na changamto ya peke yake anafika Ofisi za Serikali za Mtaa tunazungumza kunakuwa na msamaha kama ilivyo katika kodi ya majengo.”

Chanzo: Radio Times FM
 

Attachments

  • TAKATAKA.mp3
    3.4 MB
Kwa kawaida almashauri imetoa bei elekezi kutokana na maeneo kulingana na kipato..kuna kipato cha juu,cha kati na cha chini,hivyo sehem km mbezi inahesabiwa km wananchi wa kipato cha juu..lakini pia unatakiwa kulipa taka kulingana na uzalishaji wako,mzalishaji wa taka wa kiwango cha juu anaeishi mbezi beach au masaki ni tofauti mazalishaji wa kiwango cha juu anaeishi kigogo.
 
Back
Top Bottom