Wamejilipua kweli mpaka kuuweka wazi waraka wao. Kina Sheikh Ponda watakuja na waraka wao wa kuunga mkono uwekezaji bandarini na hapo pataibuka kutokuelewana kati ya dini hizi mbili.

Sioni kama ni hekima kwa TEC kuja na waraka muda huu huku wakifahamu kuwa waislam wanasimama na mheshimiwa SSH. Walichokifanya sio heshima kwa mamlaka ya juu ya nchi.
2A75D7CB-9AA4-4D66-B66E-CDC355572F05.png
 
Madhehebu yote ya dini wanapewa misamaha ya kodi kiwango fulani, kama wakiomba.
Kama ambavyo watumishi wote wa umma wanapata tax exemption kwenye bidhaa fulani, lakini pia ni mpaka uombe.

Ni juha wa kutupwa tu anayeweza fikiri kuwa kodi hazishughulikiwi na TRA, ila na hao watoa mizigo (TPA & assoc).

Ukisema taasisi za dini zinaogopa kwamba DPW wakija,misamaha ya kodi itakwisha,maana yake ni kuwa hao DPW pia watahusika na ukusanyaji wa mapato na mifumo yote ya utoaji mizigo.

Maana yake kwa mujibu wako wewe Crocodiletooth na wenzako, DPW inawaondoa TRA pale bandarini na kubadilisha sera na sheria zetu za kodi.
 
Kuondolewa kwa TICTS bandarinj ni maumivu makali sana kwa kanisa Katokiki kwa sababu walizoea kupitisha vitu bure kwa sababu ya Karamagi kuwa mmiliki wa TICTS. Alianza Kadinali Pengo kuongea mwanzoni kabisa akashughulikiwa akapumzika lakini sasa TEC wamekuja kama taasisi wanafanya yale yale wanayofanya wanasiasa. TEC mlikuwa wapi wakati wa uchaguzi wa 2020? Hamkuwa na cha kusema kama kweli mnatetea watanzania ?

TEC hawana mamlaka ya kuwasemea watanzania na hawajawahi kuwa wasemaji wa watanzania. Wao ni wasemaji wa waumini wao na wabaki wakisema mamho yao huko makanisani na hakuna mahali waliombwa kuwasemea watanzania.

TEC hawa ndiyo ambao miongozi mwao akina Kilaini walipokea rushwa kutoka pesa walizoibiwa watanzania kwenye sakata la ESCROW. TEC hawa ndiyo waliokuwa wanageuza madhabahu ya makanisa yao kufanya siasa na kujisafisha kwa bwana yule wakati nchi inavuja damu na machozi.

TEC wamelidharau bunge na kuliona halina maana yoyote na hili linapaswa kushughulikiwa na bunge kwa ukali sana ikibidi huyu Katibu wa TEC aitwe kuhojiwa na kamati ya bunge kwa sababu ameacha kazi yake ya upadre sasa anaingia kwenye siasa na upinzani dhidi ya serikali .

TEC wanadhani wao ndiyo wenye hati miliki ya kuongoza hii nchi. Hawakusema uozo wa TICTS wakati wa Mkap na Magufuli kwa kuwa ni wakatoliki wenzao. Hawakuona madudu ya TICTS kwa sababu Karamagi ni mkatoliki mwenzao na zaidi wananufaika na uwepo wa TICTS bandarini kwa kuwa wanapitisha mizigo bure. Ujio wa DO World unakwenda kufunga hii mianya na huu ujinga hautakuwepo tena.

TEC wana mamlaka gani ya kusema mkataba uvunjwe? Au kwa sababu DP World ni waarabu ba waislamu ? TEC waonywe na wambiwe wakome kudhani Tanzania ni nchi ya kidini au kikatoliki. Wakome kudhani wanaweza kulidharau bunge na kama watakata siasa wavue kanzu waache kugawa sakramenti waje majukwaani kufanya siasa.

Katibu wa TEC alikuwa mmoja ya waalikwa kwenye mkutano wa wanasiasa wanaopinga uwekezaji bandarini. Leo anakuja anapanuapanua mdomo kuwa watanzania sijui wamesema hivi mara vile.

Ifike mahaki TEC waambiwe WAKOME hii tabia na kama wanadhani wanaweza kudharau viongozi wa nchi kisa siyo wakatoliki basi wajiandae vizuri sana kwa sababu hiyo vita hawatakaa waishinde na TEC ni wahujumu wa juhudi za serikali kuboresha bandari.

:View attachment 2721636Nb,Bado tunasubiri matamko toka...!👆👆
ILI MANENO YA WENGI NI MANENO YA MUNGU YATIMIE.
NAAMINI KATIKA USAWA!
Ni nini kimekusibu mpaka ukatoa matspishi kiasi hiki?
PS.
Karamagi ni muislamu.
 
Mimi ni mkristo mkatoliki! Natoa maoni yangu kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya katiba ya Tanzania.

1.With due respect, sijaona wazo la maana la TEC. There is NO substance in it. Dunia ya leo inajengwa na uwekezaji wa kimataifa(international investments).

Hata China, Russia kuna uwekezaji mkubwa wa makampuni toka nje ya nchi. Tanzania siyo kisiwa. Lazima tuendane na sera za kiuchumi za dunia ya leo. Kuendesha mifumo ya uchumi mkubwa kama bandari, kijamaa tumeshindwa na tutaendelea kushindwa. Hata hii SGR tukisema iendeshwe kwa mifumo ya utumishi wa umma tutashindwa pia. Assets zenye sura ya kibiashara kama hii lazima ziendeshwe na private sector ili zilete faida na tija.

2. Findings za hao TEC ziko based on heresay. Wametumia axiom ya vox populi vox dei, Sauti ya watu ni sauti ya Mungu.Je ni watanzania wangapi wanapinga uwekezaji huu wa DP World? Je kuna wakatoliki wangapi hapa nchini? Je wakatoliki wote wanaupinga mkataba huo? Je wakatoliki waliomo kwenye orodha za wakatoliki bado ni wakatoliki mpaka sasa?(Wengi wameshahamia kwenye ulokole).

Ukijibu maswahi hayo utaona maaskofu wa TEC hawana uhalisia kwenye waraka wao.Ni blah blah tu. No driving facts. It is just FALLACY OF GENERALIZATION. Findings zao hazina supporting data. Wamekurupuka!

3. DINI: Naona ni hofu za masilahi yao ya kidini, wala siyo tatizo la mkataba. Wazungu toka nchi za magharibi walipoingia mikataba ya kuiba madini ya watanzania, maaskofu wa TEC walikaa kimya!!! Leo wakati wa mkataba na waarabu ETI wanajitia kuandika waraka wakijipambanua ETI wazalendo,watetezi wa rasilimali za nchi. UWONGO mtupu!

4. Serikali haina dini na mambo yote ya dini yapo nje ya mifumo ya serikali(Ibara ya 19 ya katiba ya TZ,1977). Huo waraka wao hauna mashiko wala nguvu yoyote mbele ya Jamuhuri. Ni kama makaratasi ya kufungia maandazi tu! Hayo ni maoni yao kama maoni ya mtu yoyote yule.

CONCLUSION: Serikali iendelee na mchakato wa utekelezaji wa mkataba na DP World HARAKA SANA, ili kama taifa tuanze kunufaika na uwekezaji huo HARAKA. Serikali kikatiba ina mizizi mirefu sana na mikubwa sana, isiyumbishwe na kelele za chura ambazo ni nyepesi sana.

Wananchi tuna hitaji pesa ipatikane ili tupate huduma bora za kijamii. Uwekezaji DP world ni LAZIMA ufanyike. Na ufanyike HARAKA iwezekanavyo. Serikali ina legitimacy ya kufanya maamuzi kwa niaba ya wananchi kwa sababu iliingia SOCIAL CONTRACT na wananchi kwa kushinda uchaguzi,2020.
 
Mimi nafikiri hapa hoja kubwa inayo pigiwa kelele ni ubovu wa mkataba ilio ingia Tanganyika na Dubai.
Nimesikia, mkataba mbovu ambao hauna maslahi mapana kwa taifa ndio hasa chanzo na ndipo tatizo lilipo anzia.
Kwahivyo hapa hoja sio kwamba wapingaji hawataki muwekezaji, Lah.
 
Mimi nafikiri hapa hoja kubwa inayo pigiwa kelele ni ubovu wa mkataba ilio ingia Tanganyika na Dubai.
Nimesikia, mkataba mbovu ambao hauna maslahi mapana kwa taifa ndio hasa chanzo na ndipo tatizo lilipo anzia.
Kwahivyo hapa hoja sio kwamba wapingaji hawataki muwekezaji, Lah.
........wabongo tulio wengi nadhani tuna shida kidogo, hili ulilosema limerudiwa zaidi ya mara mia lakini sijui kwa nini watu hatuelewi.......
 
Hakuna anaebisha kuwa mkataba wa DP World na Tanzania ni mbovu.

Wanaharakati wameweka bayana na sisi tusio wanasheria tumeelewa. Hilo ni jambo jema.

Shida inakuja pale Taasisi moja ya dini inajiona yenyewe ndio inaweza kuamua na kusemea taasisi zingine. That's stupidity!

Tanzania ni ya wote Christians, Muslims, Jews, Buddhists na hata wasio na dini rasmi za kigeni.

Iweje Taasisi moja idai yenyewe ndio ina mizizi kwenye kila kaya. Kwa hiyo mnatutisha sisi protestants na Waislamu eeh?

Mbona mnamwandama sana Rais na serikali, angekuwa ni muumini wenu mngefanya hivyo?

We are no longer under the yoke of Papacy regime.

Waprotestant tupo wengi tunaweza jisemea. Naomba mkae kwa kutulia.

Mkataba hatuutaki na utumwa wa kidini hatuutaki pia. Nimemaliza.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom