Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
1. Wanadai Serikali iachane na Mkataba wa Bandari kwa sababu wananchi wamegawanyika kuhusu mkataba huo!
Swali langu kwao, Ni jambo lipi nchi hii limewai kukubaliwa na asilimia 100 ya wananchi wote? Kwenye Mfumo wa vyama vingi, Mbona asilimia kubwa ya Wananchi walikataa mfumo huo ila Serikali wakauunga mkono! Je kwa nini hawakutoa tamko kipindi icho kutaka nchi iendelee kuwa ya Chama kimoja? Kwa tamko lao walilosema maamuzi ya wananchi yaheshimiwe basi wanaunga mkono Serikali i reverse maamuzi yake ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi na turudi kwenye mfumo wa Chama kimoja?
2. Kwenye tamko lao wanadai Mihimili ya dola iheshimiwe. Swali langu kwao! Juzi Mahakama Kuu wametoa maamuzi ya kutupilia mbali maombi ya watu walioshtaki mkataba wa Bandari.
Sasa kwa nini wanataka mihimili ya dola iheshimiwe na wao hawataki kuheshimu maamuzi ya Mahakama? Kama Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 hasa ibara ya 107A inasema Mahakama ndio Mhimili wa mwisho katika kutoa haki sasa kwa nini hawaheshimu maamuzi ya Mahakama alafu wanatoa tamko kusema Mihimili ya dola iheshimiwe?
3. Wao wanavyotoa tamko kutaka Serikali iachane na mkataba wa bandari kesho BAKWATA wakitoa tamko Serikali iendelee na mkataba wa Bandari wanataka Serikali imsikilize nani? Kesho kutwa mabudha wakitoa tamko pia wanataka Serikali imsikilize nani kati yao?
Kwa hali hii sasa nimejua kwa nini mapadre wa kanisa katoliki walishtakiwa kwa kuhamasisha mauaji ya kimbari Rwanda!
Pia soma
- News Alert: - Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu