Hakuna mwanasiasa/Rais aliweza kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na akashinda!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Kwa wajuzi wa historia ya Tanzania wameishajua kuwa Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) la kuhusu mkataba baina ya serikali ya Tanganyika AKA Tanzania na DP World ni kaa la moto mkali ambao unazidi kumchoma vikali muhusika mkuu na chama chake mpaka watakapokufa kisiasa mapema kama wataendelea kushupaza shingo.

Katika historia ya Tanzania hakuna mwanasiasa au Rais aliwahi kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) halafu akashinda. Haijawahi kutokea na haitawahi kutokea katika miaka hii ya karibuni. Kufanya hivyo ni kujiangamiza kisiasa(political suicide).

Unaweza kuukataa huu ukweli lakini kuukataa kwako hakuwezi kuubadilisha kuwa uongo.

Mwl. Nyerere pamoja na nguvu zote za kikatiba alizokuwa nazo katika utawala wake lakini hakuwahi kutumia nguvu katika kupitisha ajenda zake za kisiasa pale ambapo maaskofu walikuwa na shaka au kumpinga. Alitumia nguvu ya ushawishi wa hoja kwa kujadiliana nao mpaka wakamwelewa na kukubali.

Nguvu za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) zimeendelea hivyo katika tawala zote nchini. Hakuna mwanasiasa mwenye uelewa wa Tanzania na akili timamu aliweza kupuuza sauti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Muhusika mkuu wa mkataba wa DP World hakutegemea kama TEC wanaweza kutoa waraka mkali kama waliotoa kwa sababu sehemu ya 17 ya waraka imepigilia msumari wa mwisho wa jeneza la mkataba.

TEC IMEITAKA SERIKALI IACHANE NA MKATABA HUU.

Sehemu ya 17 ya waraka wa TEC inasema, “Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe. Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; niwajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu. Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu”.

Baada ta waraka kutolewa, muhusika mkuu na genge lake akaanza kuhaha akitafuta jinsi ya kukabiliana nao. Amemtuma kiongozi mkuu wa nchi mstaafu ili ajibu hoja lakini hakufanikiwa kuzima moto, amejaribu kutumia mbinu za kidini kwa kuwatuma baadhi ya mashekhe ili wawajibu TEC katika misingi ya kidini lakini pamoja na juhudi zote, moto wa waraka wa TEC ndio unashika kasi ya kumchoma kisiasa. Ametuma “wajinga” fulani washambulie haiba ya maaskofu badala ya kujibu hoja hawajafanikiwa.

Alichofanya kwa sasa ni kuwatuma baadhi ya viongozi ndani ya serikali kwenda Dubai ili kuwaeleza wenye DP World kuhusu moto unavyowaka nchini ili waangalie namna ya kufanya ili kuondokana na moto mkali kisiasa ili kuepuka maafa ya kisiasa. Kwa hivi karibuni ndege ya Rais imekuwa na safari nyingi za kwenda Uarabuni na kurudi.

Katika hali hiyo ya kutapatapa ametangaza eti tenda ya kukaribisha wawekezaji kwenye bandari Terminal 2 ili ionekane hakutaka kugawa bandari zote kwa DP World wakati mkataba(IGA) unabainisha ni bandari zote na maziwa yote ya Tanganyika AKA Tanzania bara. Mjinga gani atakuja kuwekeza kwenye terminal 2 wakati kuna IGA inasema uwekezaji wowote katika bandari na maziwa nchini lazima kwanza uridhiwe na DP World.
Tumeona pia amemuondoa waziri wa katiba na sheria ili eti ionekane kama ndiye aliyesababisha hili sakata la DP World wakati kwenye IGA kuna saini ya Rais! Huku ni kutapatapa.

Kama isingekuwa waraka wa TEC, mchakato wa kuzifuta Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohousu Rasilimali na Maliasili za Nchi za mwaka 2017 ungefanyika bungeni na hili tangazo lingine la tenda ya kukaribisha wawekezaji lisingetolewa! Hii yote ni imefanyika katika hali ya kutapatapa baada ya tamko la TEC.
 
Kwani TEC wamekwambia wapo kwenye Mapambano?

Nyie ndio mnaofanya struggle au jambo jema kuonekana baya na la ajabu kwa kuleta ushabiki usio na Tija?

Je, wanachosimamia hao TEC ni kwa manufaa yao kama TEC au Taifa? Ukiweza kupima hilo nadhani utaanza kuyaangalia mambo kwa jicho la nini kinapiganiwa na sio kina nani wanakipigania.
 
Bi tozo nchi imemchachia

Mkuu, Soma hii thread inadadavua vizuri uongozi wa Rais Samia;

GONGA hapo chini usome;
Kwa Rais huyu, CCM wana hali mbaya sana!

Kwani TEC wamekwambia wapo kwenye Mapambano ?!!

Nyie ndio mnaofanya struggle au jambo jema kuonekana baya na la ajabu kwa kuleta ushabiki usio na Tija ?

Je wanachosimamia hao TEC ni kwa manufaa yao kama TEC au Taifa ? Ukiweza kupima hilo nadhani utaanza kuyaangalia mambo kwa jicho la nini kinapiganiwa na sio kina nani wanakipigania

Mkuu, acha kumung’unya na kupambapamba maneno! Haya ni mapambano tena makali.

Kama huoni kuwa haya ni mapambano ya kupigania maisha ya watanzania wa sasa na vizazi vijavyo basi utakuwa na tatizo la uelewa wa maswala hata yanayohitaji akili ya kawaida(common sense).
 
Kwani TEC wamekwambia wapo kwenye Mapambano ?!!

Nyie ndio mnaofanya struggle au jambo jema kuonekana baya na la ajabu kwa kuleta ushabiki usio na Tija ?

Je wanachosimamia hao TEC ni kwa manufaa yao kama TEC au Taifa ? Ukiweza kupima hilo nadhani utaanza kuyaangalia mambo kwa jicho la nini kinapiganiwa na sio kina nani wanakipigania
Taifa na Watanganyika wote kwa ujumla.
 
Kwa wajuzi wa historia ya Tanzania wameishajua kuwa Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) la kuhusu mkataba baina ya serikali ya Tanganyika AKA Tanzania na DP World ni kaa la moto mkali ambao unazidi kumchoma vikali muhusika mkuu na chama chake mpaka watakapokufa kisiasa mapema kama wataendelea kushupaza shingo!

Katika historia ya Tanzania hakuna mwanasiasa au Rais aliwahi kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) halafu akashinda. Haijawahi kutokea na haitawahi kutokea katika miaka hii ya karibuni. Kufanya hivyo ni kujiangamiza kisiasa(political suicide).

Unaweza kuukataa huu ukweli lakini kuukataa kwako hakuwezi kuubadilisha kuwa uongo.

Mwl. Nyerere pamoja na nguvu zote za kikatiba alizokuwa nazo katika utawala wake lakini hakuwahi kutumia nguvu katika kupitisha ajenda zake za kisiasa pale ambapo maaskofu walikuwa na shaka au kumpinga. Alitumia nguvu ya ushawishi wa hoja kwa kujadiliana nao mpaka wakamwelewa na kukubali.

Nguvu za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) zimeendelea hivyo katika tawala zote nchini. Hakuna mwanasiasa mwenye uelewa wa Tanzania na akili timamu aliweza kupuuza sauti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Muhusika mkuu wa mkataba wa DP World hakutegemea kama TEC wanaweza kutoa waraka mkali kama waliotoa kwa sababu sehemu ya 17 ya waraka imepigilia msumari wa mwisho wa jeneza la mkataba.

TEC IMEITAKA SERIKALI IACHANE NA MKATABA HUU.

Sehemu ya 17 ya waraka wa TEC inasema, “Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe. Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; niwajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu. Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu”.

Baada ta waraka kutolewa, muhusika mkuu na genge lake akaanza kuhaha akitafuta jinsi ya kukabiliana nao. Amemtuma kiongozi mkuu wa nchi mstaafu ili ajibu hoja lakini hakufanikiwa kuzima moto, amejaribu kutumia mbinu za kidini kwa kuwatuma baadhi ya mashekhe ili wawajibu TEC katika misingi ya kidini lakini pamoja na juhudi zote, moto wa waraka wa TEC ndio unashika kasi ya kumchoma kisiasa. Ametuma “wajinga” fulani washambulie haiba ya maaskofu badala ya kujibu hoja hawajafanikiwa.

Alichofanya kwa sasa ni kuwatuma baadhi ya viongozi ndani ya serikali kwenda Dubai ili kuwaeleza wenye DP World kuhusu moto unavyowaka nchini ili waangalie namna ya kufanya ili kuondokana na moto mkali kisiasa ili kuepuka maafa ya kisiasa. Kwa hivi karibuni ndege ya Rais imekuwa na safari nyingi za kwenda Uarabuni na kurudi.

Katika hali hiyo ya kutapatapa ametangaza eti tenda ya kukaribisha wawekezaji kwenye bandari Terminal 2 ili ionekane hakutaka kugawa bandari zote kwa DP World wakati mkataba(IGA) unabainisha ni bandari zote na maziwa yote ya Tanganyika AKA Tanzania bara. Mjinga gani atakuja kuwekeza kwenye terminal 2 wakati kuna IGA inasema uwekezaji wowote katika bandari na maziwa nchini lazima kwanza uridhiwe na DP World.
Tumeona pia amemuondoa waziri wa katiba na sheria ili eti ionekane kama ndiye aliyesababisha hili sakata la DP World wakati kwenye IGA kuna saini ya Rais! Huku ni kutapatapa.

Kama isingekuwa waraka wa TEC, mchakato wa kuzifuta Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohousu Rasilimali na Maliasili za Nchi za mwaka 2017 ungefanyika bungeni na hili tangazo lingine la tenda ya kukaribisha wawekezaji lisingetolewa! Hii yote ni imefanyika katika hali ya kutapatapa!

Swali la kujiuliza, kwa nini Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) lina nguvu kubwa na linaheshimika nchini tokea kuanzishwa kwake mwaka 1956 ukilinganisha na taasisi zingine za kidini?
Usahihi kamili wa hoja yako ni huu:

"Hakuna serikali yoyote ya kidunia (ikiwemo ya Tanzania) inaweza kupambana na kupingana na KANISA LA MUNGU na serikali hiyo ikaendelea kuwepo na kusimama..!"

TEC ni sehemu (kipande tu cha kanisa la Mungu). Lakini ukweli mkuu ni kuwa wapo watu wengi (jeshi la Mungu aliye hai hapa Tanzania) kote nchini (ukiacha TEC ambao wametoa official statement ya kukataa mpango huu wa Rais samia) ambao wanafunga na kuomba mchana na usiku kuhakikisha kuwa Mungu anaiponya nchi hii toka Kwa hayawani hawa..

Na mfano ulio dhahiri wa kuwa KANISA LA MUNGU liko kazini ni Mch. Mbarikiwa Mwakipesile na wafuasi wake huko Mbeya wanaomba usiku na mchana wakisema kwa uwazi bila kificho wala kumung'unya maneno kuwa Mungu aiangushe na kuipoteza CCM na serikali yake huku matangazo ya ibada zake yakirushwa live katika channel yake YouTube...

But all in all, huu ulioandika kwa ujumla wake ndiyo ukweli na wote wanaopingana na KANISA LA MUNGU wanajisumbua na kujipaka kinyesi tu...

Na ni kweli hii 👇👇👇 statement ya TEC ndiyo iliyomaliza na kuua kila kitu kabisa..!!

".....Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe. Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; niwajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu. Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu”.

This is bold and most importantly powerful and authoritative statement. No any other authority will surpass this!!
 
Back
Top Bottom