Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Bado hatuungi mkono Mkataba wa Bandari

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
718
703
Habari.
Kwa mujibu wa Vatican news, Kanisa katoliki Tanzania kupitia TEC limesisitiza kuwa haliungi mkono mkataba wa kukodisha bandari uliofikiwa baina ya Tanzania na DPW.

Taarifa ya TEC imesema haiungi mkono mkataba huo kwa kuwa sauti za watanzania hazikusikilizwa.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika maadhimisho ya Siku ya 97 ya Kimisionari Ulimwenguni, tarehe 22 Oktoba 2023 linaelezea kwa muhtasari ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Siku ya 96 ya Kimisionari Ulimwenguni, Kardinali Protase Rugambwa, Kongamano la Kitaifa la Utoto Mtakatifu, Jubilei ya Miaka 50 ya JNNK, AMECEA, Jubilei ya Miaka 155 Jimbo kuu la Songea na Miaka 125 Jimbo la Iringa, Mkataba wa Uboreshaji wa Bandari Tanzania.

====

cq5dam.thumbnail.cropped.1500.844.jpeg

Ujumbe wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Siku ya Kimisionari 2023​

Na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania-TEC, Dar es Salaam - Oktoba 22, 2023

Hatimaye ni tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC kuhusu Mkataba kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na “Emirate of Dubai” juu ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa maendeleo na uboreshaji wa bandari za Bahari na Maziwa nchini Tanzania.

Ni vyema, ni busara na ni hekima Serikali kuwasikiliza wananchi, maana kutowasikiliza ni kujiletea matatizo makubwa zaidi siku za usoni kwani wananchi hawahawa watavitaka vizazi vijavyo kuondokana na unyonywaji huu, kama tunavyoona kwenye kesi nyingi zinazoendelea sasa hivi katika mahakama za kibiashara za kimataifa dhidi ya mikataba iliyovunjwa na Serikali ya Tanzania.

Tukumbuke mikataba ya madini miaka ya ’90 viongozi wa dini na asasi za kiraia walipinga uwekezaji wa namna hii, na Serikali ikatumia mamlaka zake kuridhia mikataba hii na sasa hivi tunashuhudia ikivunjwa na nchi kulipa fidia kubwa.

Tunasisitiza kwamba SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU, “Vox Populi, Vox Dei” hivyo basi kuwasikiliza wananchi na kufanya maamuzi kadiri wanavyotaka kutailetea serikali heshima kubwa ya kuwa sikivu kwa watu. Kinyume cha haya, Mwenyezi Mungu anatuonya kupitia Nabii Yeremia anaposema: “Kama kapu lililojaa ndege walionaswa, ndivyo nyumba zao zilivyojaa mali za udanganyifu.

Ndiyo maana wamekuwa watu wakubwa na matajiri, wamenenepa na kunawiri. Katika kutenda maovu hawana kikomo hawahukumu yatima kwa haki, wapate kufanikiwa, wala hawatetei haki za maskini” (Yeremia 5:27-28). Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe.

Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; ni wajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu.

Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu. Mwishoni, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linazidi kuwaalika watu wa Mungu kujibidiisha katika kutoa kwa ukarimu Zaidi kwa ajili ya ufanisi wa shughuli za kimisionari katika Kanisa.


Imetoka hapa: Ujumbe wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC, Oktoba 2023 - | Vatican News

Pia soma - Katibu wa TEC: Maaskofu wanahitaji kuisoma mikataba iliyosainiwa, walipoitwa hawakuambiwa kulikuwa na nini
 
Mbona walikuwepo wakati wanasaini?

Walivyoitwa hawakuambiwa wanaenda kufanya nini?

Kwanini wakaongelee Vatican, si waitane watoe waraka mwingine,

Huku ni kuwachanganya waumini wao,

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
Mwingine wewe hujasoma kilichomo ndani ya uzi mzima. Huyu johnmashilatu anawaingiza chaka..!!
 
Maamuzi ya TEC siyo maaamuzi ya Watanzania, msituyumbishe nyinyi sio mliyoelewa sanaa shuleni kuwashinda wasomi wa ki Tanzania wengine. After all elimu yenu ni historia ya dini. Serikali haiongozwi na kamati za kanisa
Wewe umesoma content za uzi au TITLE imekuhemsha? Huyo bwana mtoa uzi kawapotosha
 
Maamuzi ya TEC siyo maaamuzi ya Watanzania, msituyumbishe nyinyi sio mliyoelewa sanaa shuleni kuwashinda wasomi wa ki Tanzania wengine. After all elimu yenu ni historia ya dini. Serikali haiongozwi na kamati za kanisa
Maamuzi ya TEC ni maamuzi ya watanzania zaidi ya milioni 15, hao sio watu wachache. na pia, bado waprotestant zaidi ya milioni 10 ambao waliungana na kinachosemwa na TEC. hiyo itaamua pia kura kama hawataweka mambo sawa kabla ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom