Ukijilengesha mimba kwabkuwa umeina jamaa anakaupepo ka hela mtateseka tu. Kama jamaa anaonesha hana niabya kuwa na wewe on permanent term kwanini umbebee mimba?
Uko poa Padre?

hii ilinitokea sana kipindi cha nyuma kila mwanamke anajilengesha tena kwa pigo za kunizalia kwa sababu wanajua nina visenti. 🤔 most girls do this tena kuna mmoja alikuwa nurse yule single maza ni mpumbavu sana.
Unajua tulitoka kuwa marafiki sana wa karibu. Nikienda kwake namnunulia zawadi dada wa kazi na katoto Kake ka kike. Wema wangu ulinisaidia sana. Dada wa kazi alinambia usiku dada anachanganya majani na kuwasha Mishumaa na kutaja jina lako😡😡😡
Kuna vitu vingi hatuwezi sema ila kuna watu wana roho za uharibifu na huwa nazikemea kwa Jina ya Yesu. .
 
Mhh.. mkuu mimi na wewe tuna nini cha kubishana hapo?
Nilimquote Clepatina kwenye comment yako kwamba hajaijibu, kumaanisha ulikuwa umetoa point nzuri yenye mashiko.
Kwaiyo tokea kwenye comment yangu ujumuishi wako haukuwa unahitajika, unless ulitaka kupigilia msumari point uliyokuwa umeitoa, ama kama ni alijibu na sijaona ungeniquote kwenye reply yake.
Utaniwia radhi,sikuielewa vizuri ile first sentence uliyonitag
 
Mhh.. mkuu mimi na wewe tuna nini cha kubishana hapo?
Nilimquote Clepatina kwenye comment yako kwamba hajaijibu, kumaanisha ulikuwa umetoa point nzuri yenye mashiko.
Kwaiyo tokea kwenye comment yangu ujumuishi wako haukuwa unahitajika, unless ulitaka kupigilia msumari point uliyokuwa umeitoa, ama kama ni alijibu na sijaona ungeniquote kwenye reply yake.
Sikuelewa utaniwia radhi.
 
Shaloom.

Dada mmoja aliamini kuwa mtu pekee anayestahili kuitoa bikra yake ni mwanaume atakayemuoa.

Huu msimamo wa bibie ulifanya apoteze "wachumba" wengi kwani walipoambiwa hawataonja asali mpaka waingie ndoani walisepa.

Miaka ikaenda,umri wa dada ukazidi kusogea ila bibie hakubadili msimamo wake.Aliendelea kuitunza bikra yake na kuishi maisha ya heshima kama
ambvyo binti yeyote mwenye maadili anapaswa kuishi.

Walokole tuna kamsemo ketu kuwa wakati wa Mungu ndio wakati sahihi na kweli "wakati wa Mungu ulipofika" bibie akaposwa na kijana aishie huko Marekani.

Kilichomvutia kijana kwa bibie ni habari alizozisikia kuwa bibie hajawahi kuguswa na mwanaume yeyote.

Kijana akatuma washenga,akatoa mahari na kufanya taratibu zote ikabakia ndoa tu ambayo ingefungwa baada ya yeye kwenda marekani na kurudi tena Tanzania.

Basi ikawa rasmi kuwa bibie sasa ni mke mrarajiwa wa mtu aishie Marekani.Viongozi wa kanisa na wazazi wakawa wanamtumia bibie kama mfano wa kuwaasa watoto wa kike kuwa ukijitunza Mungu atakuletea mume bora.Mabinti wakaambiwa si mnaona mwenzenu kajitunza sasa anaolewa na kwenda kuishi Marekani?

Basi bwana siku za mume mtarajiwa kurudi marekani zikakaribia na akaomba aende Dar na mkewe mtarajiwa akamfanyie shopping pamoja na kumuachia mradi wa ujenzi wa jumba lao lililoko Dar ausimamie.

Kwa vile kijana alishafanya taratibu zote wazee wakaona haina shida wakamruhusu binti asafiri na mumewe mtarajiwa kutoka mkoani kwao mpaka Dar.

Kufika Dar wakashukia hotel na huko kijana baada ya kushindwa kumshawishi binti atoe uroda kabla ya ndoa akatumia njia ya kumlewesha na ndipo akafanikiwa kuitoa bikra ya binti kabla ya ndoa.

Dada alilia sana alipozinduka na kujua kikichotokea ila kijana wa marekani akafanikiwa kumtuliza dada kwa maneno matamu matamu na ahadi ya kumpenda mpaka kifo kiwatenganishe.

Dada akafanyiwa shopping kisha jamaa akakwea pipa akarudi state na bibie akarudi mkoani kwao.

Baada ya week kadhaa dada akagundua ana ujauzito wa mumewe mtarajiwa.Wazee wakajua na kijana wa marekani akajulishwa na kuombwa kufanya hima aje aoe mkewe na kuondoka nae kabla wambea hawajajua kuwa ile bikra iliyotunzwa kwa miaka mingi ishatolewa kabla ya ndoa.

Kijana wa marekani akazipokea habari kwa furaha na kuwaahidi wazee kuja ASAP lkn mpaka muda wa mtoto kuzaliwa ukafika ila kijana wa kimarekani hakutokea.

Baada ya miaka kadhaa ikaja kugundulika kuwa kijana wa kimarekani alikua ni muhuni tu aliyekua na fantansy ya kuchakata bikra na eti hata wakati anatoa ile mahari eti alikua tayari keshaoa zake huko marekani na eti wale washenga aliowatuma walikua ni wahuni wenzie tu wazee wa hovyo maana wazazi wake wa kweli walipofuatwa walishangaa maana wao wanajua kijana wao alishaoa siku nyingi tu.

Ikawa asubuhi ikawa jioni dada mrembo aliyeishi kwa maadili akajikuta akichukua kadi yake kwenye chama kubwa la single mazas nchini.

Chama ambacho wanaume wa kitanzania huwaona wanachama wote wa chama hicho ni wanawake wasiofaa sio kuoa tu bali hata kwa mahusiano ya kudumu bali kwa kuwagonga na kukimbia haraka uwezavyo kuokoa maisha yako.

Kabla sikajiunga JF nilikua nawaona single maza ni wanawake kama wanawake wengine.Wako wanaojitambua wako empty sets.Wako wanaojiheshimu wako micharuko.Wako wapole na wanyenyekevu wako vichomi pia.Inshort tabia zote za wanawake single mazas utazipata hata kwa wanawake wasio single mazas.

U single maza sio laana ambayo automatically inamfanya mwanamke awe na tabia za hovyo kama hakua hivyo mwanzo na wala kutokua single maza sio baraka/neema/kinga ya kumfanya mwanamke awe wa maadili/bora.

Mwanamke yeyote single maza or not tabia zake zinatokana na malezi au mtazamo wake katika maisha.

Mimi sio single maza ila as long as mim ni mwanamke kama ilivyokua kwa bibie mtunza bikra hata mim iko siku naweza kuangukia kwa bazaz nikalielewa tukadanganyana danganyana pale at ze end ov ze dei bila kujua imekua kuaje nikajikuta na mim nachukua kadi kwenye chama kubwa la singo mazeriz.

Ikitokea nimekua single maza sitapenda kuongelewa kwa namna single maza wanaongelewa hapa JF.

Hapa JF single maza wanaongelewa kama jamii ya watu wenye laana wanaopaswa kutengwa kama walivyotengwa wale wakoma wa kwenye biblia.

Hapa JF wanaume mnawaongelea singo maza kama viumbe wasio na akili wala maadili lakini naomba niwaambie hawa single maza ni nyie mmewatengeneza na tena ni kundi la wanawake wenye akili kubwa na ndio maana wanaweza kulea na kusomesha watoto wao ambao baadhi yenu mmewakataa na kuona ni bora hela yako ununulie msambwanda wa barmaid kuliko kununua daftari za mwanao.

Sio ajabu yule kijana wa marekani nae yuko hapa JF akiandika nyuzi za kuwaongelea single maza kama walaaniwa kumbe yeye ndio mlaaniwa.

Naombeni wanaume wa JF mtoe hiyo lebel mliyowapachika singo maza sio sawa duniani wala mbinguni sababu hamjui mwanamke amepitia mitihani gani mpaka kuishia kuwa singo maza.

Naomba viongozi wa Jamii forums muliangalie hili.Kuna singo maza anaweza kujiua akifikiria aliyopitia na kulinganisha namma jamii inavyomhukumu.

Sio sawa jamii kusema watu wote wa kundi fulani wana tabia fulani kwani hiyo sio kweli na sio sawa.

Iweje mwanamke aliyeishi maisha yake yote kwa kujitunza na kujiheshimu halafu badae jamii imuone takataka kisa tu analea mtoto/watoto wake bila baba?


NB:wanawake wa JF njooni tuwaeleweshe wanaume wetu kwa heshima na upendo kuwa kunyanyapaa single mothers sio sawa mana kama leo sio single mother kesho unaweza ukajikuta single mother au binti yako akawa single mother.Utapenda anyanyapaliwe?

Hata wewe mwanaume unayenyanyapaa single mothers leo huwezi jua iko siku wanaume wenzio watamdanganya aishie kuwa single mother.Utapenda jamii imnyanyapae?

H
Wewe unaonekana ni muongeaji sana...bila shaka wewe ni single mother mtarajiwa😀
 
.......watu wengi hudhani kwamba singo mama wanachukiwa kwa sababu ya mtoto au kudhani kwamba anachukiwa mtoto la hasha, siku ambayo singo mama wataweza kufuta kabisa hisia Kwa wale waliozaa nao ndo siku ambayo itatangazwa kuwa ndoa bora ni ile ya kuoa singo Maza na sio kuoa msichana kigori........
.........mfano mbaya ambao unahusishwa na most of single mamas ni ile hali ya kuendelea kuwawaza wenza wao waliowazalisha, unamuoa vizuri tu singo mama ila yeye kichwani anawaza kwamba siku baba mtoto akirudi akaomba msamaha atamsamehe(of which is not bad) na kurudiana nae na ww atakuacha, au akijitahidi hatakuacha ila atakuwa anamuwaza lini wakutane wawe wanachepuka.......
........nb: tukubali tu kuwa mtoto ndo strong bond ya wazazi na zaidi ya yote the first love is always the first and stronger, wewe unaeingia badae ni mvamizi tu.........
 
yule single maza ni mpumbavu sana.
Niko poa Mtumishi,
Unabahati mkono wa Bwana ulikuwa juu yako 🤣🤣🤣🤣

Zab 27:2 SUV​

Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka.
 
Umeandika adrenaline ikiwa juu sana mkuu🤣.
Relax.
Pole ila sio wote wako hivyo
sijasema wote wako hivyo ndio maana nikatoa exception kwa wale waliojikuta singo maza bahati mbaya, ila waliobakia sababu kuu ndo hizo. You are so emotional about the matter as if hizo sababu nimetaja kuna uliyo fit in
au ndo tayari...
I smell a singo maza to be
 
Her purity na kujitunza kwake ndo thamani yake sawa nakubali ila vipi akibakwa kama huyo wa kwenye uzi wangu ni sawa jamii kumuongelea kama kahaba asiyefaa?

Lengo la uzi wangu ni kuomba msi generalize maana kuna waliojikuta single maza kwenye mazingira ambayo hata wewe ungekua ni mwanamke ungejikuta tu ushakua singo maza bila kupenda
Oh! Your talking about exceptions. Kwanza fahamu naujue kuwa dunia inaendeshwa kwa generalizations, no gender is favoured there. Kuna mtoto wa kiume kazaliwa yatima nakakua akiwa chokoraa mtaani ila kwabahati nzuri Mungu akafanikiwa kupata mlo angalau wa siku moja, akitafuta mwanamke ataitwa masikini vilevile na atadharauliwa na kuchekwa na jamii hawatojali the background. That's how cruel the world is, no gender is the victim here. Pili jua, jinsia inayoongoza kwa generalization ni mtu mke kwasababu since childhood mwanaume anaonekana ni jinsia yenye tabia mbaya na haribifu kuliko mwanamke, ila have you seen complains my sister. Then just know, that is the world. You can't judge yourself, society judges you.
 
Niko poa Mtumishi,
Unabahati mkono wa Bwana ulikuwa juu yako 🤣🤣🤣🤣

Zab 27:2 SUV​

Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka.
Mkono wa Bwana haujawahi niacha. Huwa nafikiri labda kwa sababu natokea mbari ya Daud😀
 
Uko poa Padre?

hii ilinitokea sana kipindi cha nyuma kila mwanamke anajilengesha tena kwa pigo za kunizalia kwa sababu wanajua nina visenti. 🤔 most girls do this tena kuna mmoja alikuwa nurse yule single maza ni mpumbavu sana.
Unajua tulitoka kuwa marafiki sana wa karibu. Nikienda kwake namnunulia zawadi dada wa kazi na katoto Kake ka kike. Wema wangu ulinisaidia sana. Dada wa kazi alinambia usiku dada anachanganya majani na kuwasha Mishumaa na kutaja jina lako😡😡😡
Kuna vitu vingi hatuwezi sema ila kuna watu wana roho za uharibifu na huwa nazikemea kwa Jina ya Yesu. .
Ushatengenezwa tayari mshaka wa watu😂😂
 
Back
Top Bottom