Sababu ya Single mother kutengwa na wanaume

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Habari zenu wakuu,

Nimekuwa naona nyuzi nyingi sana zikiwasema wanawake waliozaa nje ya ndoa kuwa hawafai na sio wa kuwaoa abadani. Kiukweli hili suala ni nyeti na linahitaji mjadala mkubwa ila mimi nitaongelea sababu zinazofanya wanaume wenzangu wengi wawe wagumu kuoa au kuanzia mahusiano ya kudumu na Single Mothers.

Hizi ni kati ya sababu zinazofanya wanaume wenzangu kuogopa kuingia kwenye Ndoa na single mothers;
1) Ubinafsi
- Kiukwei kila binadamu duniani ni mbinafsi, na ninaweza kusema ubinafsi sio kosa maana ni moja ya njia ya kujipenda kama binadam. Unapoona Mwanaume anakataa kuoa single mother basi tambua kuwa hataki kukubali fedha zake, au mali zake zitumike na uzao wa mtu mwengine.

Ngoja nitoe mfano, Mwanaume akioa Mwanamke kwa tamaduni zetu ni kwamba Mwanaume ndio mtoaji Mkuu wa familia, na niyeye ndio anaeihudumia familia yake kwa kiwango kikubwa (Fedha).

Wanaume wengi tunaogopa fedha zetu kuchukuliwa kisiri na kumjengea Mtoto wa single mother future yake, Wanaume hatutaki hilo suala tunataka mali zetu zitumiwe na uzao wetu tu na sio nje ya hapo.

2) Amani - sisi wanaume tunaoa kwa kuangalia past ya mwanamke na sio vyenginevyo, tukigundua past ilikuwa mbaya basi ni lazima tutoke nduki.

Kuzaa nje ni moja ya dalili kuwa past ya mwanamke ilikuwa mbaya, na tukigundua hilo huwa tunakosa amani (Peace).

USHAURI
DADA ZANGU NAOMBA MJITUNZE MAANA SISI WANAUME TUKITAKA KUOA HUWA TUNAANGALIA MAISHA YA NYUMA YA MWANAMKE NA SIO VYENGINEVYO.
 
Waite single mama waje kwangu, maana mie ndio KIBUZI wao mkuu.

Msiwahukumu saana single mamaz, hawakujitia mimba wenyewe, kuna ambao walizingua wenyewe, kuna ambao sisi wanaume ndio tulizingua..

Point ulizotoa kuna sehemu zinaingia kuna sehemu zinagoma,
Je ni kweli mwanamke kuwa single mama means past yake ilikuwa mbaya, mie nasema hapana, kuna wengine hawana watoto na wana past mbooovu kuliko.
Wapo single mamaz safi tu na wapo viswaswadu pia.
 
Kwani hao single mothers huwa wanajibebesha mimba wenyewe?
Akili za kijinga hizi ndo zinazidi kuwaumiza dada zetu

Mwanaume anakumwagia tu halafu yeye anakaa pembeni wewe ndio unayebeba mzigo mzito mbona mama zenu hawakuwa wajinga hivi

Madhara ya kimwili na kihisia mwanamke ndio unayabeba. Utabeba mimba miezi Tisa, utakongoroka mwili, utapoteza mda mwingi nk

wanawake wa sasa wanataka wazae na mwanaume A ambaye mme wa mtu au 'handsome boy' halafu aje kuolewa na mwanaume B na mtoto wake alelewe na mwanaume B
 
Back
Top Bottom