Kwani mtu hawezi kuwa kazini au shambani au kwenye biashara yake huku akifuatilia yanayoendelea JF???
Mkuu uwe unaangalia ni nani unabishana nae !!, huyo zoba anafikiri watu wote wanaochati hapa JF wako mtaani, akili ya mataga isikusumbue sana, hao ccm ndio inawapenda wanaofikiria matumbo peke yake
 
Kisheria hairuhusiwi kuingia na simu ikiwa imewashwa ndani ya chumba au eneo kesi inapoendeshwa; acheni kuingiza siasa kwenye masuala ya kisheria. Kuchambua ushahidi kwenye mitandao ni kuilekeza mahakama namna ya kufikia uamuzi kitu ambacho ni kosa
Kifungu gani cha sheria kinasema hivyo...?embu kiweke otherwise utakuwa ni umama huo..
 
Polisi: Hakuna kuingia /kuingia na simu mahakamani
Mahakama:Rugemalira wa escrow upo huru
Kibatala:Hatuendelei na kesi hadi watu wote waruhusiwe
Jaji:Kuna kifungu Cha sheria kuhusiana na hili?
Jaji:Watu waingie

Kesi inaendelea
Naona serikali iliamuakufanya umafia kwa mbowe halafu wamuachie Rugemalira na attention iwe kwa Rugemalira
Lakini Bwana Kibatala akaupiga mwingi hadi hio yakwao ya kumuachia Rugemalira itaripotiwa ukurasa wa tatu

Shikamo Peter Kibatala
 
Bora hata mwendazake hakuwahi kuwapakazia wenzie kesi kubwa kama hii..huyu Chief Hangaya nimemchukia ghafla tu ingawa mimi ni ccm..yani unamtesa Mbowe afu unamuachia Ruge?
 
Msajili wa mahakama anaweza kutoa go ahead ila je kwa tanpol watatii huo mhimili unaopaswa kuwa huru?

Mara ngapi tumeshuhudia tanpol wakivunja katiba wazi wazi na hawawajibiki popote??

Statement inaweza kutoka ila bado watu wakapewa zuio kuingia hapo ! Kwani katiba si inaruhusu mikusanyiko ila mara ngapi CHADEMA wanazuiwa kukusanyika ila CCM wanafanya mikutano hata wakiwa wana misafara barabani japo.

Katiba mpya ni inevitable , hakuna aliye juu ya sheria hata Rais anapaswa kuwajibishwa akienda kinyume ila kwa katiba hii hatuwezi so anajiamulia tu atakavyo
 
Part 1.

Jaji Mustapha Siyani, anaingia ndani ya chumba cha mahakama. Saa tatu na dakika hamsini, saa za Afrika ya mashariki.

Mawakili wa Jamhuri wanajitambulisha

1. Robert Kidando snr
2. Nassoro Katuga snr
3. Ignas Mwanuka snr
4. Esther Martin yupo snr
5. Tulumanywa Majigo
6. Abdalah Chavula Snr
7. Jentreva Kitali Snr
8. ...... Sijamsikia

Mawakili wa utetezi wanatambulishwa na wakili Peter Kibatala
JOPO la UTETEZI

1.Jeremiah Mtobesya
2.Jonathan Mndeme
3.Dickson Matata
4.Michael Mwangasa
5.Nashon Nkungu
6.Gaston Garubindi
7.Seleman Matauka
8.Alex Masaba
9.Deogratius Mahinyila
10.Sisti Aloyce
11.Esther Kisanga
12.Maria Mushi

Kibatala anaomba Wakili John Malya kujoin baadae.

Wakili wa serikali anaomba kuendelea kwa upande wa mashahidi. Jaji anauliza kama Kibatala yupo tayari. Jaji anauliza Kibatala angependa washtakiwa wakumbushwe mashtaka yao? Kibatala anasema waendelee tu.. . Wakili wa serikali anaulizwa Je, washtakiwa wakumbushwe mashtaka yao..

Upande wa Jamhuri wanasema washtakiwa wasomewe tena mashtaka yao.

Jaji anauliza kuna ulazima wa kisheria?

Kimyaaaa..

Jaji anasema kuna Kifungu cha Sheria kinalazimisha?

Kimyaaa.

Jaji anasema sawa, acha tu washtakiwa wasomewe tena mashtaka yao...

Jaji anasema Kibatala asome hayo mashtaka , anayo mamlaka wa kumteua yeyote asome hayo mashtaka. Kibatala anaomba kwa Jaji pamaoja na heshima hiyo anaomba asisome yeye mashtaka. Jaji anauliza washtakiwa, je watahuzunika wakili wao akisoma mashtaka? Wote wanaitikia Ndiyooooo!

Jaji anawaambia Jamhuri wasome mashtaka. Jamhuri wanauliza kwa kiswahili au kiingereza? Jaji anasema kwa sababu ya uharaka wasome tu kwa kiingereza kama yalivyoandikwa. Serikali wanasoma upya hati ya mashtaka kabla ya kesi kuendelea. Mashtaka yote sita yamesomwa kwa sauti.

Shtaka la 1

Mshtakiwa wa 1, si Kweli
Mshtakiwa wa 2, si Kweli
Mshtakiwa wa 3, si Kweli
Mshtakiwa wa 4, si Kweli.

INA ENDELEA PART 2.
 
KESI YA FREEMAN MBOWE MAHAKAMANI.

Part2.

Mawakili wa upande wa Jamhuri wanauliza tena shtaka la 3, linamuhusu mshtakiwa wa 4 (Freeman Mbowe) pekee yake.

Mshtakiwa wa 4 anasema si, kweli...

Shtaka la 4

Mshtakiwa wa 1, si kweli
Mshtakiwa wa 2, si Kweli
Mshtakiwa wa 3, si Kweli
Mshtakiwa wa 4, si Kweli

Shtaka la 5 linamuhusu mshtakiwa wa 2 pekee.
Mshitakiwa wa 2 anaulizwa na kusema Si kweli.

Shtaka la 6
Mshtakiwa wa 1, pekee yake, anaulizwa nae anasema, Si Kweli.

Mashtaka yote 6 yamesomwa

Jaji anauliza kuna lolote au tuanze kuita mashahidi?

Wakili serikali anasema twende kuita mashahidi

Wakili serikali anatoka kumuita shahidi

Jaji anasema shahidi wa 1 Upande wa Jamhuri aitwe apande kizimbani

Sasa shahidi kapanda kizimbani tayari.

Shahidi anasema anaitwa ACP Ramadhani Kingai.

Jaji anauliza huyu ni shahidi namba ngapi?

Wakili wa Serikali anasema, namba 2.

Dini yake.?

Shaidi anasema Muislam.

Jaji anasema thibitisha.

Shahidi Wallah,billah,Subillah nathibitisha ushahidi nitakaotoa utakuwa ni wa Kweli.

Jaji anauliza, utetezi mpo tayari?

Wakili wa serikali anasema nitakuuliza maswali na utaenda kwa utaratibu sababu Jaji ataandika

Wakili wa Serikali umejitambulisha ACP Ramadhani Kingai Unafanya Kazi gani?

Shahidi ni Afisa wa Polisi

Wakili wa Serikali upo kituo gani cha Kazi?

Jaji anauliza, tunamskia wote Shahidi?

Wakili Kibatala anasema aongeze sauti

Wakili wa serikali anamuuliza shahidi, unaweza kusema ukiwa kamanda wa polisi majukumu yako ni nini?

Shahidi anasema nikiwa RPC wa Kinondoni Jukumu langu kulinda watu na mali zao 2. Kuzuia uhalifu

Wakili wa serikali; una amuda gani tangu uwe kamanda wa polisi Kinondoni?

Shahidi; miezi 10 tangu nihamie kutoka Arusha

Jaji; Arusha ulikuwa RPC?

Shahidi; Hapana, Arusha nilikuwa RCO

Wakili wa serikali; ulikuwa RCO muda gani?

Shahidi; tangu 2018 hadi November 2020.

Wakili wa Serikali; Elezea Dennis Urio unamfahamu?

Shaidi; Ni Luteni wa JWTZ

INAENDELEA PART 3.
 
MWENENDO MZIMA WA KESI YA MH. FREEMAN MBOWE MAHAKAMANI LEO.
PART3.

Wakili wa Serikali; Elezea Dennis Urio unamfahamu?

Shaidi; Ni Luteni wa JWTZ

Wakili wa Serikali; Ulimfahamu lini?

Shahidi; 2020 nikiwa Oysterbay kikazi nilipigiwa simu na Afande aliyekuwa kamishina wa upepelezi wa makosa ya Jinai, aliyekuwa kamishina wa polisi Robert Boazi

Alinipigia simu akitaka niende ofisini kwamba niende kuna maelekezo ya kazi

Nilipoenda ofisini kwake ndipo nilipomkuta Luteni Dennis Urio

Wakili wa Serikali; Ofisi ipo wapi?

Shahidi; Ofisi ipo Mtaa wa Ohio hapa Dar es salaam

Wakili wa Serikali Elezea Baada ya Kufika.

Shahidi baada ya kufika kwa Afande Boazi, aliniambia kuwa Dennis alikuwa na taarifa ya Kihalifu

Alimuomba Dennis Urio ambaye ni Luteni wa JWTZ aanze kutuelezea kwa pamoja mimi na DCI

alitueleza kuwa kuna kundi la kihalifu ambalo linaandaliwa na Freeman Mbowe

Shahidi; Kundi hilo lilikuwa na lengo la kudhuru viongozi wa serikali

Kundi hilo pia lilikuwa limejipanga kufanya vitendo vya kuchoma vituo vya mafuta kwa kuvlipua na masoko yenye watu wengi

Lakini pia kukata miti katika barabara kubwa kuzuia magari yasipite.

Shahidi; Lengo lilikuwa kuonyesha Nchi haitawaliki kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu

Wakili wa Serikali; elezea Dennis Urio aliwaeleza taarifa hizi alipata wapi.

Shahidi; alieleza kaambiwa na Freeman Mbowe

Mbowe alikuwa anamueleza kwa vyovyote vile lazima tuchukue mamlaka ya nchi

Shahidi; Freeman Mbowe akamueleza Denis kwa kuwa yeye ni homeboy wake, angempa mamlaka makubwa pale ambapo angekuwa amepata mamlaka ya nchi

Wakili wa Serikali; elezea ni kwa nini Mbowe alimueleza Luteni Dennis na siyo mtu mwingine

Shahidi; Dennis alieleza Mbowe amemuomba amtafutie watu wa kutekeleza mambo hayo, wawe Makomandoo wastaafu au waliofukuzwa kazi

Wakili wa serikali; Makomandoo kutoka wapi?

Shahidi; Makomandoo kutoka Tanzania

Wakili wa Serikali; wawe Wstaafu kutoka wapi?

Shahidi; kutoka JWTZ

Shahidi; Vitendo hivi vilikuwa vimepangwa kufanyika MOSHI, Arusha Mbeya, DSM na Mwanza

Lakini vitendo vya kukata miti na kuzia magari yasipite ilikuwa imekusudiwa barabara ya Morogoro kuelekea Iringa

Wakili wa Serikali; baada ya kupewa taarifa hiyo kiliendelea kitu gani?

Shahidi;Afande Boazi alimshauri Dennis Urio, aendelee kutoa ushirikiano na kushirki vitendo hivyo lakini aendelee kuripoti vitendo hivyo polisi

Jaji; Kama nimekuelewa Luteni Dennis alipaswa kuripoti kwako?

Shahidi; Ndiyo

Shahidi; nilichukua namba ya Ltn Dennis Urio 0787555200.

Shahidi; mimi nilimalizia kazi yangu ilikuwa imenileta DSM, nikarudi kazini kwangu, Arusha.

Wakili wa Serikali; Baada ya Kurudi Arusha, ulifanya nini?

Shahidi; samahani, wakati naelekea Arusha Afande Boazi alinielekeza nifungue Jalada la Uchunguzi, kuhusu njama hizo..

Shahidi; na mimi nikamuelekeza Askari anayeitwa Swila afungue Jalada hilo, na kufuatilia kilichokuwa kinaendelea

Wakili wa Serikali; ulimulekeza Swila afungue uchunguzi kuhusu suala gani?

Shahidi; Uchunguzi ulikuwa upelelezi mipango iliyokuwa inataka kufanyika

JAJI; huyu Swila ni nani?

Shahidi; Swila ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi

Shahidi; baada ya hapo nilikuwa naendelea kuwasiliana na Ltn Dennis Urio na kwamba ameshatumiwa nauli na katika kipindi i hicho walikuwa wameshapatikana vijana wawili

Wakili wa Serikali; Elezea kama hao vijana wawili walikuwa na sifa hizo alizoelekezwa

Wakili Kibatala anasimama, anasema "Objection your honor, Wakili anamfundisha shahidi cha kusema

JAJI; Rudia swali vizuri au jibu Objection

Wakili wa Serikali anarudia swali vizuri

SHAHIDI; Luteni Dennis alinieleza Mbowe amefamfanya Khalfan Bwire kuwa mlinzi wake, huyu alikuwa komandoo alifukuzwa kazi kutokana wizi wa mafuta wa Standard Gauge. Moses Lijemje alifukuzwa Ukomandoo kwa makosa ya Kinidhamu. Baadae nilimuelekeza Swila afungie jalada la KIJANAI

INAENDELEA PART 4.
 
MWENDELEZO MZIMA WA KESI YA MH. FREEMAN MBOWE MAHAKAMANI LEO.
PART 4.

SHAHIDI; ikafunguliwa kesi ya kula njama ya kutekeleza Matendo ya kigaidi.

Wakili wa Serikali; ilifunguliwa wapi?

Shahidi; Police Central Dar es salaam. °

JAJI; ulifungua kesi gani?

SHAHIDI; Kula njama ya kutenda vitendo vya kigaidi.

Wakili wa Serikali; ACP kingai, unasema ulimueleleza Inspector Swila kufungua jalada la kesi ya kula njama ya kutekeleza matendo ya Kigaidi, kwanini?

Shahidi; nature ya makosa yenyewe, yangeweza kufanywa yangeweza kuleta madhara kwa watanzania haswa katika kipindi tulichokuwepo.

Wakili wa Serikali; baadae nini kilifuata?

Shahidi; tarehe 04.8.2020 nilienda kukutana na Ltn Denis Urio, aliniambia kwamba alishapata tena vijana wawili na amewaunganisha na Freeman Mbowe

Akanitajia vijana hao ni Adam Kasekwa maarufu Adamoo na Mohammed A. Ng'wenya.

JAJI; Endelea

Wakili wa Serikali; baada ya taarifa nini kiliendelea?

Shahidi; alinieleza tayari vijana wamefika Moshi

JAJI; elezacni vijana wapi, wote wanne au wawili wa mwisho

Shahidi; ahsante Mheshimiwa, aliniambia vijana 3 kati ya hao wa 4

Waikili serikali; tarehe ngapi?

Shahidi; tarehe 04.8.2020

Wakili wa Serikali; akina nani hao Luteni Dennis Urio aliokueleza wamefika tayari Moshi?

Shahidi; ni Mohammed A. Lingwenya, Adam Kasekwa na Moses Lijenge

Wakili wa Serikali; Eleza walikuwa wamefikia kwa madhumuni gani?

Shahidi; Watu hao walikuwa wamefikia wilaya ya Moshi, na walikuwa wamekusudia kumdhuru Lengai Ole Sabaya, ambaye kwa kipindi kile alikuwa Mkuu wa wilaya ya Hai

Wakili wa Serikali; Baada ya kupokea taarifa hiyo ulichukua hatua gani?

Shahidi; Niliwasiliana na DCI nikamfahamisha na baada ya kumfahamisha alielekeza niunde timu itakayofanya ufuatiliaji na hatimaye kuwakamata watu hao. Kabla awajafanya Madhara yoyote kwa wahusika

Nilimtafuta ASP wa Polisi ambaye sasa ni mkuu wa upelelezi Arumeru, Jumanne.

Shahidi; Mwingine Inspector Mahita, Detective koplo Francis, Detective Constable Goodluck na Dereva wangu Constable Azizi. Tulianza Kuweka amiundo Mbinu ya kuwakamata watuhumiwa kabla hawajafanya madhara yoyote.

Wakili wa serikali; Elezea Ulifanya nini baada ya Ufuatiliaji

Shahidi; Siku ya Jumanne nilieleka Moshi, ambapo hao watuhumiwa walikuwa, na kwamba Jioni ile tulianza ufuatiliaji wa hao watuhumiwa kwa ajili ya kuwakamata. Baada ya mawasiliano na wasoro wetu tulihairisha zoezi na usiku ule tukawa tumelala Moshi.

Shahidi; Asubuhi 05.8.2020 tuliamka na kuweka miundombinu na wasiri wetu kwa ajili ya ya ufuatiliaji. Tulipata taarifa kuwa watuhumiwa wapo maeneo ya RAO, Moshi

Wakili wa Serikali; baada ya kupata taarifa hiyo ulichukua hatua gani?

Shahidi; tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 2, Adam kasekwa na Mohammed Ling'wenya. Wakati tumewakamata, tumewaweka chini ya ulinzi nilimuelekeza ACP Jumanne awapekue maungoni. Adama kasekwa alivyopekuliwa alipatikana akiwa na Pisto 1 aina ya Ruvern iliyokuwa na namba 53A 5340

Shahidi; Pia alikutwa na risasi 3. Alikuwa na kete 58 za Heroine, madawa ya kulevya. Mohammed Kingwenya alikuwa na Kete 25 za Madawa ya Kulevya.

Wakili wa Serikali; Eleza upekuzi huu ulifanyika mbele ya nani?

Shahidi; ulifanyika palepale mbele ya mashahidi.

Shahidi; Mmoja namkumbuka anaitwa Anita na mwingine anaitwa Esther. Baada ya kujaza hati ya kuchukua vitu, tuliwachukua watuhumiwa na wale mashahidi hadi kituo cha Polisi mjini kati, eneo la RAU lilikuwa siyo Rafiki kwa kuandika Maelezo yao Pale, ilikuwa la Fujofujo.

JAJI; Spelling za hilo eneo,

Shahidi; Ni RAO

JAJI; Mwanzo tulikuwa tunasikia ni RAU. Kwa hiyo ni RAU au RAO?

Shahidi; ni RAO, Madukani.

Baada ya Kufika ofisi ya mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro nilimuachia Jumanne aendelee kufanya Mahojiano

INAENDELEA PART 5.
 
MWENENDO MZIMA WA KESI YA MH. FREEMAN MBOWE MAHAKAMANI LEO.
PART 5.

Shahidi; Wakati huo tukawa tunaendelea na watuhumiwa kumtafuta Moses Lijenje hatukuwa tumemkamata na wenzake

Wakili wa Serikali; Elezea ufuatiliaji wa Moses Lijenje ulifanyikaje

Shahidi; Wakati Mchana, tulitoka na watuhumiwa na Moses lakini zoezi lile lilituchukua mpaka usiku

Shahidi; Tulipofika usiku tuliamua kupumzika na kulala tena, na kuendelea kesho yake 06.8.2020.

Wakili wa Serikali; 05/8 milipokuwa mmekamata Adam na Lingwenya ni nani aliyekuwa anawaelekeza kumleta Moses

Shahidi; ni watuhumiwa wenyewe

Wakili wa Serikali; Meneo gani mlipita?

Shahidi; Boma Ng'ombe, Machame na Arusha

Wakili wa Serikali; elezea ikawaje

Shahidi; Mpaka September 2020 tulikuwa hatujafanikiwa kumpata Moses Lijenje

Wakili wa Serikali; ufuatiliaji wa 06/8 ikawaje,

Shahidi; tulishindwa Kumpata baada ya ufuatiliaji na kupita maeneo mengi

Wakili wa Serikali; naomba kukurudisha nyuma. Siku 05/8 watuhumiwa uliwapeleka wapi?

Shahidi; Central Station Moshi

Wakili wa Serikali; Saa ngapi?

Shahidi; Sikumbuki...zaidi ya saa 4:30

Wakili wa Serikali; maeneo mliyomtafuta Moses Lijenje Moshi Boma Ng'ombe ni Maeneo gani?

Shahidi; Maeneo waliyokuwa wanamtafuta Lengai Ole Sabaya

Wakili Mtobesya anasimama na kusema "Objection naona kama Wakili anaongea mambo ambayo bado shahidi hajaongea"

Jaji anaomba serikali wamjibu Wakili Mtobesya

Wakili wa Serikali anasema, nimemuuliza Shahidi ACP kingai, umemfuatilia Moses Moshi, Boma Ng'ombe na Machame, Maeneo gani haswa?

Jaji anamuuliza Wakili Mtobesya kuna tatizo na hilo swali?

Mtobesya anasema nimefanya Objection kwenye Line wakili wa serikali aliyokuwa anaelekea

JAJI; Shahidi amevuka mipaka kwa shahidi anayoelekeza kuhusu fact, Ukisoma section 6 ya Evidence Act

Jaji anauliza je, kuna msingi ya kuendelea na Objection?

Wakili Mtobesya; tunaondoa Objection baada ya ushauri na wenzangu

JAJI; taja maeneo shahidi

Shahidi: ni Moshi Mjini.

Jaji; hayo tumeshayasikia

Shahidi; maeneo mengine ni yale waliyokuwa wamefikia wakati wanatoka Dar es salaam na maeneno mengine waliyokuwa wanamfuatilia Ole sabaya

JAJI; Wakili wa Serikali, hayo yanatusaidia nini?

Wakili wa Serikali; Unasema ulienda Machame, ulienda eneo gani?

Shahidi; Kuna Hotel inaitwa AISHI ambayo ni mali ya Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali; na Boma Ng'ombe?

Shahidi; ni Hapo hapo Boma Ng'ombe

Wakili wa Serikali; nitaenda kwenye swali lingine Baada ya Tarehe 06 baada ya kurudisha
 
Kisheria hairuhusiwi kuingia na simu ikiwa imewashwa ndani ya chumba au eneo kesi inapoendeshwa; acheni kuingiza siasa kwenye masuala ya kisheria. Kuchambua ushahidi kwenye mitandao ni kuilekeza mahakama namna ya kufikia uamuzi kitu ambacho ni kosa
Taja hicho kifungu cha sheria kinachokataza watu kuingia mahakamani na simu zikiwa zimewashwa acha kubwanbwaja ujinga
 
MWENENDO MZIMA WA KESI YA MH. FREEMAN MBOWE MAHAKAMANI LEO.
PART6.

Wakili wa Serikali; elezea ni taratibu gani ambazo ulizitumia

Shahidi; kwanza nilimfahamisha mtuhumiwa haki zake. Haki hizo ni pamoja na mimi kujitambulisha kwake, Lakini pia kumueleza Kosa lake. Nilimuonya halazimishwi kusema lolote.

Shahidi; Nilimueleza anaweza kuwepo Ndugu, Jamaa na Rafiki au Mwanasheria wakati wa kutoa maelezo yake. Alinijibu kuwa yupo radhi kuandika maelezo pekee yake. Haya yote alikuwa anayaongea nikiwa naandika, na Mwisho akawa tayari kusaini maelezo yake akiwa mbele yangu.

Wakili wa Serikali; ulisema ulimfahamisha kosa lake na Sheria?

Shahidi; Kosa la kula njama na kutenda vitendo vya ugaidi

Wakili wa Serikali; baada ya kumuonya na kuandika maelezo ulifanya nini?

Shahidi; niliyafunga

Wakili wa Serikali; Unasema kasaini, kwa namna gani?

Shahidi; kwa saini ya kalamu na dole gumba

JAJI; aina gani ya kalamu?

Shahidi; kalamu kwa maana ya peni

Wakili wa Serikali; Baada sasa kumaliza kuandika maelezo yake, ulifanya nini?

Shahidi; Nilitengeneza jalada la kesi

Wakili wa Serikali; unayatambuaje Maelezo yako?

Shahidi; nayatambua kwa mwandiko wangu, sahihi ya Adam na sahihi yangu

Wakili wa Serikali; Mheshimiwa Jaji naomba kumkabidhi karatasi hii aione

Shahidi; natambua haya ni maelezo niliyoandika kwa mwandiko wangu, na sahihi yangu au Mtuhumiwa

Wakili wa Serikali; Ungependa statement itumike mahakamani kama ushahidi?

Shahidi; ndiyo itumike kama sehemu ya Ushahidi

Mawakili wa Utetezi wamepewa kupitia Hati ya Maelezo aliyoyatoa Shahidi ACP kingai

Mawakili wa Utetezi wamesimama Kuielezea Hati ya Maelezo iliyotolewa

Kibatala anasema hati ya maeelezo ina matatizo

1.Maelezo yamechukuliwa nje ya muda wa kisheria. yamechukuliwa zaidi ya saa 48 tangu mshtakiwa atiwe kizuizini

Huko RAU, Moshi n kifungu husika kimeweka masharti ya lazima, yamechukuliwa nje ya muda hawezi kupokelewa mahakamani

2. Kabla na wakati maelezo ya mtuhumiwa yanachukuliwa, kwa Mshtakiwa Adam Kasekwa aliteswa (Tortured) na zoezi hilo la kumtesa lilisimamiwa na shahidi namba 1 ACP kingai na maafisa wengine wa polisi

Anaendela kueleza Wakili Peter Kibatala..

INAENDELEA....
 
MWENENDO MZIMA WA KESI YA MH. FREEMAN MBOWE MAHAKAMANI LEO.
PART 7.

Wakili Peter Kibatala anaendelea..

Sehemu ya kwanza ya pingamizi letu kuhusu ushahidi wetu ni kuhusu jambo la sheria na sehemu ya pili ni namna ushahidi ulivyopatikana

Naiomba mahakama ifanye kesi Ndogo katika kesi Kubwa..

Wakili Kibatala anaendelea

Jaji kwa maana hiyo tutoe hukumu sehemu ya 1 Au tufanye hukumu kwa zote mbili?

Kibatala; tutoe hukumu sehemu ya 1 kisha tufanye kesi ndani ya kesi

JAJI; unafikiri inawezekana utaratibu zote na uchukuaji wa ushahidi unaweza kuwa sehemu ya kesi ndogo?

Wakili Kibatala; ndiyo inawezekana kwa sababu sisi tunataka tuzingatie kifungu 169 CPA

Wakili Mtobesya; ukisoma kifungu cha 151 kinaruhusu kuondoa muda pale mtuhumiwa anakuwa anaendelea na upelelezi, lakini kwa ushahidi wa shahidi wa 1 waliwakamata tarehe 05 na waliwaweka lockup

Maelezo labda kama pangelikuwa na ushahidi Mbele yako unaonyesha pana sababu iliyosababisha wasichukue maelezo

Ukisoma hukumu mbalimbalimbali za Mahakama Kuu, zinaeleza kuwa labda kama palikuwa na mazingira yaliyopeleka msichukue maelezo wakati wanafanya Maelezo

Tarehe 06 walikuwa nao wote na akasafiri kuja DSM na wakafika tarehe 07 Alfajiri

Mheshimiwa Jaji Kuna muda hapa haujaelezewa, Ukisoma ushahidi wa Shahidi wa kwanza anasema hawa watu walihifadhiwa majira ya saa 4 Usiku, Ukiangalia sioni sababu kuna nini kiliwazuia wasichukue

JAJI: je unaona unahitaji kesi ndogo Nlndani ya kesi hii kama Wakili Kibatala alivyosema kwa Kifungu cha 169 cha CPA?

Wakili Mtobesya: Vifungu vya ushahidi vinamtaka shahidi yeye ndiyo aeleze, tukienda upande wa pili wa kesi ndogo inampa shahidi kuelewa ambayo hajayaleza,

Jaji; Je, Mshtakiwa wa pili alitoa hayo maelezo au hajayatoa? Je, washtakiwa walitoa maelezo au hawajatoa iwe kwa mateso au lah?

Wakili Mtobesya; Maelezo yaliyochukuliwa kinyume na Sheria hayawezi kuwa maelezo halal

Wakili Mtobesya; Mheshimiwa Jaji baada ya kujiridhisha kama walifuatisha vifungu vya sheria ndiyo twende Kwenye kesi ndani ya kesi ya msingi.

Wakili wa Serikali wanasimama na kusema tumesikia mapingamizi yote...

Kwa maoni yetu, Mapingamizi hayo yaliyowasilishwa na Upande wa Utetezi, yanaweza kuteuliwa baada ya mahakama hii kufanya kesi ndogo ndani ya kesi..

Ni baada ya Wakili Kibatala sehemu ya Pili Kulalamikia ukiukwaji wa taratibu za kisheria wakati wa kuchukua maelezo

Jambo lingine hata wakati Wakili Mtobesya alikuwa anaelezea anashindwa kujitenganisha na ushahidi.

Wakili wa pili wa serikali; Mheshimiwa jaji ni msimamo wetu kuwa mapingamizi haya yasikilizwe kupitia kesi ndogo, Baada ya ushahidi kuwa umepokelewa mahakama ituruhusu kuwasilisha

Na hata sehemu ya Kwanza ya maelezo ya kwanza ya wakili Kibatala pia ina uhusiano na kesi kubwa

Sasa sisi tunaona pingamizi la kwanza lina uhusiano na Pingamizi la Pili, Mahakama ijielekeze kwenye kesi ndogo katika Kesi ya msingi

Kibatala alisema shahidi na maafisa wengine wa polisi waliwatesa washtakiwa, atusaidie kuwataja pasipo kutuacha, je ni akina nani?

Wakili Kibatala; tunaomba tupate ruhusa ya mahakama twende kwenye kesi ndogo katika kesi ya Msingi (Trial within a trial)

Ukimya unatawala kidogo

Tunasubiri Maamuzi ya Jaji juu ya mapingamizi 2 ya kupokelewa ushahidi wa ACP kingai ambao Umewekewa mapingamizi mawili na upande wa mawakili wa utetezi

1. Maelezo ya watuhumiwa kuchukuliwa nje ya muda.

2.Maelezo ya watuhumiwa kutolewa kwa mateso kwa watuhumiwa.

Lakini kwa Pingamizi la pili linataka mahakama ihairishe kusikiliza kesi ya msingi, tusikilize Kwanza kesi kuhusu pingamizi la pili kuhusiana na watuhumiwa kama waliteswa au sivyo..

BAADA YA DAKIKA 10

Jaji anasema kama ambavyo mawakili wasomi wamebainisha kuhusu maelezo yanayosadikiwa kuwa ni maelezo ya Onyo, Kimsingi pingamizi la kwanza lilikuwa linaweza kutatuliwa bila kuwa na kesi ndogo katika kesi ya Msingi.

Jaji anasema, nakubaliana na mawakili wasomi kusimamisha kesi kuu ya msingi kwanza na kuanza kusikiliza kesi ndogo, hivyo, nahairisha kesi hii ya msingi hadi saa nane mchana, tuanze kesi kusikiliza kesi ndogo..

Kesi imehairishwa hadi sasa nane mchana. Jaji ameondoka mahakamani

TUKUTANE SAA NANE......
 
Back
Top Bottom