OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
36,105
2,000
Freeman Mbowe na wenzake wameletwa tayari. Lakini ulinzi mkali umeimarishwa. Askari wengi. Pia kuna zuio la watu kuingia ndani ya mahakama. Wanasema ni mawakili 20 tu, wanahabari 10 (leo wameruhusiwa), ndugu 5, Viongozi 5, lakini simu marufuku.

Askari magereza wanalalamika kwamba jana tumefanya ujinga sana. Ujinga gani, tunawaukliza, wanasema tulikuwa tunatuma habari nje. Wanamueleza Benson Kigaila, NKM CHADEMA. Tumewaeleza kwamba, anayetakiwa kulalamika ni Jaji sio wao. Mahakama siyo gereza. Wajishikilie vizuri.

Mahakama imechelewa kwa dakika 40, yote hii ni kutokana na Jamhuri kutaka kuhodhi mamlaka ya mahakama, bila kujua kwamba wote hapa tuna interest na kesi hii, wao ni walalamikaji, sisi ni watuhumiwa. Kwanini watuzuie kuingia mahakamani na simu?

Watoto wote wa Freeman Mbowe, (Nicole na Dudley) pia wapo nje ya mahakama, pamoja na ndugu zao wengine.

Kama kawaida yao, makarao waliovalia kiraia, wamekaa kwenye siti karibu zote za mahakama, wamechukua nafasi kama kesi ni yao pekee yao.

Mambo ya ajabu yanafanyika

Lakini kitu cha muhimu hadi sasa ndugu zangu ni kwamba, kwa umoja wetu wote tupo nje ya mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa, Ubungo-Mawasiliano, tumeshawaelekeza MAWAKILI wetu wasomi kwamba "No ENTRANCE NO CASE"... And it's done, hii ni open court!

Updates
Jana Jaji Mustapha Siyani alisema watuhumiwa waletwe mapema, saa 3 asubuhi kesi ianze, lakini mpaka saa 5 na Dakika 24 sasa kesi haijaanza kwa sababu ya polisi kuzuia watu. Mawakili wetu walikwenda kumuona Jaji, wanatupa taarifa kwamba Jaji amekana kuzuia Jambo hilo mahakamani.

Updates
Wakili Msomi Kibatala ameandika Jaji ameruhusu watu waachwe huru

Mahakama Kuu ilipo kesi ya Ugaidi ya Mbowe, baada ya Polisi kuzuia watu kuingia Mahakamani na kuzuia simu, Jaji ameamuru kuwa na Polisi watoke na wasiwe na simu, Mawakili wa Mbowe wote wametoka Nje kwani hii ni kesi yenye maslahi ya UMMA! Mawakili wapo Nje na UMMA

E_ZWYEwXMAg2hVX.jpg
JOPO la mawakili wa Freeman Mbowe na wenzake wote wametoka nje ya chumba cha mahakama muda huu, kupinga watu kuzuiwa kuingia mahakamani, na viongozi wa CHADEMA kuingia bila simu... Saa sita na dakika sita Mchana, saa za Afrika ya mashariki, Kesi imeshindwa kuendelea..

Kesi ya ugaidi inayomkabili Mhe Mbowe na wenzake3, imeshindwa kuendelea katika Mahakama kuu baada ya Polisi kufanya fujo na hivyo watuhumiwa wamerudishwa mahabusu muda huu
Freeman Mbowe na wenzake watatu wakitolewa nje ya chumba cha mahakama ikiwa ni zaidi ya saa moja tangu kesi hiyo ilipopangwa kusikilizwa.

Kesi imesitishwa na Washitakiwa wamepelekwa Mahabusu ndogo kusubiri Uwamzi wa Jaji. Kesi zinazofanyika Open Court, watu wanaruhusiwa kuingia. Lakini hii kesi Watu wamekatazwa kuingia na wachache waliongia hawakuruhusiwa kuingia na simu.


UPDATE: Kesi inaendelea baada ya pande zote kukutana

Baada ya kuzuiwa kwa Wananchi kuingia Mahakamani kusikiliza kesi ya Mhe. Mbowe na wenzake na kupelekea Mawakili upande wa tetezi kutoka nje ya ukumbi wa mahakama, hatimae Jaji ameamuru wananchi kuingia mahakamani baada ya majadiliano ya faragha kati ya pande zote mbili.

Upande wa Jamhuri wameshindwa kuileza Mahakama kifungu cha sheria kinachokataza wananchi kuingia na simu na kutoa taarifa juu ya kinaendelea katika kesi Na. 16/2021, Jaji akasema hakuna sheria wala kanuni inayokataza watu kuingia na simu mahakamani.

Kesi inaendelea.

Jaji anaingia.
Kesi inatajwa.
Watuhumiwa wanapandishwa kizimbani.
Upande wa Mawakili wa serikali wapo nane
Upande wa utetezi wakili Peter Kibalata anatambulisha Jopo lake la mawakili wa utetezi

Mawakili wa utetezi ni;
1. Jonathan Mndeme
2. Jeremiah Mtobesya
3. Gaston Garubindi
4. Alex Massaba
5. Michael Mwangasa
6. Maria Mushi
7. Evarista Kasanga
8. Khadija Aaron
9. Nashon Nkuungu
10. Bonifasia Mapunda
11. Boniface Mwabukusi
12. Peter Kibatala

Wakili wa Serikali: Kesi imekuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa

Jaji; Shahidi aliyebakiza sehemu ya ushahidi wake aje amalizie

Wakili wa serikali; Jana uliulizwa kuhusu noteBook kama nyenzo ambayo imetajwa kwenye PGO, ulipoulizwa kama umeileta ulisema hujaileta, kwanini?

Shahidi: Note Book niliyoulizwa ilikuwa ni nyezo maalum kwa matumizi ya polisi tu.

Wakili Kibatala; OBJECTION... huko anakujibu Shahidi kuhusu matumizi note Book PGO anajadili kitu ambacho jana mimi sikumuuliza yeye.

Wakili wa Serikali: Mimi nashangaa kama ama Object kuhusu majibu ya shahidi sababu ninachojua objection ingekuwa kwenye swali

Wakili Kibatala; hii notion ya kwamba Objection unatoa kwenye maswali tu sijui wakili anaitoa wapi, OBJECTION inaweza kuwa kotekote kwa swali na majibu.

Jaji: Jana mlimuuliza nini shahidi?

Kibatala: Naomba nipitie kidogo

Jaji: Sawa endelea ukiwa tayari niambie

Shahidi: Anayoosha mkono

Jaji: Shahidi unataka kufanya nini kuendelea kutoa ushahidi wakati tunasubiria?

Shahidi: Nataka kumsaidia mheshimiwa

Jaji; Hiyo siyo kazi yako

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji kama inawezekana nirahisishe mimi siendi mbali sana

Jaji: Hapana muache wakili ajiridhishe

Jaji: Wakati wakili Kibatala anaendelea ngoja niwaulize Mawakili wengine, Je, kuna kifungu cha sheria kinachovuka mipaka nini shahidi anaweza kujibu?

Wakili Mtobesya anasimama anasema sheria ya ushahidi inasema kwamba wakati shahidi anaongozwa baada ya maswali ya kudodoswa anatakiwa asitoke nje ya yale maswali ya dodoso, na kama mahakama itamruhusu basi mahakama itamruhusu mtoa dodoso arududie tena cross examination

Jaji: Sasa kuna tatizo kama mtaomba mbeleni?

Wakili Kibatala: Amemaliza kupata kifungu cha PGO 236 (3)9 anakisoma kuwa "Afisa wa polisi ambaye yupo kazini ambaye yupo mbali na kituo chake cha kazi anapomkamata mtuhumiwa anatakiwa kumtaarifu sababu za kumkamata Mtuhumiwa huyo, na kumuandika maelezo ya onyo katika notebook sehemu ya 10 inasema Afisa huyo wa Polisi atatakiwa kurekodi Jibu la mtuhumiwa huyo katika Notebook na atatikwa kutumia Notebook hiyo mahakamani

Jaji: Haya wakili wa serikali bado baada ya maelezo unataka kuendelea na swali lako?

Wakili wa Serikali: basi naomba nisiulize tena kuhusiana na PGO naliondoa swali langu tafadhali

Wakili wa Serikali: Kingai Jana uliulizwa kuhusiana na Notebook uliyotakiwa kuleta mahakamani na ukasema hujaileta, kwanini?

Shahidi: siyo lazima kuileta mahakamani

Wakili wa Serikali: Elezea sababu ya kutokuleta mahakamani

Shahidi: ile ni facility ya polisi ya kufanya kazi, kuna vitu anaandika ni siri ya police anaweza kusoma kujikumbusha. laikini siyo lazima kuileta Mahakamani

Wakili wa Serikali: Jana uliulizwa kuhusu facility zilizokwepo wakati unamchukua maelezo mtuhumiwa wa pili, Je ulikuwa unamaanisha facilities gani?

Shahidi: kama vile viti, meza na karatasi

Wakili wa Serikali: Elezea za kwanini hukutumia

Shahidi: Nilieleza kuwa palikuwa na upelelezi unaendelea na mazingira ya kutofanya kazi ile Moshi

Wakili wa Serikali: Jana uliulizwa kuhusu Afya ya Mtuhumiwa wa pili kuhusu tatizo lake la Afya, Kwanini hukumpeleka hospitali kulijua zaidi?

Shahidi: Mtuhumiwa alinieleza alikuwa na tatizo la Afya lakini wakati namuhoji alikuwa amepona na alirejea nyumbani kwake chalinze na kufungia banda la chipsi la Biashara alipotoka kupona

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu kumkuta na silaha ukasema hukumuonya, Sasa kwanini hukuonya kwa kesi ya kukutwa na silaha?

Shahidi: Niliamini kwa sababu nimemuonya kwa Kesi kubwa ya kula njama za kutenda matendo ya kigaidi hayo mengine yangeingia ndani

Wakili wa Serikali: uliulizwa hapa kuhusiana na yule askari anayeitwa Goodluck kuhusu kufika kituo cha Polisi Mbweni, elezea alifika kwa kazi gani?

Shahidi: Kwa ajili ya kazi za kiupelelezi wakili wa Serikali: pia uliiulizwa kuhusiana na Detention Register na hukuleta hapa Mahakamani, Elezea kwanini hukuleta Detention Register

Shahidi: Mheshimiwa jaji mimi siyo custodian wa Detention kama Dention Register itahitajika basi custodian watakuja kutoa ushahidi

Wakili wa Serikali: uliukizwa kuhusu kuwatumia Adam na Mohammed kuhusu kumtafuta Moses Lijenje na kama wasingekwepo Ungetumia Njia zingine, ieleze Mahakama ni njia gani ungetumia? Shahidi: tunatumia taarifa za wasiri wetu, katika hili tuliwatumia wote, na hata hivyo hatukumpata

Wakili wa Serikali: Ni hayo Mheshimiwa Jaji JAJI: kuna lolote kwa upande wa Utetezi? wakili Peter Kibatala: Hapana mheshimiwa Jaji JAJI: kuna lolote kwa upande wa Serikali?

Wakili wa Serikali: Ni huyu SHAHIDI pekee tuliyekuwa naye leo, naomba ahirisho la kuendelea kesho, sababu mashahidi wengine wapo nje ya Dar es Salaam, na ikukupendeza Mheshimiwa Jaji leo tulichelewa kuanza kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu, kesho tunaomba kuanza saa nne kamili.

JAJI: Utetezi...?

Wakili Peter Kibatala: Hatuna pingamizi kwa Maombi waliyoleta wenzetu.

Jaji anasema, kama ilivyoombwa na Wakili wa serikali na kuungwa Mkono kwa niaba ya Mawakili wote wa washtakiwa nahairishs kesi mpaka kesho Asubuhi kuendelea na shauri

Jaji anasimama anatoka mahakamani baada ya Polisi kuamrisha... Na watuhumiwa wanaondolewa mahakamani kurejeshwa rumande.


Kwa hisani ya Martin MM - Twitter

---- MWISHO-----
 

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
544
1,000
Baada ya Jana jamii kupata habari ya kila kilichotokea Mahakamani kwa ufasaha bila kupindisha Leo jeshi la Polisi limedhibiti uingiaji Mahakamani pamoja na kuzuia matumizi ya simu. Sababu zakufanya hivyo hazijawekwa wazi. Ikumbukwe ACP Ramadhani Kingai ambaye ni mkuu wa Polisi Kinondoni leo anaendelea kuhojiwa katika kesi ndogo iliyoibuka kutoka kesi ya msingi.

Wakati jana anahojiwa kuhusu uwepo wake Mahakamani hapo Mara kwa mara kesi hii inapokuwa inasikilizwa alikiri kuwa anafika Mahakamani hapo na kwa mazingira haya yeye akiwa ni shahidi pia yeye ndiyo kiongozi wa Askari kwa eneo hili la mahakama na hivyo yawezekana baada ya Jana kuona Hali ya utata na maswali yaliyoibuka Mahakamani Leo hii amejiwekea ulinzi kuepusha taarifa za ushahidi wake kutokufika kwa jamii.

Hali hii imelalamikiwa muda mrefu na tatizo halijawekwa wazi kwamba serikali ndiyo inafanya haya au mahakama yenyewe ndiyo imeamua kutokuonekana matendo yake kwa wananchi. Katika ulimwengu wa Sasa nchi nyingi Duniani zimeruhusu live cavarage Mahakamani tofauti na Tanzania ambapo hata waandishi wa habari wanaoruhusiwa kuingia mahakamani ni wale tu ambao Jamhuri inaamini wataripoti kile ambacho wao wanataka.

Mfano mzuri ni tukio la Jana ambalo hakuna chombo Cha habari kilichokuwa mahakamani kiliweza kuweka updates ya kinachoendelea mahakamani. Vyombo vyote vilikaa kimya isipokuwa JF na Kurasa za tweeter.

Mahakama kwa mwendo huu inaonyesha wazi kwamba siyo chombo huru, vinginevyo itoe tamko kwa dola kuruhusu watu kuingia kulingana na ukubwa wa ukumbi wa mahakama na ikumbukwe hakuna sheria inayokataza kesi kuripotiwa moja kwa moja kwa wananchi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom