Update Kesi ya wananchi kuhusu bandari mahakama kuu Mbeya

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
#Updates
Mheshimiwa Jaji Ndunguru ameingia Mahakamani 5:00 .

Karani wa Mahakama amewaita Walalamikaji na wamekaa kwenye Kizimba chao.

MAWAKILI Wanajitambulisha;

1. Kwaajili ya Wajibu Maombi (Serikali)

Adv. Hangi Chana (principal state attorney)

Adv. Ayoub Sanga -state attorney

2. Kwaajili ya Walalamikaji;

Adv. Boniface MWABUKUSI - Wakili kiongozi

Adv. Philip Mwakilima

Adv. Livino Ngalimitumba

CHANA SA: Mhe Jaji, Sisi upande wa Wajibu Maombi tulipokea Nyaraka za Shauri hili siku ya tarehe 26.06.2023.

CHANA SA: anaendelea.... Marekebisho sehemu yoyote ukiona SA namaanisha wakili wa serikali.

Mhe Jaji kwakuwa shauri hili limefunguliwa kikatiba chini ya Ibara ya 108 (2) ya Katiba, ambapo sheria inahitaji shauri la namna hii kuendeshwa kama shauri la kawaida,

Ni kwa sababu haijaletwa chini ya sheria ya BRDEA na hivyo shauri hili linatakiwa liendeshwe chini ya Sheria ya Civil Procedure husuani Order VIII Rule 1 ya CPC ambayo inataka Majibu tuyalete ndani ya Siku 21 tangu tarehe ambayo tumekabidhiwa Hati ya Madai.

CHANA SA: Kwa msingi huo, tarehe ya Mwisho ya kuleta majibu yetu ni tarehe 17.07.2023 kwakuwa tulipokea hati hizo tarehe 26.06.2023.

Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji, bado tunazo siku za kuandaa majibu yetu na tutayaleta.

Ni hayo tu. Na mwenzangu SA hana la kuongeza.

Jaji anamkaribisha wakili Mwabukusi.

WAKILI MWABUKUSI: Mheshimiwa Jaji, kama alivyosema mwenzangu Wakili Mwandamizi Chang'a, kimsingi sisi hatupingani na hoja zao.

Lakini Mheshimiwa Jaji, wakati tunasubiri majibu yao; tunaomba kuitaarifa Mahakama kwamba tumeshasajili Maombi Madogo chini ya Hati ya Dharura, na hivyo tunasubiri maelekezo ya mahakama yako tukufu.

Wakili Mwabukusi: Mhe Jaji kwa kuzingatia aina ya shauri lililoko chini ya Mahakama hii tukufu, na kwa kuzingatia kwamba Wajibu maombi wanahitaji muda wa kujibu maombi yetu na kuyaleta mahakamani,

Hivyo Chini ya Order XLIII (2) Proviso na Kifungu cha 68 (e) ya CPC, CAP 33 R.E 2019, Mheshimiwa tunaiomba Mahakama hii tukufu ione kwamba kuna umuhimu wa kutoa "Conservatory Orders" kwamba Hali ibaki jinsi ilivyo mpaka pale shauri litakapokuja kutajwa tena baada ya Wajibu maombi kuleta majibu yao, na Mahakama kupata fursa ya kuona na kuyapokea maombi yaliyopo mbele yake au kutoa Amri zozote.

Wakili MWABUKUSI: Mheshimiwa Jaji, hii ni kuleta maana kwamba, kisifanyike kitu ambacho kitafanya Maombi/Shauri lililoko Mahakamani kuonekana halina Mashiko au kuharibu jambo hilo kiasi cha kutotengenezeka.

Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji

Anasimama wakili wa serikali.

SA: Mheshimiwa Jaji, licha ya Mawakili wa Waleta Maombi wamekubaliana na ombi letu,

Kimsingi ameleta maombi haya kwa Order XLIII (2) na Kifungu 68 Ambayo inalenga kuleta maombi kwa mdomo bila formal applications.

SA: Mheshimiwa Jaji, licha ya Mawakili wa Waleta Maombi wamekubaliana na ombi letu,

Kimsingi ameleta maombi haya kwa Order XLIII (2) na Kifungu 68 Ambayo inalenga kuleta maombi kwa mdomo bila formal applications.

SA: Hata hivyo Mheshimiwa Jaji, kifungu hicho alichokitaja kinaweka wazi kwamba hilo ni suala la mamlaka ya Mahakama (discretionary powers) na kwamba kinaeleza zaidi kwamba inaombwa kwa namna ya mdomo pale ambapo Wadaawa wanakuwa wameridhia kwamba maombi yafanyike kwa mdomo, sisi upande wetu wa Wajibu Maombi hatujakubaliana.

SA: Hata hivyo Mheshimiwa Jaji, kifungu hicho alichokitaja kinaweka wazi kwamba hilo ni suala la mamlaka ya Mahakama (discretionary powers) na kwamba kinaeleza zaidi kwamba inaombwa kwa namna ya mdomo pale ambapo Wadaawa wanakuwa wameridhia kwamba maombi yafanyike kwa mdomo, sisi upande wetu wa Wajibu Maombi hatujakubaliana.

SA: Mheshimiwa pia sheria inaelekeza mahakama kutazama mazingira ya jambo husika, tunaiachia mahakama, pia nyaraka ambazo wenzetu wanasema wamesajili kimsingi hadi sasa haijapokelewa mahakamani na sisi hatujapewa.

SA : Mhe Jaji pia vigezo vilivyowekwa kwenye kesi ya ATILIO MBOWE ni muhimu vikidhi.

SA: Wameleta shauri ambalo wamesema Serikali na Bunge wameshafanya maamuzi, na hawajasema yanatarajiwa kufanyika. Maombi haya ya kutaka mambo yabaki kama yalivyo, amri hizo zitawasaidia nini?

Mhe Jaji sisi tunafikiri maombi yao yasikubaliwe kwa mdomo, tusifanyie kazi kwenye "speculations" kwamba watu hawa watafanya hivi na vile.

Tunasisitiza maombi yao yasikubaliane yatupiliwe mbali.

Anasimama wakili Mwabukusi kwa ajili ya REJOINDER

WAKILI MWABUKUSI: Mheshimiwa Jaji, Msomi Sanga ametafsiri vibaya (misconstrued) kifungu cha Proviso, ameshindwa kutambua kwamba Conditions zilizowekwa zinajitegemea.

Wakili Mwabukusi: Mheshimiwa Jaji Wakili Sanga amefanya mawasilisho yake kwa kitu kipya, hakujibu hoja zetu. Hivyo tunaomba Mahakama hii tukufu iweze kupuuza (disregard) hoja zake.

Wakili MWABUKUSI: Mhe Jaji, Wakili Sanga amesema tumefanya "a mere statement from the Bar." Na huu ndio msingi wa Kifungu tulichotumia kuomba maombi yetu kwamba mazingira ya namna hii yanamruhusu Wakili kutoa maombi directly from the Bar.

Naomba kumkaribisha Wakili Mwakilima kuongeza kidogo.

WAKILI MWAKILIMA: Mhe Jaji, Wakili Sanga ametaja kesi ya ATLIO v. MBOWE. Kesi hiyo haiwezi kusaidia Mahakama kutatua jambo hili kwani katika kesi hiyo ilihusu ugomvi wa Mpangaji na Mwenyenyumba.

Shauri letu hapa ni la Wananchi kuhusu upotevu mkubwa na kupotezea kabisa rasilimali za nchi.

Anamaliza Mwakilima.

MHE JAJI NDUGURU: Wajibu Maombi mnafikiri majibu yenu mnaweza kuleta lini? Mkizingatia nature ya shauri imeletwa chini ya Hati ya dharura na sisi (Majaji) tumejipanga angalau tarehe 17 au 18 tuanze kusikiliza kesi hii.

SA: Sisi tutakuwa tayari kuleta majibu yetu ifikapo tarehe 14.07.2023.

MWABUKUSI: Na sisi tuanze kuhesabiwa tarehe 15 na tupo tayari kuleta majibu yetu hadi ifikapo tarehe 19.07.2023.

Mheshimiwa Jaji anaandika Uamuzi mdogo wa kutoa maelekezo na ratiba (schedule) ya namna ya kufikisha nyaraka Mahakamani

JAJI NDUNGURU;

Kuhusu maombi yaliyoletwa, Mahakama inaona kwamba Maombi hayo kama yalivyo semwa yanasajiliwa Mahakamani, basi inafaa yafanyiwe kazi katika namna yake pale yatakapokuwa tayari Mahakamani.

AMRI:

1. Shauri linaahirishwa.

2. Shauri litaanza kusikilizwa tarehe 20.07.2023 kwa Mfululizo.

=====
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya itaanza kusikiliza maombi ya kupinga mkataba uwekezaji wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kupitia Kampuni DP World baada ya kupokea majibu ya Serikali.

Katika maombi hayo ya kikatiba, waleta maombi wanaitaka Serikali kuieleza mahakama sababu za kile wanachodai kuwa ni kusaini mkataba pasipo ushirikishwaji wa wananchi.

Shauri hilo litaanza kusikilizwa Julai 20, 2023, ikiwa leo Jumatatu limefikishwa kwa mara ya kwanza mbele ya Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Dastan Ngunguru likiwasilishwa na mawakili wa utetezi, Boniface Mwabukusi na Philipo Mwakilima dhidi ya wateja wao wanne waliopeleka malalamiko hayo.

Waliopeleka malalamiko hayo ni Alphonce Lusako, Raphael Ngonde, Emmanuel Chengula na Frank Nyalusi.

Mwanasheria wa Serikali, Hangi Chang'a ameeleza mahakamani hapo kuwa walipokea nyaraka za shauri hilo Juni 26, 2023 na kupata siku 21 kulipitia na kujibu.

Awali, Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Dastan Ndunguru baada ya kusikiliza pande zote ameshauri upande Serikali kujibu maombi hayo kwa umakini mkubwa kwani kesi hiyo ni ya kikatiba na msingi ambayo itasikilizwa na majaji watatu.
 
Tusianze kutoa maamuzi ya kesi yatakavyokua wakati bado haijaanza, tutaona mwenendo wa kesi itakavyokua inaendelea,kuna mambo ambayo hayahitaji utaalam wa sheria kuyaelewa.

mfano mzuri ni ile kesi ya ugaidi iliyomuhusu Mbowe, mwenendo wa kesi ulikua unajionyesha wazi ni kesi ya aina gan
 
Back
Top Bottom