Tamko la kulaani kusimamishwa kiholela kwa Wakili Mpale Mpoki na tishio kwa mawakili wa kujitegemea nchini

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko taarifa ya kusimamishwa kiholela kufanya kazi za uwakili iliyomkumba Wakili Mwandamizi Mheshimiwa Mpale Mpoki ambaye alikuwa akiongoza jopo la Mawakili wa utetezi katika shauri la kinidhamu linalomkabili Wakili Boniface Mwabukusi mbele ya Kamati ya Maadili ya Mawakili iliyoketi tarehe 20 Novemba, 2023 katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, Dar –es- Salaam mbele ya Mheshimiwa Ntemi Kilekamajenga, Jaji- Mwenyekiti wa Kamati.

Aidha, Chama kimeshtushwa na kinalaani mikakati inayoashiria nia ovu ya Serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sasa imedhihirika kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mawakili na kupitia baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu kwa nyakati tofauti kuendeleza vitisho dhidi ya mawakili wanaotumia haki yao ya kikatiba ya kutoa huduma ya uwakilishi Mahakamani na wakati mwingine kutoa maoni mbadala, kutishiwa kuondolewa katika orodha ya Mawakili Tanzania.

Kama Chama, Tunaamini hili sio tishio tu dhidi ya Wakili, Boniface Mwabukusi au Wakili Mpale Mpoki na Jopo lake lote, bali ni tishio dhidi ya taaluma ya Sheria na Mawakili wote nchini na tishio dhidi ya vyombo vya utoaji haki nchini. Tunafahamu kwamba njama hizi zilianza na kuondoa Uwakili wa Wakili Fatma Karume ambaye Mpaka sasa hajarudishiwa Uwakili wake, Wakili Edson Kilatu, Wakili Jebra Kambole na Mawakili Wengine ambao wameshitakiwa kwa nyakati tofauti ili kuwatisha Mawakili wawe wanaiabudu serikali hata pale ambapo inakiuka utawala wa Sheria. Ikumbukwe kwamba Tanzania imeridhia mikataba na matamko mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo Tamko la Umoja wa Mataifa la tarehe 7 Septemba, 1990 Mjini Havana, Cuba ambalo liliweka sharti kwa mamlaka za Serikali kuwalinda Mawakili dhidi tishio lolote la kiusalama wanapotimiza wajibu wao.

Chama kinamtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mawakili Mheshimiwa Ntemi Kilekamajenga, Jaji kuwajibika kwa kujiondoa katika nafasi yake ya Uenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mawakili ili kuruhusu Jaji mwingine kuendelea kusikiliza shauri husika. Pili, kinawashauri Mawakili wote Tanzania na Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) kutumia vikao vyake vya kikatiba na kama Maafisa wa Mahakama kwa mujibu wa Sheria ya Mawakili, kuchukua hatua za dharura kuhami wanachama wao wanaoonewa na Serikali na kuhakikisha kwamba uamuzi wa Jaji Ntemi Kilekamajenga unafutwa kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu.

Tunasisitiza kwamba, Mahakama inatakiwa kuwa sehemu ya kutoa haki bila upendeleo wala kuonea watu ili jamii inapoonewa iwe na imani kuwa wakikimbilia Mahakamani watapata haki bila kujali aliyeonewa kaonewa na Mtu au taasisi gani.

Imetolewa leo Jumanne tarehe 21 Novemba, 2023

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya NjeView attachment 2820990
IMG-20231121-WA0058.jpg
 
TTa

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya NjeView attachment 2820990View attachment 2820991
Tatizo Tulilonalo kwa sasa ni sa100 tu
 
Fatma Karume ofisi yake ilipigwa bomu ofisi ipo karibu na maeneo ya ofisi za jeshi kabisa hakukamatwa mtu.

Fatma Karume akavuliwa uwakili bila sababu za msingi ikapita.

Watanzania wakadanganywa uongozi umebadilika na tusahau yaliyopita!

Leo hii naona tunarudi kule kule je watu wana cha kujifunza?
 
Inasikitisha sana walivyotendewa mawakili hawa wasomi. Sheria izingatiwe bila kuingiza siasa kwenye taaluma. Mawakili kupitia TLS tunategemea kuona umoja wenu kukemea uonevu Kwa mawakili mwabukusi na mpoki.
 
Siasa za hovyo za CCM zimeanza kuingia mpaka kwenye taasisi/idara za utoaji haki nchini, hili likiendelea kufumbiwa macho, kwa kuwaacha majaji wajinga wanaojipendekeza kwa mamlaka ya uteuzi waendelee kuminya haki za watanganyika kwa makusudi, hii nchi iko siku tutavuna tunachopanda.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kila mtu amekuwa kama ni mateka wa hawa watu (wachache kabisa wanaoiendsha CCM hii mbovu).

Mi nawaza tu. Hawa mawakili, na wengi wengine sehemu mbalimbali za nchi hii ni wasomi wazuri, tena wanaojitambua vizuri kabisa.
Inakuwaje, sote nchi nzima tubaki tunayumbishwa namna hii na hawa watu?
Hivi haiwezekani kamwe watu wakajipanga na kuwa na lengo maalum moja tu, linalo waunganisha, kuhakikisha kupambana na hali hii kwa pamoja?

Ni wazo tu linalopitia akilini kwa sasa.
Why can't there be a unity in purpose, even if it is only for this issue of changing this dismal outlook in our nation!
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko taarifa ya kusimamishwa kiholela kufanya kazi za uwakili iliyomkumba Wakili Mwandamizi Mheshimiwa Mpale Mpoki ambaye alikuwa akiongoza jopo la Mawakili wa utetezi katika shauri la kinidhamu linalomkabili Wakili Boniface Mwabukusi mbele ya Kamati ya Maadili ya Mawakili iliyoketi tarehe 20 Novemba, 2023 katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, Dar –es- Salaam mbele ya Mheshimiwa Ntemi Kilekamajenga, Jaji- Mwenyekiti wa Kamati.

Aidha, Chama kimeshtushwa na kinalaani mikakati inayoashiria nia ovu ya Serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sasa imedhihirika kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mawakili na kupitia baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu kwa nyakati tofauti kuendeleza vitisho dhidi ya mawakili wanaotumia haki yao ya kikatiba ya kutoa huduma ya uwakilishi Mahakamani na wakati mwingine kutoa maoni mbadala, kutishiwa kuondolewa katika orodha ya Mawakili Tanzania.

Kama Chama, Tunaamini hili sio tishio tu dhidi ya Wakili, Boniface Mwabukusi au Wakili Mpale Mpoki na Jopo lake lote, bali ni tishio dhidi ya taaluma ya Sheria na Mawakili wote nchini na tishio dhidi ya vyombo vya utoaji haki nchini. Tunafahamu kwamba njama hizi zilianza na kuondoa Uwakili wa Wakili Fatma Karume ambaye Mpaka sasa hajarudishiwa Uwakili wake, Wakili Edson Kilatu, Wakili Jebra Kambole na Mawakili Wengine ambao wameshitakiwa kwa nyakati tofauti ili kuwatisha Mawakili wawe wanaiabudu serikali hata pale ambapo inakiuka utawala wa Sheria. Ikumbukwe kwamba Tanzania imeridhia mikataba na matamko mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo Tamko la Umoja wa Mataifa la tarehe 7 Septemba, 1990 Mjini Havana, Cuba ambalo liliweka sharti kwa mamlaka za Serikali kuwalinda Mawakili dhidi tishio lolote la kiusalama wanapotimiza wajibu wao.

Chama kinamtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mawakili Mheshimiwa Ntemi Kilekamajenga, Jaji kuwajibika kwa kujiondoa katika nafasi yake ya Uenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mawakili ili kuruhusu Jaji mwingine kuendelea kusikiliza shauri husika. Pili, kinawashauri Mawakili wote Tanzania na Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) kutumia vikao vyake vya kikatiba na kama Maafisa wa Mahakama kwa mujibu wa Sheria ya Mawakili, kuchukua hatua za dharura kuhami wanachama wao wanaoonewa na Serikali na kuhakikisha kwamba uamuzi wa Jaji Ntemi Kilekamajenga unafutwa kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu.

Tunasisitiza kwamba, Mahakama inatakiwa kuwa sehemu ya kutoa haki bila upendeleo wala kuonea watu ili jamii inapoonewa iwe na imani kuwa wakikimbilia Mahakamani watapata haki bila kujali aliyeonewa kaonewa na Mtu au taasisi gani.

Imetolewa leo Jumanne tarehe 21 Novemba, 2023

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya NjeView attachment 2820990View attachment 2820991
CHADEMA mnapaswa kuwa pro active kwa namna hii Kila papohitajika kwa kutoa tamko haraka na mapema kama mlivyofanya sasa ili kuupa umma a common stand kutoka ktk chama kwa suala lolote la kijamii...

Tunataka CHADEMA ya wakati ule aliyekuwa Afisa habari Tumaini Makene chini ya Katibu mkuu Dr Willbroad Slaa irejee...

Wakati ule ilikuwa kila burning issue yoyote iliyohitaji clarification na msimamo wa chama, haraka chama kilikuwa kinatoa msimamo wake (Press Release) na kuwa published kwenye vyombo vya habari (main streams) na social medias zote...

Kuna matukio mengi sana yanapita bila kusikia kauli wala msimamo wowote wa chama ulio rasmi zaidi ya kusikia kila kiongozi akijsemea mwenyewe tu kivyake bila utaratibu kiasi cha kutokea kupingana na mivurugano isiyo ya lazima..

Mimi nafikiri kuna kupwaya kwa mtendaji mkuu wa chama yaani katibu mkuu wa chama (John John Mnyika) na ofisi yake Kwa ujumla..

Kuna maswala (very hot burning issues) zinazo -trend katika jamii wa sasa hivi, lakini jamii haioni msimamo wowote serious toka katika chama chaoCHADEMA wanachokitegemea ambacho kwa vyovyote vile hiki ndicho mbadala wa CCM..

Mfano kwa kutaja machache tu ni;

1. Kuna tatizo la uhaba na mgawo umeme ambalo limeathiri shughuli za kiuchumi za wananchi Kwa takribani mwaka sasa. Je, CHADEMA mliwahi kusema lolote officially?. Honestly, mimi sikumbuki zaidi ya vijitamko vya reja reja na vinavyopingana toka kwa viongozi mbalimbali visivyo na impact yoyote kwa CCM na serikali Ypyao..

2. Vipi kuhusu gharama za maisha kupanda kunakosababishwa na kupanda kwa kutisha kwa nishati ya mafuta ya petrol na uhaba wa umeme? Mmewahi kutoa serious statement yoyote?

## Tunaihitaji CHADEMA ya wakati wa Dr Wilbroad Slaa ambayo ilikuwa very aggressive kwani ilikuwa ikitoa msimamo wake fulani tu juu ya jambo lolote kuhusu nchi na jamii, panya wote wa CCM na serikali waliokuwa wakitoka mashimoni ili kutafuta hewa safi ya kuvuta..!!
 
Back
Top Bottom