1631788073153.png
 
Freeman Mbowe na wenzake wameletwa tayari. Lakini ulinzi mkali umeimarishwa. Askari wengi. Pia kuna zuio la watu kuingia ndani ya mahakama. Wanasema ni mawakili 20 tu, wanahabari 10 (leo wameruhusiwa), ndugu 5, Viongozi 5, lakini simu marufuku.

Askari magereza wanalalamika kwamba jana tumefanya ujinga sana. Ujinga gani, tunawaukliza, wanasema tulikuwa tunatuma habari nje. Wanamueleza Benson Kigaila, NKM CHADEMA. Tumewaeleza kwamba, anayetakiwa kulalamika ni Jaji sio wao. Mahakama siyo gereza. Wajishikilie vizuri.

Mahakama imechelewa kwa dakika 40, yote hii ni kutokana na Jamhuri kutaka kuhodhi mamlaka ya mahakama, bila kujua kwamba wote hapa tuna interest na kesi hii, wao ni walalamikaji, sisi ni watuhumiwa. Kwanini watuzuie kuingia mahakamani na simu?

Watoto wote wa Freeman Mbowe, (Nicole na Dudley) pia wapo nje ya mahakama, pamoja na ndugu zao wengine.

Kama kawaida yao, makarao waliovalia kiraia, wamekaa kwenye siti karibu zote za mahakama, wamechukua nafasi kama kesi ni yao pekee yao.

Mambo ya ajabu yanafanyika

Lakini kitu cha muhimu hadi sasa ndugu zangu ni kwamba, kwa umoja wetu wote tupo nje ya mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa, Ubungo-Mawasiliano, tumeshawaelekeza MAWAKILI wetu wasomi kwamba "No ENTRANCE NO CASE"... And it's done, hii ni open court!

Updates
Jana Jaji Mustapha Siyani alisema watuhumiwa waletwe mapema, saa 3 asubuhi kesi ianze, lakini mpaka saa 5 na Dakika 24 sasa kesi haijaanza kwa sababu ya polisi kuzuia watu. Mawakili wetu walikwenda kumuona Jaji, wanatupa taarifa kwamba Jaji amekana kuzuia Jambo hilo mahakamani.

Updates
Wakili Msomi Kibatala ameandika Jaji ameruhusu watu waachwe huru

Mahakama Kuu ilipo kesi ya Ugaidi ya Mbowe, baada ya Polisi kuzuia watu kuingia Mahakamani na kuzuia simu, Jaji ameamuru kuwa na Polisi watoke na wasiwe na simu, Mawakili wa Mbowe wote wametoka Nje kwani hii ni kesi yenye maslahi ya UMMA! Mawakili wapo Nje na UMMA

JOPO la mawakili wa Freeman Mbowe na wenzake wote wametoka nje ya chumba cha mahakama muda huu, kupinga watu kuzuiwa kuingia mahakamani, na viongozi wa CHADEMA kuingia bila simu... Saa sita na dakika sita Mchana, saa za Afrika ya mashariki, Kesi imeshindwa kuendelea..

Kesi ya ugaidi inayomkabili Mhe Mbowe na wenzake3, imeshindwa kuendelea katika Mahakama kuu baada ya Polisi kufanya fujo na hivyo watuhumiwa wamerudishwa mahabusu muda huu
View attachment 1940178
Freeman Mbowe na wenzake watatu wakitolewa nje ya chumba cha mahakama ikiwa ni zaidi ya saa moja tangu kesi hiyo ilipopangwa kusikilizwa.

Kesi imesitishwa na Washitakiwa wamepelekwa Mahabusu ndogo kusubiri Uwamzi wa Jaji. Kesi zinazofanyika Open Court, watu wanaruhusiwa kuingia. Lakini hii kesi Watu wamekatazwa kuingia na wachache waliongia hawakuruhusiwa kuingia na simu.


UPDATE: Kesi inaendelea baada ya pande zote kukutana

Baada ya kuzuiwa kwa Wananchi kuingia Mahakamani kusikiliza kesi ya Mhe. Mbowe na wenzake na kupelekea Mawakili upande wa tetezi kutoka nje ya ukumbi wa mahakama, hatimae Jaji ameamuru wananchi kuingia mahakamani baada ya majadiliano ya faragha kati ya pande zote mbili.

Upande wa Jamhuri wameshindwa kuileza Mahakama kifungu cha sheria kinachokataza wananchi kuingia na simu na kutoa taarifa juu ya kinaendelea katika kesi Na. 16/2021, Jaji akasema hakuna sheria wala kanuni inayokataza watu kuingia na simu mahakamani.

Kesi inaendelea.
Mitano tena kwa jaji
 
Demka na mashairi ya tusonge mbele kama nini..ngoma hii hadi ifike mwisho hili bonge la series breaking bad haifui dafu. Either mwamba atoke huru ama ale mvua za kutosha
baada ya kumsikiliza huyo shahidi wa DPP jana nikajua hamna kesi humo ni aibu tupu.
 
Ni jambo la kushangaza sana mhimili wq mahakama kuingiliwa na vipolisi.. chief judge usikubali mahakama yako kudhalilishwa kiasi hicho!
 
Upande wa Jamhuri wameshindwa kuileza Mahakama kifungu cha sheria kinachokataza wananchi kuingia na simu na kutoa taarifa juu ya kinaendelea katika kesi Na. 16/2021, Jaji akasema hakuna sheria wala kanuni inayokataza watu kuingia na simu mahakamani.
aisee..... yaani jeshi linafanya kazi bila vifungu cha sheria bila kujua kwamba ukiwa mahakamani ukitoa kauli lazima uisindikizie na sheria. kazi ipo tena pevu.
 
Back
Top Bottom