Wakili Peter Madeleka akamatwa na polisi baada ya Mahakama Kuu kufuta Plea Bargain aliyoingia na DPP

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Wakili Peter Madeleka amekamatwa na Polisi Arusha,

Amekamatwa mara baada ya High Court Arusha kufuta Plea Bargain aliyoingia na DPP

Taarifa zaidi kukujia

========
Tweet yake ya mwisho ilikuwa .... Mahakama Kuu ya Tanzania Arusha Leo tarehe 17 Julai 2023 IMEFUTA PLEA BARGAIN iliyoingiwa Kati ya DPP na PETER MADELEKA. Hata hivyo RCO ARUSHA ametuma ASKARI WANIKAMATE nikiwa Mahakamani. Bado sijatoka kwa JAJI.

Baadhi ya kauli zake kuhusu sakata la bandari

1. Wakili Madeleka: Rais Samia nakusihi, Futa huu Mkataba wa Bandari
2. Wakili Madeleka: Dubai sio nchi kama ilivyo Zanzibar hivyo haiwezi kuingia mkataba na nchi nyingine

Pia soma
1. Wakili Madeleka ataka Jaji Biswalo achunguzwe suala zima la Plea Bargain

---
Wakili wa kujitegemea nchini, Peter Madeleka amekamatwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Jumuishi cha utoaji haki baada ya kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Madeleka kabla ya kukamatwa alilazimika kung'ang'ania kwa zaidi ya dakika 30 katika chumba cha Mahakama cha Jaji Aisha Bade ambaye awali ndiye alitoa maamuzi katika kesi yake ya kupinga makubaliano ya kukiri kosa ‘Plea bargaining.’

Wakili Madeleka aliwasilisha maombi namba 80 ya mwaka 2021 kutokana na kesi aliyokuwa amefunguliwa ya uhujumu uchumi namba 40/2020.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi iliyotolea uamuzi Aprili 27 mwaka huu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, wakili Madeleka alikuhukumiwa kulipa faini ya Sh200,000 au kutumikia kifungo cha nje cha miaka mitatu.

Katika uamuzi huo, pia alilipa Sh2 milioni kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ili kuondolewa shauri hilo baada ya kulazimika kukiri makosa.

Hata hivyo wakili huyo alifungua kesi Mahakama Kuu, kupinga uamuzi wa Hakimu Mkazi Arusha, kumtia hatiani katika kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Wakili Madeleka pia aliiomba Mahakama Kuu itoe amri ya kurejeshewe faini ya Sh200,000 aliyolipa kwa sababu mchakato mzima ulikuwa ni kinyume cha sheria.

Amesema baada ya hukumu hiyo, alilazimishwa kufanya makubaliano ya kukiri kosa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) na baada ya kuachiwa alikata rufaa.

Leo mara baada ya kusomwa kwa hukumu yake na wakili huyo alibakia kwenye chumba cha mahakama hadi alipofika Wakili wake, Simon Mbwambo na wanahabari ndipo alipotoka kwenye chumba hicho na kukamatwa na polisi.

Awali Madeleka amesema kuwa Jaji Bade amekubaliana na hoja yake kuwa upande wa mashtaka kabla ya kuingia katika makubaliano ya kukiri makosa ulipaswa kuwa na ushahidi wa kosa alilotenda

“Hata hivyo, Jaji Bade ameagiza kesi hiyo kuanza upya kusikilizwa katokana na baadhi ya upungufu katika shauri hilo” amesema

Akizungumzia kuhusu kukamatwa kwa mteja wake, Wakili Simon Mbwambo, amesema hajui kosa analokabiliwa nalo wakili Madeleka.

"Sijui kosa naona polisi wamemkata na wanampeleka Ofisi ya RCO (Mkuu wa Upelelezi Mkoa Arusha) kwa mahojiano, labda wanataka kuanza upya kusikiliza kesi hii ya leo," amesema.

Polisi waliomkamata wakili Madeleka hata hivyo hawakuwa tayari kuelezea tuhuma zake na kuwataka wanahabari kufuata taratibu za kupata habari kwa kuzungumza na viongozi wa juu wa polisi.

Wakili Madeleka katika siku za karibuni amekuwa katika harakati za kupinga Makubaliano ya uwekezaji wa bandari kati ya Tanzania na Dubai na wiki iliyopita alikuwa jijini Dar es Salaam katika mkutano ulioandaliwa na Balozi mstaafu Dk Wilibroad Slaa na Wakili Boniface Mwabukusi wakielezea ubovu wa makubaliano hayo.
 
Itabidi kuangalia upya vigezo vya polisi. Badala ya kuifanya kazi ya polisi kuwa ni kazi ya watu wenye uwezo mdogo wa akili iwe ni kazi ya watu wenye upeo mkubwa, weledi na watu wenye akili ya kutosha.

Mkiwa na polisi wasiojitambua wanaweza kuifanya nchi kuonekana ni ya ajabu.
 
Hatari sana juzi ripoti ya Haki Jinai aliyotoa jaji mstaafu Mohamed Othman Chande na baadaye kauli ya mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. Samia Suluhu Hassan kuwa taasisi na viongozi waliopo katika mfumo wa haki jinai wabadilike bado haijaweza kuwafikia watendaji waliopo katika kuhakikisha haki ndani ya mfumo wa haki jinai Tanzania

1689585532943.png

Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 15 July 2023 amepokea ripoti ya Tume ya Rais ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai kutoka kwa Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Mohammed Othman Chande, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
Ripoti ya Haki jinai ulikuwa wazi kabisa yakuwa wale waliokuwa wanashitakiwa na walipo ingia makubaliano na Dpp hawakumalizia madeni Yao.

Na ripoti imeenda mbali zaidi na kusistiza wachukuliwe hatua maana kitendo hicho kinaalalisha yakuwa zoezi rile lilikuwa bariki.

Ninachotaka kusema hapa wale mliokamatwa mlidhani mmekamatwa na magufuli kiunevu na kifo chake mkaona mmepona umekula kwenu kimbieni fasta Kwa Dpp mmalize madeni yenu haraka kinyume chake sero zinawasubiri.

Popote ulipo Waitu Ta kabendera njoo ulipe mkopo wa uovu wako.

Popote mlipo waovu wote wa ple bagarning mjitokeze haraka mlipe mikopo ya matendo yenu machafu.
 
Itabidi kuangalia upya vigezo vya polisi. Badala ya kuifanya kazi ya polisi kuwa ni kazi ya watu wenye uwezo mdogo wa akili iwe ni kazi ya watu wenye upeo mkubwa, weledi na watu wenye akili ya kutosha.

Mkiwa na polisi wasiojitambua wanaweza kuifanya nchi kuonekana ni ya ajabu.
Police hawana kosa wao wanatii maagizo ya wanasiasa toka juu.
 
Kuna wale wanatishia watu kuwakabidhi kwa machief!

Hii inadhihilisha kuwa, ccm, uovu wao wanaulinda kwa uovu! Wanatuma mapolisi kuwadhibiti watu ili wautetee uovu kwa nguvu zao zote! Na sisi kama watanganyika,

Watu wema wanaotetea haki, tutawakabidhi kwa Mungu mkuu wa haki na mwenye hukumu za haki dhidi ya uovu!

Nijualo ni moja tu! Jambo lenye haki, halilindwi kwa njia haramu!

Rudisheni bandari na ama mboreshe mkataba
 
Wakili Peter Madeleka amekamatwa na Polisi Arusha,

Amekamatwa mara baada ya High Court Arusha kufuta Plea Bargain aliyoingia na DPP

Taarifa zaidi kukujia

========
Tweet yake ya mwisho ilikuwa .... Mahakama Kuu ya Tanzania Arusha Leo tarehe 17 Julai 2023 IMEFUTA PLEA BARGAIN iliyoingiwa Kati ya DPP na PETER MADELEKA. Hata hivyo RCO ARUSHA ametuma ASKARI WANIKAMATE nikiwa Mahakamani. Bado sijatoka Kwa JAJI.

Baadhi ya kauli zake kuhusu sakata la bandari

1. Wakili Madeleka: Rais Samia nakusihi, Futa huu Mkataba wa Bandari
2. Wakili Madeleka: Dubai sio nchi kama ilivyo Zanzibar hivyo haiwezi kuingia mkataba na nchi nyingine
3. Wakili Madeleka ataka Jaji Biswalo achunguzwe suala zima la Plea Bargain
alitoa elimu ya mkataba,

Kwa hiyo kosa lake ni kuelimisha wananchi wa Tanganyika juu ya mkataba, wakaona walale nae mbele. Maigizo kutoka juu yameanza sio
 
Ripoti ya Haki jinai ulikuwa wazi kabisa yakuwa wale waliokuwa wanashitakiwa na walipo ingia makubaliano na Dpp hawakumalizia madeni Yao.

Na ripoti imeenda mbali zaidi na kusistiza wachukuliwe hatua maana kitendo hicho kinaalalisha yakuwa zoezi rile lilikuwa bariki.

Ninachotaka kusema hapa wale mliokamatwa mlidhani mmekamatwa na magufuli kiunevu na kifo chake mkaona mmepona umekula kwenu kimbieni fasta Kwa Dpp mmalize madeni yenu haraka kinyume chake sero zinawasubiri.

Popote ulipo Waitu Ta kabendera njoo ulipe mkopo wa uovu wako.

Popote mlipo waovu wote wa ple bagarning mjitokeze haraka mlipe mikopo ya matendo yenu machafu.
Hizo ni mbinu chafu tu za kuwafunga watu midomo wasiupinge ule mkataba mbovu wa bandari, hakuna cha watu kutolipa madeni wala vyovyote vingine, kwanza tulishaambiwa zile pesa hazijulikani zilipo, na hata wengine wakaanza kudai pesa zao.

Bandari zitaendelea kudaiwa kwa njia zote halali ilimradi haki ya mtanganyika aliyopewa na muumba ipatikane.
 
20220421_064652.jpg
Mahakama Kuu ya Tanzania Arusha leo tarehe 17 Julai 2023 imefuta Plea Bargain iliyoingiwa Kati ya DPP na PETER MADELEKA. Hata hivyo RCO Arusha ametuma Askari Wanikamate nikiwa Mahakamani. Bado sijatoka Kwa Jaji.

Hukumu iliyosomwa leo na Mahakama Kuu ya Tanzania Arusha mbele ya JAji Bade, licha ya Kufuta Plea Bargain Kati ya DPP na PETER MADELEKA, ilikuwa imeshajulikana Kwa Polisi na DPP Kabla ya kusomwa na Mahakama ikasaidia Mazingira ya Mimi kukamatwa.

Ameandika Wakili Peter Madeleka, Twitter
 
Ripoti ya Haki jinai ulikuwa wazi kabisa yakuwa wale waliokuwa wanashitakiwa na walipo ingia makubaliano na Dpp hawakumalizia madeni Yao.

Na ripoti imeenda mbali zaidi na kusistiza wachukuliwe hatua maana kitendo hicho kinaalalisha yakuwa zoezi rile lilikuwa bariki.

Ninachotaka kusema hapa wale mliokamatwa mlidhani mmekamatwa na magufuli kiunevu na kifo chake mkaona mmepona umekula kwenu kimbieni fasta Kwa Dpp mmalize madeni yenu haraka kinyume chake sero zinawasubiri.

Popote ulipo Waitu Ta kabendera njoo ulipe mkopo wa uovu wako.

Popote mlipo waovu wote wa ple bagarning mjitokeze haraka mlipe mikopo ya matendo yenu machafu.

Ripoti ya Haki jinai ulikuwa wazi kabisa yakuwa wale waliokuwa wanashitakiwa na walipo ingia makubaliano na Dpp hawakumalizia madeni Yao.

Na ripoti imeenda mbali zaidi na kusistiza wachukuliwe hatua maana kitendo hicho kinaalalisha yakuwa zoezi rile lilikuwa bariki.

Ninachotaka kusema hapa wale mliokamatwa mlidhani mmekamatwa na magufuli kiunevu na kifo chake mkaona mmepona umekula kwenu kimbieni fasta Kwa Dpp mmalize madeni yenu haraka kinyume chake sero zinawasubiri.

Popote ulipo Waitu Ta kabendera njoo ulipe mkopo wa uovu wako.

Popote mlipo waovu wote wa ple bagarning mjitokeze haraka mlipe mikopo ya matendo yenu machafu.
Ndugu hufi leo kwani nawe ni wakili wa shetani 🤔
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Arusha leo tarehe 17 Julai 2023 imefuta Plea Bargain iliyoingiwa Kati ya DPP na PETER MADELEKA. Hata hivyo RCO Arusha ametuma Askari Wanikamate nikiwa Mahakamani. Bado sijatoka Kwa Jaji.

Hukumu iliyosomwa leo na Mahakama Kuu ya Tanzania Arusha mbele ya JAji Bade, licha ya Kufuta Plea Bargain Kati ya DPP na PETER MADELEKA, ilikuwa imeshajulikana Kwa Polisi na DPP Kabla ya kusomwa na Mahakama ikasaidia Mazingira ya Mimi kukamatwa.

Ameandika Wakili Peter Madeleka, Twitter
Mchongo kujifanya wanafanya kazi kumbe sifuri rushwa tupu
 
Back
Top Bottom