Ni wazi kua watu wengi walidhani Corona itakua ni ugonjwa wa labda muda mfupi kisha utadhibitiwa, lakini hali ni tofauti kwani hadi sasa kesi zinaongezeka kila uchao, hata huko Marekani ambako wameamua kuondoa lockdown sio kwa sababu mambo yamekaa sawa, keshi bado ni nyingi na watu wanaendelea kufariki.

Nadhani ni wakati sasa tukiwa tunajadili ni jinsi gani ya kuushinda huu ugonjwa pia tujadili ni jinsi gani ya kuishi na huu ugonjwa kama ilivyo UKIMWI na Malaria. if the situation will remain unchecked,hali itazidi kuwa mbaya na huenda hata elimu yetu ikawa taabani kabisa achilia mbali casualties.
 
Ni kheri serikali ikawa inatoa idadi kamili ya wagonjwa na wanaokufa kila siku. Pia ikawa inatoa sababu sahihi cha viongozi waliokufa karibuni. Na serikali ikae itambue huu ugonjwa sio kwa wananchi tu au Watanzania walala hoi.

Taarifa zisizo jenga maswali au taharuki, ni moja wa njia ya kuzuia ugonjwa huu kusambaa. Unapitia taarifa kamili isiyokuwa na sintofahamu zaidi hujenga hata uelewi kwa wananchi juu ya ugonjwa huu.

Moja wa taarifa ambazo zinapaswa kuwekwa sawa.
Ni ugonjwa unaitwaje na unasababishwa na Nini. Ukisikiliza radio nyingi nchini husema ugonjwa wa virusi vya Corona. Hii Ni miongoni mwa taarifa isiyo sahihi. Ugonjwa unaitwa Corona, husabishwa na virus mwenye jina Covid-19.

Pili ni taarifa kamili juu ya wagonjwa waliopo nchini na wangapi wanakufa.
Kuna picha zinaonyesha watu wanazikwa usiku na tena chini ya usimamizi wa jiji, serikali haizungumzi hili swala. Picha zipo mitandaonj, haswa mtandao wa Twitter zipo nyingi.

Tatu Ni taarifa kamili za Hawa viongozi waliofuatana kufa.
Hii ni taarifa inabidi iwekwe wazi, mfano wa kifo Cha babake Simbachawene walihudhurulia watu mashuhuri na wa vyeo tofauti tofauti Serikalini, msiba ulifanyika wilayani Mpwapwa mkoa wa Dodoma. Hapakuwa na tamko la kusema wahudhuriaji wawe kumi.

Lakini hii misiba ya viongozi waliokufa karibuni unajenga taharuki kidogo, haswa kusema watu kumi ndio wahudhurie msibani na jiji lisimamie mazishi na waje kuaga baada ya kuzika.

Kuna usemi unasema information is power, huenda serikali haitambui usemi huu.
Ukiniambia Mimi niamini taarifa za serikali nitakataa za serikali kabisa Bora za mitandao.
 
Hii Ndiyo akili halisi ya mtu mweusi.

Hataki Kabisa Kuumiza Kichwa.

Anachoweza, ni kupenda SHORTCUTS, USHIRIKINA na KUISHI NA MATATIZO.

Yaani badala ya kutafuta namna ya kupambana kudhibiti ugonjwa eti unataka watu wajifunze KUISHI NAO.

Unafikiri ni MAFUA YALE au HOMA ??!!
 
Kama kuna kitu hukijui ndugu kitu kinaitwa UKWELI na utawala wa sasa ni usiku na mchana. Katika jambo linalochukiwa na utawala wa Magufuli ni ukweli. Tuanzie kwa uchaguzi wa wabunge wa marudio tunajua cheating ya wazi wazi iliyofanyika mpaka askari wetu wanaingiza mabox ya kura ndani hapo kinondoni, tuje serikali za mitaa tuangalie zile sarakasi zilizofanyika hii yote ni kuogopa ukweli.

Tuje pesa iliyochangwa na wadau kusaidia korona mpaka leo hatuambiwi zimefanya nini, hii yote ni kuogopa ukweli. The man in the "white house" is inclined to cheating behaviour, ndo maana hata ile PHD yake in mashaka makubwa, he cheated.

Kumbuka alivyoambiwa ukweli kwamba popularity yake imeshuka toka 96% mpaka 50%+ alimnyanganya mtafiti pasport na kutunga "sheria" kukataza taasisi binafsi kufanya utafiti, huu wote ni woga wa ukweli.
 
MoseKing,
sawa wewe mwenye akili ya kiulaya ila nimesema "nadhani ni wakati sasa tukiwa tunajadili ni jinsi gani ya kuushinda huu ugonjwa pia tujadili ni jinsi gAni ya kuishi na huu ugonjwa kama ilivyo UKIMWI na malaria."
 
sawa wewe mwenye akili ya kiulaya ila nimesema "nadhani ni wakati sasa tukiwa tunajadili ni jinsi gani ya kuushinda huu ugonjwa pia tujadili ni jinsi gAni ya kuishi na huu ugonjwa kama ilivyo UKIMWI na malaria."

Huyo alisoma ili aje abishane na si kusoma ili aelewe ☹️☹️
 
Kiremba, nakubaliana na wewe mtoa post.
mwisho wa siku watu wajifunze kuishi na hili gonjwa kwa tahadhari huku jitihada za kupata chanjo na tiba zikitiliwa mkazo.

itafika wakati maisha yataendelea ilhaki gonjwa halijaisha maana dunia haiwezi kukubali kusimama kwa muda mrefu usiojulikana kikomo chake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njia sahihi ya kujikinga na huu ugonjwa ni kufuata maelekezo ya wataalamu na kuendelea kuchukua tahadhari zaidi. Ila kwa kuwa sisi waTZ ni wajuaji sanaa, huu ugonjwa hauwezi kutuacha salama.
 
Haonekani kwa macho(invisible)
Habagui na hachagui(democratic)
Hafichiki
Adhaniaye amesimama ajiangalie asije akaanguka
Mdharau mwiba mguu huota tende
Mficha maradhi vifu humuumbua

Ongezea nyingine ..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza walianza na imani kuwa sisi waafrika corona haiwezi kutudhuru.Waliposikia na hatimae kushuhudia vifo,wakaja na maelezo mengine.

Kwamba wazee na wenye kinga dhaifu hasa wenye pressure,kisukari na magonjwa ya moyo ndio watakufa.
Nahisi huenda wameona kuna watu hawa kuwa na magonjwa hayo wameugua na huenda kupoteza maisha.Wengi kama sio sote tumeshuhudia vijana hawakuachwa katika janga hili.Sasa wamekuja na jambo jingine.

Kwamba watu wanene tu ndio wanakufa na corona.Kwa hiyo nawaona watanzania wenye milli midogo wakijiachia kwenye party,vijiweni wakicheza pool table na kunywa kahawa,na kila aina ya shughuli.
Ila ikitokea mtu amekufa,kuna watu wanatoa kashfa na matusi sana kwa watu wanene kwamba hawasikii acha wafe!

Kwa kweli hakuna asiyependa kuishi,ila kumekuwa na tabia ya kujaribu kuingiza hofu kwa makundi ya watu na huku mkijitoa kuwa ninyi hamhusiki na ugonjwa huu na hivyo kuwa na sababu ya kujiachia.

Tumeona ugonjwa huu ambao hata kwa watu waliokuwa wakitumia muda wao mwingi kusali mfano Italia,wamekufa na ugonjwa huu.Tumeona misikiti Saudia imefungwa kwa hofu ya ugonjwa huu.Kwa nini sie watanzania kila siku kutafuta sababu ya kukwepa wajibu wetu?

Mimi nawaomba muwe makini,mchukue tahadhari zote,na hata suala la kujifukuza sio rahisi tu kama ambavyo wengine wanachukulia. Mvuke unaweza kuua.Iwapo utajifukiza maji yakiwa ya moto sana na mvuke mwingi,unaweza kuunguza mapafu.Mwili wa binadamu hauwezi kuhimili joto linalofikia jotoridi nyuzi 100.Niko tayari kukosolewa.

Tuwasikilize wataalamu na tuombe Mungu atunusuru na janga hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Screenshot_2020-05-02-11-13-05.png
 
Kumekuwepo na mapungufu mengi jinsi ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Njia moja ya maambukizi ya ugonjwa huu hatari ni kwa njia ya mate. Wahudumu wote wa mahoteli, mama ntilie wahudumu wa bar hawana kinga yoyote ya kuzuia mate kudondokea kwenye sahani ya ubwabwa, kuanzia mpishi jikoni hadi anapopelekewa mteja. Utakuta wahudumu wanaongea wengine wakiimba nyimbo huku wamebeba chakula bila ya kuvaa barakoa.

Mamlaka husika zilazimishe wahudumu wote kuanzia jikoni kuvaa barakoa.

Walaji hakikisha hotel unayonunua chakula wahudumu wamevaa barakoa, kama hawajavaa waambie ukweli, kisha tafuta hoteli yenye kuuza chakula bila mate ya wahudumu.


CHAKULA.jpg


Mhudumu kama huyu bila barakoa ni hatari, utaishia kula mate ya wahudumu na baada ya kitambo kidogo hospitali ya Amana inakusubiri.
 
Back
Top Bottom