Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19

Maleven

Member
Sep 8, 2019
45
150
 • Uzi huu ni mrefu.
 • Ukichangia naomba ujikite Zaidi katika kutoa maoni yako lakini kukosoa kunaruhusiwa.
Binafsi nadhani maamuzi haya yangechukuliwa mwezi mmoja uliopita pale Waziri Mkuu alipotangaza kuzifunga shule na vyuo, lakini haikuwa hivyo badala yake shule zilifungwa kisha hakukuwa na mpango mkakati madhubuti wa kukabiliana na COVID-19, Zaidi ya makatazo ya kuepuka mikusanyiko na kunawa mikono na maombi. Lakini huu sio muda wa kuendelea kulaumiana zaidi ni wakati wa kupeana mawazo na kushauriana.

Pia bado naamini athari za kiafya kama watakaofariki kutokana na Virusi hivi bado watakuwa wachache kuliko watakaoathirika kutokana na athari za kuwepo ugonjwa huu haswa suala la uchumi na elimu. Hivyo ni lazima kuwe na mpango mkakati wa haswa kuhakikisha kuwa baada ya muda fulani tuwe tumefikia jambo Fulani.

Anyway, binafsi kama ningekuwa na mamlaka ningetumia njia hii kutatua tatizo la hili |Ushauri wangu.

 • Kwanza ni lazima kila mmoja ( Serikali na wananchi kwa ujumla) kuwa na fikra ya kutatua tatizo na siyo kutengeneza faida, waswahili husema hasara roho, pesa makaratasi na zinatafuwa, huu ni wakati wa Serikali na wananchi kujua kuwa nchi iko kwenye vita kubwa sana na inapambana na adui wa ajabu asiyeonekana mwenye madhara lukuki ikiwemo kupoteza maisha na hali mbaya ya uchumi, amapo kama Serikali ni lazima iwe tayari kutumia rasilimali zilizopo katika kunusuru Taifa, rasilimali hizi kama fedha na watu na miundombinu
Nini cha kufanya?

 • Serikali inainishe maeneo ambayo yako hatarishi zaidi katika maambukizi ya virusi vya Corona, naamini yako wazi. Maeneo mengi ya mjini yana muingiliano mkubwa wa watu kutokana na shughuli zao za kiuchumi.

 • Baada ya kuanisha maeneo hayo, viongozi wa mtaa na katika maeneo yalioainishwa wapite wachukue idadi ya watu wote katika mtaa husika wakizingatia mambo yafuatayo:-
  • Idadi ya watu katika nyumba husika (hili nimesikia limefanyika maeneo ya Dar sina uhakika.
  • Hali yao ya kiuchumi
  • Kuchukua mawasiliano wa watu wawili waliopo katika nyumba hiyo na kuacha mawasiliano ya viongozi wawili wa mtaa husika.( namba za simu zenye uhakika).

 • Baada ya hatua ya kuainiasha maeneo na kujua wakazi namba ya wakazi husika na hali zao za kimaisha, Serikali ikishirikiana na wadau, waangize bidhaa muhimu kutoka nje( kwenye upungufu) pia kwa wakati huu Serikali inunue au iongoze vifaa vya kupimia Virusi vya corona Viwepo kwa wingi zaidi visambazwe kila wilaya. Kama nilivyosema huu ni wakati wa kutumia rasilimali tulizonazo katika kupamba na janga hili si wakati wa kuanza kuangalia faida.

 • Hatua ya nne ni Serikali kugawa chakula kwa familia zilizo na uchumi duni ambao hawana uwezo wa kuishi kwa siku ishirini na moja wakiwa ndani. Hatua hii inahitaji unaminifu na uadilifu kwa viongozi wa serikali wanaokadiria hali za kiuchumi za wananchi na pia kwa wananchi ambao watakua wanaeleza uhalisia wa maisha yao ili wasiibebeshe serikali mzingo ambao wanauweza, wasiwakoseshe wale wenye uhitaji na wala wasionewe. Watu wanosihi kijijini wengi chakula wanacho, shida walionayo ni hela ya kusagia mahindi, hela ya sukari chunvi na mafuta ya taa.

 • Hatua ya tano Serikali itangaze lockdown kwa siku ishirini na moja (21) . Hapa wananchi wakiwa tayari wana mahitaji muhimu hasa chakula. Katika kipindi hiki.
  • Serikali itumie vyombo vya usalama katika kuhakikisha watu wanafata utaratibu lakini wawe ni wenye kuelewa kuepuka maafa kama yaliotokea nchi nyingine.
  • Tangazo la kuwa lockdown liwe mapema na watu kufanya maandalizi ikiwa ni pamoja na wale watakao pewa msaada mapema
  • Katoka kipindi hiki cha wiki tatu, kodi za biashara, umeme na maji viwe free kwa ambao luku zao zitaisha basi wasizime, pia wakadirie matumizi ya maji ya wiki tatu wasihesabu katika bili ya maji.
  • Mawasiliano ya karibu ya viogozi wa serikali katika kujua kinachoondelea latika kila kaya, hasa kwa dharura ya wagonjwa na mama wajawazito kuweza kupatiwa uduma.
  • Wale wanaotamulika kama homeless na watoto wa mitaani, watafutiwe sehemu ya kuhifadhiwa( nashauri kwenye walo moja la kambi ya jeshi mana watakua na adabu, au watakapo wekwa wasimamiwe na wanajeshi).
  • Mipaka ifungwe kabisa.

 • Wiki ya pili ya lockdown, yaani siku ya kumi na nne (14), serikali ichukue sampuli ya watu wawili au mmoja kutoka katika kila nyumba, nashauri awe yule anaetoka toka sana( mtafutaji) na yule mtu mzima Zaidi au ambao anaumwa. Lengo na madhumuni ni kua,
  • Kwa kipindi cha wiki mbili kama kama mtu alikua na virusi basi atajulikana.
  • Lengo la kuchukua mtu mzima au yule mgojwa ni kua, mwenye virusi anaweza kua yuko na kinga madhubutu hivyo kwa mtu mzima itasaidia hugundulika mapema.
  • Kuchukua watu wawili au hata mmoja kila nyumba kutasaidia kupunguza utumiaji wa rasilimali katika upimaji. Mfano kama idadi ya watu katika kaya yenye nyumba 300 na watu 2000, then tunapima 300 au 600 (kama wakichukua kila nyumba wawili) badala ya watu 2000.
  • Baada ya kuchukua sampuli kutoka katika kila nyumba, kutegemea na siku watakazo tumia. Kasha nyumba zitakazo kutwa na maambukizi watawekwa katika ungalizi( kutotoka au kuwapeleka katika maeneo maalumu yaliotengwa ) na kui disinfect nyumba.
 • Baada ya kuchukua familia zilizokutwa positive, kutegemea na siku zilizotumika kupima na kupata majibu, na kufanya mapendekezo ya namba saba, the tunaweza kufungua shule na shughuli zikaendelea huku tukiendelea na tahadhali, suala la level seat likendelea, kunawa mikono na uvaaji wa barakoa.

 • Katika kipindi chote hicho , Serikali isisite kufanya utafiti katika jamii mbalimbali kwa asili yao kwa jinsi walivyoweza kupambana na magonjwa ya mfumo wa hela ili kuangalia uwezekano wa tiba mbadala.
Haya ni mawazo yangu ya jinsi ninavyoona jinsi gani ya kuweza kupambana na suala hili.

Amani ya Bwana iwe nanyi wote.


---MICHANGO---

Habari wadau,
Nimeona nianzishe hii mada niliyoipa jina la ushauri wangu kwa Serikali kuhusu ugonjwa wa CORONA au COVID 19( Corona Viruse Diseases of 2019)

Lengo la kuanzisha mada hii kama kichwa cha mada kinavyoeleza ni kuishauri serikali kuhusu ugonjwa huu katika maeneo yote, ikiwemo eneo la Kiuchumi, Kijamii, Kisiasa, Teknolojia n.k

Kuna ushauri umetolewa na watu wengi kuhusu ugonjwa huu ila haujatolewa katika mpangilio mzuri sababu mtu katoa ushauri kwenye mada juu ya mada hivyo inakuwa vigumu kuupata huo ushauri au mawazo hayo vizuri.

Nimeanzisha hii mada, lakini lengo ni kushirikiana na watu wote wa Jamii Forum na Tanzania kwa ujumla, Taasisi zote, Jumuia za serikali na zisizo za serikali, Vyama vya siasa n.k ili kuweza kutoa ushauri na mawazo kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweza kuchukua hatua ili kuokoa Taifa la Tanzania, Afrika na Dunia kwa kwa ujumla, pia kuokoa kizazi chetu kutoka katika huu ugonjwa.

Ningependa niweke angalizo kwamba katika kutoa ushauri au mawazo tuache itikadi za kisiasa, kidini, kikabila n.k bali tutoe ushauri na mawazo kama watoto wa baba na mama mmoja ambae ni Tanzania.

Lengo lingine la hii mada pia ni kuachana na mawazo ya kutegemea wazungu na Asia 100% kama ndio suruhisho la huu ugonjwa, ninajua kwamba Ulaya, Amerika, Asia n.k wameendelea kwenye tiba za kisasa ila tusiwategemee sana kama ndio suruhisho la huu ugonjwa sababu pia hatujui agenda zao za siri kuhusu huu ugonjwa.

Naomba kama moderators wataiacha hii mada iwe inajitegemea ili tuweze kuwa na sehemu maalumu ya kutoa ushauri au mawazo yetu kwa Serikali.

Nitaanza na mimi kwa kutoa ushauri ufuatao

1. Nimeona nchi nyingi zimefunga mipaka na nyingine kwa Afrika kama South Africa, Rwanda n.k wamechukua hatua ya lockdown kwa maana ya kusimamisha shughuli nyingi za wananchi na kuwasisitiza wananchi kutotoka ndani ya nyumba zao, hivyo sababu nasi jana tumepata kifo kimoja cha kwanza kilichotokana na huu ugonjwa
Hivyo nitashauri utaratibu huu wa lockdown sababu inawezekana na sisi hali ikiwa mbaya itabidi serikali isimamishe wananchi kufanya shughuli yeyote.

Kwa hali za kiuchumi za watanzania wengi ni ngumu sana kufanya total lockdown, sababu watakufa au watapata shida kubwa na vitu vingine kama njaa, magonjwa mengi n.k
Hivyo nitashauri Serikali ifanye half lockdown, inawezekana half lock down ni msemo mpya ila katika half lockdown nitashauri serikali ifanye mambo yafuatayo

a. (1)Kupunguza muda wa kazi kwa taasisi zote binafsi na serikali.
Kupunguza masaa ya kazi Kutoka masaa yaliyopo sasa hadi nne, lengo la kupunguza muda wa kazi ni kuwawezesha wafanyakazi kuchelewa kuingia ofisini na kuwawezesha wafanyakazi Kutoka ofisini mapema mfano. Kuingia ofisini saa nne na kutoka saa nane.
Dhumuni la kupunguza muda wa kazi ni kupunguza msongamano wa watu kwenye usafiri sababu hiyo ndio sehemu kubwa ambayo ni rahisi watu wengi kuambukizana huu ugonjwa haraka na ikikumbukwa serikali imetoa tamko kwa daladala kupakia level siti hivyo tabu ya usafiri ni kubwa sana, hivyo kitendo cha kupunguza muda wa kazi kitawawezesha wafanyakazi kusafiri bila pressure za Kuwai usafiri asubuhi au kuchelewa usafiri jioni.

(2) Njia ya pili kuhusu wafanyakazi, serikali inaweza kuanzisha utaratibu wa kufanya kazi kwa shift kama ilivyo hospital, polisi, bandari, TRA kwa baadhi ya department n.k
Lengo ni lile lile kupunguza pressure za usafiri asubuhi na jioni sababu eneo la usafiri ndio eneo ambalo rahisi sana watu kuambukizana
Izingatiwe kuwa tatizo la usafiri limekua kubwa sana asubuhi na jioni kwa karibu mikoa yote Tanzania , serikali imeanzisha utaratibu wa kuziambia daladala ziwe na level siti, ila utekelezaji wake ni hafifu hasa nyakati za jioni na usiku watu wakiwa wengi na traffic police hawapo barabarani.

2. (a)Serikali iweke akiba ya kutosha ya chakula kitakachotosha nchi kwa Miezi sita hadi mwaka sababu, nchi karibu zote duniani zimeathirika na huu ugonjwa hivyo ni ngumu sana kwa nchi moja kutoa msaada kwa nchi nyingine ikiwa kila nchi ina tatizo la njaa

(b) Ikiwezekana serikali ifunge mipaka kuuza mazao ya chakula nje ya nchi, ili kuwezesha nchi kuwa na akiba ya kutosha ya chakula, sababu tunaona jirani zetu Kenya wameshaanza kuchukua hiyo hatua hivyo ni vizuri nasi tukaiga ilo jambo zuri.

3. (a)Serikali kuanzisha utaratibu wa lazima kwa watu wote kuvaa mask ( Barakoa) kwenye mikusanyiko ya watu kama sokoni, kwenye vyombo vya usafiri vya jumuia n.k lengo ni kupunguza maambukizi ya huu ugonjwa kwa njia ya hewa, sababu tumeona hili kosa hata kwa Mheshimiwa Raisi mwenyewe anasalimiana na watu kwa kugonganisha miguu lakini ajavaa mask (barakoa) na wakati huu ugonjwa unaambukiza hata kwa njia ya hewa.

(b) Pia serikali kushauri wananchi kuvaa nguo zinazoficha sehemu kubwa ya mwili hasa suruali na mashati marefu kwa wanaume na wanawake au nguo za aina yeyote zinazoficha sehemu kubwa ya mwili

Karibuni kwa ushauri na mawazo mbalimbali

Sent using Jamii Forums mobile app
Salamu kwenu wanaJF

Hili janga la corona naona Serikali halichukulii kwa uzito unaostahili kwa sababu zifuatazo

Kushindwa kutoa vifaa muhimu Kama Mask, gloves, vipima joto n.k katika taasisi zake mbalimbali.

Hospitali nyingi na vituo vya afya vingi Sana havina hivi vifaa kwa Wafanyakazi wake achilia

Kushindwa kusimamia swala la mikusanyiko isiyokuwa ya lazima. Ukitembea sehemu nyingi Sana utaona bado vijiwe vingi vya kahawa, mabanda ya video bado watu wanajaa bila tahadhali yoyote na Serikali IPO tu, Serikali ya mtaa/ Kijiji au wilaya!!

Mfano wilaya ya Mkuranga Hali Ni mbaya Sana watu wanajaa kwenye vijiwe vya kahawa huku wakiangalia TV na mabanda ya video bado yanajaza watu tu, hii inaonyesha Serikali haiko makini ktk kukabiliana la corona

Misaada imetolewa na makampuni/ watu binafsi kuhusu kusaidia vifaa mbalimbali vya kujikinga na corona lakini mpaka Leo Hakuna tofauti yoyote mtaani kuonyesha misaada hiyo imesaidia jamii mfano mask bado Bei kubwa 2000/= , sabuni Bei juu, sanitizer bado gharama kubwa hii inatoa picha mbaya kwa Serikali pesa za Rostam Aziz 1bilion, pesa za Mwenge n.k hazijaleta msaada kbs kwa watu,

Ushauri wangu kwa Serikali naomba waonyeshe Nia na juhudi ktk kupambana na corona mfano Jiji la Dsm ndo kitovu Cha maambukizi nchi , hapo ndo itasabsbisha mikoa mingine wapate huu ugonjwa, hivyo Serikali ningethibiti mwingiliano wa watu wa Dar na mikoa mingine, wazuie usafiri wa mikoani walau kwa wiki mbili tu,

Marufuku za mikusanyiko ifanyike kwa nguvu ikibidi patrol za polisi au mgambo ili watu waepukane na maambukizi yasiyo ya lazima!!

Mwisho naomba Watanzania wenzangu tujipende sisi na wenzetu pia tuchukue tahadhari Kabla ya hatari!!


House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
Habari Wana JF,

Poleni kwa presha na taharuki ya "UPEPO WA KISULISULI (Corona Virus)" uliolikumba taifa letu pendwa. Tuzidi kumuomba Mungu atuvushe salama.

Tumeonesha uzalendo kwa kuweka "SIASA PEMBENI" na kukaa kusikiliza hali inavyoendelea, hata siasa za maji taka hatuzioni.

Nijikite kwenye mada,

Kama ilivyo tangazwa hapo juzi na Waziri mwenye dhamana (Waziri Wa Afya), kwamba Mtanzania mwenzetu aliyeingia nchini kutokea Belgium mnamo tarehe 15/03/2020, alikuja na "UGENI" uliotikisa taifa letu kwa kishindo (aliyewasili akiwa na maambukizi ya COVID-19).

Ilifuatiwa na taarifa ya mtu mwingine aliyepatikana Kasulu mwenye dalili za kukumbwa na huyu kidume Corona, ambae pia damu imetumwa Dar es Salaam kwa ajili ya vipimo.

Sambamba na Waziri mwenye dhamana visiwani Zanzibar alivyo tangaza leo 18/03/2020 kuna wageni wawili waliotokea nchini German hapo juzi, wameonesha dalili za kuwa na maambukizi ya huyu "PILATO (COVID-19)" alietikisa dunia vikali, na bila huruma. Japo alikiri uhakika bado haujapatikana, damu zimepelekwa Dar es Salaam kwaajili ya vipimo.

USHAURI KWA SERIKALI.

Huu ni ushauri wangu kwa serikali yetu (Hasa kwa Mawaziri wasiofikiria nje ya BOX), na ushauri wangu kwa wanasiasa na viongozi wa dini wote kulifanyia kazi hili swala (kuliunga mkono kwa uwezo wao).

1) Serikali inatakiwa kufanya kazi ya ziada ya kufungua MAABARA" ya kupima Corona Virus kila "MKOA" katika nchi yetu. Sio kua na maabara moja tu Dar Es Salaam.

Hii itasaidia vipimo kufanyika kwa haraka na kupatikana kwa majibu upesi, ili wanaohusika na kudhibiti hili janga huko walipo, waweze kushughulika kwa haraka sana lisisambae kwa raia wengine.

2) Serikali inatakiwa kufunga "MIPAKA NA VIWANJA VYA NDEGE VYA NCHI NZIMA" walio ndani ya nchi wabakie ndani, na walio nje ya nchi wabakie nje, mpaka dunia itakapo tangaza kulipatia "TIBA" hili janga.

Hii itasaidia kuzuia maambukizi kuingia nchini zaidi.

3) Serikali inatakiwa kufunga "MIPAKA YA MIKOA" yote iliopata maambukizi ya hili janga, ili kuzuia maambukizi kuhamia katika mikoa ya jirani na kuweza kudhibiti maambukizi haya.

4) Serikali inapaswa "KUKATAZA KWA MUDA" mikusamyiko yote ndani ya nchi, kuanzia mikisanyiko ya "IBADA (Sala za Ijumaa, Sala za Jumamosi, Sala za Jumapili, Mikusanyiko ya Harusi Na Mazishi/Misiba), mpaka mikusanyiko ya "MINADA (Masoko)" ya mifugo, mazao, nguo na kadhalika.

5) Serikali inatakiwa "KUSIMAMISHA RIBA ZA MIKOPO YOTE" ambayo raia na wafanya biashara wamechukua Bank na Taasisi za Mikopo. Mpaka hili janga litakapoweza kudhibitiwa na biashara kukaa sawa. Raia wataathirika sana kiuchumi kwasababu "RIBA" za mikopo zitakuwa zinaongezeka wakati biashara zimesimama/zimeyumba na faida katika biashara kupungua (kama sio kupata hasara katika biashara).

6) Serikali inatakiwa kutoa maagizo raia wote "WASAMEHEWE KODI YA MIEZI MITATU" za mapango/nyumba kutoka kwa wapangishaji wao, katika "MIKOA YENYE MAAMBUKIZI". Hili litasaidia raia kutokutoka na kuzurura mitaani kutafuta hela ya kulipa kodi. Jambo hili litasaidia raia kutulia ndani na kupunguza harakati, in which maambukizi yatapungua kwa kasi mitaani.

7) Serikali inatakiwa "KUNUNUA CHAKULA" na kuweka "HAZINA" kwaajili ya dharura, pindi masoko na minada itakapofungwa, chakula kitakua cha shida sana, tunaweza kukumbwa na janga lingine la njaa tusipokua makini hasa katika mikoa iliokumbwa/ itakayokumbwa na maambukizi.

8) Serilali kuzuia "PUBLIC TRANSPORT KATIKA MIKOA ILIOAMBUKIZWA" ili kuweza kuzuia maambukizo kwa wengine.

9) Serikali itengeneze utaratibu wa kupulizia dawa za "DISINFECTION" katika "ATM MACHINES" zote katika mikoa ilio athirika na Corona Virus.

10) Rais atoe tamko "BENDERA ISHUSHWE NUSU MLINGOTI NCHI NZIMA NA KILA BALOZI ZA TANZANIA KOTE DUNIANI".

11) Rais atangaze "HALI YA HATARI (State Of Emergency)" kwani hii ni "VITA YA KITAIFA DHIDI YA COVID-19", na ni kweli hii ni hali ya hatari kisawasawa.

12) SERIKALI ISIKILIZE USHAURI NA ICHUKULIE HILI SUALA SERIOUS!

Ushauri wangu

Alexander The Great
Kwanza nitoe pongezi kwa serikali ya JMT kwa juhudi na hatua wanazochukua kwenye kukabiliana na ugonjwa huu wa Covid-19.

Mchango wangu kwa leo utaangazia sekta ya elimu.

Kutokana na kuwa wanafunzi walirudishwa nyumbani ikiwa ni hatua ya kuzuia au kupunguza maambukiki ya ugonjwa huu. Na inavyoonesha kuwa kasi ya maambukizi inazidi kukua.

Sasa je tutahairisha masomo mpaka lini? Na je ugonjwa huu usipopata ufumbuzi mwaka huu ina maana utaratibu wa elimu utasimama mwaka mzima?

Kwa kuangalia inaweza ikawa ngumu kwa wanafunzi kurudi shule kwa sababu alipopatikana mgonjwa wa kwanza shule na vyuo vyote vilifungwa, lakini sasa tunawagonjwa zaidi ya 80 hivyo itakuwa ni ngumu sana kuanza masomo

Lakini serikali ikizingatia mambo flani flani katika uendeshaji wa mfumo wa elimu na mambo yanaweza kuwa 'under control' na wanafunzi wakarudi kuendelea na elimu bila kuleta taharuki zaidi.

Mambo ya kuzingatia ni:-

ELIMU, hapa kwenye elimu serikali na sekta binafsi pamoja na vyombo vya habari wamejitahidi sana,lakini naona bado haitoshi kwa kuwa watu bado hawajajua vyema matumizi ya vifaa tiba na kujikinga zaidi.

Lakini kwa kuwa ninaangazia kwenye suala la elimu basi walimu wakuu wote na wasaidizi wao wapewe semina ya kukabiliana na ugonjwa huo na matumizi sahihi ya vifaa tiba ili na wao wakawape wanafunzi elimu hiyo ili waweze kujihadhari.

Hiyo itasaidia kupunguza maambukizi mfano darasani wanafunzi inabidi wakae wangapi?, kwenye dawati wakae wanafunzi wangapi? Muda wa mapumziko wanafuzi waweze kuangaliwa kwa ukaribu ili 'kumantain distance iliyoamriwa' muda wa kufanya kazi za shule uangalizi uwe mkubwa Nk

VIFAA, pia katika kukabiliana na ugonjwa huu serikali,sekta binafsi na wadau mbalimbali waweze kutoa msaada wa vifaa kwa mashule ili kuweza kusaidia na ugonjwa huo.

Vifaa hivyo ni kama barakoa, sabuni, ndoo za kunawia na maji safi.

WATAALAMU, Pia ingependeza kwenye kila shule wangekuwepo wataalamu wa afya angalau hata wawili, wakiume na wa kike ili kuweza kutoa huduma za afya na elimu kipindi shule au vipindi vinaendelea.

USAFIRI, hii ni mahsusi hasa hapa Dar es alaam ambapo usafiri ni wa shida hivyo utekelezaji wake utakuwa mgumu.
Kutokana na kuwa sasa daladala wanataka 'level seats' hivyo wanafunzi waliozoea kusimama kulingana na kiwango cha hela yao 200/= itawawia ugumu kupata usafiri.

Hivyo wazazi wanaweza wakawaongezea hela ya nauli ili wawe wanakaa kwenye siti kwa kulipa 400/=
Au serikali itoe magari kwenye kila wilaya jijini Dar ambayo yatatoa huduma za usafiri kwa kila wilaya na wanafunzi wachangie kiasi kilichozoeleka cha 200/= ili kutoleta usumbufu na uhaba wa usafiri.

Naamini kwa kufanya hivi tutaweza kuendelea na masomo hata kwa ngazi ya chuo na itapunguza athari kwenye elimu na uchumi wetu kwa ujumla.
Jumapili kama hii watu wengi wamekaa majumbani maduka mitaani yamefungwa.

Ni ushauri wangu kwamba jumapili kama hizi au usiku wa kila siku au usiku wa weekend basi watu wanaohusika na udhibiti wa corona wangepita maeneo ya mikusanyiko kama kariakoo Dsm, Posta, masokoni, nchi nzima wakipuliza madawa ya kudhibiti corona, ili weekdays watu waingie makazini na amani.

Pia maofisi,mabenki, yangetumia muda wa weekend au baada ya kazi kupuliza madawa haya
Ni dhahiri kuwa kwa sasa ugonjwa wa Corona ndio habari ya dunia. Corona imekuwa tishio eneo kubwa la dunia kutokana na kasi yake ya kuenea, madhara yake kwa jamii na tiba yake kutogunduliwa hadi sasa. Ni ugonjwa ambao utaathiri uchumi wa dunia hasa ikizingatiwa kwamba ripoti ya dunia mwaka jana baada ya mkutano uliofanyika Ufaransa ya G7 walisema uchumi unakua kwa asilimia 2.9 na mwaka huu ulikadiriwa kufikia asilimia 3.3 yaani ongezeko la asilimia 0.4.

Hata hivyo Wataalamu wa mambo ya uchumi duniani wanadai kuwa majanga kama mlipuko wa magonjwa ni chanzo kikubwa cha kuzuia kukua kwa uchumi. Wataalamu wanakiri kuwa endapo tiba ya Corona haitatikanika haraka tutegemee mtikikisiko mkubwa wa uchumi duniani.

Ushauri wangu kwa serikali ya Tanzania, pamoja na kuanza kuchukua hatua kali za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu kwa watu wengi basi inapaswa kuchukua hatua zingine kali za kulinda uchumi wa ndani. Mimi siyo mchumi ninatambua wachumi wanaaeza kuja kunipinga kwa hoja, si mbaya. Ombi langu kwa Serikali ni kuwa isitishe miradi yote mikubwa inayoendelea nchini ambayo haina matokeo ya haraka. Ninaamini miradi mikubwa hasa iliyoshikwa na wageni ingesimamishwa kwanza kupisha ugonjwa huu. Hii inawezekana ikasaidia ku save fedha kuliko sasa wakiendelea hizo fedha watazipeleka nchini kwao na tutakosa fedha za kigeni.

Ninaamini Corona si ugonjwa wa Mungu, ni ugonjwa ambao sababu kubwa ni vita ya kiuchumi na vita ya kushindanisha teknolojia. Kuna vita kubwa kati ya mataifa makubwa duniani. Wakati mwingine ili kudhoofisha uchumi wa nchi nyingine yapo mataifa yanaweza kutengeneza magonjwa ili kufifisha uchumi wa Taifa jingine. Siyo siri kuwa kwa sasa China ndiyo nchi inayofanya biashara kubwa duniania. Unapoivuruga China unaivuruga ni Afrika ambayo inategemea bidhaa toka China. Leo hakuna Mwafrika anayekwenda kuchukua bidhaa China na viwanda vya china havizalishi. Kitakachokwenda kutokea ni mfumuko wa bei na bidhaa mhimu kuadimika. Wakati bidhaa zinaadimika kama hatua ya kustisha miradi mikubwa haitachukuliwa baadae nchi inaweza kosa fedha za kuagizia bidhaa mhimu toka nje kwa kuwa itakosa fedha za kigeni.

Historia ni mwalimu mzuri, hatuwezi kuipuuza. Historia inatukumbusha kwamba Dunia ilishawahi kubwa na mdororo wa uchumi mwaka 1929-1939, na ilianza kimzahamzaha tu. Baadae wakajikuta mabenki yanakosa fedha, maduka yanakosa bidhaa, kukakawa Na mfumuko wa bei n.k.

Ninadhani sasa ni busara wakati wanasayansi hasa madakitari wakipambana kugundua tiba basi Wachumi nao waje washauri mambo ya kuyazingatia katika kulinda uchumi wa ndani.
Heri ya pasaka kwa wakristo wote na Watanzania wote kwa ujumla.Nianze kwa kufanya mrejeo wa tamko la wizara ya Afya kupitia waziri wetu Mh.Ummy Mwalimu ya kuwa tujiandae na maambukizi ya ndani kwa ndani,ikiwa kama ndiyo hivyo.Mimi kama mtanzania nashauri yafuatayo ili kuweza kukabiliana na maambukizi hayo
1.Ikiwa kama serikali yetu tayari au tuna vifaa vya kutosha,basi visambazwe kwenye hospital zote,maabara na vituo vyote vya afya serikali na vya binafsi pia kwa idadi maalumu.
2.Mgonjwa yeyote atakayekuwa ameenda sehemu zote hizo kupata huduma za kimatibabu na akiwa na kifua,mafua au kama haelewi anachoumwa basi apimwe Corona tu.
3.Kama wagonjwa hao watapimwa na watakugundulika wana maambukizi au wana Corona basi watengwe kuanzia siku hiyo baada ya kugundulika na kupelekwa kwenye wodi mojawapo katika hospitali katika mkoa husika ambayo itatengwa kwa ajili ya wagonjwa wa Corona.

Nini faida ya hayo yote kwa mtazamo wangu
1.Tutapata kuwajua wagonjwa ambao wana corona na wapo mtaani lakini hawajijui.
2.Tutaweza kudhibiti maambukizi ya ndani kwa ndani kwani wagonjwa waliopatikana watakuwa wameshatengwa sehemu maalumu.
Mimi nimewaza hivyo kama mtanzania mwenzenu.
mazagaone@gmail.com

Mwanasayansi.
Mapendekezo ambayo Mr President anatakiwa kufanya .

1. Kwa kuwa ugonjwa umeshafika kwenye community stage transimission , Ningeshauri ile mikoa ambayo case chache zimepatikana.. kungeagizwa test kits za kutosha ili kubaini ukubwa wa Tatizo, Pili kila anayepatikana positive apelekwe kwenye vituo vya karantini.

2. Kwa kuwa ventilator zime prove low rates healing 50% compare to Hydroxychlotoquine + Zinc , pia ni very expensive .. ningeshauri Tanzania itowe order kwa ndugu zetu wa India Watutengenezee hydroxy Ch.. Zinc mseto mara moja na tutume ndege kwenda kuchukua ili zitumike kwa waliotest positive ..

3. Kiwanda cheti cha pharmaceutical kama kinaweza tengeneza mseto huo basi ni wakati mwafaka wa kufanya hivyo.

4. Kwa wagonjwa wenye mild symptoms na wenye ku prove self karantini waruhusiwe kijitibu Nyumbani.

5. Mabaa na Shughuli zote zamikusanyiko isiyo ya lazima zipigwe marufuku.

6 . Wauza masoko wapunguzwe au wauze kwa zamu.. Kuwepo Na mita 2 toka muuza soko mmmoja mpaka mwingine .

7. Serikali ingize barakoa za kutosha Na kutumia wanajeshi kugawa kwenye maeneo mbalimbali na baada ya week mbili iwe ni marufuku kutembea bila barakoa.

6. Mabasi ya mikoani.. yaagizwe kubeba mtu mmoja kwa siti ya watu wawili.. kupunguza kukaribiana kwa Abiria .

7 . Dalaldala kubeba abiria nusu ya idadi ili abiria wakae kwa nafasi Na zoezi hili lisimamiwe Na jeshi.

8 . Kusiwe Na total Lockdown , watu warujusiwe kufanya kazi , pale maeneo ya kazi yatakapokuwa ni hatarishi, basi eneo hilo tu ndio lifungwe.

9: Stendi za mabasi zisimamiwe Na Jeshi Na wale wapiga debe waondolewe wote kupunguza msongamano usio Na lazima .

10. Hospital maalaum za Korona zisifanye kazi y huduma zingine za kawaida ili kupunguza maambukizi.

11. Ibada ziendelee lakini waumini waingie kwa zamu na kuwepo kwa umbali wa mita 2 toka muhimini mmoja Na mwingine Na Usafi wa kutosha ufanyike kila baada ya Ibada moja kuisha kabla ya kuingia Nyingine.

12. Wanajeshi wapelekwe mtaani ili kuangalia maeneo ya kazi ambayo yataonekana kuwa hatarishi basi yafungwe .

13. Shughuli za kilimo na mifuko ziendelee kama kawaida Na wakulima waelimishwe namna ya kujikinga Na kuweka mita 2 toka mkulima mmoja mpaka mwingine.

14 . Wenye viwanda pia wao observe mita 2 toka mtu mpaka mtu Na uvaaji wa mask.

....
Nikipitia kwenye mitandao mbalimbali, napata picha kuwa inawezekana maambukizi ya COVID-19 hapa nchini yamesambaa zaidi kuliko fahamu zetu za kawaida zinavyotupa taarifa.

Ili kudhibiti kuenea zaidi kwa maambukizi haya, inabidi kasi ya upimaji iongezeke maradufu (mass testing) ili walioambukizwa watambuliwe na kuwa isolated accordingly.

Kuna changamoto kadhaa dhidi ya utekelezaji wa mpango huu, lakini kwa leo tuzipitie hizi kubwa 3:

1) Uwezo mdogo wa serekali kufanya mass testing.
Solution: kama walivyopendekeza wadau kupitia platforms mbalimbali, mipango yote ya maendeleo inayotumia pesa nyingi sana kwa mabilioni na matrilioni (inajulikana) isimame kwa muda kwanza ili resources zote zielekezwe kwenye mapambano dhidi ya COVID-19 ikiwamo kununua/kutengeneza mobile testing kits za kutosha zitakazokuwa zinatembea mtaa kwa mtaa, na ikiwezekana nyumba kwa nyumba.

2) Uwezo mdogo wa serekali kuwa na vituo vya kutosha kuwatunza walioambukizwa wengi kwa mkupuo.
Solution ya changamoto hii ni pamoja na iliyotajwa kwenye # 1 hapo juu lakini pia iliyotajwa kwenye # 3 hapa chini.

3) Wananchi wanaogopa kupima kwa vile wengi wao hawataki kwenda kwenye confinement (isolation) ambako mazingira yake inasemekana siyo rafiki sana kwa sababu zilizo wazi lakini pia uwezekano wa kunyanyapaliwa.
Solution: baada ya kukamilisha upimaji kwenye kila kaya na kukagundulika maambukizi, serekali ijadiliane na kaya husika kama ina uwezo wa kufanya isolation within the premises. Cha msingi serekali ijiridhishe kuwa isolation kwa waathirika pale kwenye kaya ni jambo linalowezekana (kimiundombinu na kiuchumi). Ni wale waathirika ambao kaya wanazotoka haziwezi kuwahudumia hali wakiwa majumbani mwao ndiyo wawe wanapelekwa kwenye government sponsored isolation centres.
Solution hii pia ina address changamoto # 2 hapo juu.

Nihitimishe kwa kusema hivi... bila kujali tofauti ya itikadi au imani miongoni mwetu, Watanzania tulibebe hili tatizo tukiwa pamoja kama familia moja. Tuondoe siasa kabisa kwani hazitatufikisha kokote.

Tukifanya mass testing, itakuwa rahisi sana kama nchi kuwa na mkakati mzuri wa kuhakikisha kuwa maisha ya Watanzania wengi hayapotei kwa upande mmoja lakini pia kwa upande mwingine itakuwa rahisi kujijenga upya kiuchumi kama nchi (post COVID-19) kwani tutakuwa tunajua status ya afya ya nguvu kazi yetu.
USHAURI KWA SERIKALI KUU NA HALMASHAURI ZOTE NCHINI:

Naomba S/kuu na halmashauri zipitishe sheria ndogo ya dharura kwa watu wanaokaidi kunawa au wafanyabiashara ambao hawajaweka vitakasa mikono.

1.changamoto nilizoziona w/biashara wengi wameweka Ndoo lakini hawawasisitizi wateja wao kunawa mikono.

2.baadhi ya wananchi wanadharau (coz hakuna sheria ya kuwabana)

3.Ndoo nyingi na sabuni maeneo mengi vikiisha haviongezwe wanaacha hivyo hivyo.

4.wauzaji na watoa huduma mbalimbali hawana Barakoa za kujikinga na maambukizi.

5.kuna mikusanyiko ya vijana vijiweni isio na lazima.( angalau kuwe na watu wasiozidi watatu eneo moja)

6.sheria izingatie kuwabana wakaidi na kutoa onyo na elimu kwa pamoja.

7.Mwisho: utambuzi wa wageni wanaongia kwenye kitongojini kijiji,kata, wareport kwa viongozi wa vijiji na bwana afya wa kata husika( hii itasaidia hata kupata taarifa sahihi za ufuatiliaji kwa wale watakaokutwa na maambukizi .

Corona inazuilika Tuchukue tahadhari.

BY .ADUI WA CORONA TZ.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kama mmeamua kutuaacha wananchi kila mtu ajihangaikie kivyake, kama chama tu tuna uwezo wa kugawa Tshirt, kofia, khanga, vipeperushi, mabango na posho nchi nzima kipindi cha kampeni. Serikali inashindwa ku-waorganize wafanyabiashara wakubwa na wadau wengine wa afya kushirikiana na serikali tukapata Barakoa bure kabisa kwa kila mwananchi?

Kama mmeshindwa kwa nini msitoe msamaha wa kodi kwa hizi bidhaa ili zipatikane kirahisi kipindi hiki na kwa bei nafuu angalau ya tsh 500? Angalia sasa watu wanakimbilia kusafiri kurudi kijijini bila kupimwa nyie serikali ni kama hampo, siku si nyingi huko vijijini nako ugonjwa unaenda kutapakaa.. Jamani hivi nini kazi yenu?

Hao migambo na polisi mnaoweka kukamata wasiovaa Barakoa ni wa nini wakati upatikanaji wake bado ni kizungumkuti? Gawa kwa watu halafu wakamate wasipovaa, sio kama mnavyotaka kufanya hivi sasa.

Katibu mkuu wangu bashiru saidia kuwashauri hawa watu maana mpaka sasa raia hawajui wafuate lipi Ummy alishawahi kusema wanaotakiwa kuvaa barakoa ni wale waliopatwa na maambukizi tu juzi makonda kasema watu wavae barakoa hata za vitambaa vya khanga, naibu waziri wa afya akatoa kauli bungeni kwamba kuna barakoa maalum kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya corona sio kuvaa yoyote watu hawajui washike lipi?

Kuna video na picha zinatrend mitandaoni zikionesha watu wasio na nia njema wamekusanya barakoa zilizotupwa wanazifua, wanazipiga pasi halafu wanaziuza tena kwa watu jambo ambalo ni hatari kwa afya, wapo wanaovaa barakoa zilizotengenezwa kwa material ya sidiria za mitumba ambapo pia kiafya sio rafiki.

Mko wapi serikali MKO KIMYA:cool:, mnawezaje kukaa siku mbili hadi tatu bila kutoa maelekezo yoyote kipindi hiki,taarifa hazitolewi, tetesi zinaachwa zisambae na kuleta taharuki mitaani

Mmetuacha tujiiendee kama meli isiyokuwa na nahodha, mnajua kwa nini tunawahudumia kila kitu bure na familia zenu kwa malipo ya kodi zetu? Hapa mnacheza sandakarawena maisha yetu.

Viongozi wetu kuweni serious na maisha yetu, ni kama mmewatelekeza watanzania na sasa kila mmoja anapambana kivyake..., angalieni hapo kenya tu serikali inagawa hivi vifaa vyote bure, kwa nini sisi? Jamani
Kwa habari zaidi. soma:

Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga - JamiiForums

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus) - JamiiForums
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,030
2,000
Pitia taarifa za habari za nchi zilizokumbwa na hili tatizo mkuu, ni hatari sana jinsi Corona inavyosambaa kama moto wa nyika. Kuna baadhi ya nchi hata chakula hakuna, watu wamejifungia ndani na vyakula vya miezi kadhaa na hawatoki nje.

Tafakari maisha ya mtu wa kwetu tanzania, anae ishi kwa kiwango cha chini ya "Sh 2,200/= (Under USD 1$)" kwa siku??? Anaweza vipi kujifungia ndani mwezi mzima wakati chakula cha siku moja hana uhakika wa kupata.

Kama mambo gani nliovutia kwangu mkuu?
 

havier jr

Senior Member
Sep 2, 2018
148
250
Acha tulipie uzembe uliosabishwa na serikali toka mwanzo ilishindwa kuonyesha reaction yoyote unashindwa funga mipaka kisa watalii nani bora kati ya mwananchi na mtalii pesa ina thamani kuliko uhai wetu

Nb: Serikali imehusika kwa uzembe ktk hili.
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,030
2,000
acha tulipie uzembe uliosabishwa na serikali toka mwanzo ilishindwa kuonyesha react yoyote unashindw funga mipaka kisa watalii nani bora kati ya mwananchi na mtalii pesa ina thaman kuliko uhai wetu
Nb:serikali imehusika kwa uzembe jtk hili.
Je, uzembe wa kuwa na MAABARA moja tu nchi nzima? Mgonjwa akipatikana Bukoba au sehemu yoyote ya nchi, inabidi damu itumwe Dar halafu wasubiri majibu ya vipimo kwa muda usioeleweka.
 

ngusillo

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
1,068
2,000
Mbona hujashauri serikali kusitisha malipo ya mikopo ya nje pamoja na matumizi ya fedha kwenye miradi inayoendelea?

Ushauri wangu ni kuisitisha miradi yote na kujihami kwa kuweka pesa zote za nchi kwenye mfuko wa tahadhari. Mambo yakirejea normal tutaendelea na ujenzi.
 

Youngstunna

Senior Member
Jul 5, 2016
191
250
Wakuu ,habarini poleni na majukumu poleni pia na hili janga la corona ,kiufupi mimi niseme corona sio tishio kubwa ila limekuwa overrated,

Ebu kumbuka lile janga la dengue ebu assume dengue ingewapata wazungu au wachina wangekuwa katika hali gani?

Katika kufikiri tu mi nadhani hao mabwana wana weak immune system na pia nadhani dengue is more serious than corona.

Kumbuka hata kipindi cha kujenga railway uko marekani walitumia watu weusi maana ngozi nyeupe they are very weak hata malaralia ambayo asilimia kubwa huku kwetu ni kama homa ya kawaida wenzetu wakipata inakuwa tragedy

Yani corona ni ugonjwa ambao unapata nafuu kwa kujitenga mwenyewe ndani ya siku kadhaa !!! Na pia ni ugonjwa ambao unawakumba wazee sana sana 50+

Wanasema watoto na vijana asilimia kubwa wanaweza hata wasioneshe dalili japokuwa ugonjwa huo wanao mimi nadhani ni kwakua tu maambukizi yake niyakasi na haraka ndo maana umepewa promo ila sio janga kubwa kiivyo cha msingi ni kuzingatia kunawa na sabuni mara kwa mara ,kuvaa mask na gloves ,kuepuka misongamano hutaisha fastaa.

images%20(51).jpeg
images%20(50).jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
11,944
2,000
Waafrika tulifahuru hesabu za kurahisisha tu😂
Ngoja zije za kugawa na kutoa hapo tutajua how serious Corona it is!
 

Kalpana

JF-Expert Member
Jun 16, 2017
6,201
2,000
Yani structure za Virus huwa complicated compared na bacteria na amoeba. Sijui ili kututisha? mstructure wa HIV ulikua unaniboa kuchora Advance.
 

Elius W Ndabila

Senior Member
Jul 17, 2019
152
500
Na Elius Ndabila
0768239284

Ni dhahiri kuwa kwa sasa ugonjwa wa Corona ndio habari ya dunia. Corona imekuwa tishio eneo kubwa la dunia kutokana na kasi yake ya kuenea, madhara yake kwa jamii na tiba yake kutogunduliwa hadi sasa. Ni ugonjwa ambao utaathiri uchumi wa dunia hasa ikizingatiwa kwamba ripoti ya dunia mwaka jana baada ya mkutano uliofanyika Ufaransa ya G7 walisema uchumi unakua kwa asilimia 2.9 na mwaka huu ulikadiriwa kufikia asilimia 3.3 yaani ongezeko la asilimia 0.4.

Hata hivyo Wataalamu wa mambo ya uchumi duniani wanadai kuwa majanga kama mlipuko wa magonjwa ni chanzo kikubwa cha kuzuia kukua kwa uchumi. Wataalamu wanakiri kuwa endapo tiba ya Corona haitatikanika haraka tutegemee mtikikisiko mkubwa wa uchumi duniani.

Ushauri wangu kwa serikali ya Tanzania, pamoja na kuanza kuchukua hatua kali za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu kwa watu wengi basi inapaswa kuchukua hatua zingine kali za kulinda uchumi wa ndani. Mimi siyo mchumi ninatambua wachumi wanaaeza kuja kunipinga kwa hoja, si mbaya. Ombi langu kwa Serikali ni kuwa isitishe miradi yote mikubwa inayoendelea nchini ambayo haina matokeo ya haraka. Ninaamini miradi mikubwa hasa iliyoshikwa na wageni ingesimamishwa kwanza kupisha ugonjwa huu. Hii inawezekana ikasaidia ku save fedha kuliko sasa wakiendelea hizo fedha watazipeleka nchini kwao na tutakosa fedha za kigeni.

Ninaamini Corona si ugonjwa wa Mungu, ni ugonjwa ambao sababu kubwa ni vita ya kiuchumi na vita ya kushindanisha teknolojia. Kuna vita kubwa kati ya mataifa makubwa duniani. Wakati mwingine ili kudhoofisha uchumi wa nchi nyingine yapo mataifa yanaweza kutengeneza magonjwa ili kufifisha uchumi wa Taifa jingine. Siyo siri kuwa kwa sasa China ndiyo nchi inayofanya biashara kubwa duniania. Unapoivuruga China unaivuruga ni Afrika ambayo inategemea bidhaa toka China. Leo hakuna Mwafrika anayekwenda kuchukua bidhaa China na viwanda vya china havizalishi. Kitakachokwenda kutokea ni mfumuko wa bei na bidhaa mhimu kuadimika. Wakati bidhaa zinaadimika kama hatua ya kustisha miradi mikubwa haitachukuliwa baadae nchi inaweza kosa fedha za kuagizia bidhaa mhimu toka nje kwa kuwa itakosa fedha za kigeni.

Historia ni mwalimu mzuri, hatuwezi kuipuuza. Historia inatukumbusha kwamba Dunia ilishawahi kubwa na mdororo wa uchumi mwaka 1929-1939, na ilianza kimzahamzaha tu. Baadae wakajikuta mabenki yanakosa fedha, maduka yanakosa bidhaa, kukakawa Na mfumuko wa bei n.k.

Ninadhani sasa ni busara wakati wanasayansi hasa madakitari wakipambana kugundua tiba basi Wachumi nao waje washauri mambo ya kuyazingatia katika kulinda uchumi wa ndani.
 

Al Zagawi

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
2,113
2,000
Na Elius Ndabila
0768239284

Ni dhahiri kuwa kwa sasa ugonjwa wa Corona ndio habari ya dunia. Corona imekuwa tishio eneo kubwa la dunia kutokana na kasi yake ya kuenea, madhara yake kwa jamii na tiba yake kutogunduliwa hadi sasa. Ni ugonjwa ambao utaathiri uchumi wa dunia hasa ikizingatiwa kwamba ripoti ya dunia mwaka jana baada ya mkutano uliofanyika Ufaransa ya G7 walisema uchumi unakua kwa asilimia 2.9 na mwaka huu ulikadiriwa kufikia asilimia 3.3 yaani ongezeko la asilimia 0.4.

Hata hivyo Wataalamu wa mambo ya uchumi duniani wanadai kuwa majanga kama mlipuko wa magonjwa ni chanzo kikubwa cha kuzuia kukua kwa uchumi. Wataalamu wanakiri kuwa endapo tiba ya Corona haitatikanika haraka tutegemee mtikikisiko mkubwa wa uchumi duniani.

Ushauri wangu kwa serikali ya Tanzania, pamoja na kuanza kuchukua hatua kali za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu kwa watu wengi basi inapaswa kuchukua hatua zingine kali za kulinda uchumi wa ndani. Mimi siyo mchumi ninatambua wachumi wanaaeza kuja kunipinga kwa hoja, si mbaya. Ombi langu kwa Serikali ni kuwa isitishe miradi yote mikubwa inayoendelea nchini ambayo haina matokeo ya haraka. Ninaamini miradi mikubwa hasa iliyoshikwa na wageni ingesimamishwa kwanza kupisha ugonjwa huu. Hii inawezekana ikasaidia ku save fedha kuliko sasa wakiendelea hizo fedha watazipeleka nchini kwao na tutakosa fedha za kigeni.

Ninaamini Corona si ugonjwa wa Mungu, ni ugonjwa ambao sababu kubwa ni vita ya kiuchumi na vita ya kushindanisha teknolojia. Kuna vita kubwa kati ya mataifa makubwa duniani. Wakati mwingine ili kudhoofisha uchumi wa nchi nyingine yapo mataifa yanaweza kutengeneza magonjwa ili kufifisha uchumi wa Taifa jingine. Siyo siri kuwa kwa sasa China ndiyo nchi inayofanya biashara kubwa duniania. Unapoivuruga China unaivuruga ni Afrika ambayo inategemea bidhaa toka China. Leo hakuna Mwafrika anayekwenda kuchukua bidhaa China na viwanda vya china havizalishi. Kitakachokwenda kutokea ni mfumuko wa bei na bidhaa mhimu kuadimika. Wakati bidhaa zinaadimika kama hatua ya kustisha miradi mikubwa haitachukuliwa baadae nchi inaweza kosa fedha za kuagizia bidhaa mhimu toka nje kwa kuwa itakosa fedha za kigeni.

Historia ni mwalimu mzuri, hatuwezi kuipuuza. Historia inatukumbusha kwamba Dunia ilishawahi kubwa na mdororo wa uchumi mwaka 1929-1939, na ilianza kimzahamzaha tu. Baadae wakajikuta mabenki yanakosa fedha, maduka yanakosa bidhaa, kukakawa Na mfumuko wa bei n.k.

Ninadhani sasa ni busara wakati wanasayansi hasa madakitari wakipambana kugundua tiba basi Wachumi nao waje washauri mambo ya kuyazingatia katika kulinda uchumi wa ndani.
Umeongea vyema ingawa sidhani kama wanahitaji ushauri wako...

#HAWAPANGIWI

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom