Uchaguzi 2025 Uwe Ni Upigaji Kura Wa Serikali 3 Au 2.

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
17,339
43,270
Mwalimu Nyerere akipinga azimio la Bunge lililopitisha azimio kwa kauli moja kuwa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar uwe wa Serikali 3, alisema kuwa CCM ilienda kwa wananchi wakati wa uchaguzi na ajenda ya kuendelea na Muungano wa Serikali 2. Baada ya kuchaguliwa, kisha Bunge kuamua kwa kauli moja kuunda Serikali 3, itakuwa ni kuwasaliti wananchi waliowachagua wabunge na Rais wakiamini wanaenda kuendeleza muundo wa serikali 2.

Kisha Mwalimu Nyerere akasema,

"Wanaotaka muundo wa serikali 3, wasubiri wakati wa uchaguzi, waende kwa wananchi na agenda ya Serikali 3, wakichaguliwa, warudi waunde Serikali 3".

Kwa maneno ya Mwalimu Nyerere, kuubadilisha muundo wa Muungano siyo dhambi, alimradi wananchi wakubali, siyo kama baadhi ya wanafiki wanaotaka kuwaaminisha watu kuwa kuubadilisha muundo wa Muungano ni dhambi. Kufafanua mapungufu ya muundo wa muungano kama alivyofanya Tundu Lisu ili wananchi wakuunge mkono katika hoja yako, siyo dhambi kama wale wenye upeo duni wanavyodhania. Kwani ili wananchi waweze kukuchagua ili ukabadilishe muundo wa Muungano, ni lazima ufanye kampeni, uifafanue agenda yako, na ukieleweka wananchi wakuunge mkono.

Hoja na vuguvugu la kutaka kuundwa kwa Serikali 3, lilififia kiasi kwa sababu ya majibu ya wananchi waliyoyatoa wakati wa Tume ya Jaji Warioba. Wananchi kutoka pande zote za Muungano, walisema wanataka Muungano wa serikali 3. Wazanzibari wakaongeza kuwa kama Muungano wa Setikali 3 hauwezekani basi kuwepo na Muungano wa mkataba.

Kwa bahati mbaya sana, watu wabaya wasioitakia mema Tanzania, Tanganyika na Zanzibar, waliyapindua na kuyapuuza matakwa ya wananchi.

Kwa vile wahuni wameusaliti umma kwa manufaa yao binafsi, mwaka 2025, uwe ni uchaguzi kati ya serikali 3 au 2. Kila mgombea ajipambanue kwa uwazi kwenye majukwaa ya kampeni kama yeye ni wa serikali 2 au 3. Na wananchi pia tujipambanue kama ni wa serikali 2 au 3. Na kufanya hivyo siyo kosa hata kidogo. Kwa mujibu wa shetia zetu, kosa na kupiga kampeni au kuhamasisha kuvunja Muungano.
 
Back
Top Bottom