Kwa kuwa kiongozi wetu mkuu ameelekeza tupambane na corona huku tukichapa kazi kama kawaida.

Tuzingatie tahadhari zote za kinga tupate na uzoefu wenzetu kinga.
Wazee wetu na wagonjwa wenye upungufu wa kinga tuweke mfumo maalumu kuwakinga.Wengine sisi haitakuwa shida kubwa, ni kama mafua kiasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa uzi please wewe lweli unaishi hapa nchini,hakuna siasa hapa ,LOCKDOWN ndio njia kuu ya kupunguza uambukizi wa hii pandemic,angalia kule ilikoanzia China lile jiji lilikuwa shutdown,halafu unakuja hapa unasupport uongo huu,its so sad our no 1 anafanya masihara,angalia Italy,angalia Rwanda ,Tunisia,Misri ,SA hizi nchi zimechukua hatua madhubuti kukabiliana na ugonjwa huu na marais wao ndio wanasimamia kamati ya kupambana,huwezi ukapiganisha vita wakati jemadari mkuu anakimbizana na wahandisi wakati nchi ipo vitani,mkuu hii kitu sio masihara na kwa faida ya kwako na familia yako kuwa msafi hasa mikono yako(nawa kwa sabuni sio chini ya 20s) na epuka by all cost mikusanyiko ya watu its a contact pandemic.na please my no 1 take charge NOW huu sio wakati wa politics!!
 
Uganda vs dona country!
millardayo_B-BxCnsgqyW.jpeg
millardayo_B-B6p_wglHK.jpeg
_20200322_141105.JPG
 
Si kama nataka kuwa kinyume na Rais wetu kuwa watu tuendekeze woga kwenye suala hili la Ugojwa wa Corona hapana, bali tu nataka watu wakati tukijipa ujasiri wa kuendelea kupambana na ugonjwa huu basi tujaribu kujifunza kwa kina kutoka kwa wale ugojwa huu ulikoanzia pamoja na zile nchi ulikoshika kasi zaidi kama Italia na nchi nyinginezo za Ulaya na hata Marekani yenyewe.

Wakati Corona ilipofikia kilele chake nchini Uchina, nchi za Ulaya na Marekani kama kawaida yao kutokana na nguvu na uwezo wa kiuchumi waliokuwa nao hawakuona umuhimu mkubwa wa kuchukua tahadhari za kiwango cha hali ya juu. Kwa kifupi walifikiria kuwa Corona ingeliweza kuleta maafa makubwa kwa zile nchi tu zilizokuwa na mifumo dhaifu ya kiafya kama nchi za Kiafrika na baadhi ya zile za Asia. Hata Donald Trum mwenyewe akasikika ‘akijimbwambafy’ kuwa Marekani ingeliweza kuishinda vita ya corona mara moja sawa na ifanyavyo katika vita za kawaida za kutumia bunduki na mabomu.

Waitaliano, Waingereza na Wafaransa kama kawaida yao, hasa hasa watu wa kawaida kama sisi(Siyo Serikali) waliendelea kula bata mitaani kama kawaida yao huku wakidumisha utamaduni wao wa UHURU NA HAKI ZA KIBINADAMU wa kutotaka kubanwabanwa au kufungiwa ndani, makarantini nk. Wakati huo wenzao Wachina walishashituka na kama ulivyo mfumo wao mzima wa maisha ya kuheshimu amri toka serikali kuu walitekeleza barabara maagizo ya wakuu wao wa afya jambo lililoharakisha sana kupungua kwa hatari ya janga hili lililokuwa limeonekana kama kiama chao. Kila Mchina aliogopa kupatwa na Corona na kuchukua tahadhari zote kama ilivyotakiwa. Hamna aliyejifanya shujaa wala mwamba kizembe na matokeo yake tumesikia janga linapungua kwa kasi.

Kwa upande mwingine wa shilingi Mataifa ya Ulaya na Marekani baada ya kuiona Uchina ilivyofanya na wao sasa wameanza kuzingatia tahadhari zote ikiwemo si kufunga tu mipaka ya nchi na chi zenye maambukizi bali hata vitongoji, wilaya na mikoa ndani ya nchi zenyewe, hatua ambazo wiki kadhaa nyuma walidhani ni ndoto kwao kuzichukua.

Kwa Upande wetu Watanzania, binafsi naona Serikali yetu inajitahidi sana lakini bado wengi wetu wananchi bado tupo katika hali waliyokuwepo wenzetu wa Ulaya wiki chache zilizopita. Nadhani tunasubiri mpaka ugumu wa tatizo uje utugutushe. Ujasiri aliomaanisha Rais wetu John Magufuli si ule wa kukaa tu na kusema “Corona haitatuweza” bali ni ule wa kusema hivyo huku kila mmoja wetu akichukua hatua stahiki. Ujasiri wetu ulenge zaidi katika mapambano na siyo kwenye kujibweteka tu na kusema “Corona haituwezi” bila kufanya lolote

Serikali pia mimi nadhani ingeenda mbali zaidi na kuzuia wageni hasa kutoka nchi yeyote yenye maambukizi au kuzidisha hatua za karantini kwa watu hao wajapo nchini kwani tumeshuhudia nchi zote zilizopata wagonjwa kwa mara ya kwanza wagojwa walitokea nchi zenye maambukizi. Tusiombe maambukizi yaingie mitaani kama Italia itakuwa vigumu sana kupambana na gonjwa hili ukizingatia hali zetu kiuchumi zilivyo. Tupambane huku shughuli zetu za kiuchumi zikiendelea kwa tahadhari zote.
 
Nimejaribu kuwaza juu ya maisha yetu watanzania tulio wengi, namna ambavyo tunajitafutia riziki zetu za kila siku.

Kama soko la kkoo lingefungwa, masoko mengine yangefungwa pia, kama watu tungeamrishwa kukaa nyumbani,

Machinga wangeishije? Vibarua site wangeishije? Mama lishe je? The majority tungeishije?

Ni kweli Corona ni janga la dunia, tusichukulie poa, tufuate maelekezo tunayopewa na serikali ili kujilinda na kuenea kwake.

Mungu awape hekima viongozi wetu na sisi pia katika kupambana ili tusiangamie lakini pia isifikie hatua ya kutuweka lockdown katika mikoa yetu na mitaa yetu. Ee Mola tuepushe.

Tupige kazi huku tukichukua tahadhali.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa, utepushe na hili janga la Corona.

Mtingi1.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wameshasema jamaa ni jeur, anajimwambafy. Sasa wanasubir tatizo liwe kubwa tuanze kuomba misaada.

Na atakayeumia hapa ni yule yule mnyonge. Wao wameshakimbilia dodoma kujificha.

Nilitegemea jna Rais aseme mkakati alyoweka kupambana na hili janga mfano kuagiza mashine na vifaa vya kupima huu ugonjwa ili ziwekwe kwenye kila zahanati. Hata bashite kamzidi akili katika hili. Bashite kwapamatumain watu wake kuwa kwaagiziavifaa vya kupima ugonjwa.

Jamaa kaomba msaada kwa mbinu ya kuwalazimisha. Subiri baada ya muda wakimpa zile dollari utaona anatangaza watu tujifungie ndani.
 
N
Jamaa kaomba msaada kwa mbinu ya kuwalazimisha. Subiri baada ya muda wakimpa zile dollari utaona anatangaza watu tujifungie ndani.
Ni bora tukamuiga Mseven tusimungunyemungunye maneno kuhofia misaada, hiyo misaada itatoka wapi wakati hata wao wanalia na Corona? Dawa ni kufunga mipaka tu.
 
N

Ni bora tukamuiga Mseven tusimungunyemungunye maneno kuhofia misaada, hiyo misaada itatoka wapi wakati hata wao wanalia na Corona?Dawa ni kufunga mipaka tu
Hizo hizo wanazotumia watugawie na siye. Pia kuna zile zilizuiliwa kwa barua ya Zitto, wakitoa tunafuata mdundo wao, wasipotupatia tunasubiria natural selection.
 
Mimi ombi langu tufunge mipaka kabisa hasa abiria toka nchi zenye ugonjwa.
Tuweke utaratibu wa kufanya mazishi kunapokuwa na misiba.

Sokoni kuwe na utaratibu wa kukaa mbali mbali, soko kama limebana waruhusu biashara kuwekwa hata nje lakini kwenye meza sio chini.

Ibada za kukusanya watu wengi zisitishwe, tuendeshe ibada kwa njia ya television, radio, na mitandao ya internet.
Sadaka watu watume kwa namba za simu au bank.

Vinginevyo kuna watu tutakuja kuonekana manabii bila ya sababu za msingi, maana hili gonjwa litakuja kutufanyia mabaya sana, Mungu atuepushie mbali huo msiba.

Angalia Italia, Spain, na Ufaransa.
Nchi tajiri kama France nao sasa hali tete kiasi kwamba jeshi limeingilia kati kusaidia kusafirisha wagonjwa na marehemu.
 
Mawazo yako ni mazuri mkuu. Japo kwenye suala la kufunga mipaka Bado sikubaliani nalo kwa sasa maana nadhani Bado tunahitaji muingiliano na wenzetu katika kulisukuma gurudumu la maendeleo, inawezekana katika mipaka yetu kuweka vifaa madhubuti vya uchunguzi wa afya. Ili kutoruhusu wagonjwa kuingia nchini, ni mawazo yangu tu.
Mimi ombi langu tufunge mipaka kabisa hasa abiria toka nchi zenye ugonjwa.
Tuweke utaratibu wa kufanya mazishi kunapokuwa na misiba.

Sokoni kuwe na utaratibu wa kukaa mbali mbali, soko kama limebana waruhusu biasha kuwekwa hata nje lakini kwenye meza sio chini.

Ibada za kukusanya watu wengi zisitishwe, tyendeshe ibada kwa njia ya television, radio, na mitandao ya internet.
Sadaka watu watume kwa namba za simu au bank.

Vinginevyo kuna watu tutakuja kuonekana manabii bila ya sababu za msingi, maana hili gonjwa litakuja kutufanyia mabaya sana, Mungu atuepushie mbali huo msiba.

Angalia Italia, Spain, na Ufaransa.
Nchi tajiri kama France nao sasa hali tete kiasi kwamba jeshi limeingilia kati kusaidia kusafirisha wagonjwa na marehemu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnataka wafe wangapi ili mfunge mipaka?
Mawazo yako ni mazuri mkuu. Japo kwenye suala la kufunga mipaka Bado sikubaliani nalo kwa sasa maana nadhani Bado tunahitaji muingiliano na wenzetu katika kulisukuma gurudumu la maendeleo, inawezekana katika mipaka yetu kuweka vifaa madhubuti vya uchunguzi wa afya. Ili kutoruhusu wagonjwa kuingia nchini, ni mawazo yangu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mawazo yako ni mazuri mkuu. Japo kwenye suala la kufunga mipaka Bado sikubaliani nalo kwa sasa maana nadhani Bado tunahitaji muingiliano na wenzetu katika kulisukuma gurudumu la maendeleo, inawezekana katika mipaka yetu kuweka vifaa madhubuti vya uchunguzi wa afya. Ili kutoruhusu wagonjwa kuingia nchini, ni mawazo yangu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hivyo wewe unaamini sisi ndio tunaweza kuweka vifaa vizuri vya uchunguzi wa afya kuliko Marekani, Ufaransa, Italia, Spain na Uingereza?

Kwanini wale hali imekuwa vile na vifaa vyao vyote?
Subiri huo muingiliano na wenzetu utatupa majibu karibu, tena nasema umeshaanza kutupa majibu.
Si tulikuwa na wagonjwa sita mara siku mbili tatu wakafika 12, na wengi wao ndio wametokana na huo muingiliano unaotaka tuendelee nao.
 
Back
Top Bottom