Serikali imekusudia kuboresha Mradi wa Mwendokasi DSM, Watu watapaki magari na kutumia Mwendo Kasi

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI- Mohamed Mchengerwa amesema Serikali inatambua changamoto za mradi huu.

Ameahidi mpaka ifikapo Mwezi September-Oktoba 2024 matatizo yote yatakuwa yamekwisha na kilio cha Wana Dar Es Salaam juu ya changamoto za mradi huu kitakuwa historia.

1. Serikali itaongeza mabasi mapya zaidi ya 170 kuweza kudumia DSM yote.

2. Uzembe wa Madereva na Wafanyakazi wengine wa mabasi haya muarobaini umepatikana, Mh. Mchengerwa anasema madereva wote ambao huwa hawasimami kuchukua watu na magari hayana abiria kudhibitiwa vitali, wale wahudumu wenye lugha chafu na kupiga abiria kiama chao kimefika.

3. Serikali inakusudia kuboresha nakurekebisha miundo mbinu iliyoharibika katika vituo vya mwendokasi.

N.B. Ni jambo la kujivunia kuona Serikali ya awamu ya sita imeamua law dhati kuboresha usafiri wa mwendo kasi, ni furaha kuona Serikali ina taka kupeleka usafiri huu kwenye majiji.

Kwa watu wa Dar Es Salaam tunaotumia usafiri huu tutafarijika saana, ni usafiri salama na wa haraka, kinachotesa

1. Kusubiri muda mrefu kupanga foleni kupata tiketi. Pengine ni muda muafaka kuweza kulipia online kwa malipo ya mwezi, wiki, etc- kama kuna app ya Farasi inawezekana kukawa na app ya UDART na malipo yakafanyika direct.

2. Kusubiri Magari ya njia fulani yafike wakati kituoni Kuna magari ambapo supervisor wa vituo wangeweza saidia kuwaokolea watu muda na kuwahi katika shughuli za kujenga Taifa kwa kuruhusu mabasi yaliyopo.

3. Baadaye inaweza kujengwa hata viti kuboresha sehemu hizi za vituo.

4. Kwa juzingatia Idadi na hali ya hewa ya Dar Es Salaam ni vizuri mabasi haya yote yawe na AC.

5. Kujengwe njia za chuma kuhakikisha watu wasio fuata utaratibu wa foleni hawavamii gari likifika na kuwasumbua watu wanaofuata utaratibu wa FIFO

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mungu ibariki Tanzania
 
Screenshot_2024-03-19-13-09-19-1.png
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI- Mohamed Mchengerwa amesema Serikali inatambua changamoto za mradi huu.

Ameahidi mpaka ifikapo Mwezi September-Oktoba 2024 matatizo yote yatakuwa yamekwisha na kilio cha Wana Dar Es Salaam juu ya changamoto za mradi huu kitakuwa historia.

1. Serikali itaongeza mabasi mapya zaidi ya 170 kuweza kudumia DSM yote.

2. Uzembe wa Madereva na Wafanyakazi wengine wa mabasi haya muarobaini umepatikana, Mh. Mchengerwa anasema madereva wote ambao huwa hawasimami kuchukua watu na magari hayana abiria kudhibitiwa vitali, wale wahudumu wenye lugha chafu na kupiga abiria kiama chao kimefika.

3. Serikali inakusudia kuboresha nakurekebisha miundo mbinu iliyoharibika katika vituo vya mwendokasi.

N.B. Ni jambo la kujivunia kuona Serikali ya awamu ya sita imeamua law dhati kuboresha usafiri wa mwendo kasi, ni furaha kuona Serikali ina taka kupeleka usafiri huu kwenye majiji.

Kwa watu wa Dar Es Salaam tunaotumia usafiri huu tutafarijika saana, ni usafiri salama na wa haraka, kinachotesa

1. Kusubiri muda mrefu kupanga foleni kupata tiketi. Pengine ni muda muafaka kuweza kulipia online kwa malipo ya mwezi, wiki, etc- kama kuna app ya Farasi inawezekana kukawa na app ya UDART na malipo yakafanyika direct.

2. Kusubiri Magari ya njia fulani yafike wakati kituoni Kuna magari ambapo supervisor wa vituo wangeweza saidia kuwaokolea watu muda na kuwahi katika shughuli za kujenga Taifa kwa kuruhusu mabasi yaliyopo.

3. Baadaye inaweza kujengwa hata viti kuboresha sehemu hizi za vituo.

4. Kwa juzingatia Idadi na hali ya hewa ya Dar Es Salaam ni vizuri mabasi haya yote yawe na AC.

Hongera saaana MMK kwa kuamua kuhakikisha huduma ya mabasi yaendayo kasi inakuwa bora na Watanzania waweze kujivunia kwa kupata huduma bora na za kiwango cha juu.

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania.
Maneno mengi tatizo lipo kwenye usimamizi!
 
Back
Top Bottom