Jumapili kama hii watu wengi wamekaa majumbani maduka mitaani yamefungwa.

Ni ushauri wangu kwamba jumapili kama hizi au usiku wa kila siku au usiku wa weekend basi watu wanaohusika na udhibiti wa corona wangepita maeneo ya mikusanyiko kama kariakoo Dsm, Posta, masokoni, nchi nzima wakipuliza madawa ya kudhibiti corona, ili weekdays watu waingie makazini na amani.

Pia maofisi,mabenki, yangetumia muda wa weekend au baada ya kazi kupuliza madawa haya
 
Yaani leo nimeona watu wengi kinoma kanisani. Dah. Raia wabishi aisee.
 
Tangu ugonjwa wa Corona alimaarufu Covid-19 uanze kutangazwa nilikuwa sijaufuatilia kiundani!

Nilishtuka na kuanza kuufuatilia baada ya watoto wangu waliokuwa boarding schools kuwa wamerudi baada ya serikali kufunga shule kwa dharura.

Pamoja na serikali kuchukua hatua madhubuti hapo awali, naona kwa athar za ugonjwa huu na unavyoenea baado hatua zaidi zinahitajika.

Dharura inayotakiwa ni kama Nchi ya Rwanda walivyofanya, watu na watumishi wa umma watakiwa wabaki nyumbani, masoko yafungwe, usafiri usitishwe, mipaka ifungwe.

Nionavyo kuzuia Ni rahisi kuliko kutibu. Nimeangalia makala moja ikionesha Italy, Rais wa nchi analia watu wake 4000, wamekufa, mapadri 29 wamekufa kwa Corona, ugonjwa ulipoanza hawakuwa serious hivyohivyo kwa Spain na Iran.

Wamekuja kugundua watu wameshachangamana muda.Viongoz wa dini wasitishe ibada, watu wazuiliwe kutoka kama hakuna ulazima, tufanye kama Rwanda.

Tusifanye maigizo wala tusihurumie raia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna ugonjwa hapo.....hasahasa kwetu sisi waafrika
Kuwa na akiba ya maneno na ujifunze kuchuja maneno ya kutoa hadharani na kuyaacha nafsini. Watu wanateseka, wengine wanakufa ,kilio kila mahali lakini hujali labda mpaka familia yako wakiugua au kufariki ndio utapata akili.
 
Mshauri pia na polepole kwa maneno haya haya, na ulete ushahidi hapa ukienda kuchukua buku7.
 
Imagine nchi kama Uganda hakuna corona mseven kapiga stop, sheria nilianza kazi Jana sisi kwetu sijui nini shida.sidhani kipima watu airport inatosha.

Maskini Italy😢😢😢
 
Serikali iziagize mamlaka zote za maji zipunguze gharama za maji japo kwa 50% ili kuunga mkono harakati za kudhibiti COVID-19.

Tumeshuhudia matumizi ya maji yakiwa maradufu katika usafi, hivyo tusiwaongezee wananchi gharama ama kuwa fanya wabane matumizi huku wakihatarisha na maambukizi ya Corona.

Hii iende hadi kwa viwanda vya maji, wao pia wapunguze bei.

Mkibisha tutampelekea Rais Magufuli, kitakacho wakuta msiseme mzee anawaonea.

Tuitokomeze Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app

Updates:

Naibu waziri Mh. Juma Aweso awaonya mameneja wa mamlaka za maji kutumia shida hii ya corona kuwabambikia wananchi bill.

Awaonya pia kutokukata maji kwa namna yeyote.

Source...clouds fm

Leo pia ni maadhimisho ya wiki ya maji.

Lakini pia ni siku ya kuzaliwa Mh naibu waziri wa maji Ndugu Juma Aweso.

Happy birthday comrade! Waambie washushe na bei ya maji japo kwa miezi 3 tu.
 
Watu wahimizwe kuvaa mask kwenye mikusanyiko na kunawa mikono mara kwa mara
 
Kwanza Hio dawa ipo?

Huku mtaa wa saba kutoka chato mask tu kichekesho.ukivaa kila mmoja macho kodo kwako wakidhani umeshaikwaa corona
 
Jumapili kama hii watu wengi wamekaa majumbani maduka mitaani yamefungwa.

Ni ushauri wangu kwamba jumapili kama hizi au usiku wa kila siku au usiku wa weekend basi watu wanaohusika na udhibiti wa corona wangepita maeneo ya mikusanyiko kama kariakoo Dsm, Posta, masokoni, nchi nzima wakipuliza madawa ya kudhibiti corona, ili weekdays watu waingie makazini na amani.

Pia maofisi,mabenki, yangetumia muda wa weekend au baada ya kazi kupuliza madawa haya
Kwahioo WAFE JTATU-JMOSI
LOH
 
Back
Top Bottom