Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
5,754
2,000
Bikra ni alama ya uaminifu na baraka kwa kizazi chako

Habarini Wakuu.

Naweza kuwa tofauti na wengi, Naweza nisiungwe mkono na wengi hasa wale waliooa na walioolewa. Lakini ninachojaribu kueleza hapa ni suala lenye manufaa kwa familia, jamii, taifa na dunia kwa ujumla. ni suala litakalo iweka dunia salama hasa katika kipengele cha mahusiano ndani ya ndoa.

Haijalishi tulikosea wapi na kujikwaa wapi. Makosa tuliyoyafanya tuhakikishe hayajitokezi kwa wana na binti zetu. Ili familia zetu ziweze kuwa bora na zenye baraka kwa Mungu.

Bikra ni alama aliyopewa mwanamke kuthibitisha kuwa hajaguswa na mwanaume. Kwa nini Mwanamke apewe alama hii? Nitakupa mfano, Ukienda kununua kitu dukani kuna alama fulani huwekwa katika kitu husika ikiashiria kitu hicho ni kipya. Ndivyo ilivyo kwa mwanamke, bikra ni uthibitisho namba moja kuonyesha mwanamke husika ni kigoli, mwanawali na ambaye hajaguswa. Mwanaume hajapewa alama hii kwani yeye hayupo kwaajili ya mwanamke bali mwanamke kwaajili ya mwanaume. Hivyo ni kusema mwanaume ndiye mwenye wajibu wakumtafuta mwanamke kama bidhaa yenye thamani kushinda zote duniani.

Ili ndoa zetu zidumu lazima jambo hili lizingatiwe. Watu wengi wanachukulia ni jambo jepesi lakini athari zake zinaonekana. Usishangae kusikia watu kudhihakiana kwa majina elfu. Mara kibamia, sijui Bwawa haya yote ni matokeo ya kuoa wanawake wasio bikra.

Tuje kwenye maandiko;
Kumbukumbu la torati 22:
13 Mtu akitwaa mke, akamwingilia na kumchukia,
14 kisha akamshitaki mambo ya aibu kumzushia jina baya, akasema, Nimemtwaa mwanamke huyu, nami nilipomkaribia sikuona kwake alama za ubikira;
15 ndipo babaye yule kijana na mamaye watakapotwaa alama za yule kijana za ubikira, wawatolee wazee wa mji langoni;
16 na baba yake yule kijana awaambie wazee, Mwanamume huyu nilimpa binti yangu awe mkewe, naye amchukia;
17 angalieni, amemwekea mambo ya aibu, asema, Sikuona kwa binti yako alama za ubikira, nazo hizi ndizo alama za binti yangu za ubikira. Na wayakunjue yale mavazi mbele ya wazee wa mji.
18 Basi wazee wa mji ule na wamtwae yule mtu mume na kumrudi,
19 wamtoze shekeli mia za fedha, wampe babaye yule kijana, kwa kuwa amemzulia jina baya mwanamwali wa Israeli; naye awe mkewe; hana ruhusa ya kumwacha siku zake zote.
20 Lakini likiwa ni kweli neno hili, la kutoonekana kwake yule kijana alama za ubikira;
21 na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na waume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Aya hizo zinaonyesha jinsi gani Bikra ilivyomuhimu kwa watu makini. Mwanamke asiye na alama za ubikira humdhalilisha Baba yake kwani inatafsirika alifanya ukahaba katika nyumba ya baba yake. Au huenda Baba yake ndiye aliyembikiri.
Pia hufanya familia husika kuonekana ni familia ya kikahaba na uzinifu jambo ambalo ni aibu kwa familia na ukoo kwa ujumla.

Aya hizo pia zinaonyesha kuwa mwanaume anayohaki ya kudai bikira kwa mke wake endapo hajaikuta. Jambo ambalo kwa ulimwengu wa sasa wanawake wengi wasingeolewa na kuishia kuwa makahaba wa mjini.

mambo ya walawi 21
13 Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake.
14 Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe.
15 Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi Bwana nimtakasaye.

Aya hizo zinamhusu mtu yeyote makini, mwenye kumcha Mungu, anayetaka utakatifu na anayetaka ukoo na kizazi chake kiwe kitakatifu.

Ili familia isiwe najisi basi lazima mwanaume aoe mwanamke Bikra, Asioe mjane au mwanamke aliyeachwa na mtu mwingine au kuokota wanawake kwenye mabaa. Lengo ni kutokitia kizazi chake unajisi.

Kutokana na shetani kutamalaki, watu siku hizi huokota okota tuu wanawake popote. Wengine huokotana Baa na kwenye kumbi za starehe. Wengine huenda kabisa kwenye madanguro na kujichukulia wake ilimradi tuu. Watu wa namna hii hukutwa na madhila makubwa ndani ya ndoa. Kama si kuzaa watoto mashoga,basi ni wasagaji. Kama si wasagaji hupata watoto malaya na makahaba. Ni rahisi watoto kuzalia nyumbani kwani Baba na mama ni wale wale tuu.

Hapo hapo utasikia mwanaume anakibamia au hana nguvu za kiume. Au mke wangu ana K kubwa au sio mtamu. Ulijuaje mkeo sio mtamu kama hukuwahi onja vya nje.

Mwenye jukumu la kulinda bikra ya mtoto ni nani?
Jibu ni moja, Ni mzazi.
Wazazi ndio watu pekee wenye jukumu la kuilinda bikra ya mtoto wao. Changamoto inatokea pale endapo Mama hakuweza kulinda bikra yake sembuse ya mtoto. Baba naye aliuziwa mbuzi kwenye gunia hawezi kuwa na muda huo.

Lutu alikuwa ni mzazi wa kiume lakini aliweza kujua kuwa mabinti zake ni bikra. Utajiuliza alijuaje. Ni rahisi kwa Baba mwenye kujali familia yake kujua kinachoendelea kwa watoto wake. Lakini wababa wazembe na wanaoaibisha ubaba wao huuliza maswali yakijinga kama Mimi ni Baba nitawezaje kulinda bikra ya binti yangu. Jibu ni kuwa huwezi ikiwa mwenyewe ulichukua mtu asiye na bikra.

Kwa upande wa wachungaji, maaskofu na mapastor. Hii kwao ni moja ya sheria kubwa na muhimu. Mchungaji hawezi kukamilika ikiwa amechukua vitu vya mtumba. Ndio maana baadhi ya Wachungaji wa siku hizi wapo wapo tuu. Hawana tofauti na watu wa mitaani.
mambo ya walawi 21
13 Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake.
14 Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe.
15 Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi Bwana nimtakasaye.

Nawasilisha.

Nakaribisha hoja na mapovu yenye hoja pia. Hoja zijikite kwenye maandiko ya kwenye biblia.

==============

Kwa nini maaskofu/ wachungaji hawaoi bikra; Je, wameasi kanuni zao?

Habari wakuu.

Mada hii ni ngumu kidogo na inagusa watu muhimu kwenye jamii. kitu pekee nitakachokihitaji toka kwa wataonipinga na nukuu na aya kutoka kwenye Biblia.

Askofu/Mchungaji au kuhani yeyote aliyepakwa mafuta moja ya masharti yatakayomfanya atimie ni pamoja na kuoa mwanamwali yaani bikra na tena kuoa mke mmoja. Jambo hili ni kiashiria cha usafi na utakatifu kwa mtumishi wa Mungu. Sijui kwa nini jambo hili halizingatiwi ndio maana siajabu watumishi wengi wa Mungu hata waombe kwa kujirusha na kujikata kata lakini maombi yao hayajibiwi kutokana na kutofuata taratibu za kikuhani.

Siwalaumu wale wanaoenda kuombewa na watumishi hawa wasiofuata sheria za kikuhani.

Zifuatazo ni nukuu kutoka kwenye Biblia Zinazoonyesha kuwa mtumishi wa Mungu(Waliolengwa zaidi ni makuhani, wachungaji, Maaskofu n.k) kuwa wasioe mtu asiye bikra, mjane, kahaba wala aliyeachwa na mumewe.

Mambo ya walawi 21:
13 Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake.
14 Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe.
15 Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi Bwana nimtakasaye.

Mambo ya walawi 21;
7 Wasimwoe mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake.

Ezekiel 44;
22 Wala hawataoa wanawake wajane, wala mwanamke aliyeachwa na mume wake; lakini watatwaa mabikira wa wazao wa nyumba ya Israeli, au mjane aliyefiwa na mumewe kuhani.
23 Nao watawafundisha watu wangu tofauti iliyopo kati ya vitu vitakatifu na vitu vya sikuzote, na kuwafundisha kupambanua kati ya yaliyo machafu na yaliyo safi.

Karibuni kwa mjadala nipo tayari kwa mafundisho lakini sitaki maneno matupu bali nahitaji Aya na nukuu kutoka kwenye Bible.

===============

Somo Muhimu la Kuhusu Bikra

Wakuu Kwema!

SOMO MAALUM LA BIKRA

UTANGULIZI
Nimeona niandike humu Somo hili kwa Lengo la kuelimisha kizazi cha sasa, hasa Vijana. Siku za hivi karibuni kumezuka mjadala mkubwa sana kuhusu umuhimu wa ubikira katika imani na jamii kwa ujumla, wote tunafahamu kuwa Maandiko katika Agano la kale na Agano jipya na hata tamaduni kwa ujumla yalisisitiza sana umuhimu wa kuoa mwanamke bikira!, Mila nyingi na tamaduni nyingi pia zinathamini sana umuhimu wa mume kuoa au kupata mwanamke Bikira, Bikira ni nini na ina umuhimu gani kiimani? Je kuna ulazima wa kuoa mwanamke Bikira?
\
Kwa nini Mungu aliiweka bikira na kwa nini alisisitiza mwanamwali kuolewa bikira kuna jambo gani katika ulimwengu wa kiroho kuhusu ubikira, je kuoa mwanamke ambaye hakuwa na bikira kuna faida gani au hasara gani? Maswala haya yote yote yanatufikisha mahali hapa ambapo tunapaswa kuliangalia swala hili kwa kina na mapana na marefu.


Mabinti Bikira Uko Afrika ya Kusini hupewa uthamani mkubwa sana katika tamaduni zao

Maana ya Neno Bikira kimaandiko!
Kwa mujibu wa tafasiri za Agano la kale neno bikira lilitumika kumaanisha Mwanamwali yaani mwanamke kijana asiyejua Mume au ambaye hajawahi kushiriki tendo la Ndoa, na kuna maneno kadhaa ya kiebrania yaliyotumika kuwataja wanawake hao, yaani BETULAH mwanamwali bikira asiyejua mwanaume au ambaye hajaingiliwa na uume bado kwa kiarabu BATULI, na BAHUR mwanamke au mwanamwali kijana na ALMAH mwanamwali bikira aliyetolewa mahari au ambaye yuko karibu kuolewa, Almah pia ilitumika kumaanisha mwanamke safi ambaye hakuna maswali katika kuthibitisha usafi wake.

Neno hili ALMAH ndilo analolitumia Isaya Nabii katika Unabii unaohusu Mwanamwali atakayemzaa Masihi Isaya 7: 14. “Tazama Bikira (ALMAH) atachukua Mimba!.” Kwa hiyo kibiblia hii ilikuwa ndio maana ya neno Bikira. Hata hivyo Neno la Mungu lilikuwa na maana ya ndani zaidi kama tutakavyoiona baadaye.

Umuhimu wa Ubikira katika Ndoa.
Ni ukweli usiopingika kabisa kuwa kwa mujibu wa mafundisho ya kibiblia yaani Agano la kale na Agano jipya na katika mtazamo wa Mungu, Ndoa ilithibitika kuwa ni halali na takatifu endapo alama za ubikira zingeonekana katika tendo la kwanza la ndoa, Damu ambayo ingemwagika kwa mara ya kwanza ingeweza kuthibitisha kuwa mwanamke huyu ameingiliwa kwa mara ya kwanza, Damu hii ilihusianishwa kama damu ya agano lililo wazi kabisa kuwa ndoa hiyo ni ya halali na ni safi na kwa mume na kwa sababu hiyo huyo ndio angekuwa mkeo halali na mwenye kumuingilia ndio mmiliki halali wa Mume huyo

Walawi 21: 1,7 Biblia inasema hivi “ Kisha Bwana akamwambia Musa Nena na hao makuhani wana wa Haruni kuwaambia, Mtu ASIJINAJISI……. Wasimumwoe mwanamke aliye Kahaba, au huyo aliye mwenye UNAJISI, wala wasimuoe mwanamke aliyeachwa na mumewe: kwa kuwa yeye ni kuhani ni mtakatifu kwa bwana Mungu wake” ni wazi kuwa hapa BIBLIA iliwakatza Makuhani kuoa wanawake wenye UNAJISI yaani ambao sio safi yaani ambao wameshabikiriwa hivyo kwa ufupi walitakiwa kuoa mwanamke Bikira! Yaani ASIYENAJISIWA!

Ubikira katika agano la kale na wakati wa sheria uliinua sana thamani ya mwanamke, licha ya kuweko kwa mahari maalumu (Waebrania waliita Mohar Betulot) kiarabu (Mahar al Batul) sawa na “bride price for virgin” Mahari maalumu ya Ubikira, kwa sababu ya kukutwa Bikira, heshima kwa wazazi kwa matunzo mazuri ya binti yao, heshima kwa binti kwa kujitunza lakini pia ilithibitisha uwezo na kiwango cha juu cha uadilifu.

Katika Torati ya Musa mwanaume alipolala na mwanamwali aliyeposwa “ALMAH” na kuharibu uanawali wake alitakiwa kumuoa yeye, na kama Baba yake angekataa asimuoze binti yake kwa mtu aliyembikiri, mwanaume huyo alipaswa kulipa mahari sawa tu na ile ya muoaji wa mwanamke Bikira “Kutoka 22:16-17

Kama mwanamume angembaka mwanamke Bikira alipaswa kwa mujibu wa torati kulipa shekel 50 sawa na mahari ya mwanamwali bikira na alilazimika kumuoa na hakupaswa kumuacha maisha yake yote Kumbukumbu 22:28-29
Kumbukumbu 22: 13-22
Biblia inasema hivi “13.Mtu akitwaa mke, akamwingilia na kumchukia, 14. kisha akamshitaki mambo ya aibu kumzushia jina baya, akasema, Nimemtwaa mwanamke huyu, nami nilipomkaribia sikuona kwake alama za ubikira; 15. ndipo babaye yule kijana na mamaye watakapotwaa alama za yule kijana za ubikira, wawatolee wazee wa mji langoni; 16. na baba yake yule kijana awaambie wazee, Mwanamume huyu nilimpa binti yangu awe mkewe, naye amchukia; 17. angalieni, amemwekea mambo ya aibu, asema, Sikuona kwa binti yako alama za ubikira, nazo hizi ndizo alama za binti yangu za ubikira.

Na wayakunjue yale mavazi mbele ya wazee wa mji. 18. Basi wazee wa mji ule na wamtwae yule mtu mume na kumrudi, 19. wamtoze shekeli mia za fedha, wampe babaye yule kijana, kwa kuwa amemzulia jina baya mwanamwali wa Israeli; naye awe mkewe; hana ruhusa ya kumwacha siku zake zote. 20. Lakini likiwa ni kweli neno hili, la kutoonekana kwake yule kijana alama za ubikira; 21. na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na waume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Kupoteza ubikira kungegharimu adhabu ya kifo kwa kijana wa kike na, kuondoa bikira ya mwanamwali kulilazimu kulipa mahari na kumuao hii ilikuwa sheria nzima ya uanawali au ubikira katika agano la kale au torati ya Musa

Katika agano jipya pia mwanzoni Ubikira ulichukuliwa kuwa ni sehemu ya Maisha ya kujitoa na kumtumikia Mungu, mtu alipaswa kuishi maisha ya uanawali siku zote za maisha yake ni hii ingekuwa ni sadaka Sacrifice kuwa ameyatoa maisha yake kwa Yesu na hataki kuruhusu Unajisi katika maisha yake hivyo wazee wengi nyakati za Kanisa la kwanza waliwatunza binti zao, wasiolewe waishi maisha ya kumtumikia Mungu, jambo hili lilifanywa kwa usimamizi wa mzazi vilevile kama ilivyokuwa katika agano la Kale kwa vile kama binti angenajisiwa au kubikiriwa aibu ingekuwa kwa familia nzima, lakini ingekuwaje sasa kama binti anajisikia kutaka kuolewa Paulo mtume akashauri

1Wakoritho 7: 8-9 Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane Ni heri wakae Kama mimi nilivyo, Lakini kama hawawezi kujizuia na waoe; maana ni afhadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa”
1Wakoritho 7: 25-28 “ Kwa habari za wanawali sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za Bwana kuwa mwaminifu. Basi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo. Je! Umefungwa kwa mke? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? Usitafute mke. Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.

Wanawali wanaotajwa hapo ni vijana wa kike walio bikira kwamba kwa mujibu wa Paulo kama wanaamua kujitoa na kuishi maisha hayo ya utawa ni vema na kama wanaamua kuolewa hawana hatia yaani sio dhambi
Kwa hiyo katika falsafa za agano jipya kuishi maisha ya ubikira ilikuwa ni aina ya sadaka Sacrifice ambayo madada wengi wanaishi maisha ya utawa hulazimika kuwa bikira na hawasumbuki katika maisha yao kwa vile hawajui lolote HAWAJANAJISIKA!.

Umuhimu wa Ubikira kwa mujibu wa Tamaduni za kiyahudi.
Kwa mujibu wa tamaduni za Kiyahudi na katika vitabu vya tamaduni zao vijulikanavyo kama Talmud, Halakhah na Hagadah Marabi wakuu kama Gamaliel na Eliezer na Joshua bin Hananiah wanatoa maoni yao kuwa kulikuweko na utata kadhaa katika kuziangalia alama za ubikira kwani wakati mwingine alama za Damu hazikuonekana kabisa katika harusi kadhaa huku kikiwa na uhakika kuwa mabinti hao walikuwa safi na hawakuwa wamenajisiwa ugumu wa uume kuingia katika uke ulionekana na ulisumbua katika hatua za awali za ndoa au tendo la ndoa hii ilipelekea kuondoa umuhimu wa Damu katika kuthibitisha ubikira wa mwanamke hata ingawa damu ya ubikira ina kiherehere na humwagika kwa wingi tu katika mtindo ulio wazi kuwa mwanamke huyu ni bikira lakini sio wote wanakuwa na alama hiyo na hivyo labda kungekuweko uwezekano wa kuhukumiwa kwa mabinti wasio na hatia ambao ubikira wao uliweza kutokuthibitika katika mazingira mengine

Mkazo mkubwa wa ubikira unapochunguzwa vyema Katika maandiko ulimaanisha KUTOKUNAJISIKA, ASIYENAJISIKA, UNAJISI ni lazima kujiuliza unajisi ni nini kunajisika kunakozungumzwa hapo ni nini? Neno unajisi kwa urahisi ni kuchafuka, kuchafuliwa n.k. kuingiliwa kwa mwanamke katika tendo la ndoa kungepeleka taarifa ya uzuri au ubaya wa tendo hilo katika Ubongo na ungerekodiwa mara moja, taarifa ya utamu wa tendo la ndoa ingekuwa imeingizwa kwa mwanamwali ambaye hakuna mtu wa kumuoa bado, uhitaji wa tendo ungeingizwa mapema kwa binti katika ubongo wake, angeanza kuwakwa tamaa ya kutaka mume huku hakuna wa kumuoa na hivyo roho ya ukahaba ingeingia kichwani na hivyo kumbikiri mwanamke kungeitwa kumnajisi au kumfanya kuwa kahaba, na kama binti aneshindwa kujitunza angeitwa mpumbavu kwa hiyo maana kubwa ya kiroho kuhusu UBIKIRA ni KUTOKUNAJISIKA.

Nisiwachoshe sana.

Kauli mbiu Yetu Miaka kumi hii: Usioe mwanamke asiye na bikra, usinajisi kizazi chako mwenyewe.

Jokajeusi

===========

Mwanamke Bikra ndiye Mke bora

Habari Wakuu!

Tangu nijiunge humu JF nimekuwa nikiwapigia chapuo wanawake wenye bikra ndio wake bora.

Asilimia 90% ya wanaume tuliooa wanawake wenye bikra hatuna kesi za ajabu ajabu ndani ya ndoa. Wanawawe sio malaya, wanaadabu, hawana tamaa ya hovyo hovyo. Wakati 10% iliyobakia ya waliooa wanawake wenye bikra wanapata mikasa na vitimbwi vya ndoa.

Hii ni tofauti na wale wenzangu na miye waliooa wanawake wasio na bikra ambao 90% wanahenyeka, wanaipata fresh ya shamba. Huku 10% ndio wakineemeka.

Wakati 99% ya wanaume waliooa single mother wakiiona dunia jehanamu, ndoa chungu na maruweruwe. Huku 1% ya wanaume waliooa single mother ndio wakienjoi.

Sisi tuliooa wanawake wenye bikra mpaka hivi leo tunapeta na wengi tunaenjoi maisha.

Faida ya kuoa mwanamke mwenye bikra

1. Hawezi kukuona kibamia
2. Kiroho mnamafungamano
3. Mtazaa kizazi kisicho cha zinaa tofauti na kuoa mwanamke ambaye tayari ameshafanya uzinzi. Ambapo mtoto wako atapitia kwenye uke ulionajisiwa na wanaume wengine na kumwagiwa manii zingine.

4. Heshima na adabu
Siku zote mwanamke anayekuheshimu atakupa kitu kipya na sio mtumba. Wanawake wa siku hizi wanawadharau wanaume kwa sababu wanaume wengi siku hizi wameamua kula makombo, kula mtumba. Mwanamke hawezi kukuheshimu ikiwa ulimuoa akiwa hana bikra. Hata Mungu mwenyewe hapendi makombo, Mungu kumpa sadaka au zawadi used ni kama umemdharau. Ndio maana akawaambia hata watu wake waoe wanawake bikra, ili wasijitie unajisi wao na kizazi chao.

5. Ukioa Bikra huwezi pata sijui mwanamke aliyetoa mimba, sijui aliyezaa.
Siku hizi wanaume wanaoa wanawake wauaji bila ya wao kujua. Unakuta unaoa jianamke lisilo na bikra kumbe tayari limeshaua watoto kwa kutoa mimba nyingi tuu. Sasa njia bora kuzuia mashaka hayo ni kuoa mwanamke bikra.

6. Mwanamke hatakuwa na Kumbukumbu za Ma-ex wake
Ukioa mwanamke bikra huna wasiwasi, unajiamini kwa sababu wewe ndio wa kwanza. Huwezi linganishwa na mwanaume mwingine kwa sababu hakuna wa kulinganishwa naye. Ila ukioa mwanamke asiye na bikra ni lazima afanye ulinganisho baina yako na wanaume waliompitia. Siku zote awali ni awali. Na siku zote upendo wa kwanza ndio upendo halisi.

Nafahamu mada hii itawaumiza wanawake wengi ambao hawana bikra na hawajaolewa, au waliombioni kuoa mwanamke ambaye hajamkuta bikra. Lakini huo ndio ukweli. Wewe kama huna bikra au uliolewa bila bikra na ukaolewa na mwanaume mwingine ambaye hajakutoa bikra basi tambua wewe ni malaya.

Sisemi malaya wasiolewe, ila lazima mtu kabla hajaoa atambue kuwa changamoto za kuooa malaya ni zipi.
Siku hizi watu wanakuambia ndoa ndoano, au ndoa uvumilivu moja ya sababu ni kuoa wanawake wasio na bikra. Kuoa mwanamke asiye na bikra yataka moyo. Yaani unaoa mwanamke ambaye unafahamu fika kuwa mwanamke huyu ni malaya yaani tayari keshalala na mwanaume mwingine. Kabla hujaoa mwanamke asiye na bikra jiulize utaweza vumilia changamoto za malaya?

Ni tofauti na sisi tuliooa wanawake bikra ambao kimsingi tunakuwa waalimu wa wake zetu tukiwafundisha kila mazuri na mabaya. Lakini unapooa mwanamke asiye na bikra basi tambua yale aliyojifunza kwa waliomtoa bikra basi anakuja ku-apply kwako.

Wakuu bikra zipo, mabinti wapo kibao wenye bikra, acheni kusema bikra hakuna, bikra zipo nyingi kidato cha tano, cha sita, chache zipo chuo.

Nafahamu kuna bikra za kutengeneza, lakini mwanamke bikra hata akili yake huwa bikra hilo ni muhimu.

Bikra matters!

Povu Ruksaa


=========

Bikra ni kapu la ndoa

Habari Wakuu!

Bikra ni kapu la ndoa lililobeba mambo yafuatayo;
  • Uaminifu
Ni rahisi kumuamini mwanamke uliyemkuta bikra. Ni rahisi kumtetea kuwa yeye sio mzinzi kwa kuwa ulimkuta akiwa na bikra. Ni rahisi kuweka rehani kwa mwanamke uliyemkuta bikra. Mwanamke mwenye bikra anahaki ya kuaminiwa. Ni halali kumuamini mwanamke mwenye bikra. Mwanamke uliyeitoa bikra yake ukamuoa anakuamini kuliko unavyofikiria.

Huwezi kumuamini mwanamke usiyeikuta bikra. Mwanamke asiyebikra kamwe hawezi kuwa mwaminifu hata angekuwa mcha Mungu kiasi gani. Ikiwa alishindwa kutunza bikra yake kabla ya ndoa atawezaje kuilinda nyeti zake baada ya wewe kumuoa. Mwanamke asiye na bikra kamwe hawezi kukuamini kutokana na kuwa tayari alishatendwa na hivyo anajua kuwa wanaume wote ni sawa.

Ikiwa yeye hakuamini wewe unaanzaje kumuamini?

  • Heshima.
Kuoa mwanamke uliyeikuta bikra ni heshima. Sio tu kwa binadamu hata falme za kiroho. Kizazi chenu kitaheshimiwa hasa na falme za kiroho. Kitakuwa kizazi kisicho za zinaa. Lakini nakuhakikishia kama ulichukua mwanamke asiye na bikra utashangaa unaletewa mimba za watoto wako hata kabla hawajaolewa.
Unao uwezo wa kutangaza kwenye harusi kuwa mwanamke uliyemchukua umemkuta mpya hajatumika. Kisha ukatoa zawadi kwa waliomlea. Bikra ni heshima mpaka kwa wazazi wa mwanamke na jamii kwa ujumla. Mwanamke asiye na bikra sio tuu yeye ndiye anatabia mbaya bali hata waliomlea nao walishindwa kumlea mtoto wao katika maadili mpaka wakakupa litoto lililoharibiwa.

  • Uvumilivu
Mwanamke uliyemkuta bikra kuna uwezekano mkubwa wa kukuvumilia kwa asilimia 90. Kama alivyoivumilia mbo*o wakati ukiitoa bikra yake ndivyo atakavyokuvumilia wakati ukiishi naye. Wanawake wengi walioolewa na bikra ni wavumilivu kwa kila hali. Najua wengi hawajui. Lakini sisi tuliobahatika kuwapata wanawake wenye bikra tumeshuhudia mambo haya. Hata ndoa za zamani wanawake wengi walikuwa wavumilivu kwa sababu wengi wao waliolewa na waliowatoa bikra.

  • Role model
Mke uliyemuoa akiwa na bikra ni role model mzuri kwa watoto. Mke atajua namna ya kuwafundisha watoto wa kike umuhimu wa bikra. Atakuwa na ujasiri wa kuwaambia kuwa Baba yao alimkuta bikra. Lakini ukioa jianamke lisilo na bikra sio tuu umechanganyikiwa bali unaenda kuzaa watoto watakaochanganyikiwa zaidi.
sio ajabu kizazi hiki kila kijana anawaza ngono. Sasa unafikiri atawaza nini ikiwa mama yake alikutwa ni mzinzi. Hakukutwa na bikra. Mwanamke mwenye bikra ni role model mzuri kwa mafunzo kwa watoto.

  • Kuridhika
Mwanamke aliyeolewa akiwa na bikra huridhika na maumbile na mapenzi ya mume wake. Hakuna kibamia ukioa mwanamke mwenye bikra. Lakini ukiona mwanamke anajadili maumbile ya wanaume ujue ameathirika na masuala ya uasherati. Kamwe hutokuja usikie mwanamke aliyeolewa bikra akiongea kauli za hovyo. Sijawahi kuona.

Mwanamke ni kiumbe mzuri sana akikutwa na bikra. Kabla hajaharibiwa na mashetani. Wanawake wanaridhika ikiwa utawaoa wakiwa bikra

  • Usikivu na Utii
Mwanamke uliyemuoa akiwa na bikra lazima atakusikiliza na kukutii. Hawezi kukudharau. Hawezi kufundisha watoto upuuzi wa kukupuuza. Lakini ukioa mwanamke asiye na bikra lazima atakudharau. Atakuona wewe ni mtu wa makombo. Mtu usiyeweza kuchukua vitu vipya. Mbaya zaidi ukitaka uharibu kabisa. Mpende sana ndio utakiona cha mtema kuni. Jinsi unavyozidi kumpenda ndivyo anavyozidi kukudharau. Lakini mwanamke uliyemkuta bikra jinsi unavyompenda ndivyo unavyozidi kuuteka moyo wake.

Usishangae kwa nini mwanamke unalihudumia bado halikuheshimu, linakudharau, linachepuka na kukutungia majina ya hovyo. Usishangae mpaka majina ya hovyo liliyataja mbele ya watoto wako. Ndio madhara ya kuchukua vitu vilivyooza, kuchukua mitumba. Wewe uliona wapi mla mizoga akiheshimiwa, hata viumbe wanaokula mizoga huoni majina yao na jinsi wanavyodharaulika.

Wakati mwingine mwanamke ambaye hana bikra anatamani akuheshimu lakini nature haimruhusu. Lazima atajikuta anakudharau tuu. Atakuheshimuje ilhali umemchukua hana bikra. Nature italazimisha udharaulike.

  • Kumbukumbu
Mwanamke mwenye bikra atatunza kumbukumbu isiyofutika. Hata ufe leo atakukumbuka miaka yote. Ukioa mwanamke mwenye bikra wewe ndio unaandika historia ya mapenzi katika maisha yake. Hana kumbukumbu ya zamani kwani wewe ndio wa kwanza. Wewe ndio mwalimu wake utakayemfundisha kusoma. Hatasahau irabu na konsonanti utakazo mfundisha mpaka mwisho wa maisha yake.
Lakini ukioa hawa madunga embe utaumia. Unaenda kufundishwa historia ya mwanaume mwenzako. Mara mbona mwenzako alikuwa anapiga vitatu kwa mpigo. Mara mbona mwenzako alikuwa akinibeba au kunipa hela. Yaani utalinganishwa na Ex wake kwa kila kitu.

  • Kuwekeza na Siri
Mwanamke aliye na bikra huwekeza moyo na mali kwa mume wake. Atakupa mapenzi yote na mali zake zote. Mtashare kila kitu. Waliowahi kuwa na wanawake wenye bikra wataungana na mimi kuwa mwanamke aliyetolewa bikra sio mbinafsi. Mnashare mali zenu ila hiyana. Lakini hawa mashankupe utasikia chake ni chake, na chako ni cha wote. Hao ndio unashangaa linajenga nyumba kwao kisiri wewe huna ujualo. Wanawake walioolewa na bikra hawana siri. Watakuambia kila kitu chao.

  • Kujiamini
Mwanaume akioa mwanamke mwenye bikra anajiamini mara elfu moja tofauti na yule aliyeoa mwanamke asiye na bikra. Mwanaume ukioa mwanamke mwenye bikra hata ukienda ukweni hunawoga. Unajua kabisa mtaani hapo hakuna anayemjua mke wako kwa kuwa ulimkuta bikra. Lakini ukioa asiye na bikra huwezi kujiamini. Unaweza kwenda ukweni hata uwe na gari kali sijui BMW X6 bado utakuwa hujiamini ukipita na mke wako. Kwanza utajiaminije wakati huenda kuna mwanaume mwenzako anakucheki tuu unavyotembea na gari lako wakati mkeo wanamjua enzi hizo akiwa ua saa sita.

Alafu mbaya zaidi siku mkeo akienda mwenyewe kusalimia kwao hapo ndio huenda kucharazwa na ma- Ex wake. Nani asiyejua kuwa wanawake wengi walioolewa wanato*ombwa wakirudi kwao kwenye misiba au harusi za ndugu zao. Huchapwa na wapenzi wao wa zamani. Nani asiyelijua hilo.

Najua kuna watu watakataa jambo hili. Lakini wataonekana ni wajinga kwa sababu ikiwa ulimkuta mkeo hana bikra kwa nini upinge jambo hili. Utamuamini kwa kipi. Nini kinakufanya umuamini mkeo ikiwa hukumkuta bikra.

Bikra ndio alama ya uaminifu kwa mwanamke. Maneno ya mwanamke hayamfanyi mwanaume mwenye akili kumuamini mke wake ikiwa hakumkuta bikra.

Mimi mke wangu hata kama nikisikia anatoka na fulani sitaamini miaka mia mpaka nimfumanie kwa kuwa nilimkuta bikra. Bikra yake ndio inambeba. Lakini kama hana bikra hata nisipoambiwa anachepuka mimi nitajua anachepuka kwa vile sikuikuta bikra.
Mwanamke asiye na bikra hata nikimsingizia kuwa kuwa anachepuka hana uhalali wa kunipinga ikiwa sikuikuta bikra. Lakini mke wangu nitamwambia akatae mara mia kuwa hachepuki mpaka nimfumanie kwa vile niliikuta bikra.

Nitamsamehe mwanamke niliyeikuta bikra kwa vile nitajua kuwa ameteleza na wala sio tabia yake. Lakini jitu sikulikuta bikra bado liniambie limeteleza hiyo sasa ni dharau.

Kwanza lilinidharau kunipa bidhaa iliyotumika. Alafu leo tena liniambie imenywewa bahati mbaya.

Mwisho; Natoa wito kwa vijana ambao hawajaoa kuwa usijeoa mwanamke asiye na bikra. Oa mwanamke mwenye bikra. Utakuja kunishukuru badae. Achana na porojo za watu humu hasa wanawake kuwa ati bikra haina uhusiano na tabia. Mwanamke atakayekuambia hivyo mwambie sharti awe nayo kwanza hiyo bikra ndio umskilize. Ukitaka ndoa iwe ndoano basi oa pagama. Ukitaka gari likusumbue nunua gari used. Mpya ni mpya tuu.

Kwa wale mliooa pambaneni na hali zenu.

JokaJeusi.
Mpiga kampeni wa kurudisha heshima ya ndoa kwa kuwamahasisha watu watambue thamani ya bikra

Michango:

===============

Madhara makuu ya kuoa mwanamke asiye na bikra

Wakuu habari!

Jambo hili nimelivalia njuga na naona matunda yake yanaanza kuonekana, nafikiri nikiendelea hivi kwa mfululizo wa miaka mitano kwa kiasi kikubwa jamii itarudi kwenye mstari.

Moja ya matokeo chanya katika nyuzi zangu za ubikra ni kuwa wale walioolewa bila ya bikra na wale ambao bado hawajaolewa na hawana bikra wanapiga kelele wakitapa tapa, wengi wamekuja Pm wakiniomba niache. Ujumbe wangu ni huu; Asiyefunzwa na Mama yake hufunzwa na ulimwengu. Mandhali Jokajeusi nipo mada hizi zitaendelea mpaka nitakapoondoka duniani. Hivyo wale wanaaoumia nawapa pole kwa sababu huu ni mwanzo tuu.

Madhara ya Makuu ya kuoa mwanamke asiye na bikra, Kijana usiyeoa soma kwa umakini ukitumia akili zaidi ya hisia zako.

1. MTALAKA HATONGOZWI
Kabla hujaoa mwanamke asiye na bikra kaa ukijua kabisa mtalaka hatongozwi, popote pale duniani. Pia kumbuka awali ni awali hakuna awali mbovu. Pia kumbuka, Mavi ya kale hayanuki. Hivyo mwanamke anapokuwa tayari alishakuwa kwenye mahusiano na wanaume huko nyuma ya kimapenzi kisha wakaachana kwa sababu abc kisha wewe ukampata akakuambia ameachana na ma-ex wake jua kuwa anakudanganya, kuachana labda kama wamekufa lakini kama wapo hai hesabu umeumia ndugu yangu.
Nina ushahidi usio na shaka kuhusu jambo hili na hata humu JF kila siku tunasikia malalamiko ya wanawake kurudiana na ma-ex wao au kufumaniwa nao. Hiyo ni kawaida sana, na mara zote mimi siwalaumu wanawake kwa kufanya hivyo kwani hiyo ndio asili. Mtalaka hatongozwi.

Usipokubali maneno yangu na ukashindwa kujifunza kwa yanayotokea kwa wenzako basi subiri wewe ndio uwe funzo na mfano kama walivyo wabishi wengine.

2. KUBAMBIKIZIWA MIMBA
Wanawake wengi wasio na bikra wamewaingiza wanaume katika magonjwa makuu kwa kuwabambikizia watoto wasio wao. Hata ule utafiti usemao kuwa 60% ya wanaume wanalea watoto wasio wao unalandana(correlation) na idadi ya wanaume waliooa wanawake wasio na bikra.
Kuna uwezekano wa kuingia kwenye mahusiano na mwanamke mwenye mimba changa ikiwa tuu ulimkuta hana bikra, mifano ipo ya kutosha hata huku mitaani achilia mbali watu maarufu kama vile Muna Love na Casto Dickson Vs Baba patrick, Mama Diamond na Babab Ricardo Vs Mzee Abdul, na wanawake kukubambikizia mtoto hawaoni shida kwa sababu tayari wameshakuona wewe ni maandazi, tayari umejidharau, yaani uache kuoa mtoto mbichi uchukue used alafu wakuheshimu. Hiyo hakuna mwanamke wa hivyo.

Usijedhani ukimuoa mwanamke asiye na bikra na single mother ataona umemuonea huruma kwa kumsitiri, yeye atakachojua kuwa uzuri wake ndio sababu umedata naye, hivyo suala la kuonewa huruma hilo sahau, na ndio maana wao wakifanya matukio yao kwako wala hawatakujali kuwa uliwastiri. Nafikiri mifano mnayo hata huko mitaani.
Hivyo kuoa mwanamke asiye na bikra kuna uwezekano mkubwa wa kubambikiziwa mtoto achilia mbali kuchetiwa ambapo ni costant

3. WATOTO KUWA NA TABIA ZA AJABU AJABU
Ukioa mwanamke asiye na bikra na malaya, sio ajabu watoto wako wakawa na vitabia vya ajabu ajabu yaani mchanganyiko kulingana na idadi ya wanaume waliolala na mke wako. Angalia wanawake wengi ambao ni malaya kisha angalia tabia za watoto waliowazaa. Watoto wamenajisiwa. Mtoto akipimwa DNA ni wakwako lakini tabia zipo mbali sana na wewe na ukoo wenu na ukoo wa mama yake. Hii ni kutokana na kuwa mwanamke anapolala na wanaume tofauti tofauti hujinajisi na kujipa maroho machafu kwani tendo lenyewe ni chafu.
Kama unabisha jaribu sumu kwa kuonja. Waliooa wananielewa zaidi kwani wanayaona hayo kwa macho yao.

4. WATOTO KUUNGANA NA MAMA YAO.
Ukioa mwanamke asiye na bikra ni rahisi sana kwa watoto kumsikiliza Mama kuliko kukusikiliza wewe Baba, au ni rahisi sana kwa watoto wako kumsikiiza Baba mwingine kuliko kukusikiliza wewe. Hii ni kutokana na kuwa tayari wewe sio namba moja, wewe sio kichwa tena bali mkia. Unapoambiwa Baba ni kichwa cha nyumba wanamaanisha Namba moja, yaani Baba ndio mwenye maamuzi, mwanzo, na ndio maana popote pale kichwa ndio hutangulia, sasa kama kwa mkeo hukutangulia kumjua unafikiri utakuwaje kichwa kwake au namba moja kwake. Wakati mwingine wapo wanawake wachache wema wanaojitahidi kuwa wema licha ya kuolewa bila ya bikra lakini bado nature inawavuta kufanya mabaya.

Zamani Baba alikuwa ndio nguzo ya familia kwa sababu nyingi mno, watoto walikuwa wanamsikiliza Baba, hii ni kutokana na kuwa wamama wengi waliolewa wakiwa na bikra. Lakini tangu wanawake waanze kuolewa bila bikra siku hizi Baba sio lolote tena, na ndio maana ongezeko la watoto wasemao nani kama Mama ni kubwa, na sababu nimeshaieleza.
Kama unabisha jaribu sumu uone.
Baba kama unataka heshima sikiliza ninachokuambia, ukijifanya unajua na unaheshimiwa kisa sasa unanguvu subiri miaka 60 huko utakumbuka maneno ya Jokajeusi.

5. KUOA MAMA WA WAFU
Kuoa mwanamke asiye na bikra kunaweza kupelekea kuoa mama wa wafu, unaoa mwanamke aliyetoa mimba nyingi nawe huwezi kulijua hilo na huna uhakika, Lakini ukioa mwanamke bikra unaoa mke unayejua ni msafi na aliyejitunza. Tayari unaoa mwanamke ambaye anakesi ya mauaji na laana ambayo huijui, ni bora ungekuwa unaijua hii itakusaidia kumlilia Mungu amsamehe na awasamehe, jambo moja la kuzingatia ni kuwa kuomba msamaha kwa makosa makubwa hakuombwi kwa kusema tusamehe makosa yetu, hiyo ni sala ya jumla ambayo watu huomba wakiwa kwenye halaiki, Jokajeusi nashauri, mwanamke kama umetoa mimba ni vyema umjulishe mumeo mtarajiwa ili muweke mambo sawa, sio umuingize Mwanaume wa watu kwenye mikosi na mabalaa bila ya yeye kujua.

6. MWANAMKE ASIYE NA BIKRA SIO MKEO BALI MSHIRIKA.
Kuna tofauti kubwa kati ya mke na mshirika wa maisha. Mke ni sehemu yako yaani ni ubavu wako, mshirika sio sehemu yako bali mmeamua kushirikiana katika maisha. Mke hukupenda wewe na familia yenu, naye ni sehemu ya ukoo wenu. Lakini mshirika sio sehemu ya ukoo wenu kwanza huwaza kuwapa faida wazazi wake zaidi. Siku hizi wanaume wengi wanaoa wanawake wasio na bikra na ndio maana hao washirika wao hupendelea makwao kwani sio mwili mmoja na waume zao. Mwanaume mwenye mke anaouwezo wa kumwambia mke wake kuwa asienda kwenye msiba hata wa mama yake(mama wa mke) na mke wake akamtii, lakini mwanaume aliyeoa mshirika wa maisha hana uwezo wa kumzuia mshirika wake asiende kwenye msiba wa mama yake(mama wa mshirika).
Kwa kifupi mume anakuwa anamamlaka kwa mke wake na sio kwa mshirika. Kumbuka mshirika ni mwanamke aliyeolewa bila ya bikra, na bikra aliiotoa kwa makusudi kabisa.
Mke ukishamuoa hawazi tena nyumbani alipozaliwa mpaka mume mwenyewe umkumbushe kwamba aende kusalimia, lakini mshirika kwa mwaka huenda nyumbani mara mbili mpaka mara tatu.
Hapa hoja kubwa ni kuwa huwezi mtawala mwanamke ambaye sio mkeo, mkeo lazima akusikilize kwa chochote kile Lakini ukiona mwanamke unayeishi naye hakusikilizi jua sababu ni hiyo hapo juu, hukuoa akiwa bikra.

Waliooa wananielewa, sumu aionjwi

7. UMILIKI
Ukioa mwanamke asiye na bikra, cha mwanaume ni cha wote na cha mwanamke ni chake mwenyewe. Watu wanasema wanawake ni wabinafsi, mimi nawaambiaga kuwa mwanamke sio mbinafsi mpaka pale atakapoolewa bila ya kuwa na bikra. Wanawake wengi walioolewa bila bikra ni wabinafsi kupitiliza. Hii ni tofauti na mwanamke aliyeolewa na bikra yake, ambaye chake ni cha wote na cha kwako ni chawote. Mkeo(aliyeolewa bikra) anajua kuwa yeye ni mali yako na kila kitu anachomiliki yeye. Mkeo yaani uliyemuoa bikra anapenda umlinde yaani umchunge kwani anajua yeye ni malkia, yeye ni wathamani, lakini mwanamke ambaye hajaolewa akiwa na bikra hapendi umchunge, umlinde wala kumfuatilia, wana msemo wao wanasema mwanamke hachungwi, msemo huo sio wa mke bali mshirika. Hata humu JF wapo na wanajijua.
Mkeo uliyemuoa bikra hata watoto atakuambia watoto wako wanasumbua, au wanashida abc, au hata ukiwaadhibu atakuambia utawaua wanao Mume wangu. Lakini ambaye hajaolewa bikra ni kawaida kusikia wakisema muache mwanangu.

8. SIRI YA MTOTO
Mwanaume ukishaoa mwanamke asiye na bikra basi jua siri ya mtoto niwa nani anaijua Huyo mshirika wako. Ndio maana siku hizi mpaka sheria zinatungwa kuwa Baba ni mlezi sio mzazi. Kwani wanawake wengi wameolewa wakiwa bikra.

Siku hizi ndoa ni ndoano kwa sababu wanaume wengi wanaoa wanawake wasio na bikra. Mpaka wengine wanaogopa na kuiona ndoa haina maana.
Lakini ndoa ni sehemu tamu,yenye raha ikiwa utaoa mwanamke mwenye bikra. Vijana ndoa ni tamu kama utapata mke wako na sio mshirika wako.

Nitaendelea kuwafunza vijana hivi hivi mpaka wenye akili watakaponielewa.

Jokajeusi


================

Kuoa mwanamke bikra sio kinga ya mkeo kutokukusaliti

Kuna upepo ambao unaendelea sana kwenye vichwa vya vijana wengi kwamba ukipata mwanamke ambaye ni bikra baasi wewe jua umebakiza kasoro ndogo ndogo na sio ile kubwa ya kusalitiwa hivyo unanyoosha minguu ukijiamini kwamba hata iweje baasi mkeo atakusubuli wewe tu.

Rafiki yangu sio kweli, kumbuka kile ulichomfundisha atatamani kujua na kwa wengine kunafundishwaje, hivyo ingawa mwanzoni atakuwa na uoga wa kwenda ila baadae itabidi aende tu kujaribu sasa hapo ndio utajua kuwa kumbe kama haukucheza mchezo fulani utotoni jua utaurudia ukubwani hata kama ni kwa wajukuu na ukiujulia ukubwani jua utaucheza kuliko hata yule aliyeucheza utotoni.

Hivyo ni bora ambaye sio bikra lakni ameamua kutlia na wewe kuliko yule bikra ambaye anatani kuona kama umewazidi wote kweli.


Nilikuwa na rafiki wa kike ambaye tulipendana sana lakini kwa bahati mbaya/nzuri sikuwahi kufanya nae mapenzi ingawa mara moja nilishamwingiza room ila tulitoka hivi hivi. Tuliishi maisha hayo mimi nikiwa chuo na yeye akisoma Olevel na baadae Advanced level mikoa tofauti lakini likizo tukikutana Mara chache.

Nilifahamika kwao, wazazi wake wote walikuwa walimu tena kama wazungu maana nilikuwa naingia hadi kwao na binti ananisindikiza wakati wa kuondoka. Tulipendana tu japo sikumla ila kitandani tushacheza Sana na matembezi ya mtaani tukifatana kama kumbikumbi tulipanga tuoane, tulitoa hadi majina ya watoto wetu tutakaowapata. Lakini badaye tukatofautiana kwenye simu tukaachana kwa hasira ingawa kila m1 kwa shingo upande hakuna ambaye alitaka kujishusha.

Nilipomaliza chuo nikaajiriwa nyanda za juu kusini, Iringa na yeye akawa UDSM huko ndiko alipata mume aliye naye hadi Leo kwa harusi ya kanisani, katoliki. Pamoja na kwamba tuliachana hivyo na kufuta namba yake lakini alinipigia kila mwaka ifikapo birthday yangu na kunitakia heri ya siku ya kuzaliwa.

Nifupishe story, wale wazazi wake kumbe wakimchosha kumwuliza Mara kwa mara kuwa yule Jack (siyo jina langu) unawasiliana naye? Hivi mlikosana nini? Maswali hayo yakawa yanamfikirisha na kumnyima Amani. Kiukweli wale walimu(wazazi wake) walipenda Sana niwe mume wa mtoto wao.
Kisa Cha kuolewa na huyo jamaa alikuta yupo bikra tena University level, hakuamini akaenda kutoa posa na kumwoa bila kupoteza muda lakini kadiri ya maelezo yake alipenda bikra itolewe na mimi otherwise aliapa lazima tugegedane hata akiwa kwenye ndoa.

Katika hali nisiyoitegemea Kuna siku akanitumia msg kuwa yupo mkoa ninaoishi tena mji huo huo, sikuamini tukapanga kuonana, na tufanye faragha. Binti wa watu alilia sana ila mwisho wa siku akasema ni mipango ya Mungu na tushukuru kwakuwa kila mmoja wetu ana familia sasa, akasema aliapa katka maisha yake na hata mama yake alimwambia kuwa lazima animtafute popote anipe tunda. Ogopa mwanamke akiweka nadhiri!! Nilimtafuna vizuri sana alinifosi nilale lodge lakini sijawahi lala nje ya home kizembe hivyo, mke wangu angestuka. Niliongea na wazazi wake wote wawili kupitia simu yake, wananikumbuka sana.

Alinionesha picha za harusi yao, mme wake ni mtu mwenye kipato kikubwa sana, simfikii hata kidogo hadi binti anasema hafurahii maisha yale amekuta mali nyingi ambayo hajachuma akiwa na yeye. Hivyo sometimes anakosa uhuru.

Mume aliagwa kuwa anaenda kusalimia wazazi, kweli binti alienda kwao na siku ya pili akaunganisha kuja kwangu. Siku ya kuondoka pia alienda mkoa wa wazazi wake ili atakaporudi kwa mumewe ionekane ameshuka kwenye bus za kwao(mmewe ana desturi ya kwenda kumpokea stand kuu).

Mwenyewe anaamini Mimi na yeye Ni soulmates. Na kiukweli ndiye binti niliyewahi kumpenda kuliko yeyote.

Huyo ni mke wa mtu aliyekutwa bikra amenituku papuchi, hawa wenzetu hawana formula. Na anavyokazia kuwa sisi ni soulmates, hatuwezi kuachana milele.
 

Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
5,754
2,000
kuna watu wameolewa wakiwa na watoto lkn mpaka leo wanaheshimu ndoa zao, hapo utasema mwanaume ameoa laana..? jibu ni hapana. kila mwanaume anatamani aoe bikra lkn unaweza kuta huyo huyo mwanaume ametoa bikra zaid ya 10 na bado akaoa malaya.


Kutokuoa bikra si laana bali ni najisi Mkuu
 

Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
5,754
2,000
Mademu wa humu watakuambia hivi

""Kama unataka bikra Zaa wakwako""".

Ili hali kuna mdada humu katoa uzi Yupo bikra bado na anamiaka 32..hapo utagundua kua wao walitolewa Wakiwa sekondar .

Maisha uchaguzi buaaana!!


Kweli Mkuu Maisha uchaguzi.

Si mbaya mara moja moja kuelezea mambo ya moto kama haya
 

Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
5,754
2,000
yetooooo!!!!!!!


Ndio hivyo Dadaangu, kama wewe ulikosea jitahidi kwa wanao. Kwani unashindwa kumwambia mtoto wako wa kike kila baada ya muda fulani nitakuwa nakukagua kama umeanza mchezo mbaya au laa. Wazazi wanachakujibu kuhusu hizi ishu.

Embu fikiria Lutu ni mzazi wa kiume lakini anauhakika kabisa mabinti zake wako sildi. je wewe utashindwa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom