Vigezo na sifa za Mwanamke wa kuoa kwa 2024 - 2050

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
VIGEZO NA SIFA ZA MWANAMKE WA KUOA KWA 2024 - 2050

Anàandika, Robert Heriel.
Mtibeli

Pasipo kupoteza muda. Ikiwa wewe ni mwanaume unatafuta mke wa kuoa ili ujenge naye familia basi vigezo na sifa zifuatazo sharti Mwanamke huyo utakayemuita mkeo lazima awe nazo. Ili uishi maisha ya furaha.

Wanaume nitawagawa katika makundi matatu kulingana na umri kama ifuatavyo;
1. Wanaume wenye Miaka 20 - 35
2. Wanaume Wenye miaka 36 - 50
3. Wanaume wenye miaka 51 -. 85

1. Wanaume wenye Miaka 20-35
Ikiwa upo katika age hiyo na unatafuta Mke wa kuoa basi vigezo na sifa zifuatazo ni lazima, nasisitiza ni lazima uzingatie VIGEZO hivi ili ndoa na maisha ya familia yako yawe na furaha.
Vigezo na sifa hizo ni kama ifuatavyo;
1. Mwanamke lazima awe Bikra.
Piga ua garàgaza, ukiwa na miaka kati ya miaka 20 - 35 na unatafuta kuoa basi hakikisha unaoa Mwanamke Bikra.
Elewa kama ilivyo ngumu kupata Mwanamke Bikra ndivyo hivyohivyo ni ngumu kuishi kwa furaha na Mwanamke asiye Bikra.
Elewa kuwa karne hii uzinzi na uasherati upo kwa kiwango cha juu kabisa.
Matumizi ya P2, utoaji wa mimba kwa kiwango cha kutisha, matumizi ya madawa na teknolojia ya kuzuia mimba yanaathari kubwa katika familia utakayoianzisha.
Sijazungumzia mambo ya kihisia kuhusu umuhimu wa bikra kwani Jokajeusi alivyokwisha kueleza.

Ni ngumu ukioa Mwanamke Bikra akasumbua kwenye mambo ya ujauzito, sijui homoni imbalance,
Elewa kuwa ukioa mke Bikra hakuna msamiati Ex kwani wewe ndio namba moja. Na wewe ndio utakuwa Ex wake wa kwanza ikiwa mtaachana.

Elewa kuwa ukioa Mwanamke Bikra hana makovu ya kihisia ya kutendwa hivyo wewe ndiye utakuwa muongozo wake. Hivyo wewe ndiye mwalimu wake namba moja. Hivyo kuanguka kwake itagemea na wewe lakini ukioa asiye na bikra huna utakachomfundisha kwani tayari msingi walijenga wengine. Hayo maelezo walishaelezaga wadau humu.

Ingawaje nampingaga Jokajeusi kuwa Bikra sio kila kitu lakini kwa umri wako kijana bikra inanafasi kwa zaidi ya asilimia 70

2. Mwanamke Mzuri
Mwanamke sifa yake kuu ni uzuri. Kuna Mwanamke alafu kuna Mke.
Kigezo cha uzuri katika kutafuta Mke hakitakuja kuondolewa kwa sababu huo ndio sababu ya Mwanamke kuitwa Mwanamke.
Lazima uoe Mwanamke mzuri. Inyeshe mvua Liwake jua. Achana na wale wanaoogopa Wanawake wazuri. Wakisingizia kuoa tabia njema.
Tabia njema ni sehemu ya seti ya lazima katika kuchagua mke lakini haiondoi sifa ya uzuri wa Mwanamke.
Lazima uoe mwanamke mzuri mwenye tabia nzuri.
Asije akakudanganya kuwa hao wanawake hawapo. Wanaosema hivyo ni waongo na usijifunze kwa Watu walioshindwa.
Hujawahi kuona Mtu fulani Mke wake ni mzuri, anatabia njema, anaelimu nzuri, na anafanya kazi yenye kipato?
Kama hujawahi kuona njoo nikuonyeshe.
Usisikilize maneno ya Watu walioshindwa ndio maneno yao hayo.

3. Mwanamke lazima awe na Kipato.
Sio kipato chako. Hapana kipato chake binafsi.
Kijana ukiwa katika umri huo. Lazima uchague Mwanamke mwenye sifa nilizotaja hapo juu na hii. Zote kwa pamoja.
Mwanamke kama hana kipato uzuri wake hauna maana yoyote kwako. Hakuamini kitu kizuri kikawa maskini, hakizalishi kipato na hakijitegemei. Hakuna uzuri wa hivyo.
Bikra, uzuri, kipato.

Mwanamke asiye na kipato huwaga namfananisha na nyumba isiyo na ghala la chakula. Lazima atakuwa tuu mnafiki, Malaya na mnyonyaji.
Mwanamke Mzuri, mwenye kipato na bikra mkikaa mnajadili vitu pasipo kuburuzwa.
Unauwezo wa kumuachia watoto wako na ukajua wako mikono salama.

Unaishi kwa raha. Sio ukiumwa kidogo unapata presha kuwa ukifa itakuwaje watoto watateseka.
Raha ya kufa ufe ukiwa na tumaini kuwa uliowaacha wako katika mikono salama ya Mwanamke anayejua nini chakufanya.

Ogopa Mwanamke asiye na kipato.
Ndoa itakuwa utapeli kama wadau dronedrake na wenzake wasemavyo.

4. Imani ya Mungu.
Mwanamke yeyote mwenye imani na Mungu anajua umuhimu wa kuolewa akiwa Bikra. Hiyo weka akilini kabisa.
Kwa umri huu huna haja ya kuuliza ilikuwaje huna Bikra. Swali hilo watauliza wakubwa zako wenye umri kuanzia miaka 36-50 hao ndio wanaruhusa ya kuoa Wasio na bikra.

2. Wanaume wenye miaka 36- 50
Hawa ni wakaka wakubwa na Wababa fulani hivi.
Hawa ndio wanaruhusa ya kuoa Wanawake wasio na bikra lakini hiyo haimaanishi waoe wanawake single Mothers(Yaani wenye watoto).

Vigezo vingine ni vilevile kama wenye miaka 20-35. Hawa tofauti yao ni kuwa wanaruhusiwa kuoa Wasio na bikra lakini wasiwe single Mothers.

3. Wanaume wenye miaka 51-85
Umri huu kila kitu kwenye maisha yako kitakuwa bayana. Yaani kama ni future yako itakuwa wazi machoni mwako.
Umri huu kama utahitaji kuoa basi unaruhusiwa kuoa Mwanamke Mwanamke asie na bikra na mwenye watoto ukipenda, pia waruhusiwa kuoa Mjane yaani Mwanamke aliyekwisha wahi kuolewa.

Zingatia; wakati unafanya jambo hili, uwe ushaweka mambo yako sawa kwa watoto wako ili baadaye isijeleta shida huko mbeleni. Kila mtu apewe kile anachostahili.

Hivyo ndivyo Watibeli tunavyofanya mambo yetu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Awe bikra hapo hapo awe” mzuri” na awe na kazi (Kipato). Ningekuambia kitu ila basi tu.

Ila mnatukoroga sisi ma jobless, jana tu si mmetoka kusema mwanamke mwenye kazi ni mwanaume mwenzenu muoe ambaye hana kazi?

Amehlo tujipange upya sasa😂😂
 
Awe bikra hapo hapo awe” mzuri” na awe na kazi (Kipato). Ningekuambia kitu ila basi tu.

Ila mnatukoroga sisi ma jobless, jana tu si mmetoka kusema mwanamke mwenye kazi ni mwanaume mwenzenu muoe ambaye hana kazi?

Amehlo tujipange upya sasa😂😂

Hiyo ni kwa Watibeli mkuu. Usiwe na shaka.
Watibeli wapo wachache wala wasikupasue kichwa

Hao wasiopenda Wanawake wenye kazi ni jamii nyingine kabisa.
Ila sisi Watibeli mwanamke asiye na kazi hayupo kundi la kuitwa Mtu.
 
Wanawake ambao hawana imani na mungu wapo kweli? Nawatafuta ile sana yaani.

Una uhakika matatizo ya ubebaji wa mimba na hormone imbalance yanasababishwa na utoaji/uzuiaji wa mimba?

Lazima awe na kipato ndio, watu wa jf ni wanafki sana, familia zinazoendeshwa na baba peke yake ni chache mno. Lakini mnawananga wasisome, wasifanye kazi.

Oa asiye na kipato halafu wewe ni maskini uone
 
Hiyo ni kwa Watibeli mkuu. Usiwe na shaka.
Watibeli wapo wachache wala wasikupasue kichwa

Hao wasiopenda Wanawake wenye kazi ni jamii nyingine kabisa.
Ila sisi Watibeli mwanamke asiye na kazi hayupo kundi la kuitwa Mtu.
Sawa tuanzie kwenye Bikra.
Kila mwanamke anazaliwa bikra si ndio?
Ila mazingira ndio yanapunguza au kuongeza chance ya hiyo bikra kuendelea kuwepo.

Binti akiwa mzuri chance ya ku survive na hiyo bikra hadi ndoa inapungua sana kwa asilimia kubwa. Unajua kwanini?? Kwa sababu nyie wanaume mkiona mtoto mzuri tu baaasiii, mnatumia mbinu zote za “kitibeli” mpaka muonje. Binti mzuri anazungukwa na vishaWishi vingi sana kuanzia shuleni (walimu) kwenye nyumba za ibada hadi mtaani. Kila mtu anataka aonje.

Unasema tena awe na kazii😂😂😂. Hapo uwezekano wa hiyo bikra kuendelea kuwepo ni ya kusaka kwa manati. Mabosi wenyewe ndio hawa hawa???😂😂😂 Tena mtoto ni mzuri??

Wewe oa jobless tu
 
Sawa tuanzie kwenye Bikra.
Kila mwanamke anazaliwa bikra si ndio?
Ila mazingira ndio yanapunguza au kuongeza chance ya hiyo bikra kuendelea kuwepo.

Binti akiwa mzuri chance ya ku survive na hiyo bikra hadi ndoa inapungua sana kwa asilimia kubwa. Unajua kwanini?? Kwa sababu nyie wanaume mkiona mtoto mzuri tu baaasiii, mnatumia mbinu zote za “kitibeli” mpaka muonje. Binti mzuri anazungukwa na vishaWishi vingi sana kuanzia shuleni (walimu) kwenye nyumba za ibada hadi mtaani. Kila mtu anataka aonje.

Unasema tena awe na kazii😂😂😂. Hapo uwezekano wa hiyo bikra kuendelea kuwepo ni ya kusaka kwa manati. Mabosi wenyewe ndio hawa hawa???😂😂😂 Tena mtoto ni mzuri??

Wewe oa jobless tu

Watibeli tunatumia kanuni isemayo hatuwezi haribu ambacho hakijaharibika au haribiwa. Yaani ukiwa Bikra na hatuna mpango wa kukupa hatuwezi kukugusa.

Ila tunaharibu vilivyoharibiwa na kuharibika. Hiyo kwetu ni Haki.

Kuhusu kuoa jobless naweza fanya hivyo lakini siwezi ishi naye kama hataki kufanya kazi. Never
 
Back
Top Bottom