Dodoma

Zoezi la kupiga kura limekamilika katika vituo vya Chamwino na kata ya Kizota.

Zoezi la kuhesabu kura laendelea.
 
Yaani hujui kuwa walipokuwa wakirudisha fomu majina yao yalikuwa yakiandiwka kwenye daftari la wagombea na list hiyo ndiyo imetumika kwenye ballot? Ulitaka iwe alphabetical kwa msingi gani, jina la kwanza, surname au jina la chama?
Kwani ratiba ya kuchukua na kurudisha form walijipangia vyama vyenyewe au Tume ndo iliwapangia???

Tusaidiane kueleweshana katika hili
 
Alikuwepo Jitu la miraba minne jina lake ni Farao aliitawala Misri pamoja na wana wa Israel lakini mwisho wake ulifika,nasema hivi ccm mwisho wenu umefika na mwisho wenu ni mbaya sana tena mmegeukana wenyewe kwa wenyewe.
Mimi pamoja na kulipia kadi yangu ya ccm miaka yangu yote ya uanachama lakini mwaka huu nimewanyima kura zangu zote.kuanzia udiwani hasi urais nimewapa upinzani
 
Kiukweli mimi sijawapa kura ccm kwasababu kuu 3.
1. Mafao ya nssf
2. Baadhi na dawa na vipimo kuondolewa kwenye bima ya afya
3. Nimewachoka, kwanini tangu tupate uhuru hadi sasa watutawale? kwanini wasije wengine? tuone nao uongozi wao miaka yote hiyo bado huduma ya afya mbovu,umeme shida,maji safi shida, maisha yanazidi kua magumu tu mfumuko wa bei na huku hataki hata kuongeza watu mishahara. Huyu baba ni mbinafsi sana,mbaguzi na anatugawa Watanzania. Mimi siwezi kuipigia kura ccm never
 
Tatizo hawana evidence, wanaonesha picha ya kula wanazosema wamezikamata, ila waliomkamata nazo hayupo
Hahahaha kweli umkamate mwizi uchukue na kuonesha kilichoibwa tu na sio mwizi, huu ni uongo
 
Yaani hujui kuwa walipokuwa wakirudisha fomu majina yao yalikuwa yakiandiwka kwenye daftari la wagombea na list hiyo ndiyo imetumika kwenye ballot? Ulitaka iwe alphabetical kwa msingi gani, jina la kwanza, surname au jina la chama?
Jina la chama. Ndivyo ilivyo miaka yote; na hata huu kwa wagombea wengine, kasoro uraisi wa muungano
 
2A2A2AC4-DD53-4C25-9D91-4F218B0FDA6A.jpeg
 
Tuacheni propaganda za kutafuta scapegoats za kushindwa na kuchafua jina la nchi kwa sababu za kipuuzi.

Nashindwa kuelewa chama kisichokuwa na grassroots kudai kuwa kinaibiwa kura! Mwaka 1995 mimi nikiwa NCCR-mageuzi tulihamasika sana pale Dar tukajua Mrema atachukua nchi, lakini tukasahau kuwa tulikuwa maarufu Dara na miji michache tu kwani hatukuwa na network kuzunguka nchi yote.

CHADEMA imerudia makosa hayo ya kudhani kuwa ushabiki wa kwenye mitandao ndio kura za nchi nzima; ng'o!
 
Tuacheni propaganda za kutafuta scapegoats za kushindwa na kuchafua jina la nchi kwa sababu za kipuuzi. Nashindwa kuelewa chama kisichokuwa na grassroots kudai kuwa kinaibiwa kura! Mwaka 1995 mimi nikiwa NCCR-mageuzi tulihamasika sana pale Dar tukajua Mrema atachukua nchi, lakini tukasahau kuwa tulikuwa maarufu Dara na miji michache tu kwani hatukuwa na network kuzunguka nchi yote. CHADEMA imerudia makosa hayo ya kudhani kuwa ushabiki wa kwenye mitandao ndio kura za nchi nzima; ng'o!
Una mtindio wa Ubongo sio bure. Karne hii huwez kumdanganya hata mtoto mdogo kwa maneno kama haya.
 
Kwani ratiba ya kuchukua na kurudisha form walijipangia vyama vyenyewe au Tume ndo iliwapangia???

Tusaidiane kueleweshana katika hili
Kila mtu alikuwa anarudisha kwa muda wake. Hakukuwa na ratiba ya kurudisha; ila tume ilikuwa inazuia wasirudishe wagombea zaidi ya momoja katika muda ule ule. Ilikuwa inawezekana kabisa wagombea wengi kurudisha kwa siku moja, ila tume ilikuwa inapokea mmoja mmoja kwa utaratibu wa first come, first serve.
 
Una mtindio wa Ubongo sio bure. Karne hii huwez kumdanganya hata mtoto mdogo kwa maneno kama haya.
Mliokulia katika mazingira ya kulalamika ndio mna matatizo ya ubongo; wengine tumekulia katika mazingira ya maarifa na ubongo wetu umekamilika sawasawa.
 
Back
Top Bottom