LHRC: Sheria Mpya za Uchaguzi zimeacha maoni ya Wadau kuhusu maamuzi ya Tume ya Uchaguzi kuhojiwa Mahakamani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,100
12,558
WhatsApp Image 2024-04-04 at 17.55.03_fcb6c5c7.jpg
Siku chache baada ya uwepo wa taarifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kusaini miswaada ya Sheria za Uchaguzi na kutangazwa kuwa Sheria, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC, kimeeleza kuwa Sheria hiyo hajazingatia baadhi ya mambo muhumu kama ilivyoshauriwa na Wadau kwenye mchakato wa kutoa maoni.

Katika tamko lao ambalo wamelitoa leo Aprili 4, 2024, miongoni mwa mambo ambayo wamedai kuwa waliyashauri kwenye maoni yao ni kwamba Watumishi wa umma kutoendelea kusimamia uchaguzi badala yake Tume huru iwe na Watumishi wake.

"Miongoni mwa mambo ambayo LHRC na Wadau wengi tulishauri, Tume kuajiri Watumishi wake wenyewe ili kuipa uhuru wa kutosha katika utekelejazi wa majukumu yake na kuongeza uaminifu kwa wadau wa uchaguzi.

"Hata hivyo pendekezo hilo halikuchukuliwa badala yake Watumishi wa Umma wameendelea kuwa sehemu ya Tume. Mathalani, kifungu cha 6 cha Sheria hii imeondoa neno Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji, na kuweka neno watumishi wa umma waandamizi kuwa wasimamizi wa uchaguzi," wameeleza LHRC katika tamko hilo.

Akisoma tamko hilo Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga amesema pia Kifungu cha Sheria kimeendelea kuwatambua Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa Maafisa uandikishaji wapiga kura, huku akieleza Kifungu cha 8 kimeendelea kuwatambua Watumishi wa Umma kuwa waratibu wa uchaguzi katika ngazi za mikoa.

Amesema Wakurugenzi wa Halmashauri kwa nafasi zao ni Watumishi waandamizi wa umma, hivyo licha ya kutotajwa wazi kwa nafasi zao bado wanaweza kuwa wasimamizi wa uchaguzi suala ambalo anadai kuwa halileti afueni ya mifumo ya uchaguzi ambayo anadai kuwa imekuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu.

Masuala mengine ambayo yametajwa kuachwa kwenye Sheria hiyo ni pamoja suala la mgombea binafsi, ambapo imeelezwa wazi kuwa Sheria hiyo bado haimtambui mgombea binafsi, jambo ambalo wanadai kuwa wao wanaamini kwamba uwepo mgombea binafsi unaweza kuchochea ukuaji wa demokrasia pamoja na kuongeza wigo wa watanzania kuwa na haki ya kuchagua na haki ya kuchaguliwa bila kulazimika kupitia mkondo wa vyama vya siasa.

Aidha, suala lingine ambalo wamedai limeachwa kwenye Sheria hiyo ni uamuzi wa Tume kuendelea kutohojiwa Mahakamani.

"Kwa upande mwingine, LHRC na wadau wengine tulipendekeza maamuzi ya Tume ya Uchaguzi kuhojiwa Mahakamani kwa njia za mapitio au mashauri ya kikatiba hata hivyo bado maamuzi ya Tume yatakuwa ya mwisho na hayatohojiwa Mahakamani."

LHRC imeeleza kwa mujibu wa vifungu vya 36(6), 53(6) na 65(7) vya Sheria, maamuzi ya Tume juu ya Mgombea Urais, Ubunge na Udiwani kukatikiwa uteuzi maamuzi yatakuwa yamwisho na hayatohojiwa Mahakamani kitendo ambacho wamedai ni kinakiuka Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.

Pamoja na hayo masuala mengine ni ambayo wamedai kuwa hajazingatiwa kwenye Sheria hiyo ni Uchaguzi wa Serikalini za Mitaa, Vijiji kuendelea kusimimwa na TAMISEMI, suala lingine ni Wajibu wa vyombo vya habari, Matumizi ya Teknolojia.

Kuhusu matumizi ya Teknolojia wamesema "LHRC pamoja na wadau wengine wa demokrasia tulipendekeza matumizi ya teknolojia katika mchakato wa uchaguzi kwenye hatua zote yaani uandikishaji.

Hata hivyo LHRC imeshauri kufanyike marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 ili kuweka takwa la ulazima midahalo ya wagumbea katika ngazi zote.

Pia wametoa wito kwa Serikali kuwasilisha mswaada wa Sheria utakaotoa fursa ya kufanya mabadiliko ya Katiba ili kuruhusu baadhi masuala ambayo kwa uasili wake hayawezi kufanyiwa marekebisho bila kugusa Katiba.

Sambamba na hilo wametoa wito kwa Serikali kuwasilisha mswaada wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 10(1) (C) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024.

Lakini pia wametoa wito wao kwa Serikali kutekeleza uamuzi wa Mahakama Kuu katika shauri la Tito Elia Magoti dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyowapa wafungwa haki ya kupiga kura.

Hata hivyo katika tamko lao wameahinsha baadhi masuala chanya ambayo wamebaini katika Sheria hizo mpya, kati ya masuala hayo ni kwamba, Sheria imefuta suala la wagombea kupita bila kupingwa katika ngazi zote (Rais, Ubunge na Udiwani), jambo lingine ni Sharti la Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume kufanyiwa usaili.

========= =================

UCHAMBUZI WA LHRC KUHUSU SHERIA ZA UCHAGUZI BAADA YA KUSAINIWA NA MHE. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Dar es Salaam, tarehe 4 Aprili, 2024
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimewaalika leo ili kutoa maoni yake baada ya kufanya uchambuzi wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2024; Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, 2024 na Sheria ya Masuala ya Vyama vya Siasa na Gharama za Uchaguzi, zilipotishwa na Bunge na baadae kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Tamko hili linatolewa kwa msingi wa kwamba, LHRC imehusika kikamilifu katika jitihada za uchechemuzi na maboresho ya mfumo wa uchaguzi na vyama vya siasa, pia kama mdau aliyefanya uchambuzi wa miswada na baadae kuwasilisha maoni mbele ya Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria jijini Dodoma.

Mnamo tarehe 02 Februari 2024, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilijadili na kupitisha miswada mitatu (3) ikiwemo Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2024; Muswada wa Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi, 2024 na Muswada wa masuala Vyama vya Siasa, 2024. Bunge kwa mamlaka liliyonayo kwa mujibu wa Ibara ya 64 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 na Kanuni ya 84 hadi 88 ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la mwaka 2021.

Itakumbukwa kwamba, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ilifanya vikao vya kupokea maoni ya wadau (public hearing) kuhusu miswada hiyo siku ya tarehe 6 hadi 10 Januari 2024, Bunge lilijadili na kuipitisha miswada hiyo mapema mwezi Februari, 2024 na baadae kusainiwa na Rais Samia kuwa sheria kwa mujibu wa Ibara ya 97 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na kuchapishwa katika gazeti la Serikali la tarehe 22 Machi 2023.

Ni wazi kwamba, kuletwa kwa miswada hiyo kulileta matumaini mapya katika Taifa la Tanzania kufuatia hitaji la muda mrefu juu ya maboresho ya mfumo wa uchaguzi na vyama vya siasa. Hata hivyo, wadau tulitegemea kuletwa kwa muswada mwingine wa mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ili kuipa maana zaidi nia ya kufanya maboresho ya mifumo hiyo. Kutokuletwa kwa muswada huo kulipunguza matumaini ya wadau wa demokrasia kuhusu mustakabali ya maboresho makubwa ya mfumo wa uchaguzi na vyama vya siasa.

LHRC inaendelea kutoarai kwa Serikali kuleta Muswada wa Mabadiliko ya Katiba, 2024 ili kufanikisha maboresho makubwa yanayotarajiwa kama ilivyopendekezwa na wadau pamoja na mapendekezo ya Ripoti ya Kikosi Kazi cha Demokrasia ya Vyama Vingi iliyowasilishwa na Prof. Rwekaza Mukandala Mwenyetiki wa Kikosi Kazi hicho (tarehe 21 Oktoba 2022) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pamoja na msisitizo huo, LHRC imebaini masuala chanya kadhaa yaliyomo katika Sheria hizi mpya kama ifuatavyo;

1. Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa, Jiji na Wilaya wameondolewa kuwa wasimamizi wa uchaguzi ingawa wamebaki kuwa waandikishaji wa uchaguzi.

2. Sheria imeweka sifa ya mtu kuwa msimamizi wa uchaguzi; (i) awe hajawahi kutiwa hatiani katika shauri la nidhamu au kosa lolote la jinai;

(ii) awe hajawahi kuadhibiwa kwa kifungo kinachozidi miezi sita (6);

(iii) na hajawahi kuwa kiongozi wa chama cha siasa.

3. Pia sheria imefuta suala la wagombea kupita bila kupingwa katika ngazi zote ( Rais, Ubunge na Madiwani)

4. Sharti la Mwenyekiti, Makamu Mwenyetiki na wajumbe wa Tume kufanyiwa usaili.

5. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kusimamiwa na Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi.

6. Kufutwa kwa sharti la kulipia ada yakupata upya kadi ya mpiga kura iliyoharibika au kupotea.

7. Mashauri ya uchaguzi kusikilizwa ndani ya miezi 6 kwa nafasi ya kiti cha Ubunge tofauti na pendekezo la miezi 12 kama ilivyokuwa kwenye muswada. Hata hivyo mashauri ya uchaguzi kwa ngazi ya udiwani yatasikilizwa kwa miezi 12 ambayo bado tunaona ni muda mrefu.

1. UCHAMBUZI WA MASUALA YALIYOACHWA KWENYE SHERIA HIZI.

A. Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani No.2, 2024

Kuna mambo ya msingi ambayo LHRC na wadau wengi wa demokrasia tulitamani yawe sehemu ya sheria, lakini baada ya kufanya uchambuzi wa sheria hii (Post enactment analysis) tumebaini mambo muhimu ambayo wadau tuliyotarajia yamebaki kama yalivyo baada ya muswada huu kuwa sheria.

Masuala hayo ni kama ifuatavyo;

1. Watumishi wa umma kuendelea kuwa sehemu ya Tume.
Miongoni mwa mambo ambayo LHRC na wadau wengi tulishauri, Tume kuajiri watumishi wake yenyewe ili kuipa uhuru wa kutosha katika utekeleza wa majukumu yake na kuongeza uaminifu kwa wadau wa uchaguzi. Hata hivyo pendekezo hili halikuchukuliwa badala yake watumishi wa umma wameendelea kuwa sehemu ya Tume. Mathalani, kifungu cha 6 cha Sheria hii imeondoa neno Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji, na kuweka neno watumishi wa umma waandamizi kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Pia Kifungu cha 7 cha sheria kimeendelea kuwatambua Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa maafisa uandikishaji wapiga kura, Aidha kifungu cha 8 kimeendelea kuwatambua watumishi wa umma kuwa waratibu wa uchaguzi katika ngazi za mikoa.

Kwa tafsiri ya kisheria ni kwamba, Wakurugenzi wa Halmashauri kwa nafasi zao ni watumishi waandamizi wa umma hivyo licha ya kutotajwa kwa nafasi zao bado wanaweza kuwa wasimamizi wa uchaguzi suala ambalo linaendelea kutotibu wala kuleta afueni ya mifumo ya uchaguzi ambayo imekuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu.

2. Matumizi ya Teknolojia
Katika eneo ambalo LHRC na wadau wengine wa demokrasia tulipendekeza ni matumizi ya teknolojia katika mchakato wa uchaguzi kwenye hatua zote yaani uandikishaji, uchukuaji na uwasilishaji wa fomu za uteuzi wa wagombea, upigaji kura na kutangazwa kwa matokeo. Kwa mfano, Vifungu vya 12, 16(5), 34(2) na 50(7) vya sheria tulipendekeza uandishikishaji na uwasilishwaji wa fomu za wagombea ufanyike kwa njia za kielektroniki. Hata hivyo baada ya kupitishwa kwa sheria hii tumebaini kuwa kifungu kimepitishwa kama kilivyokuwa kwenye muswada.

Eneo lingine ni kifungu cha 166 kinachoweka takwa la matumizi ya teknolojia kuwa hiari ambapo LHRC na wadau wengine tulipendekeza matumizi ya teknolojia kwa mujibu wa kifungu cha 166 cha sheria kuwa ya lazima lakini baada ya kupitia sheria tumebaini kuwa kifungu hiki kimebaki kama kilivyo.

3. Suala la Mgombea Binafsi
Licha ya kuwepo kwa maamuzi mbalimbali ya Mahakama za ndani na za kikanda zilitoa maamuzi ya kuwepo wa mgombea binafsi lakini bado kumekuwepo na kusita kufanya maamuzi ya kurekebisha Katiba na sheria juu ya suala hili. Kwa mfano Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu katika shauri Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Serikali ya Tanzania 1, kwa mujibu wa Ibara ya 39(1) (c) na Ibara ya 67(1) ( b) pamoja na masharti ya Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 1979, mtu hatakuwa na sifa za kuchaguliwa kuwa Rais, Mbunge au diwani isipokuwa kama ni mwanachama wa chama cha siasa.

Pia kwa mujibu wa vifungu vya 32, 55 na 60 vya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2024, moja ya sifa ya mtu kuchaguliwa kuwa Rais, Mbunge au Diwani ni lazima awe anatokana na chama cha siasa, hii

1 Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Serikali ya Tanzania, Maombi No.011/2011
inathibitisha kutochukuliwa kwa maoni ya wadau tuliotaka uwepo wa mgombea binafsi, licha ya LHRC na wadau wengine kupendekeza mabadiliko madogo ya katiba katika ibara za 67(1)(b) na 39(1)(c) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ili kuruhusu uwepo wa mgombea binafsi lakini bado Serikali haijafanyia kazi.

Ni Imani yetu kwamba, uwepo wa mgombea binafsi utatachoea ukuaji wa demokrasia pamoja na kuongeza wigo wa watanzania kuwa na haki ya kuchaguliwa bila kulazimika kupitia mkondo wa vyama vya siasa.

4. Maamuzi ya Tume kutohojiwa Mahakamani
Kwa upande mwingine, LHRC na wadau tulipendekeza maamuzi ya Tume ya Uchaguzi kuhojiwa Mahakamani kwa njia za mapitio au mashauri ya kikatiba hata hivyo bado maamuzi ya tume yatakuwa ya mwisho na hayatahojiwa Mahakamani. Kwa mujibu wa vifungu vya 36(6), 53(6), na 65(7) vya sheria, maamuzi ya tume juu ya mgombea wa urais, Ubunge na udiwani kukatiliwa uteuzi yatakuwa ya mwisho na hayatahojiwa mahakamani kitendo ambacho wadau tulithitisha kinakiuka Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977. Mahakama kuu katika shauri la 1 Prisca Chogero dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania2, iliamua kwamba maamuzi ya mamlaka za Serikali kutohojiwa Mahakamani ni kukiuka ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.

5. Wajibu wa Vyombo vya Habari
Moja ya eneo ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu ni vyombo vya habari kutotenda haki kwa wagombea wote kwa usawa wakati wa urushaji wa matangazo na vipindi vya kampeni. Kumekuwa na malalamiko kwa vyombo vya habari kupendelea wagombea wa upande mmoja hii ilitokana na upungufu uliopo katika sheria zetu za uchaguzi kutokuwa na mifumo ya kuviwajibisha vyombo vya habari vinavyokiuka taratibu wakati wa kampeni.

LHRC na wadau wengine tulipendekeza kuwepo na mfumo wa kuviwajibisha vyombo vya habari vinavyokiuka taratibu au mizania ya usawa wakati wa kampeni ili kuondoa malalamiko miongoni mwa wadau. Kwa mujibu wa kifungu cha 74 cha sheria kimebaki kama kilivyokuwa kwenye mswaada huku vyombo vya habari binafsi vikiwa si sehemu ya wajibu huo.

1. Upatikanaji wa wabunge na madiwani wanawake wa viti maalumu
Moja ya eneo ambalo limekuwa na mjadala mkubwa katika miaka ya hivi karibuni ni upatikanaji na utaratibu unaotumika sasa kuwapata wabunge na Madiwani Wanawake wa Viti Maalumu. Kwa mujibu wa ibara za 66, 67,76(3) na 78 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 utaratibu unaotumika kuwapata wabunge wa viti maalumu unatokana na uwiano wa kura zote za wabunge ambazo chama husika kilipata wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Licha ya ibara ya 81 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 kuipa fursa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwamba yaweza kuweka masharti yanayofafanua utaratibu utakaotumiwa na vyama vya siasa kuteua wabunge wanawake wa viti maalumu lakini mpaka sasa vyama vya siasa ndio vimebaki kuwa na mamlaka na hatima ya ubunge huu.

Kifungu cha 112 kinachohusu uteuzi wa wabunge wanawake wa viti maalumu kimeendelea kubaki kama kilivyo. Kutokana na ukweli kwamba suala hili ni suala la kikatiba hivyo ili kufanya mabadiliko katika kifungu hiki ni lazima tufanye mabadiliko madogo ya katiba kwa kuzifumua ibara za 66, 67, 76(3), 78 na 81 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.ili kuruhusu mfumo wa uwakilishi yaani (quota system) utumike ambapo wabunge wa viti maalumu watapatikana kwa kuchaguliwa na wananchi wenyewe kama ambavyo jirani zetu wa Kenya wanafanya yaani (women representative).

Hali kadhalika kifungu cha 113 cha sheria kinachohusu uteuzi wa madiwani wanawake wa viti maalumu kimebaki kama kilivyokuwa kwenye muswada ambapo napo utaratibu unafanana na ule wa kuwapata wabunge wa viti maalumu.

2. Sharti la dhamana kwenye mashauri ya uchaguzi
Licha ya Mahakama ya rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika shauri la Julius Ishengoma Francis Ndyanabo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Rufaa No. 64 ya mwaka 2001/2002, Mahakama ya Rufani Dar es Salaam3, kutamka kwamba sharti la dhamana katika mashauri ya uchaguzi ni kukiuka ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.4 na ni kukiuka haki ya wananchi kuzifikia mahakama, na licha ya LHRC na wadau kushauri sharti hili lifutwe lakini bado vifungu vya 140 na 150(2) vya sheria vimebaki na sharti hili kwa maana ya kwamba mashauri ya uchaguzi ya ubunge na udiwani hayatasikilizwa mpaka pale mlalamikaji atakapokuwa amelipa kiasi cha fedha kama dhamana kama itavyoamuliwa na msajili wa mahakama.

3. Matokeo ya Urais kutohojiwa Mahakamani
Kwa mujibu wa ibara ya5, iwapo mgombea wa kiti cha Urais atatangazwa na Tume ya uchaguzi kuwa ameshinda ushindi wake hautahojiwa mahakamani, tunatambua kuwa sharti hili ni la kikatiba hivyo ili kufanyiwa marekebisho ni lazima tufanye mabadiliko madogo ya katiba ili kuifanya marekebisho ibara ya 41(7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ili matokeo ya Urais yaweze kuhojiwa mahakamani.

B. Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi No. 2. 2024
Sheria nyingine ambayo tungependa kuwafahamisha ni Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Kuna masuala muhimu ambayo pia tulitamani yawe sehemu ya sheria hii lakini bado yameendelea kubaki kama yalivyo.

1. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na vitongoji kuendelea kusimamiwa na TAMISEMI.
Licha ya kifungu cha 10(1)(c) cha Sheria kuanisha kwamba moja ya majukumu ya tume yatakuwa ni kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Serikali za Vijiji, Mitaa na Vitongoji Tanzania Bara, lakini ili Tume iweze kutekeleza wajibu huu ni lazima kuwe na utaratibu utakaoainishwa na sheria itakayotungwa na Bunge. Hata hivyo Bunge bado halijatunga sheria inayoainisha utaratibu huo hivyo uchaguzi huu kuendelea kuwa chini ya TAMISEMI kwa kanuni za Waziri mwenye dhamana na wizara husika.

2. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa tume waliopo sasa kuendelea na nafasi zao baada ya kuanza kutumika kwa sheria hii
Licha ya wadau wengi kufurahishwa na kuchukuliwa kwa pendekezo la muda mrefu la kuwepo kwa mfumo huru wa namna ya kupatikana kwa tume, na licha ya kifungu cha 10 cha sheria kuanzisha Kamati ya usaili kwa ajili ya kuwapata Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine wa Tume lakini kwa wakati huohuo kifungu cha 27 cha sheria kinasema Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume waliopo sasa wataendelea na nafasi zao hata baada ya sheria hii kuanza kutumika rasmi.

Kwa lugha rahisi ni kwamba kamati ya usaili iliyoanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha sheria haitaanza kazi ya kusaili Mwenyekiti, Makamu Mwenyeti na Wajumbe wengine wa tume waliopo madarakani hivi sasa mpaka pale watakapomaliza nafasi zao za utumishi baada ya miaka mitano. Kwa lugha nyingine Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine wa tume watakoma katika nafasi zao kati ya mwaka 2028 na 2029 hivyo kamati ya usaili itaanza zoezi la kusaili watu hao.

C. Sheria ya Vyama Vya Siasa 2024
1. Ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia, watu wenye ulemavu pamoja na vijana

Katika eneo ambalo LHRC na wadau wengine tumekuwa na msukumo mkubwa wa kuona mabadiliko ni ujumuishwaji wa kijinsia, watu wenye ulemavu pamoja na vijana. Kwa mujibu wa kifungu cha 10C cha sheria, moja ya nyaraka za lazima ambazo chama cha siasa kitalazimika kuwa nazo ni pamoja na sera ya jinsia na ujumuishwaji, hata hivyo bado kifungu hiki hakijaweka mfumo wa kuviwajibisha vyama vya siasa ambavyo vitashindwa kutekeleza takwa hili.

Pili, bado masuala ya kijinsia na ujumuishwaji katika vyama vya siasa hajapewa kipaumbele katika sheria hizi kama matarajio waliokuwa nayo wadau.

Licha ya LHRC kuainisha mambo muhimu ambayo hayakuzingatiwa na sheria hizi, hata hivyo tunapenda kuchukua fursa hii kuainisha baadhi ya masuala ambayo yamezingatiwa katika sheria hizi ambayo LHRC inaona ni mambo mazuri, masuala hayo ni Pamoja.

2. 1. Hitimisho
Mwisho, napenda kuchukua fursa hii kutoa wito kwa Serikali kama ifuatavyo:

1. Kuwasilisha mswada wa sheria utakaotoa fursa ya kufanya mabadiliko ya katiba ili kuruhusu baadhi ya masuala ambayo kwa uasili wake hayawezi kufanyiwa marekebisho bila kugusa katiba.

2. Serikali iwasilishe muswada wa sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kama ilivyoanishwa katika kifungu cha 10 (1) (c) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024.

3. Serikali itekeleze maamuzi ya Mahakama Kuu katika shauri la Tito Elia Magoti dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi 6 iliyowapa wafungwa haki ya kupiga kura.

4. Licha ya Serikali kukubaliana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuwa suala la watanzania waishio nje ya nchi(Diaspora) kupiga kura lina mashiko lakini haikuwa tayari kulifanya suala hili kuwa la kisheria. Hivyo LHRC inaikumbusha Serikali kurejea makubaliano yake na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.

5. Kufanya marekebisho Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2024 ili kuweka takwa la ulazima wa kufanya midahalo ya wagombea katika ngazi zote.

Imetolewa na:
Dkt. Anna Henga Mkurugenzi Mtendaji
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
 
CCM NI JANGA LA TAIFA HILI NI ZAIDI YA MKOLONI MZUNGU, WANACHOWAZA NI KUIBA TU NA KULINDANA
 
Kuna kipindi hiki kituo kilikua tawi la chama fulani ilibaki nusu tu kiongozi wake kumpigia kampeni mgombea wa chama fulani!
 
Hapo ni changa la moto ccm ndo watakaoleta vurugu nchi hii sababu hawako tayari kwa mabadiliko mpaka hapo nguvu ya umma itakapotumika vinginevyo hawa watu watatusumbua sana na wanataka kutawala milele kwa gharama yoyote ile
Nakubaliana na wewe mkuu
 
✍️🧠Nimesoma vizuri huo uzi, nilichogundua viongozi wetu ni walafi wa madaraka, yaani uongozi umegeuzwa mitaji, Sasa hivi kiongozi hatafuti uongozi ili kusimama badala ya wananchi ni kwa maslahi yake binafsi.

Ukichunguza vizuri hiyo miswaada iliopitishwa na kuwa sheria, kilichobadirika ni maneno tu ila jambo ni lile lile,

Viongozi wanatengeza mifumo ya kuendelea kuwa madarakani kwa kuipiga chenga sheria katiba na mapendekezo ya maboresho ya katiba

Huwezi sema umeondoa utaratibu wa kupita bila kupingwa ikiwa tume huru inasimamiwa na watu wale wale, wakurugenzi wa halmashauri ambao mmewafunika kwa kivuli cha kuwaita watumishi wa umma,

Tume bado inakuwa na uwezo mkubwa wa kutotoa haki stahiki kwa mgombea maana wamekikataa kifungu cha mswaada kinachoitaka tume kuhojiwa mahakamani baada ya uchaguzi

Badala yake wanasema tume ndio yenye maamuzi ya mwisho,

Kama huwezi kuhojiwa juu ya makosa yako utakoswa nguvu ya kufanya unachotaka....? !! Daaah...!!

Wananchi bila kishikamana, tutaendelea kuwanufaisha watu wachache huku familia zetu zikiendelea kuwa na maisha duni . Siasa inatuumiza saana. 😔
 
Bila ya kuongea lugha ya haya watawala ambayo wanalazimika kusikiliza,kutakua na blah blah tu hapa nchini,hapa Africa kama huishi Mauritius 🇲🇺,ushelisheli,Ghana,Botswana,Namibia,jielewe kuwa unaishi ndani ya police state,hapo SA fuatilia kampeni zao zilivyo huru na uchaguzi huru hapo 29th May,shughudia ANC wakipewa red card,future ya demokrasia Africa ni coalitions government
 
1 Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Serikali ya Tanzania, Maombi No.011/2011
inathibitisha kutochukuliwa kwa maoni ya wadau tuliotaka uwepo wa mgombea binafsi, licha ya LHRC na wadau wengine kupendekeza mabadiliko madogo ya katiba katika ibara za 67(1)(b) na 39(1)(c) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ili kuruhusu uwepo wa mgombea binafsi lakini bado Serikali haijafanyia kazi.

Ni Imani yetu kwamba, uwepo wa mgombea binafsi utatachoea ukuaji wa demokrasia pamoja na kuongeza wigo wa watanzania kuwa na haki ya kuchaguliwa bila kulazimika kupitia mkondo wa vyama vya siasa.
Mkuu Roving Journalist , asante sana kwa uzi huu, ibara za 67(1)(b) na 39(1)(c) za Katiba yetu ni ibara batili, zinakwenda kinyume cha Ibara ya 5 na 21 ya katiba, kwa kupora haki zilizotolewa na ibara moja kupokwa na ibara nyingine!.

Ibara hizo batili, zilichomekewa kiubadili ndani ya katiba yetu na Bunge letu Tukufu baada serikali kupeleka Bungeni muswada batili wa mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, ambayo ni batili!, na Bunge letu la wakati huo lilivyo Bunge goigoi, lililoshehenezwa wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, wakaupitisha ubatili huo, na kuinajisi katiba yetu!. Je ukiwaita wabunge hawa ni sawa na mazuzu, ni kuwaonea?.

Mahakama Kuu ikatoa hukumu kuwa vifungu hivyo ni batili, vinakwenda kinyume cha katiba ya JMT, na mabadiliko hayo ya katiba kwa hati ya dharura ni mabadiliko batili!.

Japo serikali ilikata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi huo, Mahakama ya Rufaa haikupinga the contents za uamuzi wa Mahakama Kuu, bali ilipinga taratibu za Mahakama Kuu kutoa uamuzi wa jambo ambalo limeisha chomemekewa kwenye katiba, hata kama uchomekeaji huo ni kwa ubatili!, na kulirudisha Bungeni kwa waliolichomeka ndio walichomoe!.

Yaani mwizi baada ya kuiba, na akakamatwa ready handed na alichokwiba mkononi, unamshitaki mahakamani, na kile alichokwiba kimeletwa Mahakamani kama evidence. Mahakama inatoa uamuzi, hicho alichokwiba akabidhiwe yule yule mwizi, kwa vile yeye ndio alikiiba, ni yeye ndie akirudishe alipokiiba!, end of the case!.

Mimi mwenyewe tuu, humu ndani nimepandisha mabandiko zaidi ya 50 ya jambo hili.

P
 
Asante sana Mhe. Rais Samia kwa kuonesha njia ya kupanua Wigo wa demokrasia nchini!
 
TUME UHURU KATIKA UCHAGUZI!! Forget about this it won't happen here in Tanzania never ever!
Kwamba ccm ijichimbie kaburi la sahau?!!
 
Siku chache baada ya uwepo wa taarifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kusaini miswaada ya Sheria za Uchaguzi na kutangazwa kuwa Sheria, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC, kimeeleza kuwa Sheria hiyo hajazingatia baadhi ya mambo muhumu kama ilivyoshauriwa na Wadau kwenye mchakato wa kutoa maoni.

Katika tamko lao ambalo wamelitoa leo Aprili 4, 2024, miongoni mwa mambo ambayo wamedai kuwa waliyashauri kwenye maoni yao ni kwamba Watumishi wa umma kutoendelea kusimamia uchaguzi badala yake Tume huru iwe na Watumishi wake.

"Miongoni mwa mambo ambayo LHRC na Wadau wengi tulishauri, Tume kuajiri Watumishi wake wenyewe ili kuipa uhuru wa kutosha katika utekelejazi wa majukumu yake na kuongeza uaminifu kwa wadau wa uchaguzi.

"Hata hivyo pendekezo hilo halikuchukuliwa badala yake Watumishi wa Umma wameendelea kuwa sehemu ya Tume. Mathalani, kifungu cha 6 cha Sheria hii imeondoa neno Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji, na kuweka neno watumishi wa umma waandamizi kuwa wasimamizi wa uchaguzi," wameeleza LHRC katika tamko hilo.

Akisoma tamko hilo Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga amesema pia Kifungu cha Sheria kimeendelea kuwatambua Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa Maafisa uandikishaji wapiga kura, huku akieleza Kifungu cha 8 kimeendelea kuwatambua Watumishi wa Umma kuwa waratibu wa uchaguzi katika ngazi za mikoa.

Amesema Wakurugenzi wa Halmashauri kwa nafasi zao ni Watumishi waandamizi wa umma, hivyo licha ya kutotajwa wazi kwa nafasi zao bado wanaweza kuwa wasimamizi wa uchaguzi suala ambalo anadai kuwa halileti afueni ya mifumo ya uchaguzi ambayo anadai kuwa imekuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu.

Masuala mengine ambayo yametajwa kuachwa kwenye Sheria hiyo ni pamoja suala la mgombea binafsi, ambapo imeelezwa wazi kuwa Sheria hiyo bado haimtambui mgombea binafsi, jambo ambalo wanadai kuwa wao wanaamini kwamba uwepo mgombea binafsi unaweza kuchochea ukuaji wa demokrasia pamoja na kuongeza wigo wa watanzania kuwa na haki ya kuchagua na haki ya kuchaguliwa bila kulazimika kupitia mkondo wa vyama vya siasa.

Aidha, suala lingine ambalo wamedai limeachwa kwenye Sheria hiyo ni uamuzi wa Tume kuendelea kutohojiwa Mahakamani.

"Kwa upande mwingine, LHRC na wadau wengine tulipendekeza maamuzi ya Tume ya Uchaguzi kuhojiwa Mahakamani kwa njia za mapitio au mashauri ya kikatiba hata hivyo bado maamuzi ya Tume yatakuwa ya mwisho na hayatohojiwa Mahakamani."

LHRC imeeleza kwa mujibu wa vifungu vya 36(6), 53(6) na 65(7) vya Sheria, maamuzi ya Tume juu ya Mgombea Urais, Ubunge na Udiwani kukatikiwa uteuzi maamuzi yatakuwa yamwisho na hayatohojiwa Mahakamani kitendo ambacho wamedai ni kinakiuka Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.

Pamoja na hayo masuala mengine ni ambayo wamedai kuwa hajazingatiwa kwenye Sheria hiyo ni Uchaguzi wa Serikalini za Mitaa, Vijiji kuendelea kusimimwa na TAMISEMI, suala lingine ni Wajibu wa vyombo vya habari, Matumizi ya Teknolojia.

Kuhusu matumizi ya Teknolojia wamesema "LHRC pamoja na wadau wengine wa demokrasia tulipendekeza matumizi ya teknolojia katika mchakato wa uchaguzi kwenye hatua zote yaani uandikishaji.

Hata hivyo LHRC imeshauri kufanyike marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 ili kuweka takwa la ulazima midahalo ya wagumbea katika ngazi zote.

Pia wametoa wito kwa Serikali kuwasilisha mswaada wa Sheria utakaotoa fursa ya kufanya mabadiliko ya Katiba ili kuruhusu baadhi masuala ambayo kwa uasili wake hayawezi kufanyiwa marekebisho bila kugusa Katiba.

Sambamba na hilo wametoa wito kwa Serikali kuwasilisha mswaada wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 10(1) (C) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024.

Lakini pia wametoa wito wao kwa Serikali kutekeleza uamuzi wa Mahakama Kuu katika shauri la Tito Elia Magoti dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyowapa wafungwa haki ya kupiga kura.

Hata hivyo katika tamko lao wameahinsha baadhi masuala chanya ambayo wamebaini katika Sheria hizo mpya, kati ya masuala hayo ni kwamba, Sheria imefuta suala la wagombea kupita bila kupingwa katika ngazi zote (Rais, Ubunge na Udiwani), jambo lingine ni Sharti la Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume kufanyiwa usaili.

========= =================

UCHAMBUZI WA LHRC KUHUSU SHERIA ZA UCHAGUZI BAADA YA KUSAINIWA NA MHE. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Dar es Salaam, tarehe 4 Aprili, 2024
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimewaalika leo ili kutoa maoni yake baada ya kufanya uchambuzi wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2024; Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, 2024 na Sheria ya Masuala ya Vyama vya Siasa na Gharama za Uchaguzi, zilipotishwa na Bunge na baadae kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Tamko hili linatolewa kwa msingi wa kwamba, LHRC imehusika kikamilifu katika jitihada za uchechemuzi na maboresho ya mfumo wa uchaguzi na vyama vya siasa, pia kama mdau aliyefanya uchambuzi wa miswada na baadae kuwasilisha maoni mbele ya Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria jijini Dodoma.

Mnamo tarehe 02 Februari 2024, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilijadili na kupitisha miswada mitatu (3) ikiwemo Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2024; Muswada wa Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi, 2024 na Muswada wa masuala Vyama vya Siasa, 2024. Bunge kwa mamlaka liliyonayo kwa mujibu wa Ibara ya 64 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 na Kanuni ya 84 hadi 88 ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la mwaka 2021.

Itakumbukwa kwamba, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ilifanya vikao vya kupokea maoni ya wadau (public hearing) kuhusu miswada hiyo siku ya tarehe 6 hadi 10 Januari 2024, Bunge lilijadili na kuipitisha miswada hiyo mapema mwezi Februari, 2024 na baadae kusainiwa na Rais Samia kuwa sheria kwa mujibu wa Ibara ya 97 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na kuchapishwa katika gazeti la Serikali la tarehe 22 Machi 2023.

Ni wazi kwamba, kuletwa kwa miswada hiyo kulileta matumaini mapya katika Taifa la Tanzania kufuatia hitaji la muda mrefu juu ya maboresho ya mfumo wa uchaguzi na vyama vya siasa. Hata hivyo, wadau tulitegemea kuletwa kwa muswada mwingine wa mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ili kuipa maana zaidi nia ya kufanya maboresho ya mifumo hiyo. Kutokuletwa kwa muswada huo kulipunguza matumaini ya wadau wa demokrasia kuhusu mustakabali ya maboresho makubwa ya mfumo wa uchaguzi na vyama vya siasa.

LHRC inaendelea kutoarai kwa Serikali kuleta Muswada wa Mabadiliko ya Katiba, 2024 ili kufanikisha maboresho makubwa yanayotarajiwa kama ilivyopendekezwa na wadau pamoja na mapendekezo ya Ripoti ya Kikosi Kazi cha Demokrasia ya Vyama Vingi iliyowasilishwa na Prof. Rwekaza Mukandala Mwenyetiki wa Kikosi Kazi hicho (tarehe 21 Oktoba 2022) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pamoja na msisitizo huo, LHRC imebaini masuala chanya kadhaa yaliyomo katika Sheria hizi mpya kama ifuatavyo;

1. Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa, Jiji na Wilaya wameondolewa kuwa wasimamizi wa uchaguzi ingawa wamebaki kuwa waandikishaji wa uchaguzi.

2. Sheria imeweka sifa ya mtu kuwa msimamizi wa uchaguzi; (i) awe hajawahi kutiwa hatiani katika shauri la nidhamu au kosa lolote la jinai;

(ii) awe hajawahi kuadhibiwa kwa kifungo kinachozidi miezi sita (6);

(iii) na hajawahi kuwa kiongozi wa chama cha siasa.

3. Pia sheria imefuta suala la wagombea kupita bila kupingwa katika ngazi zote ( Rais, Ubunge na Madiwani)

4. Sharti la Mwenyekiti, Makamu Mwenyetiki na wajumbe wa Tume kufanyiwa usaili.

5. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kusimamiwa na Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi.

6. Kufutwa kwa sharti la kulipia ada yakupata upya kadi ya mpiga kura iliyoharibika au kupotea.

7. Mashauri ya uchaguzi kusikilizwa ndani ya miezi 6 kwa nafasi ya kiti cha Ubunge tofauti na pendekezo la miezi 12 kama ilivyokuwa kwenye muswada. Hata hivyo mashauri ya uchaguzi kwa ngazi ya udiwani yatasikilizwa kwa miezi 12 ambayo bado tunaona ni muda mrefu.

1. UCHAMBUZI WA MASUALA YALIYOACHWA KWENYE SHERIA HIZI.

A. Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani No.2, 2024

Kuna mambo ya msingi ambayo LHRC na wadau wengi wa demokrasia tulitamani yawe sehemu ya sheria, lakini baada ya kufanya uchambuzi wa sheria hii (Post enactment analysis) tumebaini mambo muhimu ambayo wadau tuliyotarajia yamebaki kama yalivyo baada ya muswada huu kuwa sheria.

Masuala hayo ni kama ifuatavyo;

1. Watumishi wa umma kuendelea kuwa sehemu ya Tume.
Miongoni mwa mambo ambayo LHRC na wadau wengi tulishauri, Tume kuajiri watumishi wake yenyewe ili kuipa uhuru wa kutosha katika utekeleza wa majukumu yake na kuongeza uaminifu kwa wadau wa uchaguzi. Hata hivyo pendekezo hili halikuchukuliwa badala yake watumishi wa umma wameendelea kuwa sehemu ya Tume. Mathalani, kifungu cha 6 cha Sheria hii imeondoa neno Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji, na kuweka neno watumishi wa umma waandamizi kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Pia Kifungu cha 7 cha sheria kimeendelea kuwatambua Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa maafisa uandikishaji wapiga kura, Aidha kifungu cha 8 kimeendelea kuwatambua watumishi wa umma kuwa waratibu wa uchaguzi katika ngazi za mikoa.

Kwa tafsiri ya kisheria ni kwamba, Wakurugenzi wa Halmashauri kwa nafasi zao ni watumishi waandamizi wa umma hivyo licha ya kutotajwa kwa nafasi zao bado wanaweza kuwa wasimamizi wa uchaguzi suala ambalo linaendelea kutotibu wala kuleta afueni ya mifumo ya uchaguzi ambayo imekuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu.

2. Matumizi ya Teknolojia
Katika eneo ambalo LHRC na wadau wengine wa demokrasia tulipendekeza ni matumizi ya teknolojia katika mchakato wa uchaguzi kwenye hatua zote yaani uandikishaji, uchukuaji na uwasilishaji wa fomu za uteuzi wa wagombea, upigaji kura na kutangazwa kwa matokeo. Kwa mfano, Vifungu vya 12, 16(5), 34(2) na 50(7) vya sheria tulipendekeza uandishikishaji na uwasilishwaji wa fomu za wagombea ufanyike kwa njia za kielektroniki. Hata hivyo baada ya kupitishwa kwa sheria hii tumebaini kuwa kifungu kimepitishwa kama kilivyokuwa kwenye muswada.

Eneo lingine ni kifungu cha 166 kinachoweka takwa la matumizi ya teknolojia kuwa hiari ambapo LHRC na wadau wengine tulipendekeza matumizi ya teknolojia kwa mujibu wa kifungu cha 166 cha sheria kuwa ya lazima lakini baada ya kupitia sheria tumebaini kuwa kifungu hiki kimebaki kama kilivyo.

3. Suala la Mgombea Binafsi
Licha ya kuwepo kwa maamuzi mbalimbali ya Mahakama za ndani na za kikanda zilitoa maamuzi ya kuwepo wa mgombea binafsi lakini bado kumekuwepo na kusita kufanya maamuzi ya kurekebisha Katiba na sheria juu ya suala hili. Kwa mfano Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu katika shauri Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Serikali ya Tanzania 1, kwa mujibu wa Ibara ya 39(1) (c) na Ibara ya 67(1) ( b) pamoja na masharti ya Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 1979, mtu hatakuwa na sifa za kuchaguliwa kuwa Rais, Mbunge au diwani isipokuwa kama ni mwanachama wa chama cha siasa.

Pia kwa mujibu wa vifungu vya 32, 55 na 60 vya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2024, moja ya sifa ya mtu kuchaguliwa kuwa Rais, Mbunge au Diwani ni lazima awe anatokana na chama cha siasa, hii

1 Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Serikali ya Tanzania, Maombi No.011/2011
inathibitisha kutochukuliwa kwa maoni ya wadau tuliotaka uwepo wa mgombea binafsi, licha ya LHRC na wadau wengine kupendekeza mabadiliko madogo ya katiba katika ibara za 67(1)(b) na 39(1)(c) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ili kuruhusu uwepo wa mgombea binafsi lakini bado Serikali haijafanyia kazi.

Ni Imani yetu kwamba, uwepo wa mgombea binafsi utatachoea ukuaji wa demokrasia pamoja na kuongeza wigo wa watanzania kuwa na haki ya kuchaguliwa bila kulazimika kupitia mkondo wa vyama vya siasa.

4. Maamuzi ya Tume kutohojiwa Mahakamani
Kwa upande mwingine, LHRC na wadau tulipendekeza maamuzi ya Tume ya Uchaguzi kuhojiwa Mahakamani kwa njia za mapitio au mashauri ya kikatiba hata hivyo bado maamuzi ya tume yatakuwa ya mwisho na hayatahojiwa Mahakamani. Kwa mujibu wa vifungu vya 36(6), 53(6), na 65(7) vya sheria, maamuzi ya tume juu ya mgombea wa urais, Ubunge na udiwani kukatiliwa uteuzi yatakuwa ya mwisho na hayatahojiwa mahakamani kitendo ambacho wadau tulithitisha kinakiuka Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977. Mahakama kuu katika shauri la 1 Prisca Chogero dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania2, iliamua kwamba maamuzi ya mamlaka za Serikali kutohojiwa Mahakamani ni kukiuka ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.

5. Wajibu wa Vyombo vya Habari
Moja ya eneo ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu ni vyombo vya habari kutotenda haki kwa wagombea wote kwa usawa wakati wa urushaji wa matangazo na vipindi vya kampeni. Kumekuwa na malalamiko kwa vyombo vya habari kupendelea wagombea wa upande mmoja hii ilitokana na upungufu uliopo katika sheria zetu za uchaguzi kutokuwa na mifumo ya kuviwajibisha vyombo vya habari vinavyokiuka taratibu wakati wa kampeni.

LHRC na wadau wengine tulipendekeza kuwepo na mfumo wa kuviwajibisha vyombo vya habari vinavyokiuka taratibu au mizania ya usawa wakati wa kampeni ili kuondoa malalamiko miongoni mwa wadau. Kwa mujibu wa kifungu cha 74 cha sheria kimebaki kama kilivyokuwa kwenye mswaada huku vyombo vya habari binafsi vikiwa si sehemu ya wajibu huo.

1. Upatikanaji wa wabunge na madiwani wanawake wa viti maalumu
Moja ya eneo ambalo limekuwa na mjadala mkubwa katika miaka ya hivi karibuni ni upatikanaji na utaratibu unaotumika sasa kuwapata wabunge na Madiwani Wanawake wa Viti Maalumu. Kwa mujibu wa ibara za 66, 67,76(3) na 78 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 utaratibu unaotumika kuwapata wabunge wa viti maalumu unatokana na uwiano wa kura zote za wabunge ambazo chama husika kilipata wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Licha ya ibara ya 81 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 kuipa fursa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwamba yaweza kuweka masharti yanayofafanua utaratibu utakaotumiwa na vyama vya siasa kuteua wabunge wanawake wa viti maalumu lakini mpaka sasa vyama vya siasa ndio vimebaki kuwa na mamlaka na hatima ya ubunge huu.

Kifungu cha 112 kinachohusu uteuzi wa wabunge wanawake wa viti maalumu kimeendelea kubaki kama kilivyo. Kutokana na ukweli kwamba suala hili ni suala la kikatiba hivyo ili kufanya mabadiliko katika kifungu hiki ni lazima tufanye mabadiliko madogo ya katiba kwa kuzifumua ibara za 66, 67, 76(3), 78 na 81 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.ili kuruhusu mfumo wa uwakilishi yaani (quota system) utumike ambapo wabunge wa viti maalumu watapatikana kwa kuchaguliwa na wananchi wenyewe kama ambavyo jirani zetu wa Kenya wanafanya yaani (women representative).

Hali kadhalika kifungu cha 113 cha sheria kinachohusu uteuzi wa madiwani wanawake wa viti maalumu kimebaki kama kilivyokuwa kwenye muswada ambapo napo utaratibu unafanana na ule wa kuwapata wabunge wa viti maalumu.

2. Sharti la dhamana kwenye mashauri ya uchaguzi
Licha ya Mahakama ya rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika shauri la Julius Ishengoma Francis Ndyanabo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Rufaa No. 64 ya mwaka 2001/2002, Mahakama ya Rufani Dar es Salaam3, kutamka kwamba sharti la dhamana katika mashauri ya uchaguzi ni kukiuka ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.4 na ni kukiuka haki ya wananchi kuzifikia mahakama, na licha ya LHRC na wadau kushauri sharti hili lifutwe lakini bado vifungu vya 140 na 150(2) vya sheria vimebaki na sharti hili kwa maana ya kwamba mashauri ya uchaguzi ya ubunge na udiwani hayatasikilizwa mpaka pale mlalamikaji atakapokuwa amelipa kiasi cha fedha kama dhamana kama itavyoamuliwa na msajili wa mahakama.

3. Matokeo ya Urais kutohojiwa Mahakamani
Kwa mujibu wa ibara ya5, iwapo mgombea wa kiti cha Urais atatangazwa na Tume ya uchaguzi kuwa ameshinda ushindi wake hautahojiwa mahakamani, tunatambua kuwa sharti hili ni la kikatiba hivyo ili kufanyiwa marekebisho ni lazima tufanye mabadiliko madogo ya katiba ili kuifanya marekebisho ibara ya 41(7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ili matokeo ya Urais yaweze kuhojiwa mahakamani.

B. Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi No. 2. 2024
Sheria nyingine ambayo tungependa kuwafahamisha ni Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Kuna masuala muhimu ambayo pia tulitamani yawe sehemu ya sheria hii lakini bado yameendelea kubaki kama yalivyo.

1. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na vitongoji kuendelea kusimamiwa na TAMISEMI.
Licha ya kifungu cha 10(1)(c) cha Sheria kuanisha kwamba moja ya majukumu ya tume yatakuwa ni kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Serikali za Vijiji, Mitaa na Vitongoji Tanzania Bara, lakini ili Tume iweze kutekeleza wajibu huu ni lazima kuwe na utaratibu utakaoainishwa na sheria itakayotungwa na Bunge. Hata hivyo Bunge bado halijatunga sheria inayoainisha utaratibu huo hivyo uchaguzi huu kuendelea kuwa chini ya TAMISEMI kwa kanuni za Waziri mwenye dhamana na wizara husika.

2. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa tume waliopo sasa kuendelea na nafasi zao baada ya kuanza kutumika kwa sheria hii
Licha ya wadau wengi kufurahishwa na kuchukuliwa kwa pendekezo la muda mrefu la kuwepo kwa mfumo huru wa namna ya kupatikana kwa tume, na licha ya kifungu cha 10 cha sheria kuanzisha Kamati ya usaili kwa ajili ya kuwapata Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine wa Tume lakini kwa wakati huohuo kifungu cha 27 cha sheria kinasema Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume waliopo sasa wataendelea na nafasi zao hata baada ya sheria hii kuanza kutumika rasmi.

Kwa lugha rahisi ni kwamba kamati ya usaili iliyoanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha sheria haitaanza kazi ya kusaili Mwenyekiti, Makamu Mwenyeti na Wajumbe wengine wa tume waliopo madarakani hivi sasa mpaka pale watakapomaliza nafasi zao za utumishi baada ya miaka mitano. Kwa lugha nyingine Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine wa tume watakoma katika nafasi zao kati ya mwaka 2028 na 2029 hivyo kamati ya usaili itaanza zoezi la kusaili watu hao.

C. Sheria ya Vyama Vya Siasa 2024
1. Ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia, watu wenye ulemavu pamoja na vijana

Katika eneo ambalo LHRC na wadau wengine tumekuwa na msukumo mkubwa wa kuona mabadiliko ni ujumuishwaji wa kijinsia, watu wenye ulemavu pamoja na vijana. Kwa mujibu wa kifungu cha 10C cha sheria, moja ya nyaraka za lazima ambazo chama cha siasa kitalazimika kuwa nazo ni pamoja na sera ya jinsia na ujumuishwaji, hata hivyo bado kifungu hiki hakijaweka mfumo wa kuviwajibisha vyama vya siasa ambavyo vitashindwa kutekeleza takwa hili.

Pili, bado masuala ya kijinsia na ujumuishwaji katika vyama vya siasa hajapewa kipaumbele katika sheria hizi kama matarajio waliokuwa nayo wadau.

Licha ya LHRC kuainisha mambo muhimu ambayo hayakuzingatiwa na sheria hizi, hata hivyo tunapenda kuchukua fursa hii kuainisha baadhi ya masuala ambayo yamezingatiwa katika sheria hizi ambayo LHRC inaona ni mambo mazuri, masuala hayo ni Pamoja.

2. 1. Hitimisho
Mwisho, napenda kuchukua fursa hii kutoa wito kwa Serikali kama ifuatavyo:

1. Kuwasilisha mswada wa sheria utakaotoa fursa ya kufanya mabadiliko ya katiba ili kuruhusu baadhi ya masuala ambayo kwa uasili wake hayawezi kufanyiwa marekebisho bila kugusa katiba.

2. Serikali iwasilishe muswada wa sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kama ilivyoanishwa katika kifungu cha 10 (1) (c) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024.

3. Serikali itekeleze maamuzi ya Mahakama Kuu katika shauri la Tito Elia Magoti dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi 6 iliyowapa wafungwa haki ya kupiga kura.

4. Licha ya Serikali kukubaliana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuwa suala la watanzania waishio nje ya nchi(Diaspora) kupiga kura lina mashiko lakini haikuwa tayari kulifanya suala hili kuwa la kisheria. Hivyo LHRC inaikumbusha Serikali kurejea makubaliano yake na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.

5. Kufanya marekebisho Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2024 ili kuweka takwa la ulazima wa kufanya midahalo ya wagombea katika ngazi zote.

Imetolewa na:
Dkt. Anna Henga Mkurugenzi Mtendaji
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
Waachwe tu siku zinakuja, asema bwana wa "MAJESHI"
 
Mahakama zina kazi nyingi kwa sasa, tusubiri baada ya uchaguzi 2025 tutaweka hayo maoni
 
Back
Top Bottom