Kuelekea kumpata Katibu mkuu mpya wa CCM na kama Rais Samia bado anandoto za kuendelea kuwa Rais basi afanye hiki alichofanya Hayati Rais Magufuli

YEHOVA

Senior Member
Sep 23, 2023
149
234
IMG-20231204-WA0022.jpg
Jf stori hii ni kwaufupi sana,

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 Hayati Rais Magufuli ilimbidi kutafuta mtu loyal kwake atakayeweza kufumba macho, roho na masikio ili kuchapisha fomu moja tu kwenye nafasi ya Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi ili kuzima makundi na kukiunganisha Chama kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Hata hivyo, Sote tunakumbuka baada ya hilo kufanyika wale wote walioutaka Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi mwaka 2020 waligonga mwamba kikwazo kikubwa kikiwa ni ujio wa Katibu Mkuu huyo mpya kwani alifanya "kweli" pamoja na kelele nyingi fomu ilikuwa ni moja tu ya Mzee John Pombe Magufuli,

Leo, Kama kweli Rais Samia anataka kuendelea kuwa mgombea Urais pekee kupitia Chama Cha Mapinduzi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2025 basi nafasi ya Katibu mkuu wa CCM Tanzania apewe Mhe Shaka Hamdu Shaka ambae ni mkuu wa Wilaya kama ilivyokuwa kwa Katibu Mkuu mstaafu Ndg Daniel Chongolo.

Nakama itampendeza Mhe Rais baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2024 & 25 kumalizika salama nafasi hii anaweza kupewa mtu mwingine na Mhe Shaka Hamdu Shaka pamoja na Ndg Paul Makonda wakarudi Serikalini kwani ni watendaji wazuri.

Lazima pia tufahamu, kwa aina ya haya makundi yanayojijenga Kila siku ndani ya chama ni Rai yangu Rais Samia asijipe 100% kuwa ni Yeye mgombea pekee wa Urais ndani ya CCM cause anything might happen,

Hata hivyo, Uteuzi wa Mhe Shaka Hamdu Shaka utakuwa na tija zaidi kiutendaji kwani kwa Chemistry hii baina yake na Ndg Paul Makonda vinaweza kufanya vizuri zaidi katika Siasa hizi za hoja na kuwapoteza kabisa Wapinzani wetu kisiasa na kukiletea Chama ushindi wa kishindo katika chaguzi zote za usoni.

Naandika haya nikiwa nafahamu mipango kadhaa ya wasaka Urais kuelekea mwaka wa Uchaguzi Mkuu 2025 kwani they are unstoppable ila kwa mbinu hii tu ambayo nayo haikwepeki.

Nakama Rais Samia atafanya hili, lazima kelele zitakuwa nyingi hasa huko kwenye vikao vya wakubwa tena kwenye ngazi zote kwani watafahamu fika kwa jina hilo la Katibu Mkuu kwao huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa ndoto zao za Urais kwa mwaka 2025,

Baada ya hayo, niimani yangu Umoja na amani vitatawala ndani na nje ya chama Cha Mapinduzi huku Chama kikisalia kuwa kimoja tofauti na ilivyokuwa mwaka 2015.

Nimuhimu pia kukumbuka Hayati Rais Magufuli hakumwamini mtu yoyote ndani ya CCM ndio sababu akamleta Mhe Dkt Bashiru Ally Kakurwa kutoka chama cha Wananchi CUF kwani Kila mwanasiasa unayemwona Leo ndani ya CCM tayari anakundi lake hata kabla ya Ujio wa Rais Samia kwenye siasa hizi za Urais na makundi ya Urais,

Hapa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anaweza kuchukua msamiati maarufu wa kiswahili unaosema " Zimwi linalokufahamu kamwe halikuli likakumaliza "


"Mama Samia fanya hili utakuja kunishukuru sana baada ya 2025"
 
View attachment 2833238
Jf stori hii kwa kifupi sana,

Mwaka 2020 Hayati Rais Magufuli ilibidi kumtafuta mtu royal sana kwake atakayeweza kufumba macho na roho ili

Mama Samia fanya hili utakuja kunishukuru 2025 ila usinisahau hata kauwaziri kwani Bungeni 2025 nitakuwepo.
Wewe kwa kweli una uwezo mdogo sana wa uchambuzi. Tena huwatakii wema watanzania maana wameshaonesha hawamuhitaji samia kama mgombea wa ccm au chama chochote cha siasa.
 
View attachment 2833238
Jf stori hii kwa kifupi sana,

Mwaka 2020 Hayati Rais Magufuli ilibidi kumtafuta mtu royal sana kwake atakayeweza kufumba macho na roho ili haka na Ndg yangu Paul Makonda vinaweza kufanya vizuri sana katika Siasa hizi za hoja na kuwapoteza kabisa Wapinzani Tanzania,

msamiati wa kiswahili unaosema " Zimwi linalokufahamu halikuli likakumaliza"


Mama Samia fanya hili utakuja kunishukuru 2025 ila usinisahau hata kauwaziri kwani Bungeni 2025 nitakuwepo.
Udikitete udikitete udikiteta sasa kiko wapi?
 
Back
Top Bottom