Wakati mwingine ni matumizi mabaya tu ya madaraka. Hivi juzi watia nia wa ccm walikuwa wanagawa rushwa kama njugu hadharani, hao watu wa usalama hawakufanya lolote. Lakini leo wameagizwa na wanasiasa ili waonekane wanafanya kazi, kwa kumsubiri mwanasiasa ambaye hakuwa mkimbizi, hana sifa ya kuendesha makundi ya yanayomiliki silaha, wala hajawahi kuingia msituni, anapokelewa kama gaidi.

Mambo haya ndio yanapelekea wazungu kutuita manyani. Mtu anakuja mchana kweupe, na katangaza kabisa, kuna haja gani kwa vyombo vya usalama vinavyojitambua kwenda kujenga taswira ya uhasama usio na sababu yoyote, ili kukidhi kiu ya mwanasiasa anayeongoza nchi? Hapa ndio tunapotaka katiba irekebishwe, na baadhi ya mamlaka ziondolewe kwa rais, ili taasisi zetu zibaki kufanya kazi kwa weledi, badala ya kutumiwa kwenye siasa chafu.
Kila siku wanawaita CDM wanaharakati, hawajui haya matendo yao ya hovyo ndio yanayowafanya CDM waamue kupigania haki zao kwa nguvu, na kwao mtu akilazimisha kutaka apewe haki yake anaitwa mwanaharakati au analeta vurugu, ni vyema watambue, mpaka siku watakapokoma kuonea wengine ndio hizo wanazoziita harakati za CDM zitakoma, vinginevyo hizo harakati zitaendelea tu.
 
Back
Top Bottom