Lissu: Jeshi la Polisi fanyeni kazi ya kutusaidia kwenye maandamano kama mnavyofanya kwa Makonda

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Lissu amesema sehemu nyingine duniani Polisi hutaja njia ambako maandamano yatapita na kutoa tahadhari kwa wafanyabiashara pamoja watu wanaotumia barabara hiyo wajue itatumika kwa maandamo, lakini maandamano ya CHADEMA yanafanyika huku magari yanaingilia msafara wao wa maandamano.

Akiongeza, kuchanganya waandamanaji na magari sio sawa kwani maafa yanaweza kutokea, na kuwataka polisi wafanye kazi yao ya kuwasaidia waandamanaji kuandamana kama wanavyofanya kwa Makonda. Akisema Makonda akifanya mikutano yake polisi wanahakikisha barabara inakuwa wazi lakini wakifanya CHADEMA ni tofauti, waandamanaji wanachanganywa na magari.

Lissu ameyasema haya leo tar 27/2/2024 akiongea na wananchi Arusha baada ya maandamano.
 
Wamefanya maandamano na wanadai watangaziwe.Gari la matangazo la Chadema lilikuwa linazunguka mitaani likitangaza.Kazi yake ilikuwa nini?Yaani mnataka msimamishe shughuli za wananchi kupata riziki zao za kila siku?
Wacheni kudeka.
 
Dah! Watataka na jeshi liandamane pia.. naipongeza sana serikali kwa kuwaruhusu hawa jamaa kufanya matembezi yao ya hiari ya kupunguza vitambi vya ruzuku.
 
Yaani katika mambo wanayokosea viongozi wa upinzani ni kuwapigania hao polisi na shida zao maana wala hawana shukrani kuwa na wao wanapiganiwa.

Polisi walikuwa wanaishi kwenye mabanda kama ya kuku au nguruwe, wapinzani ndio wamepambana ili utu wao uheshimishwe hawajali!

Mafao yao ya kustaafu yanasemewa kila siku hilo hawalioni huku wakistaafu mtaani wanatia huruma hali ilivyongumu hadi polisi mstaafu anatamani awe shoga ajikimu.

Pia hata hela zao za rambirambi kina IGP wanafungulia biashara za mabaa na usafirishaji lakini hao wa ccm bungeni hawasemei na polisi wanaona Wapinzani eti ni adui zao.
Highest level of stupidity

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Wamefanya maandamano na wanadai watangaziwe.Gari la matangazo la Chadema lilikuwa linazunguka mitaani likitangaza. Kazi yake ilikuwa nini? Yaani mnataka msimamishe shughuli za wananchi kupata riziki zao za kila siku?
Wacheni kudeka.
Mbona Makonda hasumbuliwi akifanya maandamano?
 
Wamefanya maandamano na wanadai watangaziwe.Gari la matangazo la Chadema lilikuwa linazunguka mitaani likitangaza.Kazi yake ilikuwa nini?Yaani mnataka msimamishe shughuli za wananchi kupata riziki zao za kila siku?
Wacheni kudeka.
Mwambieni Lisu aache kudeka.

Yaani analinganisha mikutano ya Makonda na matembezi ya chadema?

Nitayaita maandamano siku waandamaji wakijiongoza wenyewe bila Lisu au Mbowe
 
Mwambieni Lisu aache kudeka
Yaani analinganisha mikutano ya Makonda na matembezi ya chadema?
Nitayaita maandamano siku waandamaji wakijiongoza wenyewe bila Lisu au Mbowe
Watajiongozaje wakati ulikuwa ukisema kwanini wasiwe front hao viongozi? Au umesahau kauli yako ile kuwa Lissu amekimbia maandamano ameenda kucheki mechi Ivory Coast?
 
Unamlinganisha Makonda na hao mapoyoyo?
..imani ya Tanu / Ccm inasema binadamu wote ni sawa.

..kwani Bashite amewazidi nini wenzake mpaka apendelewe?

..kama tutaangalia makalio makubwa basi Bashite amewazidi wenezi wa vyama vyote.
 
Pia mazito yaongelewa katika maandamano

27 February 2024
Arusha, Tanzania

HOTUBA
Tundu Lissu, Freeman Mbowe akishambulia kwa hoja Arusha leo umuhimu wa kuweka shindikizo kupitia maandamano ya wananchi hadi kieleweke


View: https://m.youtube.com/watch?v=2CGuQTQAl3c

Makamu wa mwenyekiti CHADEMA ageukia wasomi kina Prof. Kabudi Palamagamba wanaosema rais ni mungu mtu.

Katiba ya nchi imetengeneza mungu wa nchi yaani ardhi, ardhi yote ni mali ya umma chini ya uangalizi wa rais.

Watu wanaporwa adhi kona zote za nchi kuanzia Mbarali kusini hadi kaskazini Ngorongoro


Madini ya dhahabu, tanzanite, gesi asilia ardhini na baharini ipo chini ya udhamini wa rais mungu kukodhi mali zetu ndiyo maana watanzania hawana haki na mali zao vijijini, walizorithishwa na wazazi au kununua kihalali .....

Wanyama 10,000 wapo Sharjah katika zoo kwa amri ya mungu aliyepo ikulu


Misitu, bandari vyote vimegawiwa kwa wageni kwa marafiki zake uarabuni hectare milioni 8 zimekabidhiwa kampuni ya Uarabuni ili kuuza hewa ya carboni / ukaa pia hectare milioni 6 za Mwiba Holding Serengeti amepewa mzungu na yote hii ni kutokana na katiba ya rais mungu.

Sasa wewe mwananchi umebakiwa na nini? Umasikini na kutimuliwa kutoka katika ardhi yenu ya urithi yenye mali nyingi na mazao

Tozo, kodi zote zimeanzishwa na mungu rais Samia Hassan ambaye katiba iliyopo imempa mamlaka ya kuanzisha na kukataa kodi, tozo zote ili kuneemesha wateule wa rais ili fedha hizi wale kupitia V8 kwa viongozi wateule lakini hakuna ambulance.

Juzi eneo la ajali majeruhi waliondolewa na guta, canter kwa kutumia raia wema kwa sababu fedha zote zimenunua V8 mashangingi kila kona huku hakuna ambulance, gari za zimamoto, na huduma za paramedical hakuna

Biashara ya kodi na tozo huanzia kupangwa ikulu kisha kupelekwa bungeni. Hivyo kodi hizo ni za rais Samia katiba iliyopo inasema hayo.

Hivyo hakuna namna ya mungu rais kujinasua na lawama za kodi kubwa na matumizi mabaya yaliyo ya anasa.

Wafanyakazi wamebaki kuwa masikini wana mishahara midogo wanashindwa kugoma na kila Mei Mosi wanatembeza bakuli yallah masikini rais mungu tuongezee mshahara. Katiba iliyopo inasema rais mungu ndiyo aliye na mamlaka ya kuongeza mshahara..

Hivyo haki inatafutwa kwa maandamano, migomo na katiba mpya ili kuondoa mungu rais na vimiungu wake wateuliwa

Makamu mwenyekiti CHADEMA amaliza hotuba yake na sasa kumkaribisha mwenyekiti wa CHADEMA taifa kamanda Freeman Mbowe ahutubie mamia ya wananchi wa Arusha waliojitokeza kwa wingi na watanzania popote nchini na ulimwenguni wanaotusikiliza kuhusu mustakhabali wa nchi na namna bora ya kwenda mbele.

Mh. Freeman Mbowe anasema leo tumehitimisha raundi ya kwanza ya maandamano katika majiji manne ya nchini Tanzania

Mh. Mbowe anaongeza kamati kuu ya CHADEMA imejiridhisha CCM haina nia njema bali inafanya ulaghai mtupu kwa wananchi na jumuiya ya kimataifa.

Dar es Salaam kilometa 50, kule Mbeya kilometa 42 Arusha leo kilometa 30 kuanzia eneo la KwaMrefu na kukutana na wananchi waliotueleza kero na taabu za maisha.

Tunakwenda kule Mtwara kutengeneza Azimio la Mtwara kwa mkutano wa kamati kuu na kuwapa taarifa ya maandamano haya ya majiji manne ambapo tumetembea jumla ya kilomita 160 kwa miguu kukutana na wananchi wa kada zote, vyama vyote ...
 
Lissu naye sijuwi yupoje. Sasa CHADEMA nzima na Lissu wake wanaanzaje kujilinganisha na Mheshimiwa Makonda mwamba majabali wa siasa na kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara na aliye kimbilio la wanyonge? Mheshimiwa Makonda ni kama mboni ya jicho . Heshima aliyonayo Mheshimiwa Makonda huwezi kumlinganisha na yeyote yule kutoka ndani ya CHADEMA na chama kizima. Mheshimiwa Makonda ni mkubwa kuliko CHADEMA na hazi yake siyo sawa na CHADEMA.ndio maana Mheshimiwa Makonda anaweza kutatua kero za wananchi na kutoa majibu stahiki wakati CHADEMA wao kazi yao ni kupiga makelele tu kama machinga wanaouza sumu ya panya na mende sokoni.
 
..imani ya Tanu / Ccm inasema binadamu wote ni sawa.

..kwani Bashite amewazidi nini wenzake mpaka apendelewe?

..kama tutaangalia makalio makubwa basi Bashite amewazidi wenezi wa vyama vyote.
Umekariri ya TANU/CCM ya Chadema inasemaje?
 
Wamefanya maandamano na wanadai watangaziwe.Gari la matangazo la Chadema lilikuwa linazunguka mitaani likitangaza.Kazi yake ilikuwa nini?Yaani mnataka msimamishe shughuli za wananchi kupata riziki zao za kila siku?
Wacheni kudeka.
Mbona kwa makonda wanafanya hivyo na hulalamiki?
 
Wamefanya maandamano na wanadai watangaziwe.Gari la matangazo la Chadema lilikuwa linazunguka mitaani likitangaza.Kazi yake ilikuwa nini?Yaani mnataka msimamishe shughuli za wananchi kupata riziki zao za kila siku?
Wacheni kudeka.
Lissu kaelekea kulia wewe unaenda kushoto
 
Back
Top Bottom