Ni kwanini kushambuliwa Kwa risasi Mbunge Sendeka, kushughulikiwe Kwa haraka na Polisi, wakati lile la Tundu Lissu halishughulikiwi kabisa?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,535
30,261
Tukio la kushambuliwa Kwa risasi gari alilokuwemo Mbunge Ole Sendeka, ni baya mno na linafaa Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi ili kuwabaini waliotenda uovu huo.

Hata hivyo Kwa taarifa zilizotufikia zinasema kuwa tayari hivi sasa, kuna timu ya wataalamu, kutoka Jeshi la Polisi, limetumwa kutoka makao makuu Dodoma, kwenda Somanjiro, kwenye eneo Hilo la tukio ili kushughulikia Kwa haraka tukio hilo

Hata hivyo takribani miaka Saba hivi sasa, mnamo mwaka 2017, lilitokea tukio linalofanana na hilo, wakati Mbunge wa upinzani, Tundu Lissu, naye aliposhambuliwa Kwa risasi akiwa ndani ya gari yake na kumjeruhi vibaya Mbunge Tundu Lissu, hadi akaenda kutibiwa nchi za nje Kwa muda mrefu.

Hata hivyo kinachonishangaza ni kuona tokea tukio hilo litokee, takribani miaka Saba hivi sasa, sijaona juhudi zozote za Jeshi la Polisi, kuwasaka hao watu wasiojulikana, waliotenda uovu huo wa kumshambulia Mbunge Tundu Lissu!

Je tuelewe kuwa Jeshi la Polisi, linafanya "double standard" katika utekelezaji wake wa kushughulikia na uhalifu nchini??

Ninachojua ni kuwa wajibu namba moja wa Jeshi la Polisi nchini ni kuwalinda raia wake na mali zao, bila kujali itikadi zao za kisiasa.

===

Pia soma:

Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali
 
Mhhh! Mimi nadhani labda kwa kuwa Mh. Sendeka hajashutumu mtu hivyo ni haki police kumsaka muhalifu tofauti na upande wa pili wao walimnyooshea kidole mtu hivyo pengine police hawakuona haja ya kumsaka muhalifu ambaye tayari amejulikana na washtaki.
 
Lissu iliekezwa auawe , Waelekezaji walikuwa Mamlaka ya juu , Sendeka ameshambuliwa kwa sababu ya makundi na fitna ndani ya ccm
Report ya uchunguzi imeshatoka kutoka 'kijiwe mjinga' wakati Makachero kutoka Makao Makuu ndio wanaingia Manyara
 
Report ya uchunguzi imeshatoka kutoka kijiweni wakati Makachero kutoka Makao Makuu ndio wanaingia Manyara
Tumechunguza kabla ya uchunguzi wao , hivi wewe utamuamini Kingai kuliko sisi ? labda kama umelogwa
 
Tukio la kushambuliwa Kwa risasi gari alilokuwemo Mbunge Ole Sendeka, ni baya mno na linafaa Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi ili kuwabaini waliotenda uovu huo...
Kama umefuatulia vizuri vyombo vyetu vya kimlaka mfano TRA, TAKUKURU, Polisi nk havifanyi kazi kwa mujibu wa Sheria, Bali husubiri maagizo kutoka ngazi za juu. Ukiona hawajafuatilia, jua ngazi za juu ni wahusika wa uhalifu huo.
 
Report ya uchunguzi imeshatoka kutoka 'kijiwe mjinga' wakati Makachero kutoka Makao Makuu ndio wanaingia Manyara
Wanaenda kuhalalisha imprest tu na kufanya siasa za bei che. Hao wako kisiasa zaidi kuliko kiutendaji.
 
Tundulisu alikuwa tayari amewataja wabaya wake kuwa anapokea simu za vitisho toka kwa watu wasiojulikana.Hivyo basi mahakama ya fisi mbuzi hana haki.
 
Kama umefuatulia vizuri vyombo vyetu vya kimlaka mfano TRA, TAKUKURU, Polisi nk havifanyi kazi kwa mujibu wa Sheria, Bali husubiri maagizo kutoka ngazi za juu. Ukiona hawajafuatilia, jua ngazi za juu ni wahusika wa uhalifu huo.
Umesema ukweli kabisa!
 
Back
Top Bottom