Kitaeleweka tu mkuu
Kila siku wanawaita CDM wanaharakati, hawajui haya matendo yao ya hovyo ndio yanayowafanya CDM waamue kupigania haki zao kwa nguvu, na kwao mtu akilazimisha kutaka apewe haki yake anaitwa mwanaharakati au analeta vurugu, ni vyema watambue, mpaka siku watakapokoma kuonea wengine ndio hizo wanazoziita harakati za CDM zitakoma, vinginevyo hizo harakati zitaendelea tu.
 
Salaam Wakuu,

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara Tundu Lissu anatarajiwa kuwasili nchini leo saa saba na dakika ishirini saa za afrika Mashariki.

Lissu amekaa nje ya nchi miaka mitatu sasa baada ya kuondoka kwa shambulio la risasi lililotokea mjini Dodoma ,Septemba 7, mwaka 2017, saa 7 mchana, Area ‘D’, kwenye nyumba ya makazi ya viongozi wa Serikali mjini Dodoma.

“Lissu kwa sasa anatimiza mwaka wa tatu na anarejea hapa nchini baada ya kupona kikamilifu. Watanzania na wanachama wa Chadema wanakutana hapa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), kwa lengo la kumpokea makamu mwenyekiti wa chama chao Lissu.

Hivyo timu nzima tupo hapa kukuletea kile kitakachojiri kwenye mapokezi haya.

Stay tuned.

======

UPDATE (NOTE: Picha zipo post ya 2):

1105HRS: Hapa uwanjani pametulia, hakuna fujo wala dalili za fujo, Wanachama wachache wa CHADEMA wanaonekana wakipita pita huku na kule. Bado sijabahatika kuona gari la Polisi Wala Gari la CHADEMA.


Ratiba inaonesha muda wa ndege kufika ni saa saba na dakika Ishirini. Angalia kwenye chati

1121hrs: Saa moja iliyoisha Tundu Lissu ndo amepanda ndege ya Ethiopian Airlines ET 805 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Bole Addis Ababa kuja hapa Dar Julius Kambarage Nyerere International Airport.

Safari inatazamiwa kuchukua masaa yasiyozidi Matatu kufika hapa tulipo.

1140hrs: Mwenyekiti Mkoa wa Iringa CHADEMA William Mungai, aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi(Sugu) Wakiwa Wamefika hapa Uwanja wa ndege kumpokea Lissu

1156HRS: Kutoka kushoto: Hekima Mwasipu, Wakili wa Chadema, Sugu, Catherine Ruge(Simba Jike) Viti Maalum Mara na Mgombea wa Jimbo la Segerea CHADEMA

1230hrs: Polisi Magari Mawili ya Polisi wameshusha Wanausalama wa kulinda amani wapatao kama 30 nje ya Viunga vya Uwanja wa ndege. Wamekaa mstari kama Gwaride na wanapewa Maelekezo. Wameshusha njia Panda ya kuelekea Uwanja wandege. Kuna askari wanne walikuwepo tangu asubuhi Wakihoji kila anaye ingia.

Bodaboda kama 50 wapo hapo Askari Polisi Walipo, nadhani Wamekataliwa kuingia. Vilevile Magari ya CHADEMA maarufu kama Magari ya M4C, Yapo sehemu hiyo ya njiapanda yakizunguka huku na kule. Magari ya CHADEMA yapo Matano yamejaa watu waliovalia nguo za CHADEMA.

Polisi ukijielezea unapoelekea ndo Wanaruhusu. Lalikini kuna baadhi ya Wafanyakazi(Walinzi wa Uwanja, sio Polisi) ndo wanakataza watu kuingia.

1240: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameweza kupenya na kuongia ndani sehemu ya kusubiria Wageni

1300hrs: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameruhusiwa kuingia. Wengine wapo nje ya Uwanja wanaimba nyimbo.

Polisi Tanzania Wamewaruhusu Wanachama wote wa CHADEMA na Wafuasi wa Tundu Lissu. Muda wowote ndege otawasili
Dalili zote kuna uwezekano akakamatwa kabla walioenda kumpokea hawajamuona!!
 
Utauwa watu kwa pressure.

Hapa alikuwa Bole International Airport:

View attachment 1518234
"If it had not been for LORD who was on my side, when men rose up against me, Then they would have swallowed me alive when their wrath was kindled against me"

"Blessed be LORD who has not given me as prey to their teeth. My soul has escaped as a bird from the snare of the fowlers, the snare is broken and I have escaped. My help is the name of the LORD, who made HEAVEN and EARTH"

Psalmist
 
Hi hakuna hata Online Channel inayoonesha live mapokezi haya tukaona hayo mapokezi? Au wanahabari wamepigwa mkwara kuonesha. Lakini hata CHADEMA Online nao naona wako kama hawako kwa Makamu Mwenyekiti wao. Poor Bongoland hapa ndio huwa tunakosea sana wanahabari!
 
Lissu 2.JPG
 
An enemy of the people may also be A man of the people. Dada nipe kipande cha nazi nitafune
 
Back
Top Bottom