Nipo hapa mambo ni bamba
tapatalk_1595845299213.jpeg
 
Salaam Wakuu,

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara Tundu Lissu anatarajiwa kuwasili nchini leo saa saba na dakika ishirini saa za afrika Mashariki.

Lissu amekaa nje ya nchi miaka mitatu sasa baada ya kuondoka kwa shambulio la risasi lililotokea mjini Dodoma ,Septemba 7, mwaka 2017, saa 7 mchana, Area ‘D’, kwenye nyumba ya makazi ya viongozi wa Serikali mjini Dodoma.

“Lissu kwa sasa anatimiza mwaka wa tatu na anarejea hapa nchini baada ya kupona kikamilifu. Watanzania na wanachama wa Chadema wanakutana hapa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), kwa lengo la kumpokea makamu mwenyekiti wa chama chao Lissu.

Hivyo timu nzima tupo hapa kukuletea kile kitakachojiri kwenye mapokezi haya.

Stay tuned.

======

UPDATES;

1105HRS: Hapa uwanjani pametulia, hakuna fujo wala dalili za fujo, Wanachama wachache wa CHADEMA wanaonekana wakipita pita huku na kule. Bado sijabahatika kuona gari la Polisi Wala Gari la CHADEMA.
View attachment 1518228
View attachment 1518226
Ratiba inaonesha muda wa ndege kufika ni saa saba na dakika Ishirini. Angalia kwenye chati
View attachment 1518258
1121hrs: Saa moja iliyoisha Tundu Lissu ndo amepanda ndege ya Ethiopian Airlines ET 805 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Bole Addis Ababa kuja hapa Dar Julius Kambarage Nyerere International Airport.

Safari inatazamiwa kuchukua masaa yasiyozidi Matatu kufika hapa tulipo.
View attachment 1518257
1140hrs: Mwenyekiti Mkoa wa Iringa CHADEMA William Mungai, aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi(Sugu) Wakiwa Wamefika hapa Uwanja wa ndege kumpokea Lissu
View attachment 1518269
1156HRS: Kutoka kushoto: Hekima Mwasipu, Wakili wa Chadema, Sugu, Catherine Ruge(Simba Jike) Viti Maalum Mara na Mgombea wa Jimbo la Segerea CHADEMA
View attachment 1518330
1230hrs: Polisi Magari Mawili ya Polisi wameshusha Wanausalama wa kulinda amani wapatao kama 30 nje ya Viunga vya Uwanja wa ndege. Wamekaa mstari kama Gwaride na wanapewa Maelekezo. Wameshusha njia Panda ya kuelekea Uwanja wandege. Kuna askari wanne walikuwepo tangu asubuhi Wakihoji kila anaye ingia.

Bodaboda kama 50 wapo hapo Askari Polisi Walipo, nadhani Wamekataliwa kuingia. Vilevile Magari ya CHADEMA maarufu kama Magari ya M4C, Yapo sehemu hiyo ya njiapanda yakizunguka huku na kule. Magari ya CHADEMA yapo Matano yamejaa watu waliovalia nguo za CHADEMA.

Polisi ukijielezea unapoelekea ndo Wanaruhusu. Lalikini kuna baadhi ya Wafanyakazi(Walinzi wa Uwanja, sio Polisi) ndo wanakataza watu kuingia.
View attachment 1518339View attachment 1518340
1240: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameweza kupenya na kuongia ndani sehemu ya kusubiria Wageni
View attachment 1518355View attachment 1518354View attachment 1518353
View attachment 1518375
View attachment 1518376
1300hrs: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameruhusiwa kuingia. Wengine wapo nje ya Uwanja wanaimba nyimbo.
View attachment 1518393
Polisi Tanzania Wamewaruhusu Wanachama wote wa CHADEMA na Wafuasi wa Tundu Lissu. Muda wowote ndege otawasili
wewe jamaa ni proffessional photographer, Congratulation
 
Back
Top Bottom