Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,981
IMG_20200727_151156_346.jpg

2468294_IMG_20200727_215627.jpg



Salaam Wakuu,

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara Tundu Lissu anatarajiwa kuwasili nchini leo saa saba na dakika ishirini saa za afrika Mashariki.

Lissu amekaa nje ya nchi miaka mitatu sasa baada ya kuondoka kwa shambulio la risasi lililotokea mjini Dodoma ,Septemba 7, mwaka 2017, saa 7 mchana, Area ‘D’, kwenye nyumba ya makazi ya viongozi wa Serikali mjini Dodoma.

“Lissu kwa sasa anatimiza mwaka wa tatu na anarejea hapa nchini baada ya kupona kikamilifu. Watanzania na wanachama wa Chadema wanakutana hapa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), kwa lengo la kumpokea makamu mwenyekiti wa chama chao Lissu.

Hivyo timu nzima tupo hapa kukuletea kile kitakachojiri kwenye mapokezi haya.

Stay tuned.

======

UPDATE (NOTE: Picha zipo post ya 2):



1105HRS: Hapa uwanjani pametulia, hakuna fujo wala dalili za fujo, Wanachama wachache wa CHADEMA wanaonekana wakipita pita huku na kule. Bado sijabahatika kuona gari la Polisi Wala Gari la CHADEMA.


Ratiba inaonesha muda wa ndege kufika ni saa saba na dakika Ishirini. Angalia kwenye chati

1121hrs: Saa moja iliyoisha Tundu Lissu ndo amepanda ndege ya Ethiopian Airlines ET 805 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Bole Addis Ababa kuja hapa Dar Julius Kambarage Nyerere International Airport.

Safari inatazamiwa kuchukua masaa yasiyozidi Matatu kufika hapa tulipo.

1140hrs: Mwenyekiti Mkoa wa Iringa CHADEMA William Mungai, aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi(Sugu) Wakiwa Wamefika hapa Uwanja wa ndege kumpokea Lissu

1156HRS: Kutoka kushoto: Hekima Mwasipu, Wakili wa Chadema, Sugu, Catherine Ruge(Simba Jike) Viti Maalum Mara na Mgombea wa Jimbo la Segerea CHADEMA

1230hrs: Polisi Magari Mawili ya Polisi wameshusha Wanausalama wa kulinda amani wapatao kama 30 nje ya Viunga vya Uwanja wa ndege. Wamekaa mstari kama Gwaride na wanapewa Maelekezo. Wameshusha njia Panda ya kuelekea Uwanja wandege. Kuna askari wanne walikuwepo tangu asubuhi Wakihoji kila anaye ingia.

Bodaboda kama 50 wapo hapo Askari Polisi Walipo, nadhani Wamekataliwa kuingia. Vilevile Magari ya CHADEMA maarufu kama Magari ya M4C, Yapo sehemu hiyo ya njiapanda yakizunguka huku na kule. Magari ya CHADEMA yapo Matano yamejaa watu waliovalia nguo za CHADEMA.

Polisi ukijielezea unapoelekea ndo Wanaruhusu. Lalikini kuna baadhi ya Wafanyakazi(Walinzi wa Uwanja, sio Polisi) ndo wanakataza watu kuingia.

1240: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameweza kupenya na kuongia ndani sehemu ya kusubiria Wageni

1300hrs: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameruhusiwa kuingia. Wengine wapo nje ya Uwanja wanaimba nyimbo.

Polisi Tanzania Wamewaruhusu Wanachama wote wa CHADEMA na Wafuasi wa Tundu Lissu. Muda wowote ndege itawasili

1357hrs: Abiria wameanza kutoka nje. Lissu bado hajaonekana

1430Hrs: Msafara unatoka Uwanja wa ndege kuelekea Makao Makuu Kinondoni mtaa wa Ufipa
IMG_20200727_143813_5.jpg

1450hrs: Msafara Umefika Kipawa tunaelekea TAZARA. Watu ni wengi. Speed ni 10k/h
IMG_20200727_150155_827.jpg

Msafara Unaongozwa na Vijana CHADEMA. Hakuna Polisi hata mmoja. Watu wanashangilia na kulia kwa furaha. Magari yanapisha msafara bila tatizo. Hakuna fujo bodaboda wanaongoza Msafara
IMG_20200727_152001_928.jpg

1520hrs: Msafara umefika daraja laMfugale. Barabarani hakuna Polisi.

1530hrs: Msafara umefika Buguruni Mataa. Sehemu zote tunazopita hakuna Askari wala Trafiki. Watu wamejipanga barabarani wanashangilia

1600hrs: Msafara umefika Amana unaelekea Mataa ya Karume. Barabara ni nyeupe. Watu wa Ilala wamejipanga Barabarani na matawi yamiti wakipeperusha juu. Magari yote yamepisha msafara kila sehemu Lissu anapofika

1405hrs: Trafiki aliyesimama Mataa ya Karume anaita Magari yatokayo Buguruni na kuzuia yanayoenda buguruni ili Msafara wa Lissu uweze kutembea. Tayari wamekuja askari watatu hapa Karumewanacontrol Magari yasiende Buguruni ili Msafara upite.

Kumbuka Msafara wa Lissu unaongozwa na Bodaboda ikifuatiwa na gari la Matangazo, inafuata gari ya Bavicha(Walinzi) inafuata gari ya Waandishi, inafuata gari ya Mbowe inafua gari ya Lissu inafuata gari ya Walinzi inafuata gari ya muziki wanafuata watu wanaokimbia na gari ya muziki huku wakicheza, zinafuata bodaboda na Magari mengine yanafuata. CHADEMA Wamejitahidi ulinzi.

1619hrs Msafara umefika Mataa ya Karume. Trafiki wapo wanasafisha njia

1644hrs; Msafara umefika njiapanda ya Kigogo. Watu n Wengi sana wamesubiri kumuona Lissu




1700hrs: Msafara umefika Mataa ya Magomeni. Hakuna tatizo lililoteka hadi sasa na Askari wametoka Barabarani. Bodaboda wanaongoza Magari

IMG_20200727_173131_596.jpg

1733hrs: Msafara Umefika Mkwajuni. Tumekuta gari la Polisi, sasa ndo linaongoza msafara na kuangalia Usalama. Hamna fujo, watu wanaimba tu.
IMG_20200727_174308_546.jpg

1736hrs: CCM wachache wamejipanga Barabarani wanazomea Msafara. Walinzi wa CHADEMA wamewaomba waondoke sababu wanaweza sababisha vurugu kwani tangu mchana hakina fujo iliyotokea. Wamekubali wakaondoka
IMG_20200727_175529_961.jpg
IMG_20200727_175243_557.jpg

IMG_20200727_181422_7.jpg

1750hrs: Msafara umefika makao makuu

LISSU ANAONGEA NA WAANDISHI WA HABARI

1818hrs: Viongozi wa dini Wanashukuru Mungu kwa kumfikisha Lissu salama.

1821hrs: Freeman Mbowe anasema.

Waheshimiwa viongozi wa kiroho na Wa chama chetu, wapenzi na Wanachama wetu tukiotoka wote uwanja wa ndege, tunashukuru sana.

Sisi kama Wanachama wa chadema, tukitambua nchi yetu inakabiriwa na Msiba mzito wa Rais Mstaafu Mkapa, tusimama kwa dakika moja kumuombea Mwenzetu.

Wote tulio hapa, leo ni siku tuliisubiri kwa miaka Mingi. Hadi kufika dakika hii ni salama. Mhe. Lissu mbele yako ni familia ya chadema wanahabari na Watanzania. Nakukabiribsha sana. Kazi ulioacha tumeiendeleza. Chama kipo salama na chama kipo tayari kwa uchaguzi.

1826hrs: Ndugu zangu wote popote mlipo, salaam.

Nina mambo mengi ya kusema na muda si rafiki. Tutazungumza mengi sababu hiki ni kipindi cha maneno mengi na yatakuwa mengi kwelikweli.

Kwakuwa leo ndo kwanza nimefika, toka jumatano mpaka leo nchi nne na sijalala. Nlikuwa Ujeruman uholanzi ubelgiji na leo nipo nyumbani, nmechoka kiasi

Mungu wetu ni mwema sana. Katika mazingira ya kawaida sikutakiwa niwe hai na sikutakiwa niwepo hapa. Lakini kwakuwa Mungu wetu ni mwema na ni wa haki, nipo hapa leo, nimerudi nyumbani. Ilikua miaka mitatu migumu. Leo natembea. Sikupaswa kuishi, sasa ukiniona nmevaa vaa hivi unaweza usielewe sana. Nikivua Magwanda haya wote mtakimbia. Huu mwili ni ramani ya makovu ya risasi na visu vya madaktari. Huu mwili umejaa vyuma vitupu. Huu mkono unachuma.

Kuna risasi ipo Mgongoni. Madakitari walisema kubaki ni bora kuliko kuitoa.

Nlipoanza hii safari nlianzia kwa madaktari wangu walionitibu kuwaaga.

Waliniuliza utaweza kweli? Wakasema inabidi tusubiri tukiwekee lile liantena na mfupa tuuvunje na kuunga tena. Nikawaambia hapana nimepona

Mungu wetu ni mwema. Haki huinua taifa.

Wanaopona chupuchupu kama mimi. Nlitamani na mimi nifanye hivyo, goti halikunji, kwahiyo nikija kanisani nisipige magoti msishangae. Lakini nimepona.

Wengi mnafikiria hivi, huyu bwana huyu hayo madhira aliyopona. Lakini fikirieni wazazi wa ben sananiAlfonce Mawazo, au Mke wa Azory Gwanda au Wazazi wa Akwilina wanaemaje? Mimi ni mzima mimi nina bahati. Na wengine wote tulipotishwa kwenye huu moto wa miaka mitano lakini nado tumesimama sisi tunabahati.

Tumshukuru Mungu, ametuwezesha kusimama na kutoa Ushuhuda na kuonesha dunia nzima mambo ya Tanzania hii. Tumshukuru Mungu

Mandera miaka 11 kabla ya kufungwa maisha alisema: Ili tufike tuendako wengi wetu tutapitia Kivuli cha mauti. Sio rahisi. Na sisi ndo tunapitia.

Na wasioiweza hii safari tumewaona. Wengine wamekumbia, wengine wamedanganywa, wengine wamenununuliwa. Walioshindwa kufanya hivyo wamekiona cha kitemakuni.

Thahabu inapita kwenye moto, chuma imara kinapitia kwenye tanuru la moto. Ili iwe chuma imara au dhahabu safi lazima ipitie moto..

Chama chenye wanachama zaidi ya milioni sita ambao leo wameisimamisha Dar, inabidi tupite. Hata yakobo alitenguliwa kiuno. Sasa ikitutokea sisi kuna shida gani? Haya ni maandalizi tu.

Nawashukuru watu wote. Hamkutuuacha. Kuna watu waliingizwa jela miezi kadhaa iliyofika. Hawakumaliza wiki. Tunawashukuru kwa miaka hii mitano ya kupita kwenye bonde la uvuli wa mauti.

Nlimwambia Mwenyekiti, hawa watu wameniumiza kwelikweli. Ndo nayokumbuka. Nlikuja kuzinduka kwenye chumba cha baridi kwelikweli.

Yote ni kwa sababu Viongozi hasa mwenyekiti kisema Muhimbili hapana. Vinginevyo tungekuwa tunazungumzia kuadhimisha miaka mitatu yaa.. Nawashukuru.

Sheria ya bunge inasema: Mbunge Una haki ya kutibiwa kwa gharama za bunge ndani au nje ya nchi. Mimi sikupata hata senti tano. Watanzania na watu wengine wakasema kama hawawezi kumtibu aibu iwe yao. Wa Tanzania walijichangisha na kuja kuniona Nairobi. Hakuna kitu kizuri kusaidomiwa na watu ambao huwafahamu. Nawashukuru Wakenya Wabeligiji. Mimi nina damu nyingi sana. Damu ya Wazazi wangu, Damu ya Watanzania, Damu ya Wakenya na Damu ya Wabeligiji. Nawashukuru sana kwa kujitolea damu. Nasikia mliambiwa ninyi ni marufuku kunitolea damu. Wakenya walipanga foleni kunitolea damu. Nawashukuru sana na Mungu awabariki sana. Mimi nmeokolewa na Wasamalia wema wa nchi hii na Kenya na Ulaya.

Nawashukuru Ndugu zangu hasa familia yangu. Nawashukuru watu wa Jimbo langu. Hakuna hata mmoja aliyeunga juhudi. Sio kwamba hawakutishwa, sio kwamba hawakufungwa.

Nawapa pole CCM kwa kuondokewa na mwenyekiti wao wa taifa wa Zamani. Nawapa pole watanzania kwa kuondokewa na rais wao amrijeshi mkuu kwa miaka kumi. Huu msiba ni wetu sote, si wa rais Magufuli naye nimpe Pole.

Kwakuwa ni Msiba wetu sote, kesho tuungane kutoa heshima zetu za meisho kwa rais Mkapa.

Mkapa ndo rais wetu wa kwanza wa vyama vingi. Haya ambayo tunayaona miaka miaka mitano hii hatukuyaona wakati wa Mkapa. Lazima tuseme ukweli. Tunaenda kumpa heshima kwa sababu alilea mfumo wa vyama vingi. Yalikuwepo mambo mengi. Kesi yangu ya kwanza ya Uchochezi ni Uongozi wa Mkapa. Yapo Mabaya lakiti tutatumbue huyu alikuwa rais wetu. Kesho tusindikizane. Tukawape pole ndugu zake familia yake na wanaccm wenzake. Sijajua saa ngapi.

. Niwatakieni kila la heri mwaka wa Uchaguzi. Mwaka huu utakuwa mgumu. Anayefikiria itakuwa rahisi, atakuwa hajaisoma namba.

Naomba niwashukuru wanahabari. Miaka hii mitano, habari imekua shida kwa nchi hii.

Leo mumesoma Tanzania Daima? Halipo na mengine mengi. Pamoja na shida hii ya miaka mitano kwenye sekta ya habari hamjaangusha kalamu zenu japo wapo ambao kalamu zimelegalega. Nawashukuruni nyote. Mlewe na nyia miaka hio mitano haikuwa halisi.

Kuna siku nlisema bungeni kwamba mnadhani wanatushughulikia sisi? Hadi Makamba na Kinana hawakubaki salama. Msibwage manyanga. Kesho tukamuage Mkapa baada ya hapo tuzungumze haya maneno mengi mwaka huu.

Mlidhani nitakamatwa nliwaambia nipo tayari kukamatwa. Polisi kuna chumba changu kinaitwa Lissu. Asanteni.
 
PICHA KUTOKA JNIA

======

UPDATES;

1105HRS: Hapa uwanjani pametulia, hakuna fujo wala dalili za fujo, Wanachama wachache wa CHADEMA wanaonekana wakipita pita huku na kule. Bado sijabahatika kuona gari la Polisi Wala Gari la CHADEMA.
IMG_20200727_105436_576.jpg

IMG_20200727_105223_845.jpg

Ratiba inaonesha muda wa ndege kufika ni saa saba na dakika Ishirini. Angalia kwenye chati
JamiiForums-1729159940.png

1121hrs: Saa moja iliyoisha Tundu Lissu ndo amepanda ndege ya Ethiopian Airlines ET 805 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Bole Addis Ababa kuja hapa Dar Julius Kambarage Nyerere International Airport.

Safari inatazamiwa kuchukua masaa yasiyozidi Matatu kufika hapa tulipo.
IMG_20200727_113057_193.jpg

1140hrs: Mwenyekiti Mkoa wa Iringa CHADEMA William Mungai, aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi(Sugu) Wakiwa Wamefika hapa Uwanja wa ndege kumpokea Lissu
IMG_20200727_115246_012.jpg

1156HRS: Kutoka kushoto: Hekima Mwasipu, Wakili wa Chadema, Sugu, Catherine Ruge(Simba Jike) Viti Maalum Mara na Mgombea wa Jimbo la Segerea CHADEMA
IMG_20200727_122146_598.jpg

1230hrs: Polisi Magari Mawili ya Polisi wameshusha Wanausalama wa kulinda amani wapatao kama 30 nje ya Viunga vya Uwanja wa ndege. Wamekaa mstari kama Gwaride na wanapewa Maelekezo. Wameshusha njia Panda ya kuelekea Uwanja wandege. Kuna askari wanne walikuwepo tangu asubuhi Wakihoji kila anaye ingia.

Bodaboda kama 50 wapo hapo Askari Polisi Walipo, nadhani Wamekataliwa kuingia. Vilevile Magari ya CHADEMA maarufu kama Magari ya M4C, Yapo sehemu hiyo ya njiapanda yakizunguka huku na kule. Magari ya CHADEMA yapo Matano yamejaa watu waliovalia nguo za CHADEMA.

Polisi ukijielezea unapoelekea ndo Wanaruhusu. Lalikini kuna baadhi ya Wafanyakazi(Walinzi wa Uwanja, sio Polisi) ndo wanakataza watu kuingia.
IMG_20200727_123741_321.jpg
IMG_20200727_123844_797.jpg

1240: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameweza kupenya na kuongia ndani sehemu ya kusubiria Wageni
IMG_20200727_121926_234.jpg
IMG_20200727_121920_225.jpg
IMG_20200727_121758_653.jpg

IMG_20200727_124902_929.jpg

IMG_20200727_130335_087.jpg

1300hrs: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameruhusiwa kuingia. Wengine wapo nje ya Uwanja wanaimba nyimbo.
IMG_20200727_131504_538.jpg

Polisi Tanzania Wamewaruhusu Wanachama wote wa CHADEMA na Wafuasi wa Tundu Lissu. Muda wowote ndege itawasili

8A366DB3-BD94-46D7-8037-E7A882782C36.jpeg


62A49FD3-A299-4095-B8F3-441BD8502109.jpeg


Lissu.jpg

IMG_20200727_153229_3.jpg
IMG_20200727_153233_2.jpg
IMG_20200727_154843_337.jpg
 
Back
Top Bottom