Unatuzungumziaje tunaooneshwa care na mapenzi yote ikiwa hatujakutwa bikra? Huoni kama mtazamo wa maisha unatofautiana? Kuna wanaong'ang'aniwa na hawajakutwa bikra hilo pia mnalisemeaje? Au ndo mnaita aina hiyo ya wanaume kuwa ni "Wajinga". Mimi ni mwanamke naongea kwa experience nyinyi ni wanaume mnawasemea wanaume wengine ambao si wote wapo humu ama si wote wamechangia mjadala huu,

Najaribu kufikiria tatizo hapa ninini, fikra zangu zinaniambia Shida ya vijana wadogo (ambao wengi wanaendesha mjadala huu ) ni hii, mioyo imekufa ganzi, hamna hisia za kupenda, kwanza mna hustle na mengi, hamuamini kama mnaweza kupendwa hivyo hivyo mlivyo pasina kujiweka accessories zikamilishe kujiamini kwenu. Mnaogopa sana kulinganishwa, ndio maana mnawasaka mabikra kwakuwa hawana chakulinganisha, kikawaida mtu asiyejiamini ukimlinganisha na mwingine unamuondolea kujiamini kwake, kwasababu kujiamini kwake kuna mashaka makubwa, Kingine wasichana wa umri wenu hawawataki ndio kabisa kunawavua kujiamini. Ndio yanaibuka ya ohh used mara makombo n.k

Mi nina ushauri mdogo tu kama dada yenu tafuteni maisha, mpate pesa, mkue kidogo maana ni wazi with age comes wisdom. Itafika muda katika maisha unajiweza basi automatically moyo unafunguka unampenda mtu bila vigezo vingi, sio kwamba sasa hampendi hasha! mnapenda sana ila mna mashaka yakupendwa back. Ok ama sivyo chukueni wasichana wadogo sana 18-21. Mnaanza kuwakuza taratibu ikiwa nanyi mnakua, mnaongeza age, kipato, wisdom etc itafika time mnapatana sana. Ila ndo mkiwachukua wakiwa wadogo hakikisheni mnawaoa baadae Hizi ni fikra zangu binafsi sio lazima ziwe kweli, zinaweza kuwa uongo pia.
1-wanaoonyesha maximum care kwa used ni wajinga/malimbukeni or hajapata bikra

2-tunaofunguka hapa ikiwemo Mimi si wadogo Wa kiumri na kipato (japo sio wote) kama unavyojaribu ku portray,
Na FYI , core desires z a wanaume hazibadiliki kwa age wala rank ya maisha ,hence ukweli utabaki ukweli kwa kibabu hata cha miaka 80+ ni furaha kuwa na bikra kubali au kataaa ,na ndo maana hata leo mzazi ajiua bint yake ni bikra anajisikia ufahari

Hayo yote unayasema ya kupenda makombo ni vile,hakuna bikra basi mengine ni kujifariji tu,
 
Sasa upate mwanamke mwenye sifa zote...uzuri mpaka tabiaa afu usimuoee kisa ulikuwa na mpango wa Kuoa bikraa...!?? Kuwa serious mkuu mambo ya Ubikra ni zamani siku hizi hata ukimshirikisha MTU kumwambia hiyi sababu atakuona falaa...!
Sasa naoa mimi au anaoa mtu

Mimi ndo ntakaeishi naye huyo mwanamke, kifupi kuoa mwanamke used hakunipi Amani ya Moyo (inanipa kinyaa flani )

Sasa nioe sifa Nzur afu sina feelings hapo vipi mzee
 
Sasa upate mwanamke mwenye sifa zote...uzuri mpaka tabiaa afu usimuoee kisa ulikuwa na mpango wa Kuoa bikraa...!?? Kuwa serious mkuu mambo ya Ubikra ni zamani siku hizi hata ukimshirikisha MTU kumwambia hiyi sababu atakuona falaa...!
Kwa kifup ili nioe

Lazima mwanamke awe na sifa nizitakazo(sio lazima ziwe zote coz sioi malaika)+ BIKRA
Bila hivo no thank you
 
1-wanaoonyesha maximum care kwa used ni wajinga/malimbukeni or hajapata bikra

2-tunaofunguka hapa ikiwemo Mimi si wadogo Wa kiumri na kipato (japo sio wote) kama unavyojaribu ku portray,
Na FYI , core desires z a wanaume hazibadiliki kwa age wala rank ya maisha ,hence ukweli utabaki ukweli kwa kibabu hata cha miaka 80+ ni furaha kuwa na bikra kubali au kataaa ,na ndo maana hata leo mzazi ajiua bint yake ni bikra anajisikia ufahari

Hayo yote unayasema ya kupenda makombo ni vile,hakuna bikra basi mengine ni kujifariji tu,

Nilideclare kuwa nilichosema ni fikra zangu, zinaweza kuwa kweli ama uongo. Uzuri mimi si mnafiki siwezi sema nyeupe penye nyeusi.

Shida ipo kwenu kuona wengine ni wajinga ikiwa tu walioa si bikra na wanawapenda na kuwa care hehe, Je mkuu unafahamu kuwa kwa wewe kusema ni wajinga haiwafanyi kuwa wajinga kweli? Ujinga wao unabaki katika mtazamo wako? Unafahamu? Ingeletwa maana sahihi ya mjinga tungeweza kupima ujinga wao. Or else.......

FYI core desire za wanaume?? ikiwa tu wewe ni msemaji wa wanaume wote na wamekutuma useme hivyo! Mimi pia sio msemaji wao ndio maana argument zangu zinaegamia pande zote mbili, ikiwa ninyi mnaona point A tu najaribu kuwaonesha point B, kama kuna A na B na vyote vinapatikana katika duara moja huoni kuwa wewe upo sahihi na wao pia? Je unaonaje?
 
Back
Top Bottom