Watu wamesahau msemo usemao; Mtalaka hatongozwi.

Huwezi mtongoza mwanamke uliyekuwa naye kwenye relationship, bali mnakummbushia tuu.

Lakini Mwanamke bikra ukimuoa tambua kabisa kila anayekuja lazima atongoze, na kutongoza ni mchakato, lakini kama mkeo hakuwa bikra ma-ex wake wakuja hakuna cha mchakato wowote
 
Lakini inategemea unachokiita uchanga, huwezi sema mtu mwenye uzoefu wa miaka saba kuendelea ni mchanga, labda uwe umelogwa. Hata kwenye maombi ya kazi hicho kigezo hakipo

Hujaelewa kabisa nilimaanisha nini, miaka saba bado hujapata changamoto za ndoa.

Watoto hawajakua, hawa nichangamoto za kutosha ndani ya ndoa.

....malezi na kuhifadhi hizo bikra zako
.... mahusiano ya mama kunawakati anaegamia kwa watoto nk

Bado hujapata ile maturity respect ya ndugu jamaa na marafiki... backlog yake hatari sana

Bado hujaingia effectively kwenye social responsibility ..... watoto wapo vyuoni, harusi, majirani , misiba nk

Sasahivi nitakuelimisha kidogokidogo. Ukitaka utaelewa. Usipota pia sawa
 

Unauhakika sijapata changamoto?

Hayo uliyoyataja hayawezi kuniondoa kwenye reli dunia ingalipo nami nikiwepo. Huwaga siogopi changamoto,
Kwenye maisha ukishajua wakuandamana naye basi hakuna litakalo kushinda,ukishajua yupi ni sahihi na yupi sio sahihi hakuna litakalo kushinda. Ukishajua wakati upi ni sahihi na wakati upi sio sahihi hakuna litakalo kushinda.

Naomba ujue kuwa mimi ni wale watu ambao hatushindwi na lolote tukiamua. Mimi ni mwanaume, na sifa ya mwanaume ni kutiisha mazingira yake kwa vyovyote vile, kwa wema au kwa ubaya.

Karibu sana.
 
Una hoja nzuri kwa wakti uliopita. Kwasasa hoja yako ni dhaifu. Hao bikra hawashikiki sasa, wanataka kuonja na pengine.

Mimi daima ntawatetea wanawake, kwani wanatongozwa na wanaume za watu pia. Suala la kutongoza kwa mwanaume kawaida; halikadhalika kwa mwanamke kutongozwa.
Kukubali ni suala la mtu binafsi bila kujali bikra ama la! Na suala la kuamua kutongoza ni binafs bila kujali mume wa mtu ama la!

Inashangaza sana kushutumiwa aliyepokea Mali ya wizi, kuliko aliyeiba na kuileta. Wenye akili wameelewa
 
round hii watafyata tuu
 

Uliza waliooa bikra acha kuhadithiwa propaganda na malaya.

Ni sawa ni zile propaganda za masikini kuwa ati wenye pesa hawana amani Wakati sisi wenye pesa tunakula maisha mazuri.

Ogopa propaganda za watu walioshindwa
 

Unaweza usishindwe lolote lakini ndoa nikitu kingine

Ukitaka kujuwa fanya uchunguzi changamoto za ndoa hazina :-
Tajiri
Maskini
Msomi

Hakuna theory kwenye ndoa ni practical directly

Unaweza kubishana sababu bado unakomaa hujui zaidi kifuatacho

Na hakuna ajuwae kesho yake, or else watu wasingekufa katika ajali. Wangeahilisha
 
Unazeekaje bikra zimejaa kama njugu mtaani.

Mimi wa kwangu nilimpata akiwa kidato cha tano Akiwa anasoma St. Marry, tangia hapo nikakaza mpaka nikaja nikamuoa hiyo 2013 akiwa anasoma mwaka wa nne Pale Muhimbili
Mkuu alikupenda au ,ulivokuta bikra ukaforce mpaka ukaoa
 

Mimi sishindwi Mkuu na lolote, ukiona nimeingia kwenye jambo lolote tegemea ninashinda.

Ndoa ni kitu kingine kwa watu wasiofuata itifaki na taratibu, wewe mtu haoni umuhimu wa Bikra huyo sidhani kama anaelewa maana ya ndoa.

Jambo lolote usipofuata utaratibu lazima likuchezeshe,

Ndoa sio ngumu
Maisha sio magumu
Hakuna jambo gumu,

Ugumu upo kwa wasiofuata itifaki na utaratibu.

Wewe mtu hajui umuhimu wa Bikra kwa mke atakayemuoa alafu utegemee akili zake zipo sawa?

Vijana msitishike, oeni wake zenu wenyewe, usioe mke wa mtu mwingine(ambaye hujaikuta bikra yake)
 

Theoretically yes.
 

Kua uyaone wanawake ni viumbe vigumu sana kuwaelewa. Hawana formula so usije jiandikia formula yako ukafikiri ina work kwa viumbe wanawake. Awe bikra si bikra mke mwema anatoka kwa Mungu. Hata malaya once walikuwa bikra. Dunia ya leo na utandawazi watu wanataka kuonja ladha tofauti wake kwa waume. Hadithi ulizosimuliwa na babu yako kuhusu wanawake delete anza kuwasoma ila usijaribu kuwaelewa. Kingine wanawake ni wasiri sana.
 
Mkuu alikupenda au ,ulivokuta bikra ukaforce mpaka ukaoa

Yeye ndiye alikuwa ananipenda, mimi sikuwa nampenda mpaka siku aliponiambia ni bikra. Nikamwambia naomba kuthibitisha huku nikijua ni muongo, kuchungulia vitu vimo.

Nilijifunza kumpenda tangu pale, nikiri kuwa nilikuwa nampenda mwanamke mwingine lakini alikosa kigezo kimoja cha ubikra. Hata hivyo nilifundishwa kuutiisha mwili, akili, na hisia zangu. Hivyo nilizilazimisha hisia zangu kumuelekea mke wangu niliyemkuta bikra. Hapo nilikuwa Udsm, yeye alikuwa st. Marry.
 

Mke mwema anatoka kwa Mungu, na kamwe Mungu hawezi kukupa mwanamke asiye na Bikra. Huyo mungu atakuwa mungu wa matope.

Nianze kuwasoma wakati nimeshahitimu na kuoa nimeshaoa?
 
Theoretically yes.

Ningekua sijaoa ningesema ni nadharia lakini nimeoa na watoto ninao.
SIo kwenye ndoa hata kwenye mambo mengine ya kiuchumi usipofuata utaratibu lazima ucheze shere.

Wadanganye wenzako hapo,

Nimekupa aya hapo
Mambo ya lawi 21:
13Kuhani mkuu aweza tu kumwoa msichana ambaye ni bikira. 14Haruhusiwi kuoa mwanamke mjane, mwanamke asiye bikira, wala kahaba. Ni lazima aoe bikira kutoka watu wake mwenyewe 15asije akawatia unajisi watoto wake mwenyewe. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu niliyemweka wakfu.”

Mambo ya walawi 21
7Kwa kuwa kuhani amewekwa wakfu kwa Mungu wake, kamwe asioe kahaba, wala mwanamke asiye bikira wala aliyepewa talaka.

Kama huelewi hata mimi sitaki uelewe kwani wewe sio mwanaume, ujumbe huu haukuhusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…