Nyie watu wa dar hayo sio mafuriko bali ni matokeo ya ujenzi wa hovyo hovyo, ujenzi holera, jiji halina mpangilio mnategemea maji yapite wapi? Na msipopangilia ujenzi wenu siku moja tutakuja kuwaokota baharini.
Sioni mkoa mwingine wakilalamika mafuriko tofauti na dar, mvua ya dakika tano tu ati mafuriko, je ikinyesha siku nzima si nyumba zenu itakuwa makazi ya samaki na papa wa baharini?.
Wewe ndo umemaliza kila kitu.Hii mvua ndogo wala si ya kutisha ila uholela wa wakazi. Hivi ingekuwaje kama zikija zile mvua za vimbunga kama katrina storm ambazo huwa zinapiga huko marekani na nchi za huko carribean au zinazopiga huko China ambazo huangusha hadi magorofa
rain.jpg
 

Attachments

  • katriina.jpeg
    katriina.jpeg
    1.5 MB · Views: 9
Najua hili na nilikuwa namwonyesha mjinga mmoja kwamba binadamu tumepewa uwezo wa kufanya makubwa na siyo kila kitu ni kudra za Mungu.
Alisema msomi mmoja "uwezo wa ubongo wa mwanaadamu asili yake kama umejikuja au umejinyongorota lakini ukikunjuliwa unaweza kutoka hapa Afrika mpaka bara Amerika na kurudi kama round nne hivi"

Hiyo ni falsafa na ilikuwa na maana. Chakata kichwa uelewe maana na uwezo wa mwanadamu ni mkubwa kiasi gani. 😊
 
Hiki nachokiona hapa Kwenye taarifa ya habari 🙄😳🤔
Sio mchezo jmn
Sio Kwa hii mimaji
Halafu ubaya wa haya maji yanakuwaga na choo 🙌
 
Wewe ndo umemaliza kila kitu.Hii mvua ndogo wala si ya kutisha ila uholela wa wakazi. Hivi ingekuwaje kama zikija zile mvua za vimbunga kama katrina storm ambazo huwa zinapiga huko marekani na nchi za huko carribean au zinazopiga huko China ambazo huangusha hadi magorofaView attachment 2806057
Mitaro midogo,halafu 2007/8 pale walituambia wanapanua mitaro,mjini ikawa foleni..lakini hakuna lolote
 
Ukonga Banana hapa gari haziendi Gongo la Mboto wala Mjini.

Mkandarasi amechimba chimba barabara.

Ni zaidi ya saa (li)moja sasa toka Airport gari haijafika Gongo la Mboto
Mtu anayetoka hapo anaenda kurasini apite wapi?

Azunguke kinyerezi tabata au wapi?
Ile njia ya vingunguti ndani ndani inatokea majani ya chai na vingunguti relini inapitika?
 
Kufuatia watu wengi kuziba njia za maji hasa viwanda na maghala maneno ya Tabata relini kwenda Buguruni na sehemu zingine, serikali iwatake walioziba njia hizo za maji watengeneze njia mbadala au sivyo wakubali serikali irudishe hizo njia za asili kwenye eneo.
 
Back
Top Bottom