Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
1,020
678
Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na Waandishi wa Habari

Ijumaa, Aprili 12, 2024
3:30 Asubuhi
Ukumbi wa TTCL, Jengo la TTCL, Ghorofa ya 12, Barabara ya Samora, Dar es Salaam


UPDATES
Mvua na Mafuriko
Itakumbukwa kwamba tarehe 24 Agosti, 2023, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa taarifa ya mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli nchini ambazo hutokea katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba. Aidha, mapema mwezi Februari 2024, TMA ilitoa tena mwelekeo wa mvua za msimu wa masika ambazo kwa kawaida huja mwezi Machi hadi Mei.

Misimu ya mvua za vuli na masika ni mahsusi kwa maenco ya nchi yetu yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Macneo hayo ni mikoa ya kaskazini mwa pwani ya bahari ya Hindi; kaskazini mwa nchi na kanda ya Ziwa hadi kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. Mikoa iliyobakia hupata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.

Kwa taarifa hizo za TMA za mwaka jana, Tanzania ilikuwa ikitarajia kupata mvua za El Nino kuanzia mwezi Oktoba 2023 hadi Februari na baadaye TMA ilijulisha kwamba mvua hizo zitaendelea na kuungana na masika hadi mwezi Mei 2024. Mvua za El Nino si ngeni Tanzania kwani zimewahi kunyesha mwaka 1982/83; mwaka 1997/98 na 2015/16 na kusababisha mafuriko makubwa katika baadhi ya maeneo nchini, hususani, katika ukanda wa pwani.

Pamoja na mafuriko haya kutabiriwa na tahadhari kutolewa, lakini athari zake haziepukiki. Hadi kufikia sasa, kwa mujibu wa taarifa za Jeshi la Polisi, kati ya tarehe 1 Aprili na tarehe 11 Aprili, jumla ya vifo 19 vinavyohusiana na mvua hizi kubwa tayari vimetokea katika baadhi ya mikoa. Mikoa iliyorekodi vifo hivyo ni Lindi, Njombe, Tanga, Pwani (Mkuranga na Kibaha), Manyara, Mbeya, Geita na Rukwa. Kimsingi nchi nzima ina hekaheka za mvua.

Eneo lililokumbwa na mafuriko zaidi hadi kuhitaji Kamati ya Kitaifa ya Maafa ifanye ziara za tathmii, ni mkoani Pwani katika wilaya ya Rufiji na Kibiti, wilaya mbili zilizopo kwenye ukanda wa mafuriko wa bonde la mto Rufiji. Eneo la pili ni Mlimba, wilayani Kilombero katika mkoa wa Morogoro kwenye eneo la bonde na mto Kilombero. Ifahamike kuwa mto Kilombero huchangia 62% ya maji ya mto Rufiji, ambao pia hukusanya maji kutoka mikoa mingine kadhaa ikiwemo Ruaha Mkuu na Luwegu

Kwa maelekezo ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, timu ya mawaziri na manaibu mawaziri kumi na makatibu wakuu wao, ilifanya ziara kwenye maeneo yalioathirika mnamo tarehe 10 na 11 Aprili (siku za ldi Mosi na ldi Pili), ikiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama. Mbali ya kutoa salamu za pole za Mhe, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, viongozi hao pia walitoa ahadi za misaada ya serikali na kuagiza miundombinu iliyoharibika ifanyiwe kazi.

Tathmini ya Madhara
Mpaka sasa mkoani Pwani kuna vifo vitano tofauti na ripoti ya Polisi (Rufiji 2, Kibiti 2 na Kisarawe l); majeruhi 2 Kibiti na 3 Kisaware na kisha uharibifu wa mashamba ya mazao (mahindi, mpunga, ndizi, ufuta, mihogo, matama na pamba), makaazi, miundombinu ya barabara, madaraja, nguzo za umeme, shule, kituo cha afya cha Muhoro kusombwa na maji.

Kwa ujumla kata 12 kati ya 13 za wilaya ya Rufiji:; kata 5 kati ya 13 za wilaya ya Kibiti; na kata I wilayani Kisarawe zimeathirika. Kwa ujumla watu 126,831 wameathirika mkoani Pwani: 88,768 (Rufiji), 36,900 (Kibiti) na l,163 (Kisarawe).

Hekta za mashamba zilizoathirika ni 33,930.24 (Rufiji), 71,366 (Kibiti) na 167 (Kisarawe). Hadi sasa watu 1.014 wameokolewa wilayani Rufiji.

Mkoani Morogoro zimesababisha vifo 28 katika halmashauri & na kubomoa nyumba 1 .035 zingine 6874 kuzingirwa na maji. Vifo hivi ni tofauti na vile vilivyoripotiwa na Polisi.

Ekari 34,970 za mazao mbalimbali yakijumuisha mahindi, mpunga, ufuta, pamba na mazao mchanganyiko zimeathirika na pia mifugo 1,466 imeathirika. Miundombinu ya reli, barabara, makalvati na madaraja imeharibika katika halmashauri za Malinyi, Mlimba, Ifaraka Mji, Ulanga na manispaa ya Morogoro imeharibika.

Kamati za wilaya na mikoa za maafa zinaendelea na kazi ya kufanya tathmini ya uharibifu na mahitaji huku serikali kuu ikitoa misaada mbalimbali. Aidha, misaada mbalimbali kutoka kwa wadau imeendelea kupokelewa na kufikishwa kwa waathirika.

Tayari dawa za tiba kwa binadamu na za tiba ya maji, huduma za afya, chakula, malazi, uokozi, usalama, ushauri nasaha, vimeanza kuwafīkia wananchi. Aidha, askari wa wanyamapori wamnepelekwa kwenye maeneo yote ili kudhibiti wanyama aina ya mamba.

Kamati ya Kitaifa ya Maafa imechukua jukumu lake kutokana na ukubwa wa maafa. Leoasubuhi Kamati Tendaji inayoundwa na Makatibu Wakuu imekutana na baadaye itafikisha taarifa kwa Mhe. Waziri Mkuu kabla ya Kamati ya Mawaziri kukutana haraka.

Bwawa la Umeme la Julius Nyerere
Kwa kuzingatia kwamba eneo la bonde la mto Rufiji limekuwa na historia ya mafuriko, serikali tangu miaka ya 1970 iliazimia kubuni mradi wa kuyatumia maji hayo ili kupunguza mafuriko na ndipo wazo la kujenga bwawa la kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za maji lilipozaliwa. Lengo kuu lilikuwa kupunguza mafuriko na kuzalisha umeme nchini.

Bwawa hili lenye ukubwa kilomita za mraba 1,194, lina uwezo wa kuhifadhi maji kiasi cha mita za ujazo bilioni 32.782 na likiwa na kina cha mita 184 juu ya usawa wa bahari. Kazi ya kujaza maji ilianza tarehe 22 Desemba, 2022, na ingawa tayari kulishakuwa na kina cha maji cha mita 75, lakini ilitarajiwa kwamba ingechukua miaka mitatu kujaa.

Hata hivyo, kutokana na mvua kubwa, hususani kuanzia Oktoba 2023, bwawa hilo lilifikia kina cha mita 181 ilipofika Februari 2024. Aidha, tarehe 5 Machi, 2024, bwawa hilo lilifikia kina chake cha ukomo kitaalam cha mita 184.

Mvua kubwa za El Nino zilifikia kupitisha maji kwa kiasi cha mita za ujazo 8,445 kwa sekunde (sawa na ma-simtanki ya lita 1,000 jumla ya 8,445 kwa kila sekunde) mnamo tarehe 15 Februari, 2024. Hivyo basi, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lilizitaarifu mamlaka za wilaya za Rufiji na Kibiti kwamba kwa kuwa mvua bado ni kubwa na bwawa sasa lilikuwa limejaa, litaanza kufungulia maji ili yaendelee na safari yake kuelekea baharini.

Hata hivyo, wingi huu wa maji ni kidogo kulinganisha na kiasi cha Mei 1974 kilichofikia mita za ujazo 13,212 kwa sekunde. Aidha, katika mvua za mwaka 2020, kiasi cha maji kilifikia karibu sawa na cha mwaka huu ambapo kilikuwa mita za ujazo 7,144 kwa sekunde.

Kwa kuzingatia kuwa bwawa hili lilijengwa ili lipunguze mafuriko, mara baada ya kuanza kukusanya maji mnamo Desemba 2022, uwezekano wa mafuriko ulipungua hadi hivi sasa wakati wa mvua za El Nino ambapo kiasi cha maji kimekuvwa kikubwa mno.

Licha ya kwamba kulikuwa na hatua ya lazima ya kuyafungulia maji ili kuzuia bwawa lisiharibike, lakini ni hakika kwamba maafa ya mafuriko yalikuwa yamezuiwa yasiwe makubwa zaidi ya ilivyo sasa; yasitokee tangu Oktoba 2023: na kuwataarifu wananchi.

Ingawa maji yanayopita katika mto Rufiji yalifikia wingi wa mita za ujazo 8,445 kwa sekunde mwezi Februari 2024, na kuendelea kwa wastani wa mita za ujazo zaidi ya 6,500 kwa sekunde, lakini Tanesco imekuwa ikiachia kiwango cha chini zaidi ya hapo, kimsingi kati ya mita za ujazo 3,000 na mara chache hadi 6,000 kwa sekunde kwa siku tofauti za mwezi Machi na Aprili 2024. Kama si uwepo wa bwawa hili mafuriko yangekuwa makubwa zaidi.

Bonde la Msimbazi
Serikali inapenda kuutaarifu umma kwamba ule Mradi wa Bonde la Msimbazi jijini Dar es Salaam, sasa utaanza rasmi Jumatatu, tarehe 15 Aprili, 2024, ukisimamiwa na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini Tanzania (TARURA). Mradi huu utaanza kwa kubomoa nyumba katika eneo la Jangwani, kandokando mwa mto Msimbazi.

TARURA itaanza mradi huu kwa ubomoaji kwa kuzingatia makubaliano yake na wakaazi wa eneo hilo, kwamba nyumba zao zitafanyiwa tathmini: watalipwa fidia zao; na wiki sita baada ya fedha kuingizwa kwenye akaunti zao, TARURA itavunja nyumba katika enco husika.

Kufikia tarehe 29 Februari, 2024, TARURA ilikuwa imeshaingiza malipo ya fidia ya kiasi cha shilingi bilioni 52.61 kwenye akaunti za wamiliki wa nyumba wapatao 2,155 kati ya 2.329 walioandikishwa katika daftari la kwanza.

Hivi sasa TARURA inakamilisha malipo ya fidia kwa walhusika wengine 446 waliomo kwenye daftari la pili ambao hawakufanyiwa uthamini wa awali kwa sababu mbalimbali.

TARURA itashirikiana na ofisi za halmashauri za mkoa wa Dar es Salaanm katika maeneo ambapo mradi unapita ili kuhakikisha kazi inafanyika kwa usahihi na umakini.

Mradi wa Bonde la Msimbazi umelenga kupunguza athari za mafuriko; kuongeza matumizi bora ya ardhi: kuzuia mmomonyoko wa udongo; kurejesha uto wa asili: kuruhusu maji ya mto yaende baharini; na utunzaji wa maji.

Mradi huu utachukua miaka mitano hadi mwaka 2028 na utagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 260, sawa na shilingi bilioni 675 ambazo zitatumika kujenga miundombinu ya kukabiliana na mafuriko; ujenzi wa karakana ya mabasi ya mwendokasi kwenye eneo la Ubungo Maziwa baada ya kuihamisha kutoka Jangwani; ujenzi wa daraja la Jangwani; ujenzi wa bustani ya jiji na uendelezaji wa maeneo ya makazi na biashara; kupanua mto Msimbazi na kuuongeza kina: pamoja na usimamizi wa taka ngumu.

Aidha, TARURA inawashauri wananchi watakaokuwa na maswali kuhusu zoezi hili kupiga simu nambari 0738-353854 au 0738-353855 iwapo watahitaji ufafanuzi wowote.

Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano
Tarehe 26 Aprili, 2024, nchi yetu itatimiza miaka 60 ya muungano wetu ambapo sherehe za kitaifa zitafanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi atakuwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muunga, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, uzinduzi wa sherehe hizi utafanyika tarehe 14 Aprili katika Uwanja wa Amani mjini Zanzibar ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Tarehe 19 Aprili, 2024, kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, kutafanyika maonesho ya biashara. Mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Abdullah.

Vile vile, tarehe 22 kutafanyika maombi na dua za kuliombea taifa katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Muungano, Dkt. Philip Mpango.

Tarehe 23 Aprili kutakuwa na uzinduzi wa kitabu cha historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo imefikisha miaka 60. Uzinduzi huo utafanyikia Ikulu, Dar es Salaam, na mgeni rasmi atakuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kuanzia tarche 15 Aprili hadi tarehe 31 Mei, 2024. miradi mbalimbali ya maendecleo itakuwa ikizinduliwa na viongozi mbalimbali nchini kote.

Tarehe 25 Aprili kutakuwa na tamasha la miaka 60 ya muungano litakalofanyika katika wilaya zote nchi nzimna lakini kwa Dar es Salaam litafanyikia katika viwanja wa Tanganyika Packers, Kawe.

Mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.

Itakumbukwa kwamba Jumatatu, tarehe 8 Aprili, 2024, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, alizindua kauli mbili na nembo ya maadhimisho haya.

Kauli mbinu hiyo inasema: MIAKA 60 YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA: TUMESHIKAMANA NA TUMEIMARIKA, KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU.

Nembo iliyozinduliwa inatakiwa kutumika katika nyaraka za serikali, matangazo, mialiko, mapambo, na pia kutumika kwenye vituo vya televisheni vya umma na binafsi katika kipindi hiki cha kusherehekea miaka 60 ya muungano wetu. Vyombo vya habari vinaombwa kutia hamasa katika shamrashamra hizi za nchi yetu kufikisha miaka 60 ya muungano.

Pia, soma:
 
Sura ya huyu jamaa ina reflect vitu vingi vingi sana. Hata akiwa anaongea naona tu kama niko stendi ya daladala. Sawa tutafuatilia.
 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Mobhare Matinyi, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala ya mafuriko (Rufiji na Mlimba), mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), mradi wa bonde la mto msimbazi na maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano leo Aprili 12, 2024 jijini Dar es Salaam.

FB_IMG_1712920841482.jpg
FB_IMG_1712920854153.jpg
 
Hata mseme nini, msimamo wetu tunaujua.

Tunapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kwamba, uongozi wa CCM unajaribu kutumia kila njia kuonyesha hili tatizo halijasababishwa na Bwawa la Nyerere, pamoja na kuwapa TANESCO na wasemaji wa serikali na viongozi maagizo waseme nini ili kukwepa lawama.

Tunaukumbusha umma kwamba wanasiasa sasa ndio wamekuwa mainjinia wa kutoa ufafanuzi, na mainjinia wako kimya. Wenye akili wote wanajua kwamba tatizo ni kwamba Bwawa la Nyerere lilijazwa maji kupita kiasi na bila mpangilio, na walipogundua hili wakaamua kufungulia maji mengi kulinusuru bwawa na kuepuka mafuriko makubwa hata zaidi ambayo yangeleta maafa makubwa sana ikiwa Bwawa lingepata madhara. Hii ingekuwa habari ya ulimwengu na aibu kubwa kwa Tanzania, kashfa mbaya kwa uongozi wa Tanzania. Lakini hamtaki kukiri hili na kusema ukweli. Mbaya zaidi, mnawalaumu wananchi wa Rufiji kuwa wao ndio wamewasababishia haya matatizo.

Tunajua maelezo yote haya yanatokana na maelekezo toka juu kuhusu kutoa maelezo juu ya mafuriko ya Rufiji kwa sababu tu ya kuilinda serikali na CCM. Tunawaelewa, lakini wote mnaofanya hivi mnapaswa kuelewa mnashiriki dhambi ya wanasiasa. Tunatumaini dhamiri zao zitawishitaki.

Tungenda serikali itujibu ndio au hapana kwa maswali haya mawili;
  1. Je, ni kweli kwamba maji yalipofunguliwa Bwawa la Nyerere yalifunguliwa katika flow rate ambayo ilijulikana ingepeleka maji mengi downstream ambayo yangesababisha mafuriko?
  2. Je, ni kweli kwamba katika kipindi cha mwaka mzima cha masika na kiangazi, ikiwa maji yangeruhusiwa kupita kwa kiwango cha wastani unaokubalika, mafuriko yasingetokea kwa sababu ya dry and wet season flow rates balancing effect lakini hilo halikufanyika kwa kutaka Bwawa la Nyerere lijae haraka?
Tunataka muelewe kwamba si kila mtu ni mjinga wa kukubali maelezo ya kisiasa ambayo mnatoa, na maelezo yenu hayabadili ukweli kwamba mafuriko yanayotokea Rufiji ni uzembe tu wa kuruhusu viongozi wa kisiasa kujifanya wanajua kuliko wataalamu wetu, na kuelekeza mambo yafanyike kwa kuipromote serikali iliyopo madarakani na CCM

Tunajua kwamba Tanzania hatuna utamaduni wa kukiri makosa na kuomba msamaha. CCM sio chama cha kufanya hivyo, na sidhani kama Chadema wakija kuchukua nchi watakuwa na utamaduni huo. Kwa hiyo hili sio suala la kuwalaumu CCM dhidi ya Chadema, sio suala la kisiasa, bali ni ukweli kuhusu uzembe mliofanya na kuathiri maelfu ya Watanzania masikini.

Ushauri wetu kwenu ni kwamba, badala ya kutumia ubongo wa wanasiasa ku-manage maji ya bwawa la Nyerere, tumieni computer programe kama inavyotakiwa - flow in rate-retention-flow out rate. Mngefanya hivi, angalau mngewapa tahadhari wananchi miezi minne hata mitano kabla ya mafuriko, kama kweli tatizo lilikuwa ni natural weather issue.
 
Hata mseme nini, msimamo wetu tunaujua.

Tunapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kwamba, uongozi wa CCM unajaribu kutumia kila njia kuonyesha hili tatizo halijasababishwa na Bwawa la Nyerere, pamoja na kuwapa TANESCO maagizo waseme hivi.

Tunaukumbusha umma kwamba wanasiasa sasa ndio wamekuwa mainjinia wa kutoa ufafanuzi, na mainjinia wako kimya. Wenye akili wote wanajua kwamba tatizo ni kwamba Bwawa la Nyerere lilijazwa maji kupita kiasi na bila mpangilio, na walipogundua hili wakaamua kufungulia maji mengi kulinusuru bwawa na kuepuka mafuriko makubwa hata zaidi ambayo yangeleta maafa makubwa sana ikiwa Bwawa lingepata madhara. Hii ingekuwa habari ya ulimwengu na aibu kubwa kwa Tanzania, kashfa mbaya kwa uongozi wa Tanzania. Lakini hamtaki kukiri hili na kusema ukweli. Mbaya zaidi, mnawalaumu wananchi wa Rufiji kuwa wao ndio wamewasababishia haya matatizo.

Tunajua maelezo yote haya yanatokana na maelekezo toka juu kuhusu kutoa maelezo juu ya mafuriko ya Rufiji kwa sababu tu ya kuilinda serikali na CCM. Tunawaelewa, lakini wote mnaofanya hivi mnapaswa kuelewa mnashiriki dhambi ya wanasiasa. Tunatumaini dhamiri zao zitawishitaki.

Tungenda serikali itujibu ndio au hapana kwa maswali haya mawili;
  1. Je, ni kweli kwamba maji yalipofunguliwa Bwawa la Nyerere yalifunguliwa katika flow rate ambayo ilijulikana ingepeleka maji mengi downstream ambayo yangesababisha mafuriko?
  2. Je, ni kweli kwamba katika kipindi cha mwaka mzima cha masika na kiangazi, ikiwa maji yangeruhusiwa kupita kwa kiwango cha wastani unaokubalika, mafuriko yasingetokea kwa sababu ya dry and wet season flow rates balancing effect lakini hilo halikufanyika kwa kutaka Bwawa la Nyerere lijae haraka?
Ushauri wetu kwenu ni kwamba, badala ya kutumia ubongo wa wanasiasa ku-manage maji ya bwawa la Nyerere, tumieni computer programe kama inavyotakiwa - flow in rate-retention-flow out rate. Mngefanya hivi, angalau mngewapa tahadhari wananchi miezi minne hata mitano kabla ya mafuriko, kama kweli tatizo lilikuwa ni natural weather issue.
Na mafuriko yaliyotokea 1974 Rufiji Bwawa lilikuepo? mpk wimbo kuhusu kusaidia wana rufiji ukatungwa
 
Na mafuriko yaliyotokea 1974 Rufiji Bwawa lilikuepo? mpk wimbo kuhusu kusaidia wana rufiji ukatungwa
Wakijua kuna watu kama wewe ndio maana wanatoa staement kama hizo. Mwaka 1974 hakukuwa na Bwawa la Nyerere, na Bwawa la Nyerere limejengwa kwa ajili pia ya kuzuia mafuriko, lakini lazima ujue namna ya kubalance maji ili kuzuia mafuriko.

Unachotaka kusema, kwa kuwa akili yako imezoea kumeza kila unachoambiwa na wanasiasa, ni kwamba uwepo wa Bwawa la Nyerere hautazuia mafuriko hata miaka ya mbele. Sasa hilo si kweli. Kila itakapotokea mafuriko wakati Bwawa la Nyerere lipo ujue kuna uzembe umefanyika.

Kumbuka, masika Tanzania ni kama miezi minne, na kiangazi ni kama miezi nane. Kwa nini uwe na mafuriko ukiwa na bwawa size ya Bwawa la Nyerere? Tumia akili.

Ngoja nikupe hesabu rahisi; ni mfano tu sio namba halisi

Ikiwa kuingia maji bila mafuriko ni 10 cubic meters/hr
Kujaa maximum = 6000 cubic meters
Kutoka maji bila mafuriko ni 10 cubic meters/hr
Kutoka maji yakaleta mafuriko ni 15 cubic meters/hr
Unachofanya ni kwamba unatoa maji kwa 13 cubic meters/hr wakati bwawa limefika say 3000 cubic meters capacity

Sasa kwa kuwa maji hayaendi kwa batches ni continuous flow, yaani hizo cubic meters zinakuwa katika flow rates, computer program itakuwa based na principle ya hesabu ya integration na optimization, yaani katika theory ya dy/dx, ambayo imejengwa nchini ya premise ya flow in rate-retention-flow out rate. Nikienda zaidi ya hapa nitakuchanganya. Sasa unafikiri hawa watu wa CCM, mawaziri sijui, wanaelewa hili? Wao wanatoa amri tu, jaza Bwawa, Samia anatakiwa azindue mradi tuwaambie CCM imemaliza tatizo la umeme nchini!

In fact, katika kusema mafuriko yalitokea pia 1974 wanazidi kujionyesha walivyo mbumbumbu, kwa sababu unapotengeneza water level management system ya dam, unaangalia data za miaka hata 60 nyuma ili kuwa na scenario kwamba Rufiji inaweza kuwa na maximum flow rate ya kiasi gani, na bado ile maximum flow rate unaipiga factor inaitwa safety factor katika engineering. Yaani kama maximum flow rate ni ya mwaka 1974 na lilkuwa 15 cubic meters/hr, basi wewe unaikuza kwa 15% kama factor of safety. Na pia unatumia climate change prediction model kuangalia huko mbele hata miaka 100 ijayo, what could be the maximum Rufiji flow rate, given your historical data za flow rate katika misimu ya mvua nyingi. In fact, kujua Rufiji ilipata mafuriko 1974 na kadhalika ilipaswa iwe sababu kwa nini mafuriko hayakupaswa kutokea baada ya kujengwa Bwawa la Nyerere. Hakuna injinia mjinga kiasi cha kusema mafuriko yalishawahi kutokea huko nyumba ndio maana na sasa yametokea, wakati tumejenga Bwawa la Nyerere.

Sasa usiniambie tumejenga Bwawa la Nyerere kwa ushauri wa waganga wa kienyeji wa kutabiri mvua.

Hawa watu walisubiri bwawa limefika 5800 cubic meters ndio wakashituka, jamani eeh, maji yanajaa kupita kiasi. Ikabidi, ili kuokoa Bwawa wafungulie maji kwa zaidi ya 15 cubic meters/hr, kiwango ambacho ni juu ya flow rate ya mafuriko. Na walijua kabisa wanafungulia maji juu ya kiwango cha mafuriko kwa sababu wasipofanya hivyo Bwawa litazidiwa. Halafu wakasema nyie wananchi ndio mmesababisha.

Sasa go east or west, mafuriko ya Rufiji tukiwa na Bwawa la Nyerere ni uzembe na ujinga wa viongozi wa siasa. Na TANESCO hawawezi kukwepa lawama.
 
Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na Waandishi wa Habari kuhusu Hali ya Mafuriko Nchini, Hatua Zilizochukuliwa, pamoja na Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere.
 

Attachments

  • IMG-20240414-WA0009.jpg
    IMG-20240414-WA0009.jpg
    669.5 KB · Views: 1
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Mobhare Matinyi amefanya Mkutano na Waandishi wa Habari, kuhusu hali ya mvua na Maafa ya Mafuriko nchini, Aprili 14, 2024. Dar es Salaam.
IMG-20240414-WA0039.jpg
 
Back
Top Bottom