Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 31, 2007.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 31, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,206
  Trophy Points: 280
  Leo kwa mara nyingine mbio za mwenge zimeanza tena Tanzania, na safari hii mwenge umewashwa huko Dole Zanzibar kuendeleza ile adhma ya taifa letu changa kuwa "sisi tumekwisha kuwasha mwenge na kuuweka Kilimanjaro". Mwenge huu ulipowashwa mara ya kwanza na kuwekwa kwenye kilele cha Kilimanjaro na Nyirenda, ulikuwa uwe ishara ya matumaini, upendo, na umoja wa Taifa letu.

  Matukio ya hivi karibuni hasa baada ya muasisi wa mwenge huo kufa, kuna kila dalili kuwa tunachokimbiza sasa hivi ni kivuli tu cha mwenge ule kwani miale ile ya mwanzo ya mwenge wetu wa uhuru imeanza kuzimika na inaonekana ikififia kila mwaka mpya ujapo. Mwenge huu sasa umekuwa ni alama ya watu wachache kujiangazia wao na familia zao huku sisi wengine tukiendelea kubakia gizani. Hakuna kitu kinachoonesha kufifia kwa mwenge huo kama suala la mikataba ya nishati, madini, ununuzi wa rada, ndege ya rais, n.k Zaidi ya yote kwa wanafunzi waliokwama Ukraine, mwenge huu kwao tayari umezimika ( a little strech there, but why not try..??)

  Je kuna matumaini ya kurejesha nuru yake tena? Je kuna haja ya kuuwasha tena ili uendelee "kuwamulika" wabadhirifu, wazembe maofisini, wala rushwa magendo n.k ? Au tuamue kuuzima tu, ili kila mtu ajiwashie mshumaa wake yeye mwenye na wale wenye uwezo wawashe vibatari, chemli, na taa za umeme! ?

  huu mwenge kweli tunasababu ya kuendelea kuukimbiza?
   
 2. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,751
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  naona sasa mzee unavuka mipaka kwa kuhusisha suala zima la ukraine na kila kitu. Najua hii inatuuma kwa kiasi gani, na sijakataa ulivyoeleza hapo juu, ila hilo suala la ukraine ndio limeleta utata ! Kama ukiapply hilo suala katika kila kitu kweli tutafika, tusije tukalipeleka hili suala hadi katika wimbo wa taifa, kusema walioutunga wamefariki basi pia tunaimba vivuli vya sauti zao !!

  otherwise, ni hoja nzuri !
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2007
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,474
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Mwkjj,
  Hope springs eternal. Mimi ni optimist and I believe in Tanzania. Tutafika. Kipindi cha mpito huwa kigumu. Kuna mawimbi makali na huko baharini mapirates kibao. Lakini jahazi letu, inshallah, siku moja litafika. I believe that. Hiyo mikataba ya madini ndiyo pirates ninaozungumzia, lakini nao kuna mwisho wao. Usikate tamaa, mchango wako ni muhimu na tutafika.
   
 4. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,751
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  dont get it twisted, hajakosea kutoa hoja ! nilikuwa nawakilisha !
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  May 31, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,206
  Trophy Points: 280
  kada... hakuna tatizo uzuri wa hoja ni nguvu yake.. na ile hoja ziwe na utamu lazima hoja mama iwe kali... jukumu lenu ni kukosoa hoja yangu, kuipinga kabisa au kuitetea... mimi nasema yote yanayoendelea nchini sasa hivi ni kwamba taifa limepoteza ule moto wake uliowaka zamani...!! hivyo si mikataba tu ila mambo mengine mengi.. ni kwamba tumepoteza ile tunu iliyotufanya tuone fahari kuwa sisi ni watanzania... sijasema imezimika kabisa.. ila kwa mwendo huu tutafika kweli?
   
 6. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,751
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mzee,
  hapo nimekupata ( tena wewe ni muwazi na huogopi kusema huogopi kukosolewa ) hapo napiga magoti chini, umenimaliza.
  Lakini haya mambo yalianza tokea zamani na hawa wanaoendeleza haya mambo tunaweza kusema wamerithi na kwa mwenendo huu sidhani kama tutafika. kilichobaki ni kumuomba mungu tunapumua !
  Big up mwanakijiji, nimekuamini. Endelea kujiamini na kukubali kukosolewa, hadi hapa siwezi kusema utafika mbali na kazi (fani)yako maana tayari ushafika mbali.
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 0
  Hivi Mzee MMJ,

  Originally, nia na madhumuni ya watu wazima kuacha kazi za muhimu kwa taifa na kuanza kukimbiza chuma chenye kuwaka moto nchi nzima, ilikuwa nini? Mpaka kusaidia wakimbizaji wa chuma hicho kuwa viongozi wa baadaye wa taifa ilikuwa nini?

  Nafikir tunahitaji ku-establish hilo kwanza kabla ya kuziongelea hoja zako!
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jun 1, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,206
  Trophy Points: 280
  Mzee Es, nitakujibu kwa kina baadaye kwani mimi ni mmoja wa watu walio"bahatika" kuwa wakimbiza "moto"...
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jun 1, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,206
  Trophy Points: 280
  Mzee Es, nilikuwa nimeanza kukujibu nikajikuta nimeandika kurasa tatu! so, I deceded to do a show.. so onesho la leo linauliza "Mwenge wa Uhuru-tunaukimbiza au tunaukimbia?" sikiliza kwa kubonyeza hapa chini.
   
 10. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2007
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Jamani mtanisamehe mimi navunjika mbavu......kwa kucheka.
   
 11. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,506
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  habari wana bodi,
  Kwa muda nimekuwa nje ya Jambo forum nikitafakari mwenendo wa JF,hatumkomi nyani giladi kabisa..kumekuwa na hoja dhaifu,najua kuna spinning ya Kina RA imeshaingia humu.ila kwa staili hii,Nyerere atabaki na wemnge tu..

  NIMEKUWA nikifiri kila kukicha ni namna gani watu, hasa Watanzania wanaweza kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Mungu amlaze mahali pema) kwa vitendo na kwa uwazi mkubwa.

  Wapo pia, hasa wanaojiita wasomi waodhani kumuenzi mzee yule ni kuandaa semina na makongamano kwa kutumia fedha za wafadhili na kuwaita watu wa kada kama ya kwao, kuzungumza mazuri ya Nyerere. Hili
  Ni vitendo pekee vya wahusika hao ndivyo tunaweza kuvithamini ikiwa wataona na kutambua kweli Watanzania wanateseka kwa umasikini uliokithiri na kutafuta mbinu za kuutatua. Au labda watu hao kusaidia kuikomboa jamii ya Watanzania kutoka katika umasikini mkubwa wanasubiri wakiwa marais wetu. Ajabu!
  Nina wasiwasi, ikiwa unafiki huu wa kumuenzi Baba wa Taifa utaendelea, baada ya miaka 15, hakuna hazina ya Nyerere itakayokuwa ikikumbukwa. Siyo Muungano, siyo uongozi bora, siyo uwajibikaji, siyo haki, siyo…..Azimio la Arusha limekwenda na hivyo vingine, iwapo atakosekana wa kuvisimamia na kuvipigania, navyo vitafuata.


  Kitakachobaki sana sana ni mwenge tu, kwa kuwa sijaona mtu mwenye akili timamu akiupinga kuwepo kwake hasa baada ya kuwa umechukua sura ya kitaifa zaidi na siyo itikadi za chama chochote.

  wameshindwa kukemea mabaya yanayotokea kila kukicha nchini na sasa yameanza kuota mizizi kama vile kuwepo kwa rushwa (SULA LA RDC NA PM??,).
  Mungu atupe uzima, tuone yajayo…labda tutakuwa na mchango wa kuyageuza
   
 12. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,506
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Julius Kambarage "Mwalimu" Nyerere was an outstanding leader, a brilliant philosopher and a people's hero - a champion for the entire African continent. He shall always be remembered as one of Africa's greatest and most respected sons and the father of the Tanzanian nation.

  Throughout his long life he enjoyed respect and popularity that extended far beyond the borders of Tanzania. His wise counsel was sought from around the globe, even after he resigned from the presidency in 1985.

  A legacy in his own lifetime, he served as a symbol of inspiration for all African nations in their liberation struggles to free themselves from the shackles of oppression and colonialism
   
 13. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkomboziufisadi, Heshima mbele.

  Mimi yangu machache tu:

  1. Kitu gani kimekufanya useme kuwa nyani hakomwi giladi humu JF? Umesahau hapa ni JF na "where we dare talk openly" ndio bango letu.

  2. Hizo hoja dhaifu hebu zibainishe walau kwa mifano ueleweke

  3. Yaani kweli kila kukicha unafikiria jinsi Watanzania watakavyomuenzi Mwalimu Nyerere(RIP)? Labda nikuulize kumuenzi mtu(Nyerere, in this case) maana yake ni nini haswa?

  4. Kuhusu Mwenge nao si ajabu ukawa historia. Hebu tuwe wakweli hapa, huu mwenge unawanufaisha vipi wananchi wa kawaida? Sana sana unatumika kudhoofisha mapambano dhidi ya ukimwi. Kama umeshawahi kukimbiza Mwenge au kuupokea na kukesha nao you'll know what I mean!
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  May 29, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,206
  Trophy Points: 280
  Leo mbio za mwenge zimeanza tena. Mwenge huu ulipowashwa kwa mara ya kwanza na kuwekwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro na Alex Nyirenda ulikuwa ni ishara, ulikuwa ni alama (a sign and a symbol) ya sisi kama Taifa na matamanio ya uhuru wetu. Ulipowashwa wakati ule tulitangaza kwa matumaini kuwa:

  [​IMG]

  Sisi tumekwisha kuwasha Mwenge
  Na kuuweka Juu ya Mlima Kilimanjaro
  umulike hata nje ya mipaka yetu,
  ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini,
  upendo mahali palipo na chuki na
  heshima palipojaa dharau!


  Ulikuwa pia ni alama ya uhuru wetu ambao ulikuwa unaangaza kwa mara ya kwanza. Mwenge huu ndugu zangu naamini miale yake imeacha kuchoma na mwanga wake kufifia. Katika giza la ubinafsi, na katika ukungu wa ufisadi nchi yetu kwa mara nyingine inahitaji kusimama na kumulika zaidi, na hasa kuanza kumilika ndani ya mioyo yetu wenyewe ili kuweza kuona mapungufu yetu sisi wenyewe katika ujenzi wa Taifa letu.

  Mwenge huu ambao umeanza kukimbizwa tena, uwashe ndani ya mioyo yetu moyo wa kizalendo na mawazo ya kimapinduzi na tusikubali yale matamanio ya kuwa na Taifa la kisasa, lenye haki na nafasi sawa kwa wote, na ambalo ni nyumba ya matumaini kwa wana na mabinti zake hayazimwi kwa hofu, na kamwe yasiache kufifia na kupoteza joto lake!

  Nikiwa mmoja wa watu waliobahatika kukimbiza mwenge huu mwa 1986 kule Tanga, najikuta kwa namna ya pekee navutwa na ule moyo wa mapenzi ya nchi yangu uliowashwa ndani yangu ile Mei Mosi iliyotangulia (ilifanyika Kitaifa Tanga 1985). Nafasi ya kwenda vijijini na mijini ilikuwa ni hamasa kubwa ya kulijua Taifa letu na kukutana na watu ambao ule mwenge ulikuwa ni nafasi ya pekee ya kukutana na kundi la vijana ambao wamejitoa kuhamasisha umma kuhusu maswali mbalimbali.

  Ndio maana hata leo hii binafsi naamini Mwenge huu ungefanywa kweli kuwa wa Kitaifa na si wa serikali. Baadhi ya viongozi ambao wangeupokea na kuwa wageni rasmi wangekuwa kuanzia viongozi wa serikali, vyama vya kisiasa, viongozi wa kidini, na watu wa kawaida kabisa. Wangebadilisha kabisa na kufanya experience ya mwenge kuwa ni ya watu wenyewe.

  Ni vizuri walipofanya uamuzi wa kuondoa CCM katika kukimbiza mwenge lakini bado mwenge unaonekana ni wa serikali na si wa Taifa. Mbio hizi zinapoanza itakuwa vizuri wakabadili mambo fulani hasa kwa kukaribisha watu wengine kushiriki ili mwenge huu uzidi kuwa alama ya muunganiko na umoja wetu kama Taifa na usije kugeuka utaratibu wa "kukimbizana na moto usiochoma".

  Hii ni mojawapo ya vitu ambavy are uniquely Tanzanian na nimojawapo ya tamaduni ambazo zinapaswa kuendelezwa na kuboreshwa ili mwenge huu ambao wanajeshi wetu wanauvaa kwenye ngao zao, ambao uko kwenye nembo za Taifa letu, na ukiwa katika alama kadha wa kadha za taasisi zetu uzidi kuwa kweli mwenge wa matumaini na unaoangaza katika mioyo ya Watanzania!

  Binafsi ningependa kutuma salamu za mwenge kwa watanzania wote popote pale walipo, kuwa moto wa mabadiliko ya kifikra na moto wa mapenzi ya nchi yetu uzidi kutuunguza na kutumilika kiasi kwamba kama tulikuwa gizani tuanze kuondoka wenyewe kabla hatujachomwa! Katika siku hii ya kwanza ya mbio za mwenge, Watanzania wote tusimame kama mtu mmoja na kuhakikisha kuwa Taifa letu letu halizimwi, na mwanga wa mawazo yetu haufunikwi tena! Tuzidi kuamka na kuangaza kama jua la alfajiri na kama mbalamwezi ingazayo usiku wa manane tuendelee kumilika hata kule kwenye giza bila ya sisi wenyewe kugeuka giza!!

  Mwengeee.. mwenge - mbio mbio
  Mwenge tunauikimbiza - mbio mbio
  Kuwachoma mafisadi - mbio mbio
  Mpaka waachie nchi - mbio mbio!!
  mwenge mwenge!! mbio mbio~
  mwenge tunaukimbiza - mbio mbio
  Uhuru wetu twalinda - mbio mbio!!!
  Hatuwazirii nchi - mbio mbio!!


  Habari zaidi na Picha tembelea KLH News where we bring the news.. first!
   
 15. Nikifufukammekwisha

  Nikifufukammekwisha JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji,

  Ningewaona watu wa CCM kuwa ni watu wa maana kama wangeahirisha kuuwasha mwenge mwaka huu mpaka hapo wangemalizana na ma-scandal yote yanayoumiza vichwa vya watu. Kuuwasha mwenge hakuna maana yoyote kwa sababu tumesha-prove kwamba other means za kuwamulika wahujumu uchumi ni more effective zaidi ya hili useless gimmick.

  Let's be realistic; Pesa ya kugharamia mafuta ya mwenge ingeweza kutumika kujaza mafuta ya magari ya hospitali ili kuwapeleka waja wazito hospitalini. This is a waste of resources. Wake up - CCM people!!!
   
 16. M

  Mama JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  sio mwaka huu tu, bali kusiwe na mbio za mwenge kabisaaa, mbio za mwenge ni katika matumizi makubwa yasiyo na maana kabisa, nini maana halisi ya kukimbiza mwenge baada 45 ya uhuru na hali duni ya maisha. Hivyo vijisenti ya kugharamia mbio za mwenge si zingetumika kujenga maabara na kuziequip fully katika mshule ya msingi na sekondari. Kukimbiza mwenge 1962 na sana sana 1963 kulimake sense, baada ya hapo ni ufujaji tu.
   
 17. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,096
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hivi huu mwenge hatuwezi kubadilisha structure yake na ukubwa wake? nnaliona ni la kizamani na naamini ni zito sana kiasi ambacho watoto na baadhi ya wehye afya dhaifu hawawezi kuubeba.


  maana mwenge wa olimpiki umebadilika sana na umekuwa mwepesi na ukimbizaji wake pia umekuwa mzuri jee hatuwezi kuiga tukabadilisha kama wa olimpiki?
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  May 29, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 11,572
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji,

  ..nadhani tujirudi na kuwa na mwenge unaomulika NDANI ya mipaka yetu.
   
 19. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kwa nini siufagilii mwenge.

  -Ni superstitious idea bordelining on bumper sticker propaganda.Nia yetu ya kuangaza ianzie moyoni na itawaka maradufu ya the figurative light of this torch.Sioni nia hii mioyoni mwa viongozi.

  - For a poor nation that should be as frugal and cost conscious as possible, that is a lot of fuel to burn and a lot of manhour to waste for a figurative idea that can be elucidated on the local scale through the available means of propaganda anyway.The Augustine symbolism is not worth the dear price if we are really mindful of our meagre resources, it may even send a message of bountiful jubilation in the midst of indigence.

  -The whole hullaballoo transmit a lot of communicable diseases, from the sexual to others.
   
 20. Nikifufukammekwisha

  Nikifufukammekwisha JF-Expert Member

  #20
  May 29, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pundit,

  Pound it. The harder the better!!!

  You are right; Hili likitu inapaswa liwe eiliminated. We cannot afford the cons coming with this propaganda. 20th century tulishaiacha zamani. Let's act like we are in the 21st century.
   
Loading...