Ushauri: Namna ya kupunguza gharama za Mbio za Mwenge

Mwanachama Sahihi

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
549
185
Sisi tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro. Umulike nje ya mipaka yetu. Ulete Matumaini pale ambapo hakuna Matumaini. Ulete Upendo mahali ambapo pana Chuki na ulete Heshima mahali ambapo pamejaa Dharau”.

Hili ndilo lilikuwa lengo mahususi la Mwenge wa Uhuru ambao ni ishara na alama maalumu ya Uhuru tulioupata mwaka 1961. Uhuru wetu ulilenga Matumaini, Upendo na Heshima kwa Tanganyika-Tanzania na Afrika kwa ujumla ili kuondokana na minyororo ya UKOLONI. Tulipouwasha Mwenge, tuliwasha moto kuwaunguza walioenda kinyume na hali hiyo.

Tanzania imepigana kwa hali zote na imekuwa kielelezo cha ukombozi kwa nchi nyingi hasa zilizoko kusini mwa Afrika. Hili jambo ni la kihistoria na halina ubishi. Juhudi za ukombozi ni endelevu na hazina ubishi.

Ndiyo maana kwa muda mrefu tumekuwa tukiadhimisha juhudi hizo kwa kuwasha Mwenge na kuukimbiza karibu nchi nzima. Ni lazima kuendelea kupambana kwa nguvu zetu zote ili kuhakikisha kwamba jamii yetu inaendelea kuishi kwa Upendo, Heshima na Matumaini ili kulinda dhana nzima ya UHURU wetu. Jambo hili si la kubeza ila ni la kuungwa mkono kwa hali na mali.

Katika awamu hii ya tano ya Uongozi wa Nchi yetu, tumeona jitihada ambazo hazitiliwi shaka za Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kwamba UHURU wetu unaakisiwa katika Upendo, Heshima na Matumaini kwa wananchi wake wote. Imekuwa hivyo na mpaka sasa juhudi zake zinaungwa mkono na wananchi wengi huku Jamii Forums ikiwa ni sehemu ya ukweli huo. Wito wangu ni kuwaomba watanzania wote tumuunge mkono Rais wetu na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU.

Changamoto kubwa imekuwa ni namna ya kueneza ujumbe wa Mwenge wa Uhuru kila mwaka na hasa gharama za kuukimbiza Mwenge wenyewe katika nchi nzima. Mijadala na minong’ono mbalimbali imesikika kwa nyakati tofauti ili kupunguza gharama na kuna wakati baadhi ya wachangiaji wameenda mbali na kusema mbio hizo zifutwe na Mwenge uwekwe kwenye makumbusho ya Taifa. Dhana na mitazamo hiyo napingana nayo kwa kuwa bado naamini katika misingi ya uwepo wa Uhuru wenyewe licha ya ukweli kwamba zama za sasa hazifanani na enzi za Mwalimu.

Tufanyeje? Hapa ndipo ulipo ushauri wangu kwa Mheshimiwa Rais. Ikimpendeza naomba achukue ushauri huu na aweza kuuboresha kulingana na atakavyoona unafaa. Huu ni mchango wangu kama mtanzania huru, sipendi kuendelea kulalamika tu, nachukizwa na wanaolaumu. Ni wakati wa kujiuliza tumechangia nini kuyapatia ufumbuzi matatizo ya Nchi yetu ili kutoka hapa tulipo. Huu ni wakati wa HAPA KAZI TU.

MAPENDEKEZO
Mwenge wa Uhuru utengenezewe nakala (ndogo ndogo) kulingana na idadi ya Mikoa ya Nchi yetu. Siku ya uzinduzi wa mbio za Mwenge kitaifa kila mwaka, utawashwa Mwenge (Mkuu) na wakuu wa Mikoa watapita mbele ya mgeni rasmi kukabidhiwa nakala hizo na kila nakala itawashwa siku hiyo hiyo. Maana nyepesi ni kwamba hili tukio litawahitaji wakuu wa mikoa kuhudhuria wote kwa siku moja ya uzinduzi wa sherehe hizo.

Mfano kwa mwaka huu Mheshimiwa Mama Samia angewakabidhi nakala wakuu wote wa mikoa sambamba na ujumbe wa mbio za Mwenge kitaifa pale Morogoro. Hapohapo hiyo ndiyo ingekuwa siku ya maadhimisho ya Mwenge wa Uhuru kimkoa katika mkoa wa Morogoro na napendekeza itengwe siku moja maalum-preferably weekend days na “vyombo vyetu vya habari” viwe live the whole day. Full Stop.

Hatua ya pili ni kwa wakuu wa mikoa kupangiwa ratiba. Kila Mkoa utapewa siku moja tu-preferably weekend days na “vyombo vyetu vya habari view live the whole day” siku ya kilele kimkoa. Hata hivyo katika mkoa husika wao watakuwa na shamrashamra za namna ya kuadhimisha sherehe hizo. Mfano kwa hapa Songea inaweza kuchaguliwa wilaya ya Songea na sherehe zikafanyika uwanja wa majimaji.

Wiki nzima ya kilele cha maadhimisho pale uwanja wa majimaji kutakuwa na maonesho katika mabanda mbalimbali ya watu au taasisisi. Nashauri ielekezwe zaidi kwa sekta binafsi ili serikali ya mkoa iratibu tu maadhimisho hayo. Uhuru huu ni wa wananchi wenyewe. Wapelekeeni sare pale na ruhusuni watu watengeneze na kuuza sare hizo. Gharama nilizozipunguza hapa unaweza kuziona hivi:-

Baada ya kutoka Morogoro kwa mfano, Mkuu wa mkoa angeenda na nakala yake Songea tena bila Pressure. Nasema bila pressure kwa sababu kama Morogoro umeadhimishwa Jumamosi hii basi Songea tutaiona nakala yake Jumamosi ijayo. Logistics za wakimbiza mwenge kufika Ruvuma hilo ni jukumu la kamati za ulinzi na Usalama kitaifa/kimkoa na izingatie kuondoa msululu wa magari.

Utaratibu utakuwa hivyo kwa mikoa yote, ni jukumu la mkoa na ingependeza kuwepo na rotation kiwilaya kwa kila mwaka kuandaa eneo la maadhimisho hayo. Dhana hii inalenga kuwashirikisha wananchi zaidi, kuweka ushindani wa wilaya na wilaya (maandalizi kwa mwaka kimkoa) lakini ushindani zaidi kati ya mkoa na mkoa katika kutekeleza dhana nzima ya Mwenge.

Kilele cha mbio za Mwenge kitaifa. Kama ilivyokuwa wakati wa kuwasha Mwenge, wakuu wa mikoa watarejesha nakala zao kwa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa siku hiyo kabla ya kiongozi huyo kuukabidhi Mwenge (Mkuu) kwa Mheshimiwa Rais. Hapa napo ningeshauri kilele cha mbio hizi kitaifa ibaki kuwa tarehe 14 ya Oktoba na zifanyike Butiama kila mwaka. Sehemu ya uzinduzi wa mbio hizi uendelee ku rotate kama ilivyo sasa.

Niache eneo la maswali na kwa kuwa wazo hili nimekuwa nalo muda mrefu nitakuwepo hapa kutetea bandiko langu. Nimeshiriki mbio hizi za mwenge tangu nikiwa chipukizi wa chama mid 1970, ninachokiona sasa ni namna ya kukabiliana na gharama za kukimbiza mwenge huo kitaifa. Nimeamua kushauri namna ya kuzipunguza. It can be done play your part.

Sisi tumekwisha kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro. Unamulike nje ya mipaka yetu. Unalete Matumaini pale ambapo hakuna Matumaini. Unalete Upendo mahali ambapo pana Chuki na unalete Heshima mahali ambapo pamejaa Dharau”.

Nawasilisha.
 
kwanini tunahangaika hivyo...Kwani huo mwenge ni mungu...or what is the miracles inside that mwenge...Tuachane na siasa...zama za mwenge zmepitwa na wakati
 
kwanini tunahangaika hivyo...Kwani huo mwenge ni mungu...or what is the miracles inside that mwenge...Tuachane na siasa...zama za mwenge zmepitwa na wakati
Umesoma vizuri nilichotanguliza mkuu? Tatizo lako ni nini. Hii sio miracle hata kidogo
 
Sijwahi kuona mtu akijaribu kutibu minyoo iliyoko tumboni kwa kunywa sumu.

Kama umetambua issue ni gharama za kuukimbiza huo mwenge kwanini basi uendele kung'ang'ania kuukimbiza in the first place!?
 
Sijwahi kuona mtu akijaribu kutibu minyoo iliyoko tumboni kwa kunywa sumu.

Kama umetambua issue ni gharama za kuukimbiza huo mwenge kwanini basi uendele kung'ang'ania kuukimbiza in the first place!?
Nimesema Mwenge hauepukiki kwa sasa tuulete katika nyakati hizi. Kunywa sumu sio attempt ya matibabu bali ni kukata tamaa. Hatuuachi Mwenge na tuuboreshe. Karibu sana
 
Good idea, naona mwenge huu ungewashwa kwa kuadhimisha Wiki ya Mwenge ambapo kuna siku ya kuwasha mwenge nchi nzima kwa kila mkoa kuwasha na wakuu wa mikoa, na kutembea kila Wilaya ndani ya siku 7 tu na biashara inakwisha
 
Good idea, naona mwenge huu ungewashwa kwa kuadhimisha Wiki ya Mwenge ambapo kuna siku ya kuwasha mwenge nchi nzima kwa kila mkoa kuwasha na wakuu wa mikoa, na kutembea kila Wilaya ndani ya siku 7 tu na biashara inakwisha
Umekuja vizuri sana. Kudos mkuu. Ngoja tuanzie hapa tuone tutafikaje huko.
 
Swali gharama ya maambukizi ya ukimwi inapunguzwa vipi? Je kuna ukweli wowote kuwa viongozi wa mbio za mwenge wanapukutika kwa vifo? Nini sababu?

Na washawasha!
 
Nasikia wanasemaga mwenge usipokimbizwa nchi nzima chama fulani hakitashinda uchaguzi, ni kweli?
 
Hata majirani zetu wanatushangaa! nchi inayohangaika kutumia raslimali zake kuzunguka nchi nzima na mwenge wakati asilimia zaidi ya 50 ya wananchi wake hawana umeme wala maji salama! Eti mwenge unatuletea umoja wa kitaifa, ni lini nchi yetu haikuwa au ilipungukiwa umoja wa kitaifa?
 
Back
Top Bottom