Busara iliyotumika kuzuia sherehe za pamoja za uhuru, itumike pia kusitisha mbio za mwenge wa uhuru Kila mwaka

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, sherehe nyingi za kitaifa za nchi hii, zilianza kusherehekewa kwa mtindo wa kubana matumizi katika awamu ya Tano ya utawala wa nchi yetu.

Ni muda Sasa sherehe hizi zinasherehekewa kwa namna nyingine na siyo tulivyokuwa tumezoea, Gwaride la kitaifa na mambo mengi kedekede ikiwemo mialiko ya wakuu wa nchi nyingine, ukiachia mbali gharama kubwa za uandaaji wa hizo sherehe.

Mantiki ya kubadilisha namna tulivyokuwa tunafanya ilikuwa kulinda upotevu wa fedha nyingi zilizokuwa zinaenda kwenye shughuli ya siku Moja, badala yake walitaka kuwekeza pesa hizo katika mambo ya msingi zaidi yanayodumu.

Binafsi napendezwa kabisa na mfumo wa Sasa wa sherehe hizi. Umeokoa pesa nyingi na unatufanya kama wananchi kuwa wepesi.

Kinachonishangaza Sasa, ambacho nadhani nakosa majibu, kwa nini mbio za mwenge wa uhuru zimeachwa kuendelea?

Kwanza, kubadilisha namna ya kusherekea uhuru wenyewe na kuacha by product yake kuendelea kuadhimishwa, ni kutotenda haki kwa huo uhuru wenyewe.

Unamwadhimisha mtoto, kwa gharama ya kumdharau mama aliyemzaa. Hii haikai sawa.

Lakini kama mantiki ni gharama, kwa Nini tunaharibu pesa ambayo ingeingizwa kwenye mambo muhimu, kukimbia na mwenge ambao mama yake, hatumwadhimishi tena inavyofaa?

Mwenge unatumia gharama na pesa nyingi sana kukimbizwa nchi hii, achilia gharama nyingine za uharibifu wa kimaadili na kijamii, zinazosababishwa na mbio hizi.

Wakati tunatunza uchumi na kuelekeza pesa katika mambo muhimu kwa kuepuka sherehe kubwa za uhuru, mwenge uharibu uchumi wa watu na hasa wafanyakazi wa serikali, kada ya wafanyabiashara, na hata wanafunzi mwenge huu unapokimbizwa.

Wafanyabiashara huombwa michango ya mwenge kwa nguvu, wafanyakazi hukatwa pesa mapema kutoka kwenye mapato ya. na mishahara yao, na wanafunzi huacha masomo Ili kujipanga kuhusherekea huo mwenge.

Maombi yangu, busara iliyotumika kutafuta namna ya kuokoa pesa kwa kuacha kufanya sherehe rasmi za uhuru, itumike pia kuacha kukimbiza mwenge Tena Kila mwaka, ambayo kimsingi hutumia mapesa mengi achilia mbali maana hasa kwa Nini unakimbizwa.

Kama ni lazima sana mwenge huu kukimbizwa, basi serikali ingeona utaratibu mwingine usiogharimu nchi kiasi hiki.

Vinginevyo, kama serikali namna ya kuacha ukimbizaji wa mwenge kwa mtindo huu wa Kila mwaka, basi walau wakimbize huu mwenge mara Moja Kila baada ya miaka mitano.

Utakuwa umeokoa mafedha ya kutosha kwa miaka minne, na maadili na shughuli nyingine za kijamii zitasitawi walau hiyo miaka minne ya ukimya wa kutokuwa na mbio hizo!

Kuna watu wanashauri, mwenge uwe unawashwa na kupelekwa mlima Kilimanjaro Moja kwa Moja, kama slogan yake ilivyo, " sisi tunauwasha mwenge na kuweka juu ya mlima Ili uwaangazie nchi".

Nashauri busara iliyotumika kubadilisha namna ya kuadhimishwa kwa siku ya uhuru na sherehe nyinginezo za kitaifa, itumike Tena kuacha hizi mbio za mwenge ambazo ukweli ni costly, kiuchumi, kijamii na hasa kimaadili.

Tukishindwa Hilo, tusilalamike watu wakituita wachawi tunaokimbiza moto Ili kutambika nchi kwa Miungu tusiowajua.
 
Ukitaka kugombana na watu wa ccm, wewe washauri tu kusitisha hizo mbio za mwenge!! Aisee watakukatalia katu katu.

Maana utasababisha waikose ile mikesha yao ya kula na kunywa, na pia kufanya kila aina ya uchafu uliokatazwa na Mwenyezi Mungu.
 
Mwenge ndiyo ndumba kuu ya The green mamba,hilo kufuta sahau!
 
Huo mwenge uko kiushirikina zaidi. Na ccm ni chama Cha matambiko, hakuna namna wanaweza kuachana na mwenge.
 
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, sherehe nyingi za kitaifa za nchi hii, zilianza kusherehekewa kwa mtindo wa kubana matumizi katika awamu ya Tano ya utawala wa nchi yetu.

Ni muda Sasa sherehe hizi zinasherehekewa kwa namna nyingine na siyo tulivyokuwa tumezoea, Gwaride la kitaifa na mambo mengi kedekede ikiwemo mialiko ya wakuu wa nchi nyingine, ukiachia mbali gharama kubwa za uandaaji wa hizo sherehe.

Mantiki ya kubadilisha namna tulivyokuwa tunafanya ilikuwa kulinda upotevu wa fedha nyingi zilizokuwa zinaenda kwenye shughuli ya siku Moja, badala yake walitaka kuwekeza pesa hizo katika mambo ya msingi zaidi yanayodumu.

Binafsi napendezwa kabisa na mfumo wa Sasa wa sherehe hizi. Umeokoa pesa nyingi na unatufanya kama wananchi kuwa wepesi.

Kinachonishangaza Sasa, ambacho nadhani nakosa majibu, kwa nini mbio za mwenge wa uhuru zimeachwa kuendelea?

Kwanza, kubadilisha namna ya kusherekea uhuru wenyewe na kuacha by product yake kuendelea kuadhimishwa, ni kutotenda haki kwa huo uhuru wenyewe.

Unamwadhimisha mtoto, kwa gharama ya kumdharau mama aliyemzaa. Hii haikai sawa.

Lakini kama mantiki ni gharama, kwa Nini tunaharibu pesa ambayo ingeingizwa kwenye mambo muhimu, kukimbia na mwenge ambao mama yake, hatumwadhimishi tena inavyofaa?

Mwenge unatumia gharama na pesa nyingi sana kukimbizwa nchi hii, achilia gharama nyingine za uharibifu wa kimaadili na kijamii, zinazosababishwa na mbio hizi.

Wakati tunatunza uchumi na kuelekeza pesa katika mambo muhimu kwa kuepuka sherehe kubwa za uhuru, mwenge uharibu uchumi wa watu na hasa wafanyakazi wa serikali, kada ya wafanyabiashara, na hata wanafunzi mwenge huu unapokimbizwa.

Wafanyabiashara huombwa michango ya mwenge kwa nguvu, wafanyakazi hukatwa pesa mapema kutoka kwenye mapato ya. na mishahara yao, na wanafunzi huacha masomo Ili kujipanga kuhusherekea huo mwenge.

Maombi yangu, busara iliyotumika kutafuta namna ya kuokoa pesa kwa kuacha kufanya sherehe rasmi za uhuru, itumike pia kuacha kukimbiza mwenge Tena Kila mwaka, ambayo kimsingi hutumia mapesa mengi achilia mbali maana hasa kwa Nini unakimbizwa.

Kama ni lazima sana mwenge huu kukimbizwa, basi serikali ingeona utaratibu mwingine usiogharimu nchi kiasi hiki.

Vinginevyo, kama serikali namna ya kuacha ukimbizaji wa mwenge kwa mtindo huu wa Kila mwaka, basi walau wakimbize huu mwenge mara Moja Kila baada ya miaka mitano.

Utakuwa umeokoa mafedha ya kutosha kwa miaka minne, na maadili na shughuli nyingine za kijamii zitasitawi walau hiyo miaka minne ya ukimya wa kutokuwa na mbio hizo!

Kuna watu wanashauri, mwenge uwe unawashwa na kupelekwa mlima Kilimanjaro Moja kwa Moja, kama slogan yake ilivyo, " sisi tunauwasha mwenge na kuweka juu ya mlima Ili uwaangazie nchi".

Nashauri busara iliyotumika kubadilisha namna ya kuadhimishwa kwa siku ya uhuru na sherehe nyinginezo za kitaifa, itumike Tena kuacha hizi mbio za mwenge ambazo ukweli ni costly, kiuchumi, kijamii na hasa kimaadili.

Tukishindwa Hilo, tusilalamike watu wakituita wachawi tunaokimbiza moto Ili kutambika nchi kwa Miungu tusiowajua.
Hakuna cha busara wala
 
Hakuna cha busara wala nini maana kusitisha sherehe za Uhuru ni mipango ya kukusanya hela za kuiba chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.
 
Wakuu ni vema ifike mahali Mwenge upumzishwe. Bafala yake kama ni miradi, Mawazori, Makatibu Wakuu wawe wanakagua miradi kama kawaida yao. Mwenge maandaliz yake hadi kupita huwa unaimaliza kabisa Halmashauri. Yaani matumizi ya posho na mafuta na wizi kwa chaka hilo hilo. Ukijazia na mkesha, loh, ukipita council huachwa zipo hoiiiii!
 
Zinaachwaje hoi wakati watumishi na wafanyabiashara huwa wanachangishwa michango Kwa nguvu?
 
Mwenge ni maagano umasikini ni kafara uliobeba laana ya umasikini maagizo ya mapangoni Kila mwaka ni lazima uwamulike watu ili kuwapumbaza.
Kinyume chake hakulaliki hakukaliki,yatawakuta kuRIP
 
Lengo la mwenge ni kishirikina zaidi hili la kufungua miradi ni geresha tu.
Lengo kuu ni ushirikina
 
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, sherehe nyingi za kitaifa za nchi hii, zilianza kusherehekewa kwa mtindo wa kubana matumizi katika awamu ya Tano ya utawala wa nchi yetu.

Ni muda Sasa sherehe hizi zinasherehekewa kwa namna nyingine na siyo tulivyokuwa tumezoea, Gwaride la kitaifa na mambo mengi kedekede ikiwemo mialiko ya wakuu wa nchi nyingine, ukiachia mbali gharama kubwa za uandaaji wa hizo sherehe.

Mantiki ya kubadilisha namna tulivyokuwa tunafanya ilikuwa kulinda upotevu wa fedha nyingi zilizokuwa zinaenda kwenye shughuli ya siku Moja, badala yake walitaka kuwekeza pesa hizo katika mambo ya msingi zaidi yanayodumu.

Binafsi napendezwa kabisa na mfumo wa Sasa wa sherehe hizi. Umeokoa pesa nyingi na unatufanya kama wananchi kuwa wepesi.

Kinachonishangaza Sasa, ambacho nadhani nakosa majibu, kwa nini mbio za mwenge wa uhuru zimeachwa kuendelea?

Kwanza, kubadilisha namna ya kusherekea uhuru wenyewe na kuacha by product yake kuendelea kuadhimishwa, ni kutotenda haki kwa huo uhuru wenyewe.

Unamwadhimisha mtoto, kwa gharama ya kumdharau mama aliyemzaa. Hii haikai sawa.

Lakini kama mantiki ni gharama, kwa Nini tunaharibu pesa ambayo ingeingizwa kwenye mambo muhimu, kukimbia na mwenge ambao mama yake, hatumwadhimishi tena inavyofaa?

Mwenge unatumia gharama na pesa nyingi sana kukimbizwa nchi hii, achilia gharama nyingine za uharibifu wa kimaadili na kijamii, zinazosababishwa na mbio hizi.

Wakati tunatunza uchumi na kuelekeza pesa katika mambo muhimu kwa kuepuka sherehe kubwa za uhuru, mwenge uharibu uchumi wa watu na hasa wafanyakazi wa serikali, kada ya wafanyabiashara, na hata wanafunzi mwenge huu unapokimbizwa.

Wafanyabiashara huombwa michango ya mwenge kwa nguvu, wafanyakazi hukatwa pesa mapema kutoka kwenye mapato ya. na mishahara yao, na wanafunzi huacha masomo Ili kujipanga kuhusherekea huo mwenge.

Maombi yangu, busara iliyotumika kutafuta namna ya kuokoa pesa kwa kuacha kufanya sherehe rasmi za uhuru, itumike pia kuacha kukimbiza mwenge Tena Kila mwaka, ambayo kimsingi hutumia mapesa mengi achilia mbali maana hasa kwa Nini unakimbizwa.

Kama ni lazima sana mwenge huu kukimbizwa, basi serikali ingeona utaratibu mwingine usiogharimu nchi kiasi hiki.

Vinginevyo, kama serikali namna ya kuacha ukimbizaji wa mwenge kwa mtindo huu wa Kila mwaka, basi walau wakimbize huu mwenge mara Moja Kila baada ya miaka mitano.

Utakuwa umeokoa mafedha ya kutosha kwa miaka minne, na maadili na shughuli nyingine za kijamii zitasitawi walau hiyo miaka minne ya ukimya wa kutokuwa na mbio hizo!

Kuna watu wanashauri, mwenge uwe unawashwa na kupelekwa mlima Kilimanjaro Moja kwa Moja, kama slogan yake ilivyo, " sisi tunauwasha mwenge na kuweka juu ya mlima Ili uwaangazie nchi".

Nashauri busara iliyotumika kubadilisha namna ya kuadhimishwa kwa siku ya uhuru na sherehe nyinginezo za kitaifa, itumike Tena kuacha hizi mbio za mwenge ambazo ukweli ni costly, kiuchumi, kijamii na hasa kimaadili.

Tukishindwa Hilo, tusilalamike watu wakituita wachawi tunaokimbiza moto Ili kutambika nchi kwa Miungu tusiowajua.
Hizo mara kibao zimeahirishwa mwenge haiwezi tokea!
 
Kinachonishangaza Sasa, ambacho nadhani nakosa majibu, kwa nini mbio za mwenge wa uhuru zimeachwa kuendelea?

Nashauri busara iliyotumika kubadilisha namna ya kuadhimishwa kwa siku ya uhuru na sherehe nyinginezo za kitaifa, itumike Tena kuacha hizi mbio za mwenge ambazo ukweli ni costly, kiuchumi, kijamii na hasa kimaadili.

Tukishindwa Hilo, tusilalamike watu wakituita wachawi tunaokimbiza moto Ili kutambika nchi kwa Miungu tusiowajua.
Naunga mkono hoja, enzi za Mwamba niliuliza Mwenge: Ni Mwanga Tu Au Kuna Uvumba Fulani Unafukizwa Ili Kupumbaza Watanzania? Is it Justified?. kisha nikabaini Ingekuwa ni Amri Yake, Magufuli Angefutilia Mbali Mbio za Mwenge!, Jee Ni Amri ya Nani?!.
P
 
Back
Top Bottom