Kuuliza si ujinga na aulizaye ataka kujua. Mantiki ya kuwa na mwenge unaozungushwa mikoa na wilaya zote Tanzania kwa mazingira ya sasa ni nini? bajeti yake ni kiasi gani na nani anayegharimia? Kiongozi wake huchaguliwa na nani na vigezo vya kumchagua kiongozi huyu wa Mwenge ni vipi? Kuna siku nilimwona kwenye luninga akifanya ukaguzi wa madarasa ya shule moja mkoani akilalamika kwamba fedha hazikutumika ipasavyo. Kwani yeye anahusikaje na matumizi ya fedha za halmashauri? Tafadhali mwenye uelewa atujuze.
 
Back
Top Bottom