mwenge wa uhuru

Mwenge wa Uhuru
Mwenge wa Uhuru una muundo wa tochi ya mafuta ya taa ambayo inaashiria uhuru na mwanga. Mwenge wa uhuru ulinyanyuliwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro mnamo Desemba 9, 1961 na shujaa Brigedia Alexander Nyirenda ikiashiria kuangaza nchi na kuvuka mipaka kuleta matumaini palipo kukata tamaa, upendo palipo uadui na heshima palipo chuki.

Sababu ya huyu brigedia kunyanyua mwenge huu ni kuonesha fahari ya nchi na pia kuleta matumaini kwa Watanzania wote kwa kutokata tamaa, kupendana, kuheshimiana na kutogombana ikimaanisha kuwa na ushirikiano.

Mbio za Mwenge wa Uhuru hufanyika kila mwaka kuanzia maeneo mbalimbali nchini.
  1. H

    JamiiForums Tanzania Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru azindua huduma za afya zahanati ya kijiji Ndulungu

    KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU AZINDUA HUDUMA ZA AFYA ZAHANATI YA KIJIJI NDULUNGU Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Ndg. Wazo Michael Mwang'onda, tarehe 24 Julai, 2026, amekagua na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ndulungu...
  2. H

    JamiiForums Tanzania MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA IRAMBA TAYARI KUMULIKA MIRADI YA MAENDELEO

    MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA IRAMBA TAYARI KUMULIKA MIRADI YA MAENDELEO Mwenge wa Uhuru umewasili katika Wilaya ya Iramba ukitokea Halmashauri ya Manspaa ya Singida na kupokelewa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe. Suleiman Mwenda kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Godwin Gondwe...
  3. H

    JamiiForums Tanzania Ratiba ya Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wilaya ya Iramba - Julai 24, 2026

    Ratiba ya Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wilaya ya Iramba - Julai 24, 2026 Kaulimbiu: Tanzania ni yetu sote, Tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo.
  4. DodomaTZ

    JamiiForums Tanzania Prof. Shemdoe amshukuru Rais Samia kwa kuwapatia gari la wagonjwa Lushoto, Mwenge wa Uhuru wakalikabidhi

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia wananchi wa Wilaya ya Lushoto Gari la kuhudumia wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya hiyo, ambalo limekabidhiwa kwa...
  5. SamuraiJack

    JamiiForums Tanzania HOJA Mwenge wa Uhuru: Fahari ya Taifa au Gharama kwa Taifa?

    Mwenge wa Uhuru uliwekwa juu ya Mlima Kilimanjaro tarehe 9 Desemba 1961, siku ya uhuru wa Tanganyika, ukiashiria uhuru, utaifa, amani na matumaini ya taifa jipya. Tangu hapo, mwenge huo umekuwa ukizunguka nchi nzima kila mwaka kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo, kuimarisha umoja wa kitaifa...
  6. Echolima1

    JamiiForums Tanzania Zoezi la kuwasha Mwenge wa Uhuru huko Israel limefana

    Wakati wa mazoezi ya sherehe ya kuwasha mwenge wa Siku ya Uhuru, Rais wa Argentina akiimba kwenye onyesho la zoezi hilo. Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuwashwa na Rais huyo wa Argentina siku ya jumanne usiku
  7. D

    JamiiForums Tanzania Mwenge wa uhuru wapongeza DAWASA uboreshaji huduma za maji Kigamboni

    Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, ndugu Michael Mwang'onda, ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa utekelezaji mzuri wa mradi wa usambazaji maji katika Wilaya ya Kigamboni ulionufaisha Wakazi takribani 25,000 katika kata nne za Kibada...
  8. M

    JamiiForums Tanzania Mwenge wa Uhuru wawaunganisha watoto watatu wa mama (CCM na ACT & CHAUMMA) Kibondo

    Kumekuwa na mjadala kuhusu uhusiano unaodhaniwa kati ya ACT-Wazalendo na Chama Cha Mapinduzi (CCM), jambo linalozua maswali kuhusu msimamo thabiti wa ACT kama chama cha upinzani. Wengine wanaona ukaribu huu unaweza kufanya chama hicho ionekane kama kisicho na msimamo thabiti dhidi ya chama...
  9. Think2

    JamiiForums Tanzania Leo Agosti 26 ni siku ya kuupokea mwenge wa uhuru jijini Mwanza katika viwanja vya Nyamhongoolo

    Sisi kama serikali na sisi kama wadau wa maendeleo tunawakaribisheni katika hafla ya kuupokea Mwenge wa uhuru hapa jijini Mwanza utakaopokelewa na kulala hapa viwanja vya Nyamhongolo . Kila kitu kitakuepo kama ●Pombe ●Nyama choma ●Wazee wa pisi hapa ndo kwenyewe ila tumia mpira ●Na burudani za...
  10. agudev

    JamiiForums Tanzania Mwenge wa Uhuru unahifadhiwa wapi baada ya kutembezwa?

    Habari za muda huu wanajamvi, Naomba msaada kwa anayejua wapi mwenge wa uhuru unapohifadhiwa baada ya mbio za mwenge. Mwanangu wa shule ya msingi alinipiga hili swali jana nikawa napepesa macho tu, shuleni kwao wapo katika topic inayohusiana na mambo ya uhuru wa Tanzania pamoja na mwenge wa...
  11. Mpepetaji

    JamiiForums Tanzania GE2025 Mwenge wa uhuru kutembelea miradi yenye thamani ya zaidi bilioni 6.4 manispaa ya Kahama 2025

    Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, inatarajiwa kuupokea Mwenge wa Uhuru kimkoa Agosti 3, 2025 ukitokea mkoani Tabora, na kuanza kukimbizwa siku hiyo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama. Mwenge wa Uhuru 2025 utapokelewa katika viwanja vya kituo cha mabasi Kagongwa ukitokea...
  12. Mpepetaji

    JamiiForums Tanzania GE2025 Kaliua: Mwenge wa Uhuru wazindua, na kuweka mawe ya msingi miradi tisa ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 2

    Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dk. Garald Mongela, amewaongoza maelfu ya wananchi wa wilaya hiyo kushiriki uzinduzi wa miradi ya kimkakati iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru. Katika mwaka huu Mwenge wa Uhuru umezindua, umeweka mawe ya msingina umetembelea miradi tisa ya maendeleo yenye thamani ya...
  13. Stephano Mgendanyi

    JamiiForums Tanzania Iramba: Mwenge wa uhuru wazindua miradi ya tsh. Bilioni 7.8

    IRAMBA: MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA TSH. BILIONI 7.8 Mwenge wa Uhuru 2025 Umeendelea na Mbio zake Wilayani Iramba Mkoani Singida ambapo Miradi Saba yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 7.8 imekaguliwa, Kuwekwa Mawe ya Msingi na Kuzinduliwa Waziri wa Fedha ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la...
  14. Mpepetaji

    JamiiForums Tanzania GE2025 Mwenge wa uhuru Singida kupitia miradi ya bilioni 62.6

    Miradi yenye thamani ya zaidi ya Sh.Bilioni 62.6 iliyojengwa katika halmashauri saba za zilizopo katika Mkoa wa Singida inatarajia kuzinduliwa na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru 2025 ambao utakimbizwa kwa siku saba mkoani hapa. Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Halima Dendego, akitoa taarifa leo kwa...
  15. E

    JamiiForums Tanzania Mwenge wa Uhuru watajwa kuwa sababu kusitishwa operesheni C4C CHAUMMA

    Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimesema ratiba ya Mwenge wa Uhuru mkoani Tanga ndio ilikuwa sababu ya kuzitisha ziara yao ya Operesheni C4C iliyopangwa kufanyika katika mikoa yote nchini kwa siku 16. Itakumbukwa Mei 21, katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa...
  16. R

    JamiiForums Tanzania Mwenge wa uhuru kuzindua Miradi 52 ya Billioni 84 Kilimanjaro

    Jumla ya miradi 52 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 84 inatarajiwa kukaguliwa, kuzinduliwa au kuwekewa mawe ya msingi wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika katika halmashauri saba za mkoa wa Kilimanjaro kuanzia Juni 28, 2025 Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa...
  17. M

    JamiiForums Tanzania Naomba nielimishwe juu ya umuhimu na faida za mwenge wa uhuru unaokimbizwa kila mwaka nchi nzima

    Habari ya muda huu ndugu zangu. Nimekaa nimetafakari nikashindwa kupata majibu juu ya huu mwenge wa uhuru unaokimbizwa nchi nzima kila mwaka. Mbio za mwenge za kila mwaka zinabajeti kubwa sana na zinagharimu pesa nyingi mno ambazo zingeweza kutumika katika matumizi mengine ingeleta tija sana...
  18. Think2

    JamiiForums Tanzania Uchangishaji wa fedha kwaajili ya mwenge jijini Mwanza kata ya kishiri

    Nawasalimu kwa jina la Gwajimanizer, hili la uchangishaji wa fedha kwa wanachi wa kata ya kishili jijini Mwanza ili kuwezeaha kuleta mwenge wa uhuru, ivi serikali sI huwainatenga kiasi kwaajili ya Mwenge wa uhuru inakuaje wananchi tuchangie fedha za mwenge?? Inahitajika 2M kuleta mwenge aisee
  19. Mkoba wa Mama

    JamiiForums Tanzania Miradi hiyo hiyo inakaguliwa na mwenge wa uhuru, hiyo hiyo kamati za Bunge, hiyo hiyo CCM, hiyo hiyo inakaguliwa na viongozi wa serikali

    Naomba kuuliza, mbona wakaguzi wa miradi ni wengi sana na bado miradi mingi ufanisi wake ni wa hovyo. Hizo pesa zinazotumika kwa ajili ya ziara za kukagua miradi si bora zikafanya kazi nyingine tu na miradi ikawa inakaguliwa na taasisi moja maalumu baada ya hapo inapeleka ripoti kwa wengine.
  20. M

    JamiiForums Tanzania Kukimbiza mwenge wa uhuru kitaifa

    Nimewahi kuona matangazo ya nafasi za wakimbiza mwende wa uhuru kwenye halmashauri na mikoa, lakini sijawahi kuona wakitangaza nafasi hizo kitaifa. Hawa watu huwa wanapatikanaje?
Back
Top Bottom