Utawasikia nataka mwanaume anitunze, anipende anipe pesa...yeye mwenyewe ameshindwa kujitunza mpaka kuoipoteza ile kitu kwa wahuni, kama unataka matunzo baki kwa wazazj wako wawe wanakupa pocket money
Kuna wanaume wanatetea humu, Hatukatai wao kuangalia na kuchagua wenye nazo Ila twende mbele turudi nyuma, Je, wenye nazo na wasionazo wapi no wengi? Je, bila hela wanamaanisha Mapenzi hakuna?
 
Hivi kutimiza jukumu lako la kumhudumia mke wako nako ndiyo kupenda hela? Basi tuvunje huu mgawanyo wa majukumu ili iwe rasmi sasa wote mwanaume na mwanamke waingie mzigoni kutafuta pesa wasaidiane kulipa bills halafu na kazi za nyumbani pia liwe ni jukumu la wote unaonaje hapo?
 
Kwanza ashukuriwe bwana Mungu wetu kwa kutupa kibali Cha kuiona Leo hii tena.
Kwa harakaharaka tena bila kupepesa macho nitaushika usukani wa uzi huu nikiwapeleka moja kwa moja katika mada hii ya ufumbuzi au hoja juu ya maisha yetu ya mahusiano baina yetu Sisi wanaume na wenzetu wanawake.

Mimi ukiniuliza Mapenzi ni nini kwa kifupi nitajibu mapenzi ni upendo, Na ukiniuliza upendo ni nini nitakuambia ni hisia njema au matendo mema tuyafanyayo kwetu sisi na mazingira yaliyotuzunguka, Upendo wa kweli unaanzia kwenye hisia ndipo kwenda katika akili inayotuongoza kuufanya Upendo.

Ukiniuliza kuoa/kuolewa ni nini nitakujibu ni maridhiano baina ya watu wawili me na ke kuamua kuishi pamoja Kama mume na mke, Na pia ukiniuliza ndoa ni nini nitakujibu ni kiapo baina ya watu hao wawili walioamua kuishi pamoja Kama mume na mke, Kiapo hicho hufanyika kwa taratibu maalumu na kuhusisha mashahidi.

Sasa leo nataka kuwachambua Hawa wanawake wa kisasa ambao wamegeuza Mapenzi/Kuolewa/Ndoa Kama chanzo cha kujiingizia kipato au kufanya maisha yao yaende, Ni hivi kwa Sasa kusema ukweli kasi ya watu kuoana imepungua kwa kasi sana. Nasema hayo kwa utafiti wa harakaharaka nilioufanya kwa mfano: Kundi kubwa linalohudhuria kwenye maombi kwa yule Mchungaji wa Kawe, Asilimia kubwa ya wanawake wanaokwenda pale wanachokwenda kukifuata ni Muujiza wapate Kuolewa, Sasa mimi nilifikiri maybe wanataka kuolewa kwa lengo la Upendo na Kuijaza dunia pekee kumbe wanataka kuolewa kwa kuwa maisha ni Magumu.... (So sad kwa kweli)

Yaani ndio maana unakuta mwanamke anafanyiwa ukatili kwenye ndoa na mumewe, Anapigwa anacheatiwa lakini anavumilia kwa kuwa mwanaume ana hela, Mwanamke anaona bora avumilie mateso ila asiachwe na mtu mwenye hela, Ukifuatilia background ya mwanamke alishakutanaga na mwanaume mwenye Upendo wa kweli kwake Ila akamdump kwa kuwa mwanaume hakuwa na hela

Ubaya ni kuwa wanaume wameshagundua hilo that's why wanaume wa sasa washaona kuwa wanawake wote wapo kimaslahi tu, Ni ngumu kumkuta mwanaume anaefahamu tabia za wanawake wa kisasa akioa, Ukiona mwanaume anaoa ujue kakubali kujishusha, karogwa au umri umekwenda, Ila kwa dalili zinapoelekea naona ukosefu wa ndoa kabisa, Na haya yote yanasababishwa na wanawake wenyewe imagine wao ndo wapo wengi kuliko wanaume alafu badala akipata kampenzi kake atulie na akubaliane na hali ya maisha ya mpenzi wake yeye atataka kwenda na ukisasa ambao utamshinda mpenzi wake kumhudumia hali itakayomfanya mwanamke aamue kwenda kutafuta mwenye kuweza kumtimizia mahitaji yake, Yaani kiufupi wanawake wa sasa hawataki mwanaume mwenye Upendo bila pesa, Wao wapo radhi apate hata wa kumlala tu na kumpa pesa akakidhi mahitaji yake Mahitaji yao Sasa Kusuka, Kuosha kucha,Nguo nzuri, Vyakula vya Take Away Kfc, Outing Vacation yaani wadada wa sasa hivi nisikufiche unavyomuona Gigy Money,WemaSepetu na Uwoya na wengine wengi wasanii ndivyo wadada Hawa wanataka kuishi Kama wale kitu ambacho Ukifuatilia hao watu wanaishije utagudua kuwa Kweli Decor Bysco anasema ukweli, Technology imekuja kuua Upendo wa kweli kwa Sasa Upendo wa kweli ni kwenye vitu tu, Uliobaki wote ni fake... Tuanaamini upendo Kupitia Machapisho, likes na comments Ila in reality all are fakes.

Ewe kijana unaetaka kuoa kwa muda huu jiandae kisaikolojia Mimi kijana mwenzenu naongea Kupitia experience maana nimeshuhudia wanandoa wengi wanaume wakituchekea uwongo tulio single, Utamsikia " Ndoa tamu kijana jitahidi uoe" Ukimcheki ndevu zake kazisusa nywele zipo rafu kiufupi kajisahau mzee wa watu, Anajiproud mbele yenu Ila ukimchungulia kwa dirishani akiwa amekaa barazani kwake muda mwingi kashika tama alaf kaduwaa Ila mwanamke kanawiri kazi kubadili vijora na kuudhuria shughuli za mitaani, Ile mistari ya kibibilia iliyosema "Ishini nao kwa akili" hao walikuwa wanawake wa zamani, Wanawake wa zamani ilikuwa ukitumia tu akili unamuwin Ila wa sasa Cha kwanza unatakiwa Uwe na hela, Cha pili zisiishe, Cha tatu ndo utumie Akili Cha nne ujitahidi sana kumuomba Mungu wako akuepushe na roho za mauti.

Majuzi ni kama niliona chapisho wale watu wa haki za wanawake wakidai ipitishwe sheria ya wanaume kuwalipa wanawake zao mshahara nikacheka sana maana waliotoa Hilo wazo ni wanawake hawahawa, Nilicheka kwa kuwa niliona kuwa sasa wamechoka kujificha kuonesha kuwa Malengo ya wao kukubaligi kuolewa ni kujiingizia kipato Sasa wanakuja kidada wa kazi Au nisemeje wanajamvi? Sasa mtu ukimlipa Hadi mshahara hivi huyo atakuwa hata na mamlaka ya kukuuliza Jana ulilala wapi, Yaani unaanzaje kuniuliza Mimi boss wako nililala wapi?

Anyway sijakatisha mtu tamaa Ila nimeona tusimalize huu mwaka bila kuwakumbusha tu kuwa Kuoa na Kuolewa kumedondosha wanaume wengi chini, Sisi tuliobaki embu tujitunze na tuanze kuringa maana Hawa viumbe wapo wengi sana kwa sasa, We na kiherehere chako unajifanya unaoa are you sure umeridhika na huyo? Are sure Ni akili zako na hujarogwa? Are you sure hatutokupoteza? Hawa tunatakiwa tuwasuse Hadi wajifunze ili anapopata mume wamuheshimu, Maana wao wanahisi kwa kuwa kila anapopita anapigiwa mluzi ndo anapendwa kumbe wengine wapitaji tu.

Utamsikia "Oooh unasema hivyo kisa huna hela" narudi palepale wewe Kenge unamaanisha kabla ya hela hakukuwa na Mapenzi? Au kisa wewe nimekugusa niliposema hujui kutofautisha Upendo wa mtu na vitu? Hapa nimezungumzia ule Upendo wa kweli ndo maana mnapoapa Kiapo Cha ndoa wanasema "Shida na Raha" na sio "Umasikini na Utajiri".

Decor Bysco
Uchambuzi murua kabisa na wenye mashiko
 
Kuna wanaume wanatetea humu, Hatukatai wao kuangalia na kuchagua wenye nazo Ila twende mbele turudi nyuma, Je, wenye nazo na wasionazo wapi no wengi? Je, bila hela wanamaanisha Mapenzi hakuna?
Hivi kwanini mnalazimisha wanawake tu ndiyo wawe na mapenzi ya kweli wakati dunia ya sasa wanaume ndiyo wanaongoza kukosa mapenzi ya kweli? Siku hizi usaliti umeshamiri na wanaume mnajisifia kabisa kuwa ni nature hamtosheki na mwanamke mmoja sasa kama wewe kujicommit umeshindwa kwanini utake mwanamke ajicommit?
 
Kwa ufupi anasema kwanza tumpende mtu jinsi alivyo na utu wake na si vitu vyake. Vitu au mali ni ziada na mara nyingi mtafaidi vitu vizuri ikiwa upendo ulitamalaki bila hivyo vitu.

Watu ambao wanapenda vitu mara nyingi huvurugana bila vitu na wakiwa navyo napo huvurugana! Tanguliza upendo vitu vifuate, hata visipokuwepo amani itakuwepo.
 
Hivi kutimiza jukumu lako la kumhudumia mke wako nako ndiyo kupenda hela? Basi tuvunje huu mgawanyo wa majukumu ili iwe rasmi sasa wote mwanaume na mwanamke waingie mzigoni kutafuta pesa wasaidiane kulipa bills halafu na kazi za nyumbani pia liwe ni jukumu la wote unaonaje hapo?
Kwani huo mgawanyo upo?
 
Hivi kwanini mnalazimisha wanawake tu ndiyo wawe na mapenzi ya kweli wakati dunia ya sasa wanaume ndiyo wanaongoza kukosa mapenzi ya kweli? Siku hizi usaliti umeshamiri na wanaume mnajisifia kabisa kuwa ni nature hamtosheki na mwanamke mmoja sasa kama wewe kujicommit umeshindwa kwanini utake mwanamke ajicommit?
Mapenzi ya kweli tuwape wenye Mapenzi ya uongo sio?
 
Kwa ufupi anasema kwanza tumpende mtu jinsi alivyo na utu wake na si vitu vyake. Vitu au mali ni ziada na mara nyingi mtafaidi vitu vizuri ikiwa upendo ulitamalaki bila hivyo vitu.

Watu ambao wanapenda vitu mara nyingi huvurugana bila vitu na wakiwa navyo napo huvurugana! Tanguliza upendo vitu vifuate, hata visipokuwepo amani itakuwepo.
Umeeleweka mkuu
 
Babu yangu alioa wanawake Saba,na kila mmoja akazaa nae watoto kumi na mbili,na kila mmoja alijengewa nyumba na kupewa shsmba la ekari mbili.
Mengi uliyoyataja ni mahitaji ya kawaida ya mwanamke.
Je Kuna wanawake wabaya,gold diggers,yees wapo wengi!!!je Kuna ndoa zinazoumiza wanaume,zipo kibao,
Je Kuna ndoa na wanawake wazuri,?wapo weeengi tu.
Lakini Cha msingi tangu Dunia iumbwe,hakuna ndoa isiyo na matatizo!!!
Kuna ubaya gani binti,kutaka kuolewa na mtu mwenye uwezo au na mwelekeo wa kipato!?sasa unataka aolewe na kapuku,harafu uzao wake nao uishi kwa shida!umetoka familia maskini,umesoma kwa shida,uolewe Tena na kapuku harafu wanao Tena waishi maisha magumu!!!
Kijana Bado hujakomaaa,kama unatsfuta mwanamke wa kukupenda kwa mspenzi ya muvi za kifilipino na kihindi,usioe kabisa.
Ndoa ni maisha halisi sio maagizo,unaishi na binadamu sio maraika.
Husifanishe enzi za babu zako na sasa ktk ulimwengu huu wa kwenda na wakati na mitandao ya kijamii ,Smart phones na TV ni vitu viwili tofauti.Kaa chini jiulize kwa nini viongozi wengi siku hizi wa kiroho (masheikh, mapadri na wachungaji nk),wanatumia mda mwingi kusuluhisha matatizo ya ndoa kuliko kutoa huduma nyingine za kiroho.

Babu yako aliweza kuwacontrol hao wanawake wote sababu walikuwa watii na wasikivu, sasa hivi ukioa wanawake wawili, tuu unakuwa umejitengenezea moto wako wa Jehanum humu humu duniani.Kweli zipo ndoa zenye furaha chache sana, kila siku nikienda kanisani mapadri wanakazia sana maswala ya ndoa,manake wameshaona sababu wao kila siku wana deal na maswala ya ndoa.
 
Husifanishe enzi za babu zako na sasa ktk ulimwengu huu wa kwenda na wakati na mitandao ya kijamii ,Smart phones na TV ni vitu viwili tofauti.Kaa chini jiulize kwa nini viongozi wengi siku hizi wa kiroho (masheikh, mapadri na wachungaji nk),wanatumia mda mwingi kusuluhisha matatizo ya ndoa kuliko kutoa huduma nyingine za kiroho.

Babu yako aliweza kuwacontrol hao wanawake wote sababu walikuwa watii na wasikivu, sasa hivi ukioa wanawake wawili, tuu unakuwa umejitengenezea moto wako wa Jehanum humu humu duniani.Kweli zipo ndoa zenye furaha chache sana, siku kila nikienda kanisani mapadri wanakazia sana maswala ya ndoa,manake wameshaona sababu wao kila siku wana deal na maswala ya ndoa.
 
Back
Top Bottom