thatHUMBLEguy
JF-Expert Member
- Nov 25, 2023
- 223
- 522
Inatambulika dunia kote, toka dunia hii imeanza—haijalishi kwa dhana ya Uumbaji wa Mungu au Evolution ya kisayansi— Baba, Mama na Watoto (Familia), ndio imekua jumuiko la kwanza, kuu na la msingi la wanadamu.
Siku hizi kumeshamiri wimbi [si geni kihistoria] la kupinga Uwepo wa Familia ya Baba, Mama na Watoto—KATAA NDOA.
Wafuasi wa dhana hii, naombeni mnipe mtazamo wenu juu ya masuala haya;
1. Juu ya Malezi na miongozo ya pamoja. Ni kwenye familia ndipo mtoto anafunzwa stadi za Maisha—kupika, kufua, kuosha watoto, kubeba mtoto, miongozo ya elimu ya awali, nidhamu, utiifu mfano namna ya kusalimu watu, kuheshimu watu wote, utunzaji wa mali zake na za familia, upendo, huruma—yote haya yanachangiwa na baba na mama. Nje ya familia haya mtoto atayapata vipi kwa ufanisi?
2. Juu ya Upatikanaji wa uhakika wa mahitaji ya kimwili.. Ngono ndio hisia na msukumo mkubwa wa Mwanadamu yeyote. Mtu Mzima anahitaji walau kufanya ngono mara tatu kwa wiki, Mke na Mume ndiyo wanatimiziana hayo na kupeana utulivu na hivyo kuweza kutimiza majukumu yao mengine. Bila kuoa, maana yake utakuwa na wanawake tofauti tofauti na kujiweka kwenye risk ya Maradhi, Ushirikina na kuzaa hovyo, mtapanyo holela wa kipato. Kataa ndoa, mna njia ipi mbadala yenye usalama nje ya ndoa?
3. Juu ya mahusiano ya kijamii. Familia ndio networking platform ya kwanza ya mwanadamu. Ndugu wa mke na Mume kwa ujumla wao ndio huwa chimbuko la kupeana fursa mfano Ajira au tender za kibiashara, kusaidiana katika matatizo mf Afrika hatutumii mifumo rasmi ya Bima mf Mazishi au Maradhi, sababu tunamifumo ya kusaidiana wenyewe toka ngazi ya familia. Pia kupitia familia ndipo mwanao anaweza kwenda kufanya kazi sehemu na kufikia kwa ndugu wa Mkeo au mumeo n.k n.k. Hili nyie mnalitazama vipi?
4. Juu ya kuwapa misingi ya Uwajibikaji watoto. Familia inapolea watoto kuwa watiifu na kufuata miiko mbalimbali inawafanya watoto wawe na sense ya uwajibikaji zaidi na hivyo kuwa na jamii bora zaidi, mfano unapolea mtoto usiku ni muda wa kuwa nyumbani, au anayekatazwa udokozi, anayetimiziwa mahitaji yake nafasi ya kuwa na jamii tulivu ni kubwa. Bila familia, nyie mnaona jamii itakuwa na sura gani?
5. Juu ya kujijenga kiuchumi. Mke na Mume hupeana mipango ya maendeleo. Mke humtia moyo mmewe kupambana, mke hupambana kutafutia familia kipato pia, hivyo husaidizana inapotokea kukwama, pia mahitaji ya watoto huwasukuma wazazi kutafuta zaidi. Kubwa zaidi, ukiwa na familia, huwezi zaa hovyo, hivyo hukupa utulivu wa kiuchumi. Je, Nyie hili mnalitazama vipi?
6. Juu ya mafunzo ya kimaadili— Kidini/Kimungu/Kiutu. Mwanadamu yeyote anahitaji dira ya kumuongoza kimaadili—mema na mabaya— maishani (moral compass) ambapo sehemu ya kwanza ni unaipata kwenye familia. Familia ya kiislam, itamlea mtoto kwenye maadili ya kislam na kumpa miongozo ya mema na mabaya, hali kadhalika kwa familia ya kikiristo, au hata ya kipagan ni lazima inayo moral compass yao. Nyie kataa ndoa, mnadhani watoto wanaipata vipi miongozo hiyo ya kimaadili?
Karibuni.