Kataa ndoa. Leo wamepata point 3 ugenini, ilikuwa hivi...

Teslarati

JF-Expert Member
Nov 21, 2019
1,728
6,792
Uanaume ni mateso, yaani mababu zetu ndo walifurahia uanaume ila siku hizi ni mateso mara mia.

Nina jamaa yangu aliyumba kdg kiuchumi baada ya kuachishwa kazi miaka minne imepita, jamaa alikuwa ana hela kinoma, mke aliomuoa kwa ndoa ya mapepe mengi akamwomba amfungulie biashara huku yeye anatafuta kazi. Jamaa akauza nyumba moja akampa huyo mwanamke mtaji, mwanamke akaanza kwenda china kununua mizigo na kuuza hapa DSM na mikoani.

Biashara baada ya kuiva, mwanamke akaanza kutembea na vijana wake wa kazini hapo. Jamaa alipojua mwanamke akawa mkali, biashara kila kitu kimeandikwa kwa mwanamke. Mwanamke mwishowe akaondoka jumla nyumbani akaenda kupanga kivyake bila kuachana rasmi. Huko inasemekana akawa anakaa kinyumba na dogo mmoja wa kazini kwake. Kizuri hawakua na mtoto bado.

Biashara ikafeli, inasemekana alidhurumiwa na huyo dogo alokua naye, mwanamke akaanza kutanga tanga tu.

Jamaa si kajitafuta kajipata leo hii anapokea barua eti mke kamfungulia kesi kwamba waliachana ila jamaa hakumpa talaka na gawio lake la mali uthibitisho wa ndoa anao sababu walifunga ndoa ya kanisani.

Msioe msioe msioe. Kwani nini kigumu kukaa na mwanamke ndani bila kumuoa? Kama utalazimika kuoa mpe mwanamke prenup asije kugusa mali zako.
 
Nina mwanamke mwaka wa saba huu nakaa nae na sijamuoa, kila mtu anaenijua physically anajua ni mke wangu. Kuna kipindi alileta kelele lkn akaja kugundua mimi ni mafia, ametulia anakula ugali na samaki.
Ila hata kama hakuna makaratasi ila hiyo wanaita Ndoa maana wanaoweza kuthibitisha ni majirani kisheria.

Binafsi Sina Mpango wa kufunga kinachoitwa Ndoa hapa Duniani na Niko kwenye mahusiano ya hivyo miaka 10 Sasa na Huwa nasema ukikna hapakufai na umepata anaekufaa amsha beba unachotaka but Mali kubwa kubwa Zina majina mengine ila zinafahamika.
 
Matatizo mnajitakia wenyewe. Unatumia fedha kumshawishi mwanamke akupende ili umuoe! Hii inaonyesha kabisa jamaa yako alitumia ''misuli'' ya fedha ili kumvuta huyo demu.

Na mara nyingi unakuta ni hawa ''wenzangu'' na mimi wenye elimu ndogo na pengine washamba na ulimbukeni hapo hapo, wanapofanya biashara na kupata fedha za ghafla wanakimbilia kuoa wanawake ''wavaa vimini'' ili nao waonekane ni wajanja.
 
Ila hata kama hakuna makaratasi ila hiyo wanaita Ndoa maana wanaoweza kuthibitisha ni majirani kisheria.

Binafsi Sina Mpango wa kufunga kinachoitwa Ndoa hapa Duniani na Niko kwenye mahusiano ya hivyo miaka 10 Sasa na Huwa nasema ukikna hapakufai na umepata anaekufaa amsha beba unachotaka but Mali kubwa kubwa Zina majina mengine ila zinafahamika.
Niliposema mm ni mafia nadhan hukunielewa.

Hio sheria huwa ina loophole mahala, najua ninachokisema. Lakini akishakua na copy ya cheti cha ndoa ndipo huchomoki
 
Matatizo mnajitakia wenyewe. Unatumia fedha kumshawishi mwanamke akupende ili umuoe! Hii inaonyesha kabisa jamaa yako alitumia ''misuli'' ya fedha ili kumvuta huyo demu. Na mara nyingi unakuta ni hawa ''wenzangu'' na mimi wenye elimu ndogo na pengine washamba na ulimbukeni hapo hapo, wanapofanya biashara na kupata fedha za ghafla wanakimbilia kuoa wanawake ''wavaa vimini'' ili nao waonekane ni wajanja.
Kuna ukweli fln, ndo maana nasema msioe
 
Ndoa nia yake ni kumkandamiza mwanaume....
Mambo mengine yanahitaji kufanyiwa ''update'' kila baada ya muda ili kuenda na wakati, sheria za ndoa ni mojawapo.

Imefika muda, sheria za ndoa za Tanzania zifanyiwe maboresho haraka sana, ili kuwe na uwezekano wa kufunga ndoa zenye makubaliano maalum kulingana na wanandoa wanavyokubaliana.

Kwa mfano wanaweza kukubaliana kuwa wakiwa kwenye ndoa kila mtu atachuma na atamiliki mali zake na ikitokea kuna kutengana, kila mmoja anaondoka na ''mbao zake''.
 
Back
Top Bottom