Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,034
- 6,907
Watu wa ajabu sana Hawa aisee.Ila ujue nini nilichojifunza Ili uitwe mtu bora Serikalini wewe fanya ubabe wote,kuwa jizi na upuuzi mwingine ila kikubwa jaza pesa kwenye viroba uwe unawahonga watu wa Takukuru,watu wa usalama,na wakubwa wengine kama RC,Katibu Mkuu na Waziri.DED njombe alikuwa bora kabisa...wakurugenz mbalimbali walikuwa wanakuja kujifunza kwake
Ukifanya hayo utadumu Serikalini hadi mwenyewe utakapoamua kuacha.Nawafahamu wakuu fulani in personal ni majizi na mafisadi yanalalamikiwa kila siku na wengine waliwahi kusimamishwa Kazi ila wakarudishwa,licha ya kashfa hizo zote wapo wanadunda na wanajidai hakuna wa kuwafanya chochote,Siri yao ni kufanya hayo nimeeleza hapo juu.
Ila ukijifanya wewe ni mzalendo uko na wananchi na unapenda haki na ustawi wao utakwenda na maji kwa fitina kama zote,watetezi wako watakuwa ni wananchi au watu wa chini kama madiwani ambao hakuna anaewasikiliza.
Nimekasirika Sana kuwatoa DED wa Njombe, Tunduma nk na kupachika watu waolakini kikubwa kuwaacha Ma DED wenye kashfa kama wa Sumbawanga Manispaa anaeshutumiwa kwa wizi na kushindwa kukamilisha mradi wa stand Kuu ambayo hadi sasa inatumika ila haina maji wala vyoo.