Uteuzi na Uhamisho: Rais Samia amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
11 March 2024
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu usiku huu:

1710196544965.png
Picha maktaba: ndugu Anamringi Macha

TEUZI NA UHAMISHO :
  • Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara, ndugu Anamringi Macha ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga
  • Christina Mndeme kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano (Mazingira) kabla ya hapo alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:

i. Amemteua Bw. Anamringi Macha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Kabla ya uteuzi Bw. Macha alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

ii. Amemteua Bi. Christina Mndeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Kabla ya uteuzi, Bi. Mndeme alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

iii. Amemteua Bw. Japahari Kubecha Mghamba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mghamba alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Busega.

iv. Amemteua Bw. Mussa Kilakala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kilakala alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaliua.

V. Amemteua Bw. Robert Masunya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Kabla ya uteuzi huu Bw. Masunya alikuwa Afisa Mwandamizi katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Waanawake na Makundi Maalum.

vi. Amemteua Bi. Mwashabani Mrope kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.

vii. Amemteua Bw. Jacob Simon Nkwera kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Nkwera alikuwa Afisa Mwandamizi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

viii. Amemteua Bw. Sangai Mambai kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Busega.

ix. Amemteua Bw. Raymond Mweli kuwa Katibu tawala wa Wilaya ya Kaliua.

X. Amemhamisha Bw. Frederick Damas Dagamiko kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga.

xi. Amemhamisha Bw. Bashir Muhoja kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

xii. Amemhamisha Bw. Tito Philemon Mganwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

Uapisho wa Wakuu wa Mikoa na Naibu Katibu Mkuu utafanyika tarehe 13 Machi, 2024 saa 04.00 asubuhi, Ikulu Dar es Salaam.

Screenshot_20240312-020226_1.jpg
Screenshot_20240312-020230_1.jpg
 
Kipi bora uwe mkali kuwasimamia ili kuwe na consistent ya utendaji huko walipo, na mtu akiboronga anakaa chonjo.

Au uamishe amishe kila siku watu na kukosekana consistency, siku troubleshooter anaenda huko mkurugenzi sijui mkuu wa wilaya anamwambia yeye mgeni hayajui hayo matatizo vizuri.

Serikali inatakiwa kuwa consistent kwenye civil services, matatizo ya babati, hayawezi fanana na Geita, Ifakara, Nachingwea, wala Kigamboni.

Kila sehemu ina unique core challenges zake, kuondoa wahusika na kupeleka wapya kila mara na iwapo kila mtu ana different approach ya kutatua tatizo hilo hilo ndio msingi wa kukuta kero ya eneo moja inadumu kwa miaka 10 hakuna consistency kwenye kulitatua.

Shida ya africa sio wazungu, ni sisi wenyewe.
 
Mkubwa hapangwi
 
HApo ndo keshawakaripia ujue
 
Umeongea jambo la maana sana.
Tuna safari ndefu hapo kwa hizi teua teua
 
Mkubwa hapangwi
Swala sio kupangiwa, swala ni results/performance orientation. Hakuna mtu anaeweza kwenda eneo moja na kujua changamoto zote, issue sio files anazokuta tu; bali kuna swala la ku-interact na hao wenyeji, kujifunza jinsi ya ku-communicate nao na mambo mengine ambayo kuyaelewa yanataka first hand experience ili kuja na mbinu sahihi za kutatua hizo changamoto.

Hakuna civil services duniani inayobadilishwa badilishwa ovyo kama ya Tanzania.

Msingi mzima wa local government na kupewa autonomy ni kwa sababu ya kutambua local challenges za maeneo ya nchi hazifanani, priority zinapishana na uongozi unatakiwa kuelewa hayo mambo. Sasa kama kila siku unabadili watu kutakuwa na consistency hapo.

Serikalini hakuna kubembelezana kuna targets na appraisal; mfanyakazi mzuri kutoka chini anaweza panda mpaka wizarani na mfanyakazi mmbovu anatimuliwa sio kuamishwa.
 
Back
Top Bottom