DED njombe alikuwa bora kabisa...wakurugenz mbalimbali walikuwa wanakuja kujifunza kwake
Watu wa ajabu sana Hawa aisee.Ila ujue nini nilichojifunza Ili uitwe mtu bora Serikalini wewe fanya ubabe wote,kuwa jizi na upuuzi mwingine ila kikubwa jaza pesa kwenye viroba uwe unawahonga watu wa Takukuru,watu wa usalama,na wakubwa wengine kama RC,Katibu Mkuu na Waziri.

Ukifanya hayo utadumu Serikalini hadi mwenyewe utakapoamua kuacha.Nawafahamu wakuu fulani in personal ni majizi na mafisadi yanalalamikiwa kila siku na wengine waliwahi kusimamishwa Kazi ila wakarudishwa,licha ya kashfa hizo zote wapo wanadunda na wanajidai hakuna wa kuwafanya chochote,Siri yao ni kufanya hayo nimeeleza hapo juu.

Ila ukijifanya wewe ni mzalendo uko na wananchi na unapenda haki na ustawi wao utakwenda na maji kwa fitina kama zote,watetezi wako watakuwa ni wananchi au watu wa chini kama madiwani ambao hakuna anaewasikiliza.

Nimekasirika Sana kuwatoa DED wa Njombe, Tunduma nk na kupachika watu waolakini kikubwa kuwaacha Ma DED wenye kashfa kama wa Sumbawanga Manispaa anaeshutumiwa kwa wizi na kushindwa kukamilisha mradi wa stand Kuu ambayo hadi sasa inatumika ila haina maji wala vyoo.
 
Wakuu Nawapa Taarifa Tu Kwamba, Kwa Mkoa Wa Pwani, Katika Wakurugenzi Wateule Ambao idadi Yao Ni 9, Miongoni Mwao 8 ni Waislamu na 1 Tu Ndio Mkiristo ambae Ni John Kayombo Lipesi ambae Ni DED Wa Rufiji. ... Kazi Iendelee
Kwanini wakristo mna chuki Sana na Waislamu!!????

Mbona katika hiyo idadi yote ya ma-DED, WAKRISTO ni wengi kuliko Waislamu lakini hawalalamiki?;

Ke,nge wewe
 
IMG_20210803_084957.jpg
 
Kitakachowaokoa Watanzania na CCM ya Kujuana, Sio Kupiga debe Kwanye Mitandao bali ni Kupambana (Struggle for New Constitutional) otherwise Porojo za Mitandao Mnaendelea Kuwawekea Mazingira Mazuri Kuendelea Kula KEKI ya Taifa na Familia zao kwa Niaba ya Wengi. Sasa Kama Uteuzi wa Watendaji Serikalini Unazingatia Uchama ndo Watanzania Mjue Tunaliwa na Tutaendelea Kuliwa otherwise Tujisalimia Kuwa Wanachama wa CCM. So KATIBA Mpya ndio Jibu la Masikini/Wasio na Mbereko. U-DED Ilibidi Watu wafanyishwe Interview ili kupata qualified individuals na sio Sifa ni Kuwaa Gwanda la Kijani.
 
CCM ina makada wengi....

Kila mtu na Wakati wake....

By the way katika hao wateuliwa mbona wako wasiokuwa watoto wa vigogo?!!!

Nao tumewahesabu ?!!!

Chama ni cha kila mmoja......

#SiempreCCM
 
Siasa ni sawa na biashara. Kama ambavyo wanafanyabiashara wa mlengo mmoja wanavyonapeana fursa na kuwafanyia figisu washindani wao, hata wanasiasa wa mlengo mmoja wanamegeana mapande ila wanawabania washindani wao. Kanuni ni hiyo hiyo, hata mgechagua chama cha Hashim Rungwe, naye angefanya hivyo hivyo.
 
Kifo rasmi cha CCM kilitokea wakati wa uchaguzi 2020. Waliweka wazi bila aibu mbinu zao safi na chafu za kubaki madarani.

Bila kufahamu ule uchaguzi ulifuatiliwa kwa karibu na jumuia za kimataifa. Leo hii wamemueezesha adui yao kuwamaliza kuanzia kwenye mizizi.
 
Thawabu yao iko Ahera. Ukisoma kitabu cha Shabani Roobert cha Kusadikika, ukakielewa, wala haitakupa shida. Kwenye sura za mwamzo mwanzo kuna sehemu anazungumzia baadhi thawabu ya wenye matendo mema watakapofika ahera.
 
Siasa ni sawa na biashara. Kama ambavyo wanafanyabiashara wa mlengo mmoja wanavyonapeana fursa na kuwafanyia figisu washindani wao, hata wanasiasa wa mlengo mmoja wanamegeana mapande ila wanawabania washindani wao. Kanuni ni hiyo hiyo, hata mgechagua chama cha Hashim Rungwe, naye angefanya hivyo hivyo.
Hivi huyo jamaa bado yupo? Na chama chake kinaitwaje vile?
 
kuna mida niliwazaga vijana wengi walosoma shahada ya sheria wana nafasi kubwa sana ya kupewa uongozi katika jamhuri ya Tanzani..

mekuwa nikifanya upembuzi naona ka pana ka ukweli
 


KATIBU MKUU UVCCM.

Ndugu.kenani kihongosi Amemshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaamini Vijana katika Nafasi mbalimbali za uongozi katika Taifa letu sanjari na hilo amewaasa vijana wote walioaminiwa kufanya kazi kwa weledi na uzalendo mkubwa ili kuleta tija katika Taifa letu.

Ndugu.KENANI KIHONGOSI
#Mtumishiwawote
#KaziIendelee
 
Swadakta......

Ninaunga mkono hoja....

Kongole kwa mh.Rais SSH kwa kuendelea kuwaamini vijana wenzetu ambao ni makini na wenye ari ya dhati ya kulipambania taifa letu kuntu.....

#KaziIendelee
#NchiKwanza
#SiempreSerikaliMbiliZaJMT
#SiempreSSH
 
Unaasa wenzako huku wewe ukiwa DC Arusha ulijichukulia sheria mkononi,tena huku ukitajwa na mashahidi kwa kesi ya Sabaya.
Huna sifa kuwaasa watendaji wapya
 


KATIBU MKUU UVCCM.

Ndugu.kenani kihongosi Amemshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaamini Vijana katika Nafasi mbalimbali za uongozi katika Taifa letu sanjari na hilo amewaasa vijana wote walioaminiwa kufanya kazi kwa weledi na uzalendo mkubwa ili kuleta tija katika Taifa letu.

Ndugu.KENANI KIHONGOSI
#Mtumishiwawote
#KaziIendelee
😍
 
Kwenye Kesi ya Sabaya mashaidi walioporwa pesa walisema walikuwa wanamuona Sabaya akikutana na Kihongosi baada ya kuchukua pesa zao
 
Back
Top Bottom