Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
1681460595205.png

Mke wa Ashraf Hakimi amempeleka mahakamani ili kupata talaka na alitaka Mahakama iwagawanyishe mali.

Baada ya Talaka kufanikiwa na kukubaliana kugawana mali, ikagundulika kuwa Ashraf Hakimi hakuwa na mali yoyote na hata akaunti zake benki hazikuwa na pesa yoyote.

Inaelezwa kuwa mahakama imebaini Ashraf Hakimi alishaweka mali zake zote kwa jina la mama yake muda mrefu uliopita.

==============

Aliyekuwa Mke wa Mchezaji wa Klabu ya PSG 🇨🇵, Achraf Hakimi 🇲🇦 aitwaye Hiba Abouk 🇪🇦 baada ya kuachana na Hakimi March 27,2023 alienda Mahakamani na kuwasilisha kesi ya kudai talaka huku akitaka agawiwe nusu ya mali ya Hakimi.

Baada ya Mahakama kufanya tathimini za mali za Achraf ilibaini kuwa aliyekuwa Mume wake hamiliki chochote kwani mali yake yote imesajiliwa kwa majina ya Mama yake

Hakimi anapokea Euro Milioni Moja (zaidi ya Shilingi Bilioni 2.56 kama Mshahara ndani ya PSG kila mwezi lakini 80% (zaidi ya Shilingi Bilioni 1.64) pesa hizo huwekwa kwenye akaunti ya mama yake Bi. Fatima.

"Hana mali, magari, nyumba, vito au hata nguo kwa jina lake.Wakati wowote na akitaka chochote huwa anaulizia kwa Mama yake ambaye huwa anamnunulia"

Mahakama ilitoa taarifa hiyo.

Inakadiriwa Kuwa Hakimi Achraf ana Utajiri wa Euro Milioni 17 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 45 ila Mali zote zinamilikiwa na Mama yake, Bi Fatima.
 
1681460595205.png

Mke wa Ashraf Hakimi amempeleka mahakamani ili kupata talaka na alitaka Mahakama iwagawanyishe mali.

Baada ya Talaka kufanikiwa na kukubaliana kugawana mali, ikagundulika kuwa Ashraf Hakimi hakuwa na mali yoyote na hata akaunti zake benki hazikuwa na pesa yoyote.

Inaelezwa kuwa mahakama imebaini Ashraf Hakimi alishaweka mali zake zote kwa jina la mama yake muda mrefu uliopita.
 
Msimbe mweupe huyo

If Achraf Hakimi’s wife has more assets than him now, does that mean Hakimi gets half of her money?
This is beautiful

Achraf Hakimi’s wife married a world class defender hoping she'd score 😂😂 that woman is mad dah
 
Sio yule Emmanuel Eboue aliekuwa akipata mshahara wote anatuma kwa mkewe ndo aweke uwekezaji.Mwisho wa siku Emmanuel akapigwa talaka na kuambulia zero.

Ashraf kweli Mungu alimuongoza, hawa warembo wengi wanakimbilia wacheza mpira sababu ya pesa.

Ndiyo maana C.Ronaldo hataki kufunga ndoa na Georgina.
 
Back
Top Bottom