Kisheria ipoje endapo Shilole atataka talaka watagawana mali walizochuma pamoja? Au hii ipo kwa akina mama tu kudai mali

Apr 4, 2019
31
33
Mwanamke anapoachika au kupewa talaka kisheria ipo hivi

(1) Una Haki Na Mali Mlizochuma Pamoja; Hiki ni kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kukifahamu, kuwa kama mkewe una haki ya kila mali mlizochuma pamoja, mali hizi ni zile za kuhamishika na ambazo si zakuhamishika.

Kuanzia nyumba, gari, akaunti benk, mashamba na mali nyingine ambazo zimepatikana katika kipindi cha ndoa na kutokana na ndoa.

Kuna aina tatu za mali, aina ya kwanza ni mali zilizopatikana kabla ya ndoa, mali za pamoja wakati wa ndoa na tatu mali ambazo si za pamoja ndani ya ndoa.

Hizi za kabla ya ndoa nitazizungumzia mbeleni, lakini hizi mlizochuma pamoja ni mali zote ambazo mlichangia kuchuma. Hapa nieleweke, sheria haimaanishi kwamba kama ni nyuma kila mtu alete tofali au bati au chochote, hapana wewe tu kuwa mke na kusimamia au kumpikia wakati anajenga inamaanisha mmechuna pamoja.

Hivyo hapa asijifanye eti kwakua wewe ni Mama wa nyumbani kuwa huna haki kwakua alinunua nyumba, kiwanja na kila kitu kwa mshahara wako. Je wakati ananunua kwani alikua anakula wapi, alikua anafuliwa na nani? Hivyo asikuambie hukuleta kitu, kama mali ilichumwa ukiwa kwenye ndoa ni yakwenu na una haki nayo.

Lakini kuna mali ambazo zimepatikana wakati wa ndoa lakini hazitokani na wanandoa, hizi ni mali za kama zawadi, urithi na nyingine ambazo hazikuchumwa na mmoja wa wana ndoa. Hizi hamuwezi kugawana na yule mwenye mali ndiyo atabaki nazo. Lakini nyingine zote ziwe za mke au mume bila kujali zina jina la nani ilimradi zimechumwa wakati wa ndoa basi ni zenu.

(2) Mali Zilizochumwa Kabla ka Ndoa; Umemkuta na nyumba, magari na mabiashara yake. Lakini hata yeye kakukuta na mali zako, hizi ni mali ya kabla za ndoa, mali hizi haziwezi kugawanywa isipokua kama zimegeuzwa na kuwa mali za wana ndoa.

Kuna namna mbili za kugeuza mali hizi kuwa za wanandoa na hapa naomba kuwa makini ili isije kula kwako hata kama wewe una kanyuma kako ulinunua kwa jina lako. Namna ya kwanza ni kwa wanandoa kukubaliana kwa maandishi au kubadilisha umiliki.

Kwa mfano kama ulimkuta na nyumba akaamua kubadilisha hati ikawa ya wawili, gari akabadilisha kadi, kiwanja au mali nyingine.

Mkifanya hivyo bila kujali kama ulichangia chochote au la zinakua za kwenu. Namna ya pili ni ya kuziendeleza zile mali bila kujali aina ya uendelezaji.

Kwa mfano ulimkuta ana nyumba, wakati wa ndoa mkaipaka rangi ile nyumba, mkajenga ukuta, mkaipaua. Ulikuta ana kiwanja mkakiendeleza, biashara mkaiendeleza na vitu vingine. Kwa kufanya hivyo bila kujali kama ulichangia chochote wakati wa upatikanaji basi mali zinakua za kwenu.

Hivyo kama utaweza kuithibitishia mahakama kuwa kabla ya kukuoa alikua na nyumba lakini ile nyumba haikua na fensi ila sasa ina fensi basi ile nyumba ni yenu bila kujali ulichangia kiasi gani? Hivyo wakati akijitapa kuwa huondoki na chochote hembu tafuta fundi muambie mpake rangi halafu mtakutana mahakamani!

(3) Ni Mama tu Wa Nyumbani Je Kuna Chochote Unapata? Hili ni swali muhimu sana, wanaume wengi kwakua ndiyo hufanya kazi hudhani kuwa mke hatapata kitu wakiachana kwakua hakuchangia kitu. Lakini akina Mama nao kwakua hawajui shetia basi huondoka tu mikono tupu kwakua hawakuchangia chochote.

Sheria haijasema hivyo, Mama wa nyumbani ana mgao wake katika mali alizochuma mumewe. Hii nikwakua amepoteza muda wake kukaa na huyo mwanaume, kumlelea watoto na hata kama hana lakini alikua akimpikia mwanaume, kumfulia na kulinda nyumba hivyo ana haki zake. Kwa maana hiyo anapokupa talaka usiondoke tu kama fala, dai chako na nitakufundisha hapo mbeleni nini chakufanya.

Kisheria mchango wa pamoja hujumuisha kazi anazofanya Mama wa nyumbani kama vile kufua, kupika, kuosha vyombo, kuhudumia watoto na nyingine zote. Bila kujali kama zinaingiza kipato cha moja kwa moja sheria humlinda Mama kwani kama asingekua kwenye ndoa basi angeweza kufanya mambo yake mwenyewe na hata kuweza kufanikiwa zaidi ya hapo.

(4) Je, Mgawanyo ni nusu kwa nusu? Kuna dhana imejengeka kuwa watu wakishaoana basi hugawana nusu kwa nusu kwa kile walichochuma. Hapana haiko hivyo, sheria haiweki hivyo bali hutoa mwanya kwa mahakama kuangalia mchango wa kila mwana ndoa katika kupatikana kwa ile mali.

Kwamba aliyechangia kikubwa ndiyo atapata kikubwa. Kwa Mama wa nyumbani kwa maana ya yule ambae mchango wake huwezi kuupima basi mahakama itaangalia na itakadiria muda wake na nguvu zake alizotumia katika kupatikana kwa ile mali na atagaiwa. Kwa maana hiyo hakuna lile suala la kugawana anusu kwa nusu.

(5) Utafanya Nini Ili Upate Haki Zako? Mgawanyo wa mali hutokea pale talaka inapotolewa na si kabla ya hapo. Kwa ndoa za kiislamu mwanaume anaweza kuamua tu kumpa mkewe talaka na mke akaondoka bila kuchukua chochote. Lakini kwa zile za kikiristo mwanaume anaweza kumfukuza mkewe akaondoka nayeye akaenda kuchukua mwanamke mwingine au akaishi naye.

Wanawake wenei hasa wale ambao hawakuchangia moja kwa moja wakifukuzwa au kupewa talaka hudhani kama mambo yameishia hapo. Hapana dada yangu, hizo ni talaka za kidini au kauchana kwa mtaani, ili kugawa mali nilazima utafute talaka ya mahakamani na mahakama iamue upate nini?

Sasa hatua ya kwanza ya kudai talaka ni kwa wewe kwenda kwenye baraza la usuluhishi. Kwa waislamu Baraza la usukuhishi ni BAKWATA nenda ofisi za Baraza la Waislamu Tanzania BAKWATA lililopo karibu na wewe, mwenza wako ataitwa, mtajaribu kusuluhishwa na anaweza kuamriwa kutoatalaka au asipokubali kutoa basi watawapa barua kuwa imeshindikana na hapo ndipo utaenda mahakamani.

Kwa waikristo au wale wa ndoa za kimila, baraza la usuluhishi ni Kwenye ofisi za ustawi wa jamii, hizi zipo katika kila Majiji, manispaa, halmashauri za miji na wilaya. Nenda hukokueleza matatizo yako na huko watajaribu kusuluhisha ikishindikana basi watakupa barua kwenda mahakamani kudai talaka na kugawana mali.

Hivyo dada yangu usikae kimya tu baada ya kuachwa, una haki nyingi za kudai, lakini usiachwe tu kienyeji enyeji, mtu mkatengana halafu ukaondoka bila hata senti, kama mlichuma pamoja basi jua kuwa una haki ya kile mlichochuma pamoja hata kama si nusu kwa nusu lakini haki ipo.

(6) Dhana Ya Ndoa/Sogea Tuishi; Hii ni aina ya ndoa ambayo hutokea kama watu wa jinsia mbili wataishi ndani ya nyumba moja kwa miaka miwili mfululizo kama wanandoa, wakifanya mambo kama wanandoa. Hapa muwe makini, nilazima muishi miaka miwili mfululizo, ndani ya nyumba moja kama mume na mke.

Kama utaweza kuithibirishia mahakama kama mliishi kama wana ndoa, basi utapata haki zote za mke katika kutengena (si katika mirathi). Sasa ili kuithibitishia mahakama kuna mambo ambayo nilazima yatimie. Kwanza nilazima uonyeshe mlikua mnaishi pamoja ndani ya nyumba moja.

Hapa sio ile mmoja anaishi huku mwingine kule mnakutaka kwa kipindi flani, nilazima iwe miaka miwili tena mfululizo. Kama mnatengana na kurudiana hiyo si mfululizo. Pili nilazima kuwe na kitu cha kuthibitisha hilo, labda mliingia mkataba pamoja, mali ya pamoja na namna ambavyo mlikua mnafanya mambo kwa pamoja.

Kama mahakama ikitamka na kuthibiisha dhana ya ndoa utapata haki zote ambazo anapata mwana ndoa za kidini, mila na hata serikali. Hivyo usikubali kuondoka ondoka tu akakufukuza bila kitu wakati mlichuma pamoja hata kama wewe hukutoa fedha moja kwa moja, una haki na kila kitu chake mlichochuma kipindi hicho.

Vip pale uchebe akitaka haya yawepo inakuaje hapa
 
Wewe bwana mdogo wacha kupiga makelele mitandaoni!

Sheria sio hadithi za abunuwasi unapiga piga tu blah blah na viuchambuzi vyako!

If you have an issue, visit any law chamber nearby and get help!
 
Sasa juzi tu kuna anko wangu (mtoto wasister)amenunua kiwanja sasa kwene kuandikishiana mwenyekiti akamuuliza mbona umekuja na shahidi mmoja? shahidi wapili ilitakiwa niwe mimi nasiku hiyo nilikua kibaruani ila eneo nilishaenda kuliona, akamuambia shahidi mwingine ni anko naleo yupo kibaruani kwahiyo sehemu yake atasain kesho akamuuliza nahuyu uliokuja nae ninani yako akakuambia ni mkewangu (kumbuka mke mwenyewe anahusika hapo kwene kipengele cha SOGEA TUISHI na mke nimama wanyumbani tu natangu wameanza kuishi wote hadi sasahivi nimiezi minne tu,mwenyekiti akamuambia sasa huyu hatakiwi kuwa shahidi bali ni mnunuzi mwenzako kwahiyo pale kwene kipengele cha NAMUUZIA..

Mwenyekiti akaunganisha najina lamke kwaiyo hati ikasomeka NAMUUZIA Juma Kabombe Pondamali na Salome Mkalifya(mke) .Anko akaishiwa pozi ila akashindwa lakufanya mana isingeleta picha nzuri kama pale mbele yakadamnasi angesema hapana andika jina langu tu (mme).

sasa kesho yake nimerudi nyumbani nakuta ile hati nyumbani mana alienda kuiacha nyumbani kwangu nakuahidi kuifuata kesho yake baada yamimi kukamilisha kipengele changu .sasa kesho yake nimegeuka nakuta ile hati nikaisoma kwanza kufika kile kipengele cha NAMUUZIA nikastaajabu mana kama mimi ninamke na mtoto lakini hakuna hati niliyoambatanisha jina langu na la mke wangu mana sijaona sababu.

Nikasema huyu anko hii staili kaitoa wapi ikabidi nimpigie simu aje hom kufika tu baada yasalamu akaanza kunisimulia jinsi ilivyokua kabla hata sijamuuliza,anasema anaombea wakija kupata mtoto tu aibadilishe iyo hati isomeke jina lamtoto sasa mkuu mtungi wa gesi hapo kisheria imekaaje kuhusu hiki kiwanja kama hawa watu wakaja kutengana kabla yahiyo miaka miwili (hatuombei) zaidi tunawaonbea kheri ktk ndoa yao nasiku moja waje wafunge ndoa rasmi wajaaliwe na watoto
 
Sasa juzi tu kuna anko wangu (mtoto wasister)amenunua kiwanja sasa kwene kuandikishiana mwenyekiti akamuuliza mbona umekuja na shahidi mmoja.? shahidi wapili ilitakiwa niwe mimi nasiku hiyo nilikua kibaruani ila eneo nilishaenda kuliona...
Mtoto wa sister wako sio uncle wako ni niece kama wa kike au nephew kama wa kiume.

Badilika kwenye hilo, mnawaharibu sana watoto kuwaita uncle sijui aunt badala ya niece au nephew
 
Hahaa shukrani sana chief nitajitahidi kujizoesha majina hayo japo kibongo bongo majina hayo nimageni sana nani aghalabu kukuta sehemu wanatumia majina hayo naukikuta basi hao ni full mabasi yanjano
Mnawapa shida watoto , maana shuleni wanafundisha Y , wakifika nyumbani wanakuta Y inaitwa X.
 
Sasa juzi tu kuna anko wangu (mtoto wasister)amenunua kiwanja sasa kwene kuandikishiana mwenyekiti akamuuliza mbona umekuja na shahidi mmoja.? shahidi wapili ilitakiwa niwe mimi nasiku hiyo nilikua kibaruani ila eneo nilishaenda kuliona, akamuambia shahidi mwingine ni anko naleo yupo kibaruani kwahiyo sehemu yake atasain kesho akamuuliza nahuyu uliokuja nae ninani yako akakuambia ni mkewangu...
Kwa kifupi unaweza badili hati yako kama unaona kuna dosari sehemu sema taratibu zake ni ndefu zaid
 
Hii ya kuishi ‘nyumba moja’ kama wanandoa kwa miaka miwili mfululizo, vipi hizi nyumba za kupanga tunaohama kila kukicha!!!
 
Hahaa shukrani sana chief nitajitahidi kujizoesha majina hayo japo kibongo bongo majina hayo nimageni sana nani aghalabu kukuta sehemu wanatumia majina hayo naukikuta basi hao ni full mabasi yanjano
Hayo majina siyo mageni labda lugha imekuchanganya "niece" na "nephew" maana yake ni Mpwa, hivyo mtoto wa Dada yako anayekuita mjomba wewe utamuita Mpwa (haijalishi jinsia).
 
Back
Top Bottom