martial jb
JF-Expert Member
- Oct 21, 2021
- 864
- 1,456
Habari wakuu,
Hivi karibuni kumekuwa na story inayotrend sana kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na wanandoa wawili waliofanikiwa kufikisha miaka mitatu kwenye ndoa yao na kufanikiwa kupata mtoto mmoja, Achraf Hakimi(24) ambaye ni mchezaji wa kulipwa wa PSG na mkewe Kiba Habouk(34).
Sakata hili limekuwa maarufu baada ya mkewe na Achraf mwanamama Kiba Habouk kudai talaka mahakamani ikiwemo na mgawanyo wa mali zinazomilikiwa na familia yao hiyo.
Lakini katika hali ya kushangaza mahakama imegundua kuwa Achraf licha ya utajiri wake wote huo, hamiliki chochote kwani mali zake zote amemilikisha kwa mama yake SAIDA MOAH ikiwemo na mshahara wake anaoingiza kila wiki pale PSG, kwani unaingia kwa jina la mama yake.
Imeshangaza baada ya kugundulika Achraf hela ya matumizi yake binafsi anachkua kwa mama yake, na baada ya uchunguzi zaidi imegundulika pia mama yake ndiye mwenye majina ya magari yote ya kifahari ikiwemo na assets zote za jamaa mpaka vyombo vya ndani.
Hivyo basi, bibie Kiba Habouk amebaki hana la kufanya na kubaki kushangaa tu! Kwani mahakama imemaliza ushahidi huo.
Narudi kwenu wakuu, hii imekaaje mbona kama ni dhambi tukiangalia upande wa pili wa shilingi. Umeishi na mwenzio miaka mitatu analea mwanao, na pia kukusaidia kwenye masuala mbalimbali ya kimaisha, halafu mwisho wa siku asipate chochote mnapoachana.
Sasa muda huo si bora angekua anafanya shughuli zake zingine za kumwingizia kipato inawezekana angefika mbali, kuliko kutoka kwenye ndoa na kuanza moja.
Naomba ufafanuzi wakuu, sio kwa ubaya lakini ni kueleweshana tu jamani.