Status
Not open for further replies.
Afuate taratibu kama alivyoshauriwa na Tundu Lissu ili aweze kushinda vita hii bila madhara makubwa.Aangalie mikataba ya kimataifa na jinsi ya kujinasua ili tuanze upya.
 
Kwanini nasema Raisi yuko sawa?

1. Anaonekana ni kweli anapigania kile wananchi wanataka,
2. Sio Mwoga wa maamuzi kiasi fulani,

Siwezi kumwelezea Raisi zaidi kwabasabu kile watanzania tunataka anakifanya yeye kama yeye, si kisheria, kwasababu Sheria tayari CCM wameshaharibu.
CCM wametengeneza Sheria mbovu ambazo zinampa tabu Raisi kutete Rasilimali za Nchi, Tuliona Mpambano ya Wabunge wa CCM na Upinzani kuhusu Sheria za Madini na Gesi ziweje? mpaka walifikia hatua ya kutishiana maisha na Upinzani kususia kupitisha Sheria hizo.
CCM walipitisha na Mikataba ikasainiwa na kutwambia ni Siri. Nampongeza Raisi kwa sababu katuonyesha kati ya Wabunge wa CCM na Upinzani nani alikuwa anapigania masirahi ya Nchi.
Mpaka hapo mmenielewa vizuri.

Ila Raisi nakuomba utumie sana Hawa wanasheria wako, ili kufuata utaratibu wa Kinchi na Kidunia usiweze kukwama mahali.

UVCCM mnatia aibu kama Baba zenu CCM, hivi mlifanya sherehe ya kumpongeza Raisi na Chama chenu,
Hamkusikia aibu?
kwanini msingempongeza Raisi bila kutaja Chama chenu?
Hamjaona kilichosababisha Mchanga kusafirishwa?
Hivi kabla ya kumsifia Raisi, hamkufanya uchunguzi ni nani aliingia Miakata na kutengeneza Sheria za kuwaruhusu Wawekezaji kusafirisha Mchanga?

Msiwe kama mashabiki wa Soka kushangiria Chenga na Magoli, yafaa mjue nini maana ya Nchi na matendo ya Kinchi, Chama chenu kimeferi, yafaa mfate ya Magufuli sio ya CCM, Mkitaka kutamba na CCM wafundisheni kazi Baba zetu Bungeni jinsi ya kutunga Sheria za masirahi kwa Nchi, sio kwa matumbo yao, maana Sheria wanazotunga haziifaidishi hata CCM yenyewe.

Yangu ni hayo
Tanzania mbele, CCM, CHADEMA, CUF baadae.
 
Nimefanya kazi na watu wengi sana,amini usiamini Rais wangu hakuna binadamu mkamilifu,utateuA na kutengua sana mpaka 2020, nakushauri badili style unayoenda nayo,hutakaa upate mtanzania aliyekamilika anayekwenda na wewe unavyotaka
Kumbuka Kikwete aliwapa semina elekezi,na wewe njoo na aidea tofauti uone kama hawatafanya kazi,tatizo sio wao ni kwamba hawajazoea kufanya unavyotaka
 
NYAMAZA, NYAMAZA NYAMAZA, SIPANGIWI!
 
Itakuaje kama ;

Magufuli ataamua bunge lipitie mikataba yote ya madini,mafuta na gas na ifanyiwe marekebisho kwa faida za watanzania wote

Magufuli ataamua kila mwanafunz anayejiunga na elimu ya juu na mwenye sifa ya kupata mkopo apate mkopo

Magufuli ataamua kutangaza baraza jipya la mawaziri lenye wapinzani ndani ake

Magufuli ataamua bunge lipitie rasimu ya warioba na ikiwezekana ipitishwe

Magufuli ataamua vyombo vya habari kuwa na uhuru wa kuhoji jambo lolote bila kuvunja sheria zilizowekwa

Magufuli ataamua kuwaomba msamaha jamii zote ambazo pesa zao za rambirambi zilizotumika na serikali

Magufuli ataamua kutoa ajira mpya na kujaza zile ambazo ziliachwa na wenye vyeti feki

Magufuli ataamua kuanza kusimamia moja baada ya lingine yote aliyotoa ahadi kuyafanya kipind cha uchaguzi

Magufuli ataamua mkuu wa mkoa wa dsm kutoa vyeti vyake na hadharani na kukaguliwa na mamlaka husika
 
Ikiwa ataamua hivyo nadhani bashite segerea itamwita.
 
Mh Rais napenda kukushauri kupitia haka ka JF ketu kuhusu migodi yetu, Uwe na mtu rasmi anaepokea ripoti ya siku ya uzalishaji na ya mwezi maana matatizo yote yanaanzia hapo. TMAA uliwapa jukumu lakini sizani hata wanakanzudata ya uzalishaji wa migodi yote nchini, kingine mkuu taasisi nyeti kama TMAA,TANESCO,GST,TPDC,NDC na TIC ziwe chini ya Usalama wa Taifa. Mahala hapo ukipaangalia ovyo yatatukuta mengine. Wenzetu kina Putin hizo agency wanazijua vema. Kwakesi kama TMAA laiti ingekuwa chini ya Usalama wala wasingefanya ujinga mahala kama GST hapatakiwi kuwa lose sawia na hizo zingine nilizozitaja. Leo hii tunawatu tumewasomesha Mbele uko mambo ya Mineral economics na Metallurgical accounting ili watusaidie lkn eti wanashindwa Chunguza migodi kwanini hailipi kodi. Mkuu ziweke hizi taasisi chini ya usalama hafu uone watu watakavo wajibika. Leo mkuu ni siku ya kujadili smelter? Vichwa vyote vile vilivomaliza CoET? Hapana. Tunashindwa hata kuiba technology? Usalama najua kuna watu makini ambao wanaweza Zamia popote na kuja na document yoyote. Kiufupi mkuuu tunatakiwa kuwa na agencies za kiusalama kila sector hadi utaliii uko faru john hasingekufa kizembe. Ni hilo tuuu
 
Hakika toka uingie madarakani kuna makubwa umeyafanya ambayo viongozi waliokutangulia kabla yako ama hawakuyaona au waliyaona ila hawakuthubutu kuyavalia njuga kama wewe ulivyofanya. Hongera!!

Nikupongeze hasa katika suala hili la makinikia. Nakuomba usisikilize ya wa pembeni wanaodai suala la sheria, kwani hizo sheria ndiyo zimetufikisha hapa tulipo.

Lakini binafsi kuna moja bado linanikera katika upande wa elimu yetu na mfumo wa mawasiliano katika baadhi ya mihimili ya serikali. Watafiti wengi wamezungumza na pengine kuna ukweli kuwa mataifa yote yaliyoendelea, elimu yake hutolewa kwa lugha yao na hivyo kutukuza lugha yao wenyewe. Mfano; France, China, Japan, Korea zote mbili, Italy nk. Haya yote elimu za nchi zao hutolewa kwa lugha yao.

Tukitaka tuendelee kama taifa na ninaamini ndiyo dhamira ya serikali yako, thubutu na hili.
Katika level ya mahakama ngazi za juu, kesi huendeshwa kwa lugha za kigeni (sina hakika kama ni zote). Jaji mtanzania, mshitakiwa mtanzania, mlalamikaji mtanzania, mwendesha mashitaka mtanzania, kuna haja gani kuendesha kesi kwa kingereza?

Thubutu na hili uwe shujaa wangu katika taifa hili
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom