Status
Not open for further replies.
Mh. Rais unayo mipango mingi sana tena mingi ya maana sana kwa Taifa. Pia unayo malengo makubwa sana ijàpo njia zako wakati mwingine zimekuwa ngumu sana kueleweka. Ukiacha ukanda na udini yanayosemwa juu yako bado kuna mambo mengine yana sura ya upendeleo pia. Ama kwa minajiri ya chama, ukaribu na maeneo kisiasa hasa dhidi ya maeneo pinzani.

Hayo tuyaache, nia yangu leo ni kukuonesha eneo jingine moja linalokukwamisha na litakolokuangusha usipoangalia. Kuna websites za mkoa. Hili mh. raisi ni tatizo kubwa sana, tovuti nyingi za mikoa zimekufa na zingine hazijitambui na ziko usingizini. Tunajiuliza hawa maafisa habari kwenye mikoa kazi zao ni nini? Kuna zingine hazijawahi kuwa na jambo jipya tokea 2012, kuna zingine leo 2017 bado zimejaa habari za miaka 5 iliyopita, mfano kuhusu sensa za watu na makazi. Wengine bado wanaonesha mikoa yao ikiwa na wilaya fulani ambazo leo haziko tena huko tangia 2013. Haya yote ni maajabu kwenye hizi tovuti mh. raisi.

Leo hii wakati unasisitiza uwajibikaji na watumishi kujituma, kuzingatia semina ambazo zimetolewa hivi majuzi kwa maafisa habari kila mkoa juu ya kuweka habari zao na mipango yao wazi, bado hawaonekani kwendana na kasi yako. Hazionekani si habari za biashara tu bali hata za uchumi, idadi za watu, miradi, fursa za uwekezaji zilizo tayari na vitu vya namna hiyo. Hakuna hata kimoja. Waliojaribu utakuta habari iko robo na zingine zina miezi ya kutosha kila ukiingia unaambiwa taarifa zinaandaliwa. Yaani mtu anahitaji data leo ili alete miradi yake anataka kujua baadhi ya vitu kwenye hilo eneo ama mkoa bado tovuti inaendelea kusomeka loading... Miezi mitatu yote inaload nini?

Kwa mwendo huu maendeleo ya viwanda unayapataje mh. raisi? Hakika bado kazi ya kutumbua unayo na hata kwa wale wanaoponea kutumbuliwa inaonekana bado hawako radhi kujifunza, they are too stubborn and reluctant to changes. Tunahitaji kuhusanisha maendeleo ya viwanda na kada nzima ya IT, utoaji wa habari kwa raia, wawekezaji na wadau wa maendeleo isiwe tena hisani bali iwe ni sehemu ya kimkakati kufikia hazma ya viwanda. Tunahitaji wenye weledi na ujuzi kusaidia hapa, katika ulimwengu huu ni aibu kumlazimisha kila mdau kufunga safari kwenda ofisi za mikoa na wilaya kufuata habari. Vitengo vya habari kila ofisi ni wajibu wao namba moja kufanya hilo na ku update habari hata kwa baada ya wiki Mbili kuliko leo mtu anafanya pale anapojisikia yeye.

Walio chini yako wajaribu kukusaidia kama wewe una mambo mengi, mtume PM akusaidie ili kazi yako iwe nyepesi. Twaaafa!
 
Kama hakuna hela za kulipia hiyo website(host) afisa habari awe analipia?
Ka utetezi kadogo sana haka, kujitetea hata kwenye mambo ya duni kiasi hiki nayo huwa ni sehemu ya kushindwa. Ndo maana kuna haja ya watu kufundishwa ujasiriamali. Kupewa ofisi kubwa hivyo na ukawa mweupe unaweza kila siku ukaishia kushindwa, uongozi unakwenda sambamba na creativity mkuu vinginevyo hata ofisini kwako utafika sehemu utakalia jamvi kwasababu huwezi kuwaza mbali
 
huyo mwenyewe atumbuliwe kwa kutowawezesha kifedha,usilaumu tu,sikiliza na upande wa pili
 
Thread yote Rubbish..

Rais ana mipango mingi na Nchi hii mlikutana wapi akakwambia??

Mbona unajipendekeza namna hiyo..??
Au ndio walewale.

Ongea kiume acha kulamba lamba watu miguu.
 
Ka utetezi kadogo sana haka, kujitetea hata kwenye mambo ya duni kiasi hiki nayo huwa ni sehemu ya kushindwa. Ndo maana kuna haja ya watu kufundishwa ujasiriamali. Kupewa ofisi kubwa hivyo na ukawa mweupe unaweza kila siku ukaishia kushindwa, uongozi unakwenda sambamba na creativity mkuu vinginevyo hata ofisini kwako utafika sehemu utakalia jamvi kwasababu huwezi kuwaza mbali

Mkuu humjui Magu eeeh!! Atakwambia kwanza websiste ni gharama toa kila kitu, mtu akitaka taarifa aje mwenyewe wizarani/halmashauri etc..
huoni kama anatoa vitu visivyo vya umuhimu
 
Leo hii wakati unasisitiza uwajibikaji na watumishi kujituma, kuzingatia semina ambazo zimetolewa hivi majuzi kwa maafisa habari kila mkoa juu ya kuweka habari zao na mipango yao wazi, bado hawaonekani kwendana na kasi yako. Hazionekani si habari za biashara tu bali hata za uchumi, idadi za watu, miradi, fursa za uwekezaji zilizo tayari na vitu vya namna hiyo. Hakuna hata kimoja. Waliojaribu utakuta habari iko robo na zingine zina miezi ya kutosha kila ukiingia unaambiwa taarifa zinaandaliwa. Yaani mtu anahitaji data leo ili alete miradi yake anataka kujua baadhi ya vitu kwenye hilo eneo ama mkoa bado tovuti inaendelea kusomeka loading... Miezi mitatu yote inaload nini?

Kwani raisi akitoa maelekezo, hakuna utaratibu wa kupima kama yametekelezwa?
Kama hakuna, basi anatatizo kubwa kwenye uongozi wake.

Pamoja na hayo, TZ hii sio ya kutoa maelekezo majukwaani na kuamini yatatekelezwa, naamini raisi anafahamu hilo.
Kama raisi anajambo muhimu anataka kuliagiza, ahakikishe kuwa kuna utaratibu wa kufuatilia na kupima utekelezaji wake.

Vinginevyo tusimpe visingizio raisi kwa kushindwa kufanya kazi yake. Anazo resources za kutosha na mamlaka yaliyopitiliza ya kumwezesha kufanya kazi, ashindwe mwenyewe tu.
 
Muheshimiwa Rais japo Mimi mkosoaji Mkubwa wa baadhi ya Sera zako lakini naukuunga mkono pale unavyofanya vyema mfano Mzuri ulivyosimamia kidete swala hili la mchanga wa madini na hatimaye tumepata majibu Chanya.

Ushauri Wangu kwako ni kuangalia uwezekano wa kuigawanya hii Wizara ya Nishati na Madini ili kila kimoja kijitegeme la sivyo tutegemee hii Wizara kuwa Machinjio ya Kila Waziri atakayetia mguu...
 
WANA FJ.
Nifikishieni taarifa zangu kwa rais wangu kuwa hatuibiwi kwa sababu ya mikata mibovu bali ni kwa sababu ya usimamizi mbovu hivyo afanye hili utagundua mengine mabovu zaidi.

1). Chunguza dhahabu inayozalishwa migodini utagungua mahesabu tunayopewa ni kidogo sana kulinganisha na uzalishaji wao.

Kutokana na hili huwa kila mwaka wanasema hawajarudisha mitaji yao kumbe wanapiga faida ya kufa mtu.

Pesa zinazopotea kwenye mchanga unaoenda inje kuchakatwa ni kidogo sana kulinganisha na njisi wanavyoiba kwa kutoa mahesabu ya uzalishaji kidogo kulinganisha na uhalisia.
 
Kwanza nampongeza Rais wetu kwa udhubutu. Pili tatizo la nchi yetu wapi tumekosea...nani tumlaumu....tufanye nini ili tusogeee. Nikiangalia wasomi hawa hawa wanaopewa madaraka wanatuliza.
Hebu tushuke nondo hapa tufanyeje ili kumsaidia RAIS wetu kwa sbb nchi hii kwa hili la mchanga mpaka nimelia mpaka machozi yamenitoka. Nani wa kulaumiwa hapa....hii wizara ya nishati na madini ina mdudu gani??? Escrow ilikuwa wizara hii hii. Nani ametuloga watz na waafrika madudu ni sisi tu waafrika.
Tuweke vitu gani vitusaidie kuondokana na kuibiwa kwa mali za nchi zetu
Ndugu yetu prof Muhongo this is a second saga....

Kitu gani tuandike kitatusaidia kutoka hapa tulipo!!
Maswali ambayo sina majibu
1. Je ni siasa ndio tatizo?
2. Elimu yetu ina shida??
3. Umasikini wetu wa kifikra
4. Ujinga??
5. Sheria zetu??
6. Leadership yetu
7. Umoja wetu


Wapi tumekosea kama think tanker tunao, rasilimali tunazo na resource tunazo.

RAIS tunazidi kukuombea upange upya nchi hii.
 
Tuweke maslahi binafsi pembeni, tutosheke na mishahara yetu. Uzalendo uwe kipimo. Lakini pia nahisi sheria zetu zimekua butu na ushkaji unatawala kwenye utendaji. Ni wakati muafaka wa kufanya maamuzi magumu kwa wahujumu uchumi, wenzetu wananyonga sisi tunaogopa nini?! Teuzi nyingi zimekua za kulipa fadhila na kukomoa upande fulani. We need to be rational!
 
Umekuwa mzalendo mno kwa kupigania nchi yako Tanzania na kuinyosha njia iliyopindapinda (Mungu akubariki sana maana manufaa hawatayaona waliyepo sasa ila kizazi kijacho).
Ushauri wangu kwako ni huu.
Ijengwe commercial building internationally zitakazo deal na kupokea madini yote toka machimboni na kuweza ku process ili yaweze sasa kusafirishwa kwenda nje.
Hizo commercial ziwe kama mliman city hivi . na zijengwe Dodoma na kuwepo sheria ya kuzuia madini yasipelekwe popote Duniani bila kutokuwa processed hapo.
Pili. Ikiwa kuna watu wamehamisha pesa zao kupeleka nje kwenye mabenki uundwe utaratibu pesa hizo zirudi Tanzania kwenye mabank yetu na kujua vyanzo vya mapato vya wahusika ikibainika ni hazina shida waachiwe la zitumike.
Tatu. Wekeza katika Hospital kubwa sana ya magonjwa sugu hapa Tanzania ambayo hutulazimu kwenda India na mipango hiyo ni kuwaita wafanyabiashara wazalendo waweke commitment ya kuchangia mfano wakipatikana wafanyabiashara hamsini tu na kila mfanyabiashara akachangia billion Moja kwa mwaka .tutakuwa tumepata billion hamsin zidisha kwa miaka mitatu una billion mia Mojaa na hamsini tayari tutakuwa na jengo nzuri na kunusuru gharama kubwa na madaraja kwa wananchi.

NNE.ukweli ukiona watu wanapiga kelele wameguswa penyewe na wengine wameonewa wengine hawajaonewa walioonewa wape haki zao maana chozi la mnyonge ni ombi baya kwa kizazi chako chote na ombi la masikini ni baraka pia,sasa fanyia kazi suala la mkuu wa mkoa kama yanenwayo yanauhakika na uchukue hatua kwake usiogope.

Tano. Boresha usafiri wa ndani wa ndege ,reli,majini kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa ndani, hawa wageni wanatuibia tu hawana uchungu na nchi hata kidogo.
 
Salaam Zikufikie Mh Raisi Pole Na majukumu Ya kulijenga Taifa

Sio kazi Rahisi lakini Unajituma Ingawa kuna mapungufu Yako ya hapa Na pale

Niubina damu lakini pale unapo Fanya jema destur ya wa Tanzania Nikupongezana

Hongera Kwa Kugundua Uozo Uliopo katika sekta ya Madini

Hongera dhazati kwa Tume ulio iunda Kwakuwa Waaminifu

Nakukuletea Mezani Uchunguzi Sahii bila kuficha jambo Ingawa Yapo mengi Makubwa Yenye ukakasi Nayenye kuhitaji kutizamwa pia kiumakini ..


Lengo Nadhumuni Lakukuandikia Barua hii Nikukupongeza kwa kazi nzuri Tulio iyona Lakini pia kuleta Ombi langu kwako

Mimi kama Mtanzania Nina umia sanaa kuona sekta ya madini Inanufaisha makundi flani Na kuyafanya watumwa

Makundi flani hili halivumiliki hatakidogo

Makundi Ya wachimbaji wafanyakazi au kwajina Maarufu (Wanawapolo)

Wamekuwa Wakinyanya sika sanaa Na waajir wao Nahata wengine Kuishia Kufa bila kupata hata tone la Faida Ya kazi wanazo fanya

Kutokana tuu Na sekta hii kuwa Na umimi Ulio pitiliza
ileweke Nao wana (watoto )wake ) wanahitaji

Kulisha familiar na kuzisomesha pia

Nakufanya Maendeleo yao Kimasha

ila wanashindwa kutokana Na sekta isivyo wajali wachimbaji wadogo wakuajiriwa

ilhali wao Ndio sababu ya Kukuza na kuinua sekta ya madini Tanzania

Ombi langu ukifikiria Kuteua Waziri katika sekta hiyo

Naomba Nami Nipate pendekezo ikifaa unipitishe Nanika timize wajibu Na kwenda na kasi yako

Kwanza Na ahidi kufichua Uozo Zaidi ya huu Nakusimamia sekta Ya madini kikamilifu

ili serikali iingize pato Wafanyabiashara Waingize kipato

Na waajiriwa wao pia

Ombi langu mh Naomba uniteue Kushika nafasi hii
Naahidi sitakuangusha

Ndani ya Week Moja toka Uniapishe Nitaanza Kudeal jino Kwajino

Nasita mvumilia wala kumhurumia
Atakae subutu Kufanya ujanja ujanja

Wako katika Ujenzi wa Taifa N:Abdul

317d58250b7f0fc298abf1b2edea4ddd.jpg
b28aa739f74e80f6d17ae69a717ad0fe.jpg
 
Ukiandika katika utaratibu unaotakiwa ingependeza zaidi.

Mfano, ukiacha kuweka herufi kubwa mwanzo wa maneno yaliyo katikati ya sentensi ambayo sio nomino

Kuandika maneno ya kiswahili kwa ufasaha, mfano "Iyunda sio sahihi bali ni iunda"

Pia kutumia punctuation marks kama nukta na mikato.
 
Ukiandika katika utaratibu unaotakiwa ingependeza zaidi.

Mfano, ukiacha kuweka herufi kubwa mwanzo wa maneno yaliyo katikati ya sentensi ambayo sio nomino

Kuandika maneno ya kiswahili kwa ufasaha, mfano "Iyunda sio sahihi bali ni iunda"

Pia kutumia punctuation marks kama nukta na mikato.
Sii imla mkuu Ujumbe umefika
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom